Sabaya aangua kilio mahakamani, kesi yaahirishwa

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,827
21,456
Muda mfupi baada ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Salome Mshasha kuahirisha kesi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na ndugu zake waliokuwepo mahakamani wameangua vilio mahakamani.

Kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2022 imeahirishwa hadi Septemba 26 mwaka huu kwa kutokamilika kwa upelelezi.

Hata hivyo, Sabaya amefikishwa mahakamani hapo leo Septemba 12 akiwa peke yake baada ya wenzake wanne kuachiliwa huru Septemba 6 mwaka huu baada ya kukiri makosa ya uhujumu uchumi na kulipa faini.

Wenzake hao ni pamoja na Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.
Baada ya kukiri makosa hayo, ambayo ni pamoja na kujitwalia madaraka isivyo halali na kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Alex Swai na kula njama na kumnyima na kukandamiza haki yak, mahakama iliwatia hatiani na kutoa amri ya kulipa kila mmoja faini ya Sh50,000 na fidia ya Sh1miloni kwa mwathiriwa.

Awali wakili wa upande wa mashitaka, Sabitina Mcharo, meiieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kumwomba hakimu anayesimamia kesi hiyo kupanga tarehe nyingine jambo ambalo liliwaibua mawakili wa upande wa utetezi.

"Mheshimiwa hakimu shauri hili limekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika hivyo tunaomba uipangie kesi hii tarehe nyingine," aliomba wakili huyo.

Hata hivyo, wakili wa upande wa utetezi, Hellen Mahuna alisema bado wana malalamiko kuhusu kuchelewa kwa upelelezi wa kesi hiyo na kwamba mteja wao Sabaya anaendelea kuteseka.

"Nakumbuka tarehe ya mwisho kuja hapa Agosti 29, 2022, mahakama hii iliagiza upande wa mashitaka waje leo na kutoa mwafaka wamefikia wapi, lakini tumeelezwa kirahisi rahisi tuu kwamba upelelezi bado haujakamlika.

"Tunaiomba hii mahakama imtoe huyu mshitakiwa namba moja maana hatuna hati ya mashitaka ambayo ni ‘proper’ kwa sababu alichofanya DPP ni kwamba hafuati maelekezo na mshitakiwa anendelea kuteseka, tunaomba DPP afuate sheria," amesema.

Naye hakimu Mshasha amesema kupokea maelezo ya pande zote mbili na kuuagiza upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo ili mshtakiwa ambaye ni Sabaya apate haki yake na kamba mahakama ni chombo ambacho kinatoa haki kwa kila mtu.
 
Jamhuri wanamchezea huyu jamaa kisaikolojia mpaka ameanza kutoa machozi, akikumbuka wenzake wameshaachiwa lakini yeye bado mambo yake magumu, huku anauguza operation aliyofanyiwa kichwani, lazima aangue kilio, japo najua ni suala la muda tu, watamuachia huru.
Hujaelewa bado
 
Kwani kuna kesi aliyoshitakiwa kwa kutesa watu??
Kosa la ujambazi wa kutumia silaha dhidi ya Bw Msangi February 2021 lililkuwa ubembelezaji?

Wewe labda mgeni humu ndio hatojua ila kiukweli poleni sana kwa kuondokewa na bosi wenu aliyekuwa anatuma na kuona ukatili ni dili leo hii yuko wapi?

Ni wakati saalsa mjue zama zimebadilika nanyi mbadilike mfanye kazi halali na mtende haki.
 
Kosa la ujambazi wa kutumia silaha dhidi ya Bw Msangi February 2021 lililkuwa ubembelezaji?
Hiyo kesi imefutwa.

Hakuna kitu kama hicho.

Kafungue tuone kama utakuja na ushahidi wowote.

Kesi za kubumba tu. Ila ni jambo la kikatili mno wanalolifanya.
 
Mtu anateseka namna hii kwa ajili ya kufurahisha wengine.

Haya madaraka ni ya muda tu.

Kama sio wao ni watoto au wajukuu wao. Will experience the same treatment.

Haya unayoona ni mabaya kwa Sabaya ndio njia aliyopitisha watu wengi ili kumfurahisha Magufuli. Tunajua ataachiwa huru pamoja na unyama wote aliofanyia watu, lakini iko siku hiyo jinai yake na wengine wote itafanyiwa kazi. Kwasasa bado ni warmup maana serikali ya CCM inayolinda wakatili bado iko madarakani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom