Uteuzi: Amani Karume na Anna Makinda wateuliwa kuwa Wakuu wa Chuo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,818
4,569
1692371599398.png

Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

1692371675728.png

Anne Semamba Makinda, Spika Mstaafu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Rais Samia pia amemtua Anne Semamba Makinda, Spika Mstaafu kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Ushirika Moshi (MoCU), uteuzi huu unaanza mara moja.

1692371760122.jpeg
 
Ni mwendo wa kupeana mashavu kama kawaida ila mbona tu Wazee mnaangalia Uzoefu tu au? Vijana hamna?
 
Hizo nafasi kikawaida wanapewaga viongozi wajuu, vitu vingine viachage tu ka vilivyo utanishukuru
 
Halafu wenye Akili Kubwa duniani akina GENTAMYCINE, TEC na Vatican Wakiwadharau kwa muyafanyayo mnakasirika.

Hovyo kabisa....!!
 
Katika mataifa ya Jumuiya ya Madola, kansela kawaida huwa mkuu wa chuo kikuu ambaye si mkazi, ni wa sherehe (ceremonial). Katika taasisi kama hizo, mtendaji mkuu wa chuo kikuu ni makamu wa chansela , ambaye anaweza kubeba cheo cha ziada kama vile rais (km "rais & makamu-chansela").
 
Mtanganyika anaweza kuwa mkuu wa Zanzibar University!.
Mimi naona swali zuri la sisi kujiuliza ni kwamba je na huko Nchi zilizoendelea huwa zinateua wazee waliostaafu tena waliokuwa viongozi wakuu kwenye nyadhifa zao kuwa wakuu wa vyuo ??!!
 
Mimi naona swali zuri la sisi kujiuliza ni kwamba je na huko Nchi zilizoendelea huwa zinateua wazee waliostaafu tena waliokuwa viongozi wakuu kwenye nyadhifa zao kuwa wakuu wa vyuo ??!!

Ninaamini japo sina hakika. Kwa kiasi kikubwa hata tuliokuwa tunawavhukulia kuwa ni wajinga wenzetu, wahindi na waarabu, walishaacha huu utaratibu zamani.

Siku hizi wenye akili wanaangalia mchango alioutoa wa siku zilizopita au unaotarajiwa kutolewa siku zijazo na wanayemweka.

Mchango unaweza kuwa kifedha au kimkakati hasa kipindi cha mabadiliko makubwa.

Ifike siku hawa wakubwa waangalie zaidi maslahi, mahitaji na future ya taasisi husika. Kama ndivyo wanavyofanya basi jamii yetu ione hayo mabadiliko makubwa ya hizi taasisi zetu.
 
View attachment 2720893
Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

View attachment 2720894
Anne Semamba Makinda, Spika Mstaafu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Rais Samia pia amemtua Anne Semamba Makinda, Spika Mstaafu kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Ushirika Moshi (MoCU), uteuzi huu unaanza mara moja.

Lakini hakuna mTanzania yeyote toka Bara (Tanganyika), anayeweza kuteuliwa kwa nafasi yoyote huko Zanzibar, hivi huko hakuna serikali ya Tanzania?

Hili jambo ni lazima lishughulikiwe.
 
Katika mataifa ya Jumuiya ya Madola, kansela kawaida huwa mkuu wa chuo kikuu ambaye si mkazi, ni wa sherehe (ceremonial). Katika taasisi kama hizo, mtendaji mkuu wa chuo kikuu ni makamu wa chansela , ambaye anaweza kubeba cheo cha ziada kama vile rais (km "rais & makamu-chansela").
Ni kweli unayosema, lakini pia nakubaliana na The Shah of Tanganyika kwamba ingawa si Wakazi, tunahitaji watu wenye maono au uzoefu na ushawishi. Kwa mfano Chuo cha MUST ni cha Teknolojia kingepata mtu wa ain hiyo.
Akina Amani ni wanasiasa wangepelekwa Mzumbe n.k.

Hivi kwanini Tanzania haiwatumii Wastaafu kutoa mihadhara Vyuo Vikuu?
Duniani Wastaafu na CEOs wa Mashirika na Makampuni ni sehemu ya '' Lecturer' wanaokwenda University kubadilishana uzoefu wao katika kazi. Watu kama Marais Wastaafu, Mawaziri wakuu , wakuu wa majeshi watu mashuhuri kama akina Msekwa wanaojua habari za Katiba, akina Warioba, Prof Assad , Dau n.k.

Ngongo hoja yako ina mantiki sana, mbegu waliyopanda Wazanzibar inachanua. Ni kweli kuna Mtanganyika anaweza kuteuliwa chuo kikuu Zanzibar bila kusikia mikelele ya hili si jambo la muungano, tunaonewa, wanaletwa Watanganyika na upuuzi wa aina hiyo. Halafu Wazanzibar wanalalmika Elimu ya juu imeongezwa kinyemela, wakiteuliwa hawakatai. Namsubiri OMO aachame maana... , always whining!
 
Back
Top Bottom