Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
4,576
2,000
Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert Heriel
 

Gan star

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
230
500
Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
4,576
2,000
Sio kila kitu ukiagizwa na Mkuu wako unapaswa kufanya. Ndio maana mtu umepewa akili na utashi WA kung'amua. Sabaya sio roboti, Sabaya sio mtoto, Sabaya halijawahi thibitika kuwa anamapungufu ya akili. Hivyo kivyovyote vile tayari yupo nyavuni.

Na mbaya zaidi kaongea Jambo zito ambalo Kama ni ukweli basi linazidi kumuweka pabaya.

Zingatia;
Hakuna anyemchukia Sabaya, Ila matendo yake ndio yameleta haya yote
 

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,363
2,000
Ni wasenge Tu wanaoweza mlaumu sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo , Raisi kumfukuza kazi sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofsi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo ma-mae, et ujasusi , ujinga mtupu
Ashikilie hapohapo wapi sasa
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
4,576
2,000
Hicho ndio kiwango cha uweledi wa wanakijani,ndio maana tunaona bambikiabambikia, kama silaha ya mwisho kwao kwani walishafikia kokomo cha uwezo wa matumizi ya akili.

Yaani ati umetumwa kuua alafu unakamatwa unasema nimetumwa kuua. Hivi hata mtoto mdogo si atakushangaa Kwa ujinga.

Hata Kama umetumwa kazi na mkuu wako, ukaioa jina kazi maalumu na ambayo kimsingi huenda ni Uhalifu lazima utumie akili kuitenda, na ukishikwa utakayewajibika ni wewe 100% .

Sasa hawa ndugu zetu wanakuambia Kwa vile katumwa ataachiwa, inashangaza kweli
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
11,110
2,000
Sabaya anajua anachokifanya. Bila shaka wanasheria wake sio mafala kihivyo na walichekecha pros & cons ya hiyo move na wakajiridhisha kuwa ina faida zaidi kwao kuliko madhara.

Labda Taasisi ya Urais ndio imemwambia aseme hivyo. Tutajuaje? Harafu ni kweli technically bado ni mtumishi wa Serikali ya Samia maana hakufuzwa bali alisimamishwa tu kupisha uchunguzi
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
16,514
2,000
... Sabaya kuwemo kwenye Mfumo wa ujasusi wa nchi hii haina mashaka! Toka enzi akiwa mtoto UVCCM aliwahi kukutwa na kitambulisho cha TISS kesi ikafunguliwa. Alivyoachiwa ni mamlaka yake ya uteuzi pekee ndio inajua.

In short, ameandaliwa kwa kazi maalum long time so yanayotokea kwenye sakata hili ni long time plan. Alichokisema mahakamani ni sahihi kabisa.
 

RAISI AJAYE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,750
2,000
Ina maana Alitumwa ubakaji na uporaji pesa???After all HUKUMU YA SABAYA ITAHALALISHA HUKUMU YA UGAIDI YA MBOWE !!!WAMEAMUA KUMTOA SABAYA KAMA CHAMBO ILI KUMMALIZA MBOWE KABISA KWENYE RAMANI YA MAISHA YAKE NA SIASA!!!!!!!mawazo huru!!!!
 

kirumbiu

JF-Expert Member
Feb 23, 2016
325
500
Hapo sabaya hata kama alitumwa tayari kaenda kinyume na ujasusi jesusi hatowi sir I kuwa katumwa na nani hata kama atanyongwa utetezi hafifu sana
 

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,608
2,000
kaka kuna kitu hujakielewa hapa . Tatizo kubwa lilokuwepo katika Serikali ya Mwendazake ni kama vile nchi haikuwa na Makamu wa Rais. Kazi zake zilikuwa ni kupokea wageni wa Mheshimiwa tu kazi nyingine alikuwa anarukwa ndio maana unaona hakuna connections kati ya utawala uliopita na wa sasa
 

Galileo_Gaucho

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,861
2,000
... Sabaya kuwemo kwenye Mfumo wa ujasusi wa nchi hii haina mashaka! Toka enzi akiwa mtoto UVCCM aliwahi kukutwa na kitambulisho cha TISS kesi ikafunguliwa. Alivyoachiwa ni mamlaka yake ya uteuzi pekee ndio inajua.

In short, ameandaliwa kwa kazi maalum long time so yanayotokea kwenye sakata hili ni long time plan. Alichokisema mahakamani ni sahihi kabisa.
Anamuonekano na kujiamini kwa Ki TISS, kwenye kesi hii ndio ntajua ya ziada. Namkubali that's me anyway, it doesn't concern any.
 
Aug 2, 2016
83
150
Angejiteteaje kwa mfano? Umetumwa na wakuu wa nchi lkn wakati wa matatizo wamekaa kimya wanendelea kupiga kampari tu. Lazima nao wajulikane kuwa ndio waliokuwa wakituuwa.

Da ila inasikitisha sana, kuwa awamu ya tano ya serikali ya Tz badala ya kulinda usalama wa wananchi wake serikali ndo ikawa inatengeneza vikundi vya uarifu! Da hìi hatari sana. Lkn Mungu fundi.
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,322
2,000
Sebaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.
Issue za uhalifu Sabaya anasema hazifahamu, kakana kuchukua pesa yoyote kwa mtu yeyote wala kumtishia mtu bastora
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,322
2,000
kaka kuna kitu hujakielewa hapa . Tatizo kubwa lilokuwepo kati ya Serikali ya Mwedazake ni kama vile nchi haikuwa na Mkamu wa Rais. Kazi zake zilikuwa ni kupokea wageni wa Mheshimiwa tu kazi nyingine alikuwa anarukwa ndio maana unaona hakuna connections kati ya utwala ulipita na wa sasa
Sio enzi ya mwendazake tu lakini si kila kitu anachoarifiwa Rais na makamo lazima aambiwe! Yako mengi sana makamo huwa hawaambiwi na sio Tanzania tu bali duniani kote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom