Utetezi wa Sabaya: Ametanua uwanja, ana mengi ya kuyathibitisha. Porojo hazitatosha kumnasua!

Nawe ni takataka, hujui wapi unapotakiwa kutuma doctriine ya who alleges must prove. Kasome tena
Ha ha ha ha ha ha , tutusa lingine hili hapa, tena linajifanyanga limesoma sheria he he he.
He who alleges kwenye criminal law? hujui kama hii ni princinple ipo kwenye Civil Procedure Code(CPC).

he he he he ha ha ha ha ha, daa! Hivi wewe na Mselwa mmesoma sheria ya wapi?
Principle kwenye criminology ni Moja we kibabu, the prosecution must prove the charges against the accused beyond reasonable doubt, weakeness in the defence evidences however grave can not be rellied upon to find conviction against the accused. The only duty of the accused( Sabaya) is to raise reasonable doubt in the prosecution evidences, (ndicho anachofanya Sabaya we kibabu) save, in few circumstances ambapo burden of proof inaweza shift from prosecution to the accused e.g. accused aki raise defence of alibi, au intoxication.
Wakati Sabaya ana plea Ali raise any defence ambayo ina hamisha burden of proof.
Jamhuri ndio wanatakiwa kuthibitisha kuwa Sabaya wakati anafanya hizo oparation hakuwa amepokea maagizo yoyote, siyo kazi ya Sabaya kithibitisha we Kibabu.
 
Nahisi Sabaya Kaingia Mkenge

Huends, huenda…huenda Mawakili wake wanatoka DSTV bila ya mwenyewe kujua, hivyo kawapa full picture ili wamsaidie kujinasua na wao sasa wanamuingiza kwny Mkenge bila ya kujijua tena
Sabaya ameshajimaliza, kitendo chake cha kukiri kuwepo eneo la tukio hata kama anadai alitumwa na mamlaka husika kujinasua kwake itakuwa vigumu, je, alifuata sheria kuingia eneo la mwingine? alikuwa na kibali? kama hakuwa nacho hakuwa na tofauti na jambazi alietumia silaha kufanya uvamizi, hapa Sabaya ameshakiri kosa.
 
Operation ya uhujumu uchumi inafanywaje ili tujue aliwezaje kushiriki operation bila ya kukiuka sheria?
Hivi we mwanasheria njaa unajua kuanalyze facts? Amekiri kuhusika na operation dhidi ya ujujumu uchumi ndio maana anadai alitumwa kwa kazi maalumu, hajakiri kushiriki ujambazi.

Kama mwanasheria ebu tupe ingredients za armed robbery alafu oanisha na tukio la Sabaya. Acha ushabiki
 
Nahisi Sabaya Kaingia Mkenge

Huends, huenda…huenda Mawakili wake wanatoka DSTV bila ya mwenyewe kujua, hivyo kawapa full picture ili wamsaidie kujinasua na wao sasa wanamuingiza kwny Mkenge bila ya kujijua tena
Hakuna mkenge Wala nini shida ya watu humu hamjui sheria na hamjui kwanini kaja na hiyo hoja.
Kwanza Sabaya hajakiri kutenda kosa, mtu anaweza kukiri tu au kutokiri kosa siku anaposomewa. Kwahiyo siku Sabaya anasomewa alikataa kutenda kosa.
Kuna hoja ambayo ukiingalia imemkalia vibaya Sabaya, kwamba, ilikuwaje yeye ni mkuu wa Wilaya ya Hai akaenda kufanya oparation Wilaya ya Arusha. Sasa ili kui shake hiyo hoja ndiyo maana kasema alikuwa na maelekezo kutoka kwa wakubwa, na Arusha haikuwa Mara ya kwanza, amewahi kufanya hata DSM. Sasa kama hizo oparation zilikuwa halali, hata kama alimuumiza mtu haiwezi au kumpiga mtu bado haiwezi kumfanya awe guilty kwa kosa la ujambazi wa kutumia Silaha, kwani kosa Hilo lina viini vyake ambavyo vinapaswa kuthibitishwa.
Hakuna kesi nyepesi duniani kwa mshtakiwa kama kesi za jinai!
 
Hivi we mwanasheria njaa unajua kuanalyze facts? Amekiri kuhusika na operation dhidi ya ujujumu uchumi ndio maana anadai alitumwa kwa kazi maalumu, hajakiri kushiriki ujambazi.

Kama mwanasheria ebu tupe ingredients za armed robbery alafu oanisha na tukio la Sabaya. Acha ushabiki
CCTV inaonyesha wanakusanywa wanapigwa!
 
Ninachojua Mimi Sabaya siyo mpumbavu kiasi hicho. Kakiri Hadharani yeye Hadi Sasa ni mtumishi wa Uma. Kwa sasa siyo mkuu wa wilaya hivyo ukuu wa wilaya ilikuwa ni Ziada tu katika kutimiza majukumu yake..

Ana kiapo hivyo hawezi kusema Mimi ni TISS rejea kesi yake ya mwanzo ya kufoji cheti Cha usalama wa Taifa. Ametaja tu watu watatu waliojua operation yake. Nadhani hapaswi Tena kuleta uthibitisho. Ofisi ya Rais imetajwa, Ofisi ya waziri wa Fedha ipo, ofisi ya Gavana wa B.O.T ipo ni wajibu wao wakane kama hawakujua au hawakumtuma.. wakimkana Sasa ndo yeye Ataleta ushahidi..
 
Ha ha ha ha ha ha , tutusa lingine hili hapa, tena linajifanyanga limesoma sheria he he he.
He who alleges kwenye criminal law? hujui kama hii ni princinple ipo kwenye Civil Procedure Code(CPC).

he he he he ha ha ha ha ha, daa! Hivi wewe na Mselwa mmesoma sheria ya wapi?
Principle kwenye criminology ni Moja we kibabu, the prosecution must prove the charges against the accused beyond reasonable doubt, weakeness in the defence evidences however grave can not be rellied upon to find conviction against the accused. The only duty of the accused( Sabaya) is to raise reasonable doubt in the prosecution evidences, (ndicho anachofanya Sabaya we kibabu) save, in few circumstances ambapo burden of proof inaweza shift from prosecution to the accused e.g. accused aki raise defence of alibi, au intoxication.
Wakati Sabaya ana plea Ali raise any defence ambayo ina hamisha burden of proof.
Jamhuri ndio wanatakiwa kuthibitisha kuwa Sabaya wakati anafanya hizo oparation hakuwa amepokea maagizo yoyote, siyo kazi ya Sabaya kithibitisha we Kibabu.
He who alleges must proof is not only a civil law principle, but rather evidence principle applicable to both civil and criminal cases. The difference is the burden of proof. In civil cases the burden is on balance of probabilities and in criminal is beyond reasonable doubt as you have properly stated.
By the way mambo hayo yanetajwa zaidi na Evidence Act. Do you know any section or Order/rule of CPC about "he who alleges/ burden of proof?
 
Kwa hiyo kujua kwako sheria kumefanya ujue kuwa wengine hawajui sheria?

Kajiingiza kwny Mkenge kwa circumstancial evidence ya kukiri kuwepo eneo la tukio, kukiri kushiriki kwny operation, kukiri kumfanyia hiyo 'operation' muathirika

Unaambiwa Mahakamani kila neno unaloongea kujitetea usipokuwa Makini inaweza kuwa ushahidi mzito zaid kuliko wa anaelalamika

Kama Rais alimuamuru akafanye Operation uhujumu uchumi unazijua kanuni na taratibu za operation hizo, alizifuata zote kwa mujibu wa sheria na taratibu?

Akiambiwa ataje hayo maeneo mengine aliyowahi kufanya hizo operation uhujumu uchumi ili ionekane alitenda inavyomstahiki huoni anazidi kuwarahisishia kazi Watoa hukumu?
Hakuna mkenge Wala nini shida ya watu humu hamjui sheria na hamjui kwanini kaja na hiyo hoja.
Kwanza Sabaya hajakiri kutenda kosa, mtu anaweza kukiri tu au kutokiri kosa siku anaposomewa. Kwahiyo siku Sabaya anasomewa alikataa kutenda kosa.
Kuna hoja ambayo ukiingalia imemkalia vibaya Sabaya, kwamba, ilikuwaje yeye ni mkuu wa Wilaya ya Hai akaenda kufanya oparation Wilaya ya Arusha. Sasa ili kui shake hiyo hoja ndiyo maana kasema alikuwa na maelekezo kutoka kwa wakubwa, na Arusha haikuwa Mara ya kwanza, amewahi kufanya hata DSM. Sasa kama hizo oparation zilikuwa halali, hata kama alimuumiza mtu haiwezi au kumpiga mtu bado haiwezi kumfanya awe guilty kwa kosa la ujambazi wa kutumia Silaha, kwani kosa Hilo lina viini vyake ambavyo vinapaswa kuthibitishwa.
Hakuna kesi nyepesi duniani kwa mshtakiwa kama kesi za jinai!
 
Mahakamani kunahitajika ushahidi wa kuthibitisha unachokisema. Unaweza kuwa wa nyaraka, maneno au vyote. Ushahidi mzuri ni wa wengine wanaokuja kuushadidia ushahidi wako. Kunapokosekana ushahidi, maneno yanabaki porojo isiyo na maana yoyote.
Bahati nzuri Mama SAMIA alikuwa part ya ile Mamlaka ya Uteuzi allegedly iliyomtuma Sabaya. Kwa kuwa yupo hai todate, Wakili wa Utetezi aiombe Mahakama ikubali mama aburuzwe mahakamani kama Shahidi #1 wa Sabaya. Na pia akaithibitishie Mahakama nafasi gani Serikaloi Sabaya bado anayo (kumbuka, huyu hajafukuzwa kazi bali alisimamishwa tu)
 
Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ameanza kujitetea kwenye kesi yake ya jinai yenye sura ya uporaji, kujeruhi na kutesa.

Soma hapa >> Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wake, kadiri nilivyomsikiliza, naugawa kwenye sehemu zifuatazo.

Mosi, yapo aliyoyakiri. Amekiri kufika sehemu ya tukio kwa kutaja jina hilohilo na mahali palepale. Na akamtaja mmiliki huyohuyo ambaye ametajwa kwenye mashtaka na ushahidi. Hapa, ana kazi ya kukanusha kiushahidi kutofanya yote anayoshtakiwa nayo.

Pili, amesema kuwa alifanya aliyoyafanya akitekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Ameeleza kuwa alikuwa sehemu ya tukio kutekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Hapa, Sabaya atapaswa kuwasilisha maagizo hayo ili kuona kuwa hakuvuka mipaka. Maagizo husika lazima yawasilishwe mahakamani ili aaminike. Nyaraka au sauti ni muhimu hapa.

Tatu, amejipambanua mahakamani kuwa yeye alikuwa zaidi ya Mkuu wa Wilaya. Kuwa yeye alikuwa akiongoza au kushiriki operesheni mbalimbali zilizokuwa zikiagizwa na mamlaka yake ya uteuzi. Hapa ndipo alipowataja Makamu wa Rais na Gavana wa Benki Kuu kama watu waliofahamu operesheni mojawapo iliyofanyika Dar es Salaam.

Kimsingi, hapo Sabaya anapaswa kuwasilisha ushahidi wa hilo kwa maana ya uteuzi wenye hadidu rejea za operesheni hizo pamoja na kuwapata aliowataja kama mashahidi wake. Waliotajwa wanapaswa kuja kukiri kufahamu operesheni hiyo ya Dar ambayo hatahivyo haisaidii wala haina uhusiano wowote na kesi husika huko Arusha.

Nne, Sabaya amedai kuwa yeye bado ni mtumishi wa serikali. Hakusema ni kwa nafasi ipi na ana majukumu gani. Hilo nalo anapaswa aliweke sawa kwa ushahidi.

Kiujumla, utetezi wa Sabaya umetanua sana uwanja na kumuweka kwenye kazi ngumu sana kuchomoka kwenye kesi yake. Ameanzisha mambo mengi yanayohitaji ushahidi. Na ushahidi mwingine wa maneno hautapatikana kwakuwa yeye mwenyewe amekataa kuwataja alioambatana nao kwenda sehemu ya tukio siku husika. Pia, mamlaka yake ya uteuzi haipo tena.

Mahakamani kunahitajika ushahidi wa kuthibitisha unachokisema. Unaweza kuwa wa nyaraka, maneno au vyote. Ushahidi mzuri ni wa wengine wanaokuja kuushadidia ushahidi wako. Kunapokosekana ushahidi, maneno yanabaki porojo isiyo na maana yoyote.
 
Hivi we mwanasheria njaa unajua kuanalyze facts? Amekiri kuhusika na operation dhidi ya ujujumu uchumi ndio maana anadai alitumwa kwa kazi maalumu, hajakiri kushiriki ujambazi.

Kama mwanasheria ebu tupe ingredients za armed robbery alafu oanisha na tukio la Sabaya. Acha ushabiki
Asije kusema actus reus na mens rea tu, ingredient zipo nyingi sana almost 12 ila kwa Sabaya uwezo wakumkuta na hatia upo pia itategemea prosecution side wamejipanga vipi.

Ila mbona mwamba hapo kaeleza vizuri tu kadiri ya uwezo wake Mkuu, punguza makasiriko kidogo boss
 
Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ameanza kujitetea kwenye kesi yake ya jinai yenye sura ya uporaji, kujeruhi na kutesa.

Soma hapa >> Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wake, kadiri nilivyomsikiliza, naugawa kwenye sehemu zifuatazo.

Mosi, yapo aliyoyakiri. Amekiri kufika sehemu ya tukio kwa kutaja jina hilohilo na mahali palepale. Na akamtaja mmiliki huyohuyo ambaye ametajwa kwenye mashtaka na ushahidi. Hapa, ana kazi ya kukanusha kiushahidi kutofanya yote anayoshtakiwa nayo.

Pili, amesema kuwa alifanya aliyoyafanya akitekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Ameeleza kuwa alikuwa sehemu ya tukio kutekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Hapa, Sabaya atapaswa kuwasilisha maagizo hayo ili kuona kuwa hakuvuka mipaka. Maagizo husika lazima yawasilishwe mahakamani ili aaminike. Nyaraka au sauti ni muhimu hapa.

Tatu, amejipambanua mahakamani kuwa yeye alikuwa zaidi ya Mkuu wa Wilaya. Kuwa yeye alikuwa akiongoza au kushiriki operesheni mbalimbali zilizokuwa zikiagizwa na mamlaka yake ya uteuzi. Hapa ndipo alipowataja Makamu wa Rais na Gavana wa Benki Kuu kama watu waliofahamu operesheni mojawapo iliyofanyika Dar es Salaam.

Kimsingi, hapo Sabaya anapaswa kuwasilisha ushahidi wa hilo kwa maana ya uteuzi wenye hadidu rejea za operesheni hizo pamoja na kuwapata aliowataja kama mashahidi wake. Waliotajwa wanapaswa kuja kukiri kufahamu operesheni hiyo ya Dar ambayo hatahivyo haisaidii wala haina uhusiano wowote na kesi husika huko Arusha.

Nne, Sabaya amedai kuwa yeye bado ni mtumishi wa serikali. Hakusema ni kwa nafasi ipi na ana majukumu gani. Hilo nalo anapaswa aliweke sawa kwa ushahidi.

Kiujumla, utetezi wa Sabaya umetanua sana uwanja na kumuweka kwenye kazi ngumu sana kuchomoka kwenye kesi yake. Ameanzisha mambo mengi yanayohitaji ushahidi. Na ushahidi mwingine wa maneno hautapatikana kwakuwa yeye mwenyewe amekataa kuwataja alioambatana nao kwenda sehemu ya tukio siku husika. Pia, mamlaka yake ya uteuzi haipo tena.

Mahakamani kunahitajika ushahidi wa kuthibitisha unachokisema. Unaweza kuwa wa nyaraka, maneno au vyote. Ushahidi mzuri ni wa wengine wanaokuja kuushadidia ushahidi wako. Kunapokosekana ushahidi, maneno yanabaki porojo isiyo na maana yoyote.
Kwa kweli amesaidia kupaaza sauti upatikanaji wa katiba mpya. Kilio Cha watanzania ni matumizi mabaya ya vyeo na madaraka waliopewa.

Asante sabaya kwa kupaaza sauti. CCM wanaanza kuchomoka mmoja mmoja kwenye utawala wao kijanja janja.
 
Hata Mimi amenishangaza aise huyu jamaa hadi najiuliza hapo UDSM anafanya nini. Anasema eti Sabaya katanua wigo wa kithibitisha, Sabaya ana Cha kuthibitisha kwenye hii kesi kweli?
Ha ha haha hatari sana.
Kweli mtu akizaa mtoto mjinga kama wewe ni hasara sana, kwa hiyo kwa ujinga wako ukitaja tu ulitumwa na Rais, basi kesi imeisha!!!! ?😁😁

Profesa Mahalu alipomtaja Rais Mkapa kuwa alimtuma, Mkapa aliitwa mahakamani na akatoa ushahidi. Kama Magufuli amekufa, huyo Mpango yupo na atatakiwa atoe ushahidi.
Na anavyosema alipewa maagizo, kwa kutumia njia gani? Kwa simu, emails au? Vyote vinaweza patikana. Kwa ujinga wa Sabaya na ambao unao wewe unaona kwamba rais ni Mungu, ukishamtaja kila kitu kimeisha!
 
Magufuli na makamu wanatakiwa kuthibitisha
Mpango hajashtakiwa. Kwanini tunakuwa wadhaifu kwenyw kuconsume taarifa kiasi hiki? Mpango kufahamu juu ya haimaanishi kushtakiwa. Na operation haimaanishi kufanya ujambazi au kuua ai hata kupiga. Lakini Sabaya amehalalisha uwepo wa operation aliohusika jijini Arusha. Ametoa na mfano wa operation aliofanya Temeke
 
Tumia akili kudigest info, Sabaya hajakiri kupiga au kufanya unyang'anyi wa siraha. Amekiri kuwepo Arusha kwa operation maalumu kudeal na wahujumu uchumi. Na anadai alitulwa na hayati JPM huku waziri wa fedha akiwa anafahamu. Sasa kwa nini Mpango asitoe ushahidi.
 
Back
Top Bottom