Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Yaani ati umetumwa kuua alafu unakamatwa unasema nimetumwa kuua. Hivi hata mtoto mdogo si atakushangaa Kwa ujinga.

Hata Kama umetumwa kazi na mkuu wako, ukaioa jina kazi maalumu na ambayo kimsingi huenda ni Uhalifu lazima utumie akili kuitenda, na ukishikwa utakayewajibika ni wewe 100% .

Sasa hawa ndugu zetu wanakuambia Kwa vile katumwa ataachiwa, inashangaza kweli
Binafsi sitashañgaa kuona hilo likitokea kwani kwao hiyo ilishakuwa ni sera ambayo inatekelezwa na wanajua jinsi ya kulindana.
 
Sabaya aliwahi kushitakiwa kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.

Na wakati huo alikuwa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha.

Sasa ukiniambia Sabaya ni jasusi, ninapata mashaka kwamba inakuwaje jasusi ashitakiwe kwa kujifanya jasusi?
 
Ni wasenge Tu wanaoweza mlaumu sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo , Raisi kumfukuza kazi sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofsi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo ma-mae, et ujasusi , ujinga mtupu
Hakuna kesi ni ujinga tu, sabaya tangu mwezi wa 4 anasakamwa. Na wanajua alikuwa akipewa order kama mojawapo ya majukumu. Hawakustahili kumdhalilisha kiasi kila wakati wanajua alifanya majukumu aloagizwa

Ilibidi wamlinde maana kwa sisi tunaojua siasa kila uongozi lazima watu wachache waumie wengi wapone.
Sabaya kutumwa na rais sio dhambi ilo wazi hata ungekuwa wewe ungemtuma akusaidie kazi.kisiasa hii inaeleweka wala aliemtuma yupo sahihi.
Urais ni taasisi je hawakujua hilo? Of cause walijua sana. Sasa ndo ujuwe magufuli alikuwa akichukiwa bila yeye kutambua. Yaani sasa hivi ni kama kukomoa.
Sabaya ametaja baada ya kuona hakuna msaada.kipindi hiki chote alikuwa kimya alivyoona hakuna anaemsaidia akaongea...
Najua ataumia na wenda baabae...................

Kwa sasa hana chaguo hata mimi ningefanya hivyo.
Ni mapito tu hata awamu zilizopita hapa.mambo yalikuwepo.
 
Sio enzi ya mwendazake tu lakini si kila kitu anachoarifiwa Rais na makamo lazima aambiwe! Yako mengi sana makamo huwa hawaambiwi na sio Tanzania tu bali duniani kote.
Ni sawa mkuu lakini sio katika mambo muhimu hasa ya usalama wa nchi...Angalia Kenya kwa mfano hakuna kitu atachokifanya Kennyatta na Rutto asijue( Mambo muhimu ya nchi). Tatizo letu Tanzania tulijisahau kuwa Makamu ndiye Rais number mbili na ndio maana walikuwa wanapewa saana wale wenzetu pale jirani kama kuwatuliza kuacha kelele za kudai nchi yao. Tumekujakustukia sasa hivi.
 
Ni sawa mkuu lakini sio katika mambo muhimu hasa ya usalama wa nchi...Angalia Kenya kwa mfano hakuna kitu atachokifanya Kennyatta na Rutto asijue( Mambo muhimu ya nchi). Tatizo letu Tanzania tulijisahau kuwa Makamu ndiye Rais number mbili na ndio maana walikuwa wanapewa saana wale wenzetu pale jirani kama kuwatuliza kuacha kelele za kudai nchi yao. Tumekujakustukia sasa hivi.
Nakuambiaje acha hakuna kitu anafanya Kenyata eti Ruto asijue! Vyombo vya ulinzi na usalama vyote vinareport kwa Kenyata sio Ruto! Ruto anaweza kuambiwa ila si lazima yote anayoambiwa Kenyata.
 
hakuna kesi hapo.
kama alikuwa anatekeleza majukumu yake aliyo elekezwa na aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu ktk kuhakikisha kodi ya Serikali inalipwa. sasa huo unawezaje kuuita eti ni unyang'anyi?!!
ukiangalia hii kesi kwa jicho la tatu imejaa kisasi dhidi ya sabaya kutokana na majukumu yake aliyo kuwa akiyatekeleza, kwa vyovyote vile lazima angechukiwa sana na either;
1. wafanyabiashara au wanasiasa au wote kwa pamoja. ndicho kilicho tokea.
 
aise kweli selo mbaya
kachanganyikiwa huyu sio bure na naamini huyu sio kitengo huyu..

Jambaz
 
Jambo zito unalijua wewe , yeye kasema basi , kama walishindwa kutambua Hilo na wote wapo DSM wanakula bata yeye anasota rumande leo limekuwa Jambo zito , mara ngapi tuhuma za sabaya anapelekewa Maghufuli na Maghufuli anapiga kimya , means alikuwa anajua Kwa usahihi what is going on , Leo hii ofisi hyo hyo inamgeuka na kujifanya wema , huo usenge na upumbavu hakuna anayeweza fanya.....
 
Kwamba sabaya,magufuli,na mpango waliunda genge la kijambazi la kuua kutesa na kupora watu Mali zao!!
 
Hapo kwenye special mission ndio ukweli wenyewe, beba lawama baadae utakumbukwa.

Kuna wale walimuua "jambazi" mmoja baadae ikaonekana alikuwa mkurugenzi wa taasisi nyeti. Sijui kilichotokea, lakini walipunguziwa adhabu kutoka kwa Bwana Mkapa, wakatoka wakati wa Kikwete
 
Sabaya anajua anachokifanya. Bila shaka wanasheria wake sio mafala kihivyo na walichekecha pros & cons ya hiyo move na wakajiridhisha kuwa ina faida zaidi kwao kuliko madhara.

Labda Taasisi ya Urais ndio imemwambia aseme hivyo. Tutajuaje? Harafu ni kweli technically bado ni mtumisgibwa Serikali maana hakufuzwa bali alisimamishwa tu kupisha uchunguzi
Na nusu mshahara bado inaingia kila mwezi. Akishinda kesi hela zetu za miamala zitamlipa fidia.
 
Uzuti hii kesi inaenda mbio sana tusubiri mawakili wa upande Jamhuri waki cross ....pia demand ushahidi
 
... Sabaya kuwemo kwenye Mfumo wa ujasusi wa nchi hii haina mashaka! Toka enzi akiwa mtoto UVCCM aliwahi kukutwa na kitambulisho cha TISS kesi ikafunguliwa. Alivyoachiwa ni mamlaka yake ya uteuzi pekee ndio inajua.

In short, ameandaliwa kwa kazi maalum long time so yanayotokea kwenye sakata hili ni long time plan. Alichokisema mahakamani ni sahihi kabisa.
Basi maandalizi yake yalikuwa na mashaka sana.

Hakuwahi kufundishwa kwamba kuna kutolewa sadaka, na mambo yakiharibika you are on your own. Kama kweli alitumwa which is likely ni kweli, kwa nini taasisi zile zile zinamtesa? Kuna uwezekano mkubwa alikuwa anavuka mipaka na akatengeneza maadui wengi, walikuwa wanasubiri sponsor aondoke wamshushie rungu.

Either way, alikuwa mpumbavu aliyelewa power. Hii nchi kila mwenye "kazi maalum" angekuwa kama yeye, hali ingekuwa mbaya sana.
 
Ni wasenge Tu wanaoweza mlaumu sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo , Raisi kumfukuza kazi sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofsi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo ma-mae, et ujasusi , ujinga mtupu

Katika makosa kuna kufanya kitu kinaitwa kosa kwa public interest. Kwa mfano, wakati anakamata mashine ya kutengenezea fedha haramu, ingetokea purukushani akajeruhi mtu, kujeruhi ni kosa, lakini asingekuwa pinpointed yeye mwenyewe, na Identity yake wakati wa hilo zoezi, haikuwa sabaya.

Inapotokea kwenye missiona kama hizo, amekwenda kukamata mitambo ya fedha, halafu akaanza kubaka kwa mfano, hiyo ni personal offence, na kama anageshitakiwa kwa kubaka, hapo utetezi wa kwamba alikuwa kazini ni null and void, kwa kuwa hakuwa ametumwa kwenda kubaka, na kubaka hakukuwa na uhusiano wowote wa kumsaidia akamlishie kazi yake.

Alitumwa kuwakamata waharifu, na kukamata uharifu, hiyo ndiyo JD yake. Habari za kuenda kupigia watu makele usiku kucha na kudai mamilioni ya fedha kwa wafanya biashara nako alitumwa na nani?





Ni lazima watu watambue mipaka ya kazi. Ujambazi si sehemu ya kazi na hivyo haiwezi kuwa utetezi.

Hata hivyo ninaona Sabaya anachengesha. Haongelei jinai zake, badala yake anakimbilia kusema matukio rasmi aliyokuwa anafanya kazi halali za kukamata wafua noti bandia. Lakini hakuna kesi inayohusu kosa lake la kukamata mitambo ya fedha kwa kuwa hiyo ilikuw akazi halali. Aongelee tuhuma zile zingine kama nazo alitumwa na nani?

ULEVI NA KIBURI CHA MADARAKA VINA MWISHO. HERI MTU YULE AMBAYE BWANA NI KIMBILIO LAKE. MAANA HATAONDOSHWA
 
Back
Top Bottom