Utetezi wa Sabaya: Ametanua uwanja, ana mengi ya kuyathibitisha. Porojo hazitatosha kumnasua!

mweusi asili

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
1,355
2,000
Madai ya Sabaya naweza kuyafananisha na tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu. Hivi wale waliompiga risasi TL wakifahamika na kufikishwa mahakamani, je wakijitetea kuwa walipata maagizo kutoka juu utetezi huo utawasaidia? Hapana hauwezi kuwasaidia.
Hawa maRC na maDC asilimia kubwa ni majambazi tu
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
14,116
2,000
... ghafla urais umekoma kuwa taasisi kufuatia sakata la Sabaya? Wakuu wengine wote wa wilaya na wateule wengine wa toka enzi za awamu iliyopita nao mamlaka zao za uteuzi hazipo tena au ni kwa Sabaya tu? Sijaelewa!
Kwenye ushahidi mahakamani anakuja aliyetoa amri. Kama ilitoa taasisi ije taasisi kama alitoa mtu aje huyo mtu. Taasisi inatoa amri kwa maandishi tofauti na mtu anayeweza kutoa amri kwa maneno au ishara. Mleta mada kasema anamsubiri Sabaya alete ushahidi wa huyo "Mamlaka ya Uteuzi".
 
Ibumalo

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
337
500
Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ameanza kujitetea kwenye kesi yake ya jinai yenye sura ya uporaji, kujeruhi na kutesa.

Soma hapa >> Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wake, kadiri nilivyomsikiliza, naugawa kwenye sehemu zifuatazo.

Mosi, yapo aliyoyakiri. Amekiri kufika sehemu ya tukio kwa kutaja jina hilohilo na mahali palepale. Na akamtaja mmiliki huyohuyo ambaye ametajwa kwenye mashtaka na ushahidi. Hapa, ana kazi ya kukanusha kiushahidi kutofanya yote anayoshtakiwa nayo.

Pili, amesema kuwa alifanya aliyoyafanya akitekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Ameeleza kuwa alikuwa sehemu ya tukio kutekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Hapa, Sabaya atapaswa kuwasilisha maagizo hayo ili kuona kuwa hakuvuka mipaka. Maagizo husika lazima yawasilishwe mahakamani ili aaminike. Nyaraka au sauti ni muhimu hapa.

Tatu, amejipambanua mahakamani kuwa yeye alikuwa zaidi ya Mkuu wa Wilaya. Kuwa yeye alikuwa akiongoza au kushiriki operesheni mbalimbali zilizokuwa zikiagizwa na mamlaka yake ya uteuzi. Hapa ndipo alipowataja Makamu wa Rais na Gavana wa Benki Kuu kama watu waliofahamu operesheni mojawapo iliyofanyika Dar es Salaam.

Kimsingi, hapo Sabaya anapaswa kuwasilisha ushahidi wa hilo kwa maana ya uteuzi wenye hadidu rejea za operesheni hizo pamoja na kuwapata aliowataja kama mashahidi wake. Waliotajwa wanapaswa kuja kukiri kufahamu operesheni hiyo ya Dar ambayo hatahivyo haisaidii wala haina uhusiano wowote na kesi husika huko Arusha.

Nne, Sabaya amedai kuwa yeye bado ni mtumishi wa serikali. Hakusema ni kwa nafasi ipi na ana majukumu gani. Hilo nalo anapaswa aliweke sawa kwa ushahidi.

Kiujumla, utetezi wa Sabaya umetanua sana uwanja na kumuweka kwenye kazi ngumu sana kuchomoka kwenye kesi yake. Ameanzisha mambo mengi yanayohitaji ushahidi. Na ushahidi mwingine wa maneno hautapatikana kwakuwa yeye mwenyewe amekataa kuwataja alioambatana nao kwenda sehemu ya tukio siku husika. Pia, mamlaka yake ya uteuzi haipo tena.

Mahakamani kunahitajika ushahidi wa kuthibitisha unachokisema. Unaweza kuwa wa nyaraka, maneno au vyote. Ushahidi mzuri ni wa wengine wanaokuja kuushadidia ushahidi wako. Kunapokosekana ushahidi, maneno yanabaki porojo isiyo na maana yoyote.

Kwa hilo yupo sahihi kwani tulitangaziwa kuwa Rais amemsimamisha kazi (suspend) ili kupisha uchungzi. Hadi sasa hatujaambiwa vinginevyo. Mtu akipata suspension anatambulika bado mtumishi na kupata nusu mshahara.
 
Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,522
2,000
Wewe ndiyo huna akili, Sabaya hawezi kutumia defence ya Magufuli bila ushahidi wa maandishi. Mpango kujuwa uwapo wa operesheni siyo ruksa kwa Sabaya kufanya jinai. Amekiri kuwapo kwenye duka lililotajwa na amekiri kumkuta mtu anayedaiwa kupigwa na kunyang'anywa fedha.

HACHOMOKI
Kama kutochomoka alitakiwa ashitakiwe kwa kosa la maumizi mabaya ya ofisi, sio unyanga'nyi wa kutumia siraha.

Amekiri kuwepo kwenye duka lilitotajwa kufanya operation maalumu ya uhujumu uchumi, hajakiri kufanya ujambazi.

Acha kuleta mahaba yako.
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
5,379

Kwani kuna jambazi huwa anakubali kuwa alinyang'anya? Ni ushahidi kutoka prosecution side ndiyo unaothibitisha unyang'anyi. Yeye kukiri kuwapo pale kunajenga mazingira ya kuthibitisha.

Hakimu ataunganisha maelezo yake kisha atachanganya na ya prosecution na hatimaye atatoa uamuzi
 
Acha kulazimisha mambo. Kwenda kufanya kazi maalumu ndio ujambazi?
 
Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,522
2,000
Kwani kuna jambazi huwa anakubali kuwa alinyang'anya? Ni ushahidi kutoka prosecution side ndiyo unaothibitisha unyang'anyi. Yeye kukiri kuwapo pale kunajenga mazingira ya kuthibitisha.

Hakimu ataunganisha maelezo yake kisha atachanganya na ya prosecution na hatimaye atatoa uamuzi
 
core22

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
867
1,000
Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ameanza kujitetea kwenye kesi yake ya jinai yenye sura ya uporaji, kujeruhi na kutesa.

Soma hapa >> Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wake, kadiri nilivyomsikiliza, naugawa kwenye sehemu zifuatazo.

Mosi, yapo aliyoyakiri. Amekiri kufika sehemu ya tukio kwa kutaja jina hilohilo na mahali palepale. Na akamtaja mmiliki huyohuyo ambaye ametajwa kwenye mashtaka na ushahidi. Hapa, ana kazi ya kukanusha kiushahidi kutofanya yote anayoshtakiwa nayo.

Pili, amesema kuwa alifanya aliyoyafanya akitekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Ameeleza kuwa alikuwa sehemu ya tukio kutekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Hapa, Sabaya atapaswa kuwasilisha maagizo hayo ili kuona kuwa hakuvuka mipaka. Maagizo husika lazima yawasilishwe mahakamani ili aaminike. Nyaraka au sauti ni muhimu hapa.

Tatu, amejipambanua mahakamani kuwa yeye alikuwa zaidi ya Mkuu wa Wilaya. Kuwa yeye alikuwa akiongoza au kushiriki operesheni mbalimbali zilizokuwa zikiagizwa na mamlaka yake ya uteuzi. Hapa ndipo alipowataja Makamu wa Rais na Gavana wa Benki Kuu kama watu waliofahamu operesheni mojawapo iliyofanyika Dar es Salaam.

Kimsingi, hapo Sabaya anapaswa kuwasilisha ushahidi wa hilo kwa maana ya uteuzi wenye hadidu rejea za operesheni hizo pamoja na kuwapata aliowataja kama mashahidi wake. Waliotajwa wanapaswa kuja kukiri kufahamu operesheni hiyo ya Dar ambayo hatahivyo haisaidii wala haina uhusiano wowote na kesi husika huko Arusha.

Nne, Sabaya amedai kuwa yeye bado ni mtumishi wa serikali. Hakusema ni kwa nafasi ipi na ana majukumu gani. Hilo nalo anapaswa aliweke sawa kwa ushahidi.

Kiujumla, utetezi wa Sabaya umetanua sana uwanja na kumuweka kwenye kazi ngumu sana kuchomoka kwenye kesi yake. Ameanzisha mambo mengi yanayohitaji ushahidi. Na ushahidi mwingine wa maneno hautapatikana kwakuwa yeye mwenyewe amekataa kuwataja alioambatana nao kwenda sehemu ya tukio siku husika. Pia, mamlaka yake ya uteuzi haipo tena.

Mahakamani kunahitajika ushahidi wa kuthibitisha unachokisema. Unaweza kuwa wa nyaraka, maneno au vyote. Ushahidi mzuri ni wa wengine wanaokuja kuushadidia ushahidi wako. Kunapokosekana ushahidi, maneno yanabaki porojo isiyo na maana yoyote.
safi sana
 
mkaruka ataja rinu

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,553

Wewe huna tofauti na Rais Samia kwenye kesi ya Mbowe maana umeshamtia hatiani Sabaya kabla ya maamuzi ya Mahakama. Kumbe mamlaka ya uteuzi wa Sabaya ilikoma baada ya Magufuli kufa? Kwa maana hiyo wale wote walioteuliwa na Magufuli hawana uhalali wa kuendelea na nyadhifa zao? Umeandika ki-BAVICHA mno
 
Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
9,756
2,000
Wewe huna tofauti na Rais Samia kwenye kesi ya Mbowe maana umeshamtia hatiani Sabaya kabla ya maamuzi ya Mahakama. Kumbe mamlaka ya uteuzi wa Sabaya ilikoma baada ya Magufuli kufa? Kwa maana hiyo wale wote walioteuliwa na Magufuli hawana uhalali wa kuendelea na nyadhifa zao? Umeandika ki-BAVICHA mno
Sawa, kunywa chai sasa
 
kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
4,008
2,000
Yes offcourse, lazima athibitishe ayo (solid evidence needed)
Kama alipigiwa simu basi(rycle bin ipo tarifa zitapatikana mtandao husika uliotumiwa au simu ya mezani

Kazi ipo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom