Utetezi wa Sabaya: Ametanua uwanja, ana mengi ya kuyathibitisha. Porojo hazitatosha kumnasua!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,176
25,446
Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, ameanza kujitetea kwenye kesi yake ya jinai yenye sura ya uporaji, kujeruhi na kutesa.

Soma hapa >> Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wake, kadiri nilivyomsikiliza, naugawa kwenye sehemu zifuatazo.

Mosi, yapo aliyoyakiri. Amekiri kufika sehemu ya tukio kwa kutaja jina hilohilo na mahali palepale. Na akamtaja mmiliki huyohuyo ambaye ametajwa kwenye mashtaka na ushahidi. Hapa, ana kazi ya kukanusha kiushahidi kutofanya yote anayoshtakiwa nayo.

Pili, amesema kuwa alifanya aliyoyafanya akitekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Ameeleza kuwa alikuwa sehemu ya tukio kutekeleza maagizo ya mamlaka ya uteuzi. Hapa, Sabaya atapaswa kuwasilisha maagizo hayo ili kuona kuwa hakuvuka mipaka. Maagizo husika lazima yawasilishwe mahakamani ili aaminike. Nyaraka au sauti ni muhimu hapa.

Tatu, amejipambanua mahakamani kuwa yeye alikuwa zaidi ya Mkuu wa Wilaya. Kuwa yeye alikuwa akiongoza au kushiriki operesheni mbalimbali zilizokuwa zikiagizwa na mamlaka yake ya uteuzi. Hapa ndipo alipowataja Makamu wa Rais na Gavana wa Benki Kuu kama watu waliofahamu operesheni mojawapo iliyofanyika Dar es Salaam.

Kimsingi, hapo Sabaya anapaswa kuwasilisha ushahidi wa hilo kwa maana ya uteuzi wenye hadidu rejea za operesheni hizo pamoja na kuwapata aliowataja kama mashahidi wake. Waliotajwa wanapaswa kuja kukiri kufahamu operesheni hiyo ya Dar ambayo hatahivyo haisaidii wala haina uhusiano wowote na kesi husika huko Arusha.

Nne, Sabaya amedai kuwa yeye bado ni mtumishi wa serikali. Hakusema ni kwa nafasi ipi na ana majukumu gani. Hilo nalo anapaswa aliweke sawa kwa ushahidi.

Kiujumla, utetezi wa Sabaya umetanua sana uwanja na kumuweka kwenye kazi ngumu sana kuchomoka kwenye kesi yake. Ameanzisha mambo mengi yanayohitaji ushahidi. Na ushahidi mwingine wa maneno hautapatikana kwakuwa yeye mwenyewe amekataa kuwataja alioambatana nao kwenda sehemu ya tukio siku husika. Pia, mamlaka yake ya uteuzi haipo tena.

Mahakamani kunahitajika ushahidi wa kuthibitisha unachokisema. Unaweza kuwa wa nyaraka, maneno au vyote. Ushahidi mzuri ni wa wengine wanaokuja kuushadidia ushahidi wako. Kunapokosekana ushahidi, maneno yanabaki porojo isiyo na maana yoyote.
 
...
Kiujumla, utetezi wa Sabaya umetanua sana uwanja na kumuweka kwenye kazi ngumu sana kuchomoka kwenye kesi yake. Ameanzisha mambo mengi yanayohitaji ushahidi. Na ushahidi mwingine wa maneno hautapatikana kwakuwa yeye mwenyewe amekataa kuwataja alioambatana nao kwenda sehemu ya tukio siku husika. Pia, mamlaka yake ya uteuzi haipo tena.
...
... ghafla urais umekoma kuwa taasisi kufuatia sakata la Sabaya? Wakuu wengine wote wa wilaya na wateule wengine wa toka enzi za awamu iliyopita nao mamlaka zao za uteuzi hazipo tena au ni kwa Sabaya tu? Sijaelewa!
 
Sabaya ameshajimaliza, kitendo chake cha kukiri kuwepo eneo la tukio hata kama anadai alitumwa na mamlaka husika kujinasua kwake itakuwa vigumu, je, alifuata sheria kuingia eneo la mwingine? alikuwa na kibali? kama hakuwa nacho hakuwa na tofauti na jambazi alietumia silaha kufanya uvamizi, hapa Sabaya ameshakiri kosa.
 
... ghafla urais umekoma kuwa taasisi kufuatia sakata la Sabaya? Wakuu wengine wote wa wilaya na wateule wengine wa toka enzi za awamu iliyopita nao mamlaka zao za uteuzi hazipo tena au ni kwa Sabaya tu? Sijaelewa!
Thanks Mkuu, I was about to ask the same question
Urais sio mtu Urais ni Taasisi

Sent from my TECNO KD7h using JamiiForums mobile app
 
Hivi we mwanasheria njaa unajua kuanalyze facts? Amekiri kuhusika na operation dhidi ya ujujumu uchumi ndio maana anadai alitumwa kwa kazi maalumu, hajakiri kushiriki ujambazi.

Kama mwanasheria ebu tupe ingredients za armed robbery alafu oanisha na tukio la Sabaya. Acha ushabiki
Mkuu, huna uwezo wa kuelewa jambo hili la kisheria. Cha kufanya ni kukaa kimya.
 

Similar Discussions

57 Reactions
Reply
Back
Top Bottom