Utetezi wa Sabaya: Ametanua uwanja, ana mengi ya kuyathibitisha. Porojo hazitatosha kumnasua!

Hivi we mwanasheria njaa unajua kuanalyze facts? Amekiri kuhusika na operation dhidi ya ujujumu uchumi ndio maana anadai alitumwa kwa kazi maalumu, hajakiri kushiriki ujambazi.

Kama mwanasheria ebu tupe ingredients za armed robbery alafu oanisha na tukio la Sabaya. Acha ushabiki
Mataga Pori huamini unachokiona kwa macho yako hadi unataka kubishana na radio 🤣 🤣 🤣
 
Hivi we mwanasheria njaa unajua kuanalyze facts? Amekiri kuhusika na operation dhidi ya ujujumu uchumi ndio maana anadai alitumwa kwa kazi maalumu, hajakiri kushiriki ujambazi.

Kama mwanasheria ebu tupe ingredients za armed robbery alafu oanisha na tukio la Sabaya. Acha ushabiki
Kazi aliyokuwa nayo ni kuainisha majukumu yake yalikua yapi kwenye operation na je hakuvuka mipaka katika kuyatekeleza.
Athibitishe uteuzi wake kwenye hiyo operation
 
Hivi we mwanasheria njaa unajua kuanalyze facts? Amekiri kuhusika na operation dhidi ya ujujumu uchumi ndio maana anadai alitumwa kwa kazi maalumu, hajakiri kushiriki ujambazi.

Kama mwanasheria ebu tupe ingredients za armed robbery alafu oanisha na tukio la Sabaya. Acha ushabiki
Hata Mimi amenishangaza aise huyu jamaa hadi najiuliza hapo UDSM anafanya nini. Anasema eti Sabaya katanua wigo wa kithibitisha, Sabaya ana Cha kuthibitisha kwenye hii kesi kweli?
Ha ha haha hatari sana.
 
Ndio ni mtumishi wa serikali kwa sababu bado hajafukuzwa na ... najua inauma kwa wale walidai kagushi
 
Sio mjinga Sabaya kuongea vile mahakamani, Hakuna muda yupo bize kutoingia mtegoni kama sasa.
Itachukua muda ila atatoka tu.
 
We jamaa hapo UDSM sijui ulibakije aise.
Sabaya hahitaji kuthihitisha chochote aise kwenye hii kesi. Anachotakiwa kukifanya kwa ushahidi huo anakifanya kwa usahihi mkubwa mno. Umenishangaza aise.
hoja za sabaya hazina ushahidi, inabidi alete ushahidi kuthibitusha utetezi wake
 
adhibitishe kama hajafanya uhalifu akiwa eneo la tukio
adhibitishe kama ilikua ni halali yeye kuwepo pale.
adhibitishe kama aliingia pale kihalali.
Ha ha ha majibu yako wewe hayanishangazi kwa sababu kwenye sheria wewe ni mpumbavu, nataka bwana Mselewa ambaye ni mwanasheria ajibu swali langu.
By the way under which principle of crimimology Sabaya anatakiwa kuthibitisha hayo unayoyasema kwenye hii kesi?
 
Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ameanza kujitetea kwenye kesi yake ya jinai yenye sura ya uporaji, kujeruhi na kutesa.

Soma hapa >> Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wake, kadiri nilivyomsikiliza, naugawa kwenye sehemu zifuatazo.

Mosi, yapo aliyoyakiri. Amekiri kufika sehemu ya tukio kwa kutaja jina hilohilo na mahali palepale. Na akamtaja mmiliki huyohuyo ambaye ametajwa kwenye mashtaka na ushahidi. Hapa, ana kazi ya kukanusha kiushahidi kutofanya yote anayoshtakiwa nayo.

Pili, amesema kuwa alifanya aliyoyafanya akitekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Ameeleza kuwa alikuwa sehemu ya tukio kutekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Hapa, Sabaya atapaswa kuwasilisha maagizo hayo ili kuona kuwa hakuvuka mipaka. Maagizo husika lazima yawasilishwe mahakamani ili aaminike. Nyaraka au sauti ni muhimu hapa.

Tatu, amejipambanua mahakamani kuwa yeye alikuwa zaidi ya Mkuu wa Wilaya. Kuwa yeye alikuwa akiongoza au kushiriki operesheni mbalimbali zilizokuwa zikiagizwa na mamlaka yake ya uteuzi. Hapa ndipo alipowataja Makamu wa Rais na Gavana wa Benki Kuu kama watu waliofahamu operesheni mojawapo iliyofanyika Dar es Salaam.

Kimsingi, hapo Sabaya anapaswa kuwasilisha ushahidi wa hilo kwa maana ya uteuzi wenye hadidu rejea za operesheni hizo pamoja na kuwapata aliowataja kama mashahidi wake. Waliotajwa wanapaswa kuja kukiri kufahamu operesheni hiyo ya Dar ambayo hatahivyo haisaidii wala haina uhusiano wowote na kesi husika huko Arusha.

Nne, Sabaya amedai kuwa yeye bado ni mtumishi wa serikali. Hakusema ni kwa nafasi ipi na ana majukumu gani. Hilo nalo anapaswa aliweke sawa kwa ushahidi.

Kiujumla, utetezi wa Sabaya umetanua sana uwanja na kumuweka kwenye kazi ngumu sana kuchomoka kwenye kesi yake. Ameanzisha mambo mengi yanayohitaji ushahidi. Na ushahidi mwingine wa maneno hautapatikana kwakuwa yeye mwenyewe amekataa kuwataja alioambatana nao kwenda sehemu ya tukio siku husika. Pia, mamlaka yake ya uteuzi haipo tena.

Mahakamani kunahitajika ushahidi wa kuthibitisha unachokisema. Unaweza kuwa wa nyaraka, maneno au vyote. Ushahidi mzuri ni wa wengine wanaokuja kuushadidia ushahidi wako. Kunapokosekana ushahidi, maneno yanabaki porojo isiyo na maana yoyote.
Sabaya kusema alitumwa maana yake alifanya,Yani kakiri makosa. Then sheria inachukua mkondo wake, tusubiri tu akaolewe na nyapara hakuna namna amerahisisha kazi
 
Hii kesi imefika patamu. Tungeyajulia wapi haya kama baba mzazi angekuwapo?

Hiiiiii bagosha!
 
Ile ambayo alizembea akaonekana badala ya kutokuonekana wajuba wakamwaga ila Magu akamwokota jalalani na kumpa uDC na hiyo ndio iliyokiwa inamfanya aende nje ya dola yake kudili na walioitwa wajumu uchumi kama ambavyo yeye kasema ameshaenda Arusha, Dar kwa operation maalum
angekua ni Tiss kungekua hakuna haja yeye kusema kwamba alishawahi kufanya ujambazi mwingine kwa kushirikiana na Magufuli na Mpango huko Dar na Mwanza,
angekua ni Tiss angesema alifanya kazi hiyo kama mtumishi wa Idara maalum chini ya Rais.

Inshort huyu anatafuta justification ya yeye kufanya kazi nje ya kituo chake cha kazi na tayari ameipaka mavi ofisi ya rais kuwa ilimtuma kwenda kufanya ujambazi.
 
Back
Top Bottom