Sabaya katika mchuano mkali na mawakili wa Serikali

Jun 20, 2023
54
51
Mawakili wanaomwakilisha aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, Jana walichuana vikali na mawakili wa upande wa Jamhuri wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya kupinga Sabaya kuachiliwa huru iliyokatwa na upande wa Jamhuri.

Sabaya na wenzake walihukumiwa kifungo Cha miaka 30 jela na mahakama ya hakimu Mkazi mjini baada ya kupatikana na hatia kwenye makosa ya unyanyg'anyi wa kutumia silaha.

Baada ya hukumu hiyo,Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Gabriel Mbura walikata rufaa mahakama Kuu Kanda ya Arusha kipinga hukumu hiyo na kishinda rufaa yako na kuachiliwa huru.

Baada ya uamuzi huo upande wa Jamhuri uliwasilisha Nia ya kukata rufaa kupinga kuachiliwa kwao rufaa ambayo ilinguruma Jana mbele ya jopo la majaji watu wa mahakama ya rufaa.

Majaji hao ni Jacobs Mwambele ambaye aliongoza jopo hilo la majaji,Ignas Kitusi na Leila Mgonya waliotimia saa Tano kusikiliza rufaa hiyo.

Upande wa jamhuri ukiongozwa na Sabina Silayo uliwasilisha sababu saba kupinga kiliachiliwa huru kwa warufaniwa hao ukidai kuwa waliachiliwa kimakosa.

Silayo alidai kuwa baada ya kupitia mwwenendo wa kesi wa mahakama Kuu pomoja uamuzi walibaini kuwa mahakama ilikosea.

Alisema upande wa Jamhuri haukupewq nafasi ya kuuliza maswali ya dodoso baada ya shahidi wa pili kumaliza kutoa ushahidi.

"Waheshimiwa majaji wa mahakama ya rufaa,shahidi wa pili baada ya kutoa ushahidi,upande wa Jamhuri haukupewa nafasi ya kuuliza maswali ya dodoso kama Sheria inavyotaka",alisema.

Akasisitiza kuwa i si ushahidi wa shahidi wa pili pekee uliotumiia kuwatia hatiani kwani kulikuwa na ushahidi mwingine na kudai jaji hakujielekeza vizuri katika uamuzi wake.

Baada ya kuwasilisha hizo,wakili huyo upande wa Jamhuri akaliomba jopo la majaji hao kupitia hoja zao na kuwatia hatiani warufaniwa hao kwa kile alichodai mashitaka Yao ya unyanyg'anyi wa kutumia silaha yalidhibitika.

Kwa upande wako Moses Mahina anayemwakirisha Sabaya alisema msimamo wao ni kwamba hukumu ya rufaa ya kwanza ilikuwa sahihi na haikuwa na mashaka yoyote.

Alieleza kuwa kulikuwa na mkanganyiko kwa shahidi wa 6 upande wa Jamhuri kwani wakati tukio linadaiwa kutokea Mtaa wa Bondeni,mashahidi wote walitaja tukio lilitokea sokoni.

Majaji baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili watakaa na kupitia hoja zote na kwa mujibu wa Jaji Jacobs,wahusika watajulishwa siku na tarehe ya kusomwa kwa uamuzi huo.
 
Hizo kesi ni kupoteza tu muda na kuendelea kulitia hasara taifa kwa kulipa allowance majaji,waendesha mashtaka wa serikali na mawakili wanaozisimamia tumeshajua hao hawafungwi tunafungwa sisi wamwache au wampe wanachoona kinamtosha maisha mengine yaendelee.

Hakuna mtu kiongozi nchi hii aliyewahi kufanya kosa dhahiri likaonekana hadharani kama Makonda pale alipovamia studio za radio usiku wa manane na Ak-47 tena zilizokuwa loaded full magazine lakini tunapoongea hapa leo ni mwenezi wa chama tawala anayejitapa kutoa maagizo hata kwa waziri mkuu wa nchi hii.
 
Hizo kesi ni kupoteza tu muda na kuendelea kulitia hasara taifa kwa kulipa allowance majaji,waendesha mashtaka wa serikali na mawakili wanaozisimamia tumeshajua hao hawafungwi tunafungwa sisi wamwache au wampe wanachoona kinamtosha maisha mengine yaendelee.

Hakuna mtu kiongozi nchi hii aliyewahi kufanya kosa dhahiri likaonekana hadharani kama Makonda pale alipovamia studio za radio na Ak-47 tena zilizokuwa loaded full magazine lakini tunapoongea hapa leo ni mwenezi wa chama tawala anayejitapa kutoa maagizo hata kwa waziri mkuu wa nchi hii.
Walipwe wazilete kwenye mzunguko mtaani kuliko kwenda kuliwa uarabuni hizo hazirudi
 
Back
Top Bottom