Mwenye kazi au connection ya kazi anisaidie

Mar 12, 2024
45
139
Habari za wakati huu wakubwa.

Samahani, mimi ni kijana umri miaka 26. Nina Bachelor Degree ya Ualimu. Ninapatikana Shinyanga mjini kwa sasa.

Naamini mbali na kushare taarifa mbalimbali pia tunaweza kusaidiana humu. Najua kuna watu wa aina tofauti hivyo yote yanawezekana. Kwa yeyote anaeweza kuwa na kazi ya uhakika au connection ya kazi yoyote anisaidie wakuu. Hali si nzuri upande wangu hivyo naomba sana, kama naweza kusaidika nisaidike kupata kazi ili maisha yasonge ndugu zangu. Nipo tayari kukuja popote maadamu itakuwa ni uhakika.

Najua wapo wengine hudhihaki na kufanya utani ilhali hawana kazi ili kusumbua wenzao lakini itapendeza kama watu watakuwa serious katika hili.

Natanguliza shukrani🙌
 
Back
Top Bottom