UVCCM Kagera watoa tamko kuhusu Taarifa ya Sintofahamu iliyotolewa na Emeltha Kente yenye Ujumbe Maalum kwa Rais Samia

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Kwenye Ujumbe huo, Emeltha alimpa Rais Samia siku 4 kutimiza kusudi la Mungu la Kinabii la kurudisha mali za wavuvi zilizopokonywa na Serikali, kuwatoa jela wavuvi waliopewa kesi za uwongo wakatumikie familia zao, wavuvi wavue kwa kutumia kokoro kwa nchi 4 hadi 5 na siyo nchi 6 kama ilivyo sasa pamoja na kuwachukulia hatua kali viongozi wa Serikali wasiotenda haki kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Emeltha, ikiwa siku 4 zitapita bila Rais Samia kutolea tamko mambo haya, Bunge na Ikulu vitaporomoka na Serikali itagawanyika vipande vipande

====

Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera unautaarifu Umma kwamba umepokea kwa Masikitiko makubwa tarifa ya Sintofahamu iliyotolewa na Mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Mkoa Ndg. Emeltha Joseph Kente kuhusu kile alichokiita "Ujumbe mzito kwa SSH kutoka Mbinguni" na kuisambaza yeye mwenyewe mitandaoni leo 26 Januari, 2024.

Sisi UVCCM Mkoa tunalaani na kupinga vikali kitendo hiki cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na kiongozi huyu, kwani ni kinyume na Utaratibu wa Kikanuni wa Jumuiya yetu katika kufikisha Ujumbe.

Kwa kuzingatia kwamba aliyefanya kitendo hiki ni kiongozi katika Jumuiya tunaviomba vyombo vya dola likiwemo Jeshi la Polisi limtafute Kiongozi huyu popote alipo na kumkamata mara moja ili ahojiwe na kuchukuliwa hatua kali kwa Mujibu wa Sheria kwani alichokifanya sio msimamo wa Jumuiya ndani ya mkoa wetu.

UVCCM Mkoa wa Kagera tutendelea kuwa kielelezo kizuri cha Vijana wenye kutii na kuheshimu mamlaka zote akiwemo Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Aidha, Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa itakutana kwa dharula kesho tarehe 27/01/2024 saa mbili asubuhi ili kujadili na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Kiongozi huyo Emeltha J. Kente.

IMG_9757.jpeg
.
 
View attachment 2884667

===
Kwenye Ujumbe huo, Emeltha alimpa Rais Samia siku 4 kutimiza kusudi la Mungu, la sivyo Bunge n Ikulu vitadondoka.
Samia asishupaze shingo
 
Haya mambo ya kuchoma nyavu yalifanywa na jitu la hovyo kabisa linaitwa Luhaga Mpina
 
Hawa yuvisisiemi ni waamiaji haramu!! Kente ni mtanzania mwenye uchungu na upendo kwa watanzania wenzie!!
 
Uvccm umatengeneza kizazi cha hovyo cha uoga na ujinga,kwenye ukweli semeni vijana ndio jeuri ya chama,nasio vijana wajinga na waoga.
 
Back
Top Bottom