Uzi maalum kwa wenye magari mabovu tu: Tupeane uzoefu na motisha na namna ya kuishi nayo

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Habari! ndugu zangu wenye magari mabovu tupeane faraja, ushauri na motisha wa namna ya kuishi nayo ingawa yanatupasua vichwa!

Uzii huu ni rasmi kwetu wenye magari yaliyo na changamoto! Nyie wenye magari mapya kaeni pembeni mle popcorn kidogo!

Hapo namaanisha wale ambao magari yetu tunayajuya wenyewe tulivyoyazoea kutokana na ubovu mbalimbali wa kudumu!

Mfano! Mimi nilikuwa na trekta moja mbovu ambayo kabla ya ya kukunja kona (nikikaribia kukata kona) ilikuwa lazima nianze kukata /kuzungusha steringi mita 20 kabla sijafika kwenye kona yenyewe ndo inapinda la sivyo nitapitiliza tu hakuna namna!

Baadae nikaja pata kigari kingine kibovu, aroo breki zake husimami bila kupampu pump! Uking'ang'ania breki unaweza pita nao mbeli maana kile kigari kilikuwa roho mkononi!

Sahivi ninayo nyingine mbovu inaugonjwa kushituka kama ina kifafa arooh! Unaweza ukawa kwenye mwendo mzuri tu mara inakita gudu kwa mshituko mkubwa! Nikiwa na abiria lazima ashituke lakini mie wala nishazoea naishi nayo tu maisha yanasonga!

Naomba tusimuliane magonjwa na ubovu wa magari yetu namna vile tunaishi nayo pamoja na changamoto zote, pia ikiwezekana tupeane mbinu za kutatua changamoto endapo utalielewa tatizo la ugonjwa wa mwenzako reply kwenye comment usimfuate Pm ili sote tujifunze.

Karibuni
 
Gari yangu kushtuka kpuuh! napotoa P kwenda D asubuhi.

Nishahangaika sanaa bila bila.

Transmission Fluid, Oil sample pan, sijui ujinga gani kote kushachekiwa mara kibao.

Maisha yanaenda.

Halaf hizi gari ndogo nimeona nyingi zina tatizo la kutoa mlio wa chwiichwichwiiiii kwenye FAN BELT hasa dereva anapokanyaga mafuta ku-accelerate.

Naona watu wanaishi nayo hivo hivo. Huwa ni tatizo gani lile?
 
Hapo umesahau muda mwingine latetemeka kama ina limonia asubuh
 
Kuna daladala nyingi naziona zimeegemea upande mmoja.

Hasa daladala za kutoka G'mboto kuja Ubungo, Mbagala kwenda Mbezi, Tandika kwenda Kariakoo.

Yaani ikiwa inakuja unaona kama inataka kuanguka hivi upande.

Ama ikiwa inaenda ukawa nyuma unaona ilivoinama upande (mara nyingi naona zinaegemea upande wa Konda)

Hivi ni tatizo gani lile?
Ama ni uzito wa abiria mlangoni
 
Uzito mana upande wa konda kuna mstari mmoja wa siti so wanaosimama wazid tofauti na upande wa dereva kuna mistari miwili ya siti
 
Kuna daladala nyingi naziona zimeegemea upande mmoja.

Hasa daladala za kutoka G'mboto kuja Ubungo, Mbagala kwenda Mbezi, Tandika kwenda Kariakoo.

Yaani ikiwa inakuja unaona kama inataka kuanguka hivi upande.

Ama ikiwa inaenda ukawa nyuma unaona ilivoinama upande (mara nyingi naona zinaegemea upande wa Konda)

Hivi ni tatizo gani lile?
Ama ni uzito wa abiria mlangoni
Hahah huo ugonjwa unasababishwa na vituo vya daladala mara nyingi wanaposhusha huwa wanaacha mataili upande wa kulia juu ya lami, na ya kushoto inje ya lami! Na vile watu wakipanda spring za kushoto huchoka mapema na kulifanya daladala lilalie kushoto!
Tiba yake ni pamoja na kuwa na vituo vizuri vya kushusha na kupakia ambavyo gari haitainama kushoto
 
Gari yangu kushtuka kpuuh! napotoa P kwenda D asubuhi.

Nishahangaika sanaa bila bila.

Transmission Fluid, Oil sample pan, sijui ujinga gani kote kushachekiwa mara kibao.

Maisha yanaenda.

Halaf hizi gari ndogo nimeona nyingi zina tatizo la kutoa mlio wa chwiichwichwiiiii kwenye FAN BELT hasa dereva anapokanyaga mafuta ku-accelerate.

Naona watu wanaishi nayo hivo hivo. Huwa ni tatizo gani lile?
Hii inakuaga issue ya ECU kama sikosei. Jaribu kuweka ECU mpya waiprogramu, inaweza ondoa hilo tatizo.
 
Gari yangu kushtuka kpuuh! napotoa P kwenda D asubuhi.

Nishahangaika sanaa bila bila.

Transmission Fluid, Oil sample pan, sijui ujinga gani kote kushachekiwa mara kibao.

Maisha yanaenda.

Halaf hizi gari ndogo nimeona nyingi zina tatizo la kutoa mlio wa chwiichwichwiiiii kwenye FAN BELT hasa dereva anapokanyaga mafuta ku-accelerate.

Naona watu wanaishi nayo hivo hivo. Huwa ni tatizo gani lile?
Muda mwingine ni tatizo la fan belt kulegea ama imechoka inahitaji kubadilishwa.
 
Unanunua gari bovu kwa milioni 5 sijui 6, then gharama unazotumia kwenye utengenezaji deile ikipata breakdown mara kibao, afadhali ununue chombo kipya safi kabisa hata kama ni aghali.

Hapo sijazungumzia ulaji wa mafuta, uchafuzi wa mazingira, status, etc
 
Gari mpya hazikamatiki mkuu! Maana kuna upya zero kilometers, na upya wa used kutoka Japan ambazo wengi huita mpya kwa ardhi yetu ...lakini ni mitumba !

Yote kwa yote! Kwa kipato cha mtanzania ni asilimia 5% ya watu kati mia wenye uwezo wa kumudu kununua gari mpya 0 KM, baada hapo asilimia 20% wanaweza agiza used kutoka Japan, na 25% wanauwezo wa kununua yaliyotumika na watu hapa bongo, na baada ya hapo 50% ya watanzania hawana uwezo wa kumiliki gari lolote
 
Back
Top Bottom