Sababu (10) tata za kisheria uuzwaji wa Bandari ya Tanganyika

HANGAYA THE CHIEF

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
329
947
UTANGULIZI:

Bila kugusia maudhuni yalivyoandikwa, au kukosoa kilichoandikwa, nimeandaa sababu 10 tata za kisheria ambazo zinatambainisha kwa nini mkataba wa uuzaji wa Bandari ya Tanganyika ni batili na ni wa aibu kwa nchi ambayo inawasomi wengi wa sheria;

Katika sheria za kimataifa za uwekezaji (international investment law), wawekezaji wanaokwenda kuwekeza nchi za kigeni (foreign investors), wanapashwa kulindwa na sheria za kimataifa, aidha baina ya nchi na nchi, yaani,(bilateral investment treat) kwa kifupi (BIT) au mjumuisho wa nchi mbalimbali (Multilateral investment treat) kwa kifupi inaitwa (MIT)., au baina ya nchi na mwekezaji, kwa hiyo basi endapo nchi hizo hazina, zinaweza kukubaliana kutengeza mkataba huo. kama walivyofanya JMT na Emirate of Dubai, ndio huu kwa sasa tunauita mkataba wa awali; ambao unanipeleka kwenye sababu yangu ya kwanza;

1. instrument used to endorse the document, (power of attorney), kwa Kiswahili ( Nguvu ya kisheria)

mkataba wa nchi na nchi ( a contractus cum states), utahesabika kuwa umeridhiwa na nchi hizo endopo, watia saini ni viongozi waliotajwa katika ibara ya 7(2) (a) ya sheria za Mikataba ya Kimataifa ( Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969) inataja wakuu wa nchi, wakuu wa serikali, au mawaziri wa nchi za nje ( foreign affairs), 7 (2) (b), inawataja mabalozi wawakilishi wa nchi zao, 7(2) (c) wawakilishi wa nchi wa taasisi za kimataifa.

Kinyume na ibara ya 7 (2) ya sheria za mikataba za kimataifa (Vienna Convention on the Law of Treaties), ibara 7 (1) ya sheria hizo, inatoa nafasi kwa waliopewa nguvu ya kisheria wanaweza pia kusaini mikataba baini ya nchi zao na nchi zingine.


(a) Nguvu ya kisheria ni nini? ( what is power of attorney), (full power) (instrument)
(is document that gives power to another person, to perfom duties on his/her behalf that other person would have done ), yaani ni nyaraka inayotoa uwezo, nguvu, mamlaka, kwa niaba ya mtoaji uwezo huo, kufanya kazi ambayo mtu anayeitoa nangeweza kuifanya.

watiaji saini, wa mkabata wa uuzwaji wa bandari ya Tanganyika, wanaangukia Ibara ya 7 (1) ya sheria za mikataba ya kimataifa, ( the vienne Convention, on the law of treaties, 1969), kwa maana nyingine wanatakiwa waonyeshe nani kawapa nguvu ya kisheria (power of attorneys, or full power), kuziwakilisha nchi zao, ili kukidhi takwa kuonyesha wazi kuwa nchi ndio imetoa ridhaa, (consent) kuruhusu wao wasaini mkataba/mikataba huo/hiyo.

(b)characterization of the power of attorneys, full power: (mchanganua wa nguvu ya kisheria)

nguvu ya kisheria (power of attorneys) ina sehemu kuu mbili; yaani ni lazima pawepo na mtoaji, au kisheria tunamwita (Donor ,or the giver) na sehemu ya pili, lazima pawepo na mpokeaji, yaani ( Donee, or the recepient). hawa lazima wawepo kwa majina na vyeo vyao. au ni lazima waeleze uhusiano wao na document wanayotoa nguvu ya kisheria kwa mtu mwingine.

(c) utata:

Upande wa Tanzania;

Ukisoma nyaraka zinazotembea na ambazo hazijakanushwa kuwa ni feki, utaona pasipo shaka kuwa, nguvu za kisheria, kwa upande wa JMT zimekidhi vigezo , kwa maana Mtoa ni nchi, na kiongozi mkuu wa nchi anatoa kwa kwa niaba ya nchi yaani Rais wa JMT, na anayepokea ni mbarawa, katika nafasi yake kama Waziri.

kwa Upande, wa the Emirate of Dubai
wakati kwa upande wa Emirates of Dubai, mtoaji aidha ni Emirate of Dubai, au United Arab Emirate , au Emirate of Dubai na United Arab Emirates, hayo atayaona kwenye kichwa (heading) ya appointment letter, mstari wa pili wa power of attorneys, na kwenye footing, yaani signature, ( kwa hiyo signature (saini) watoaji ni wawili, heading mtoaji ni mmoja, second line, watoaji ni wawili) (Emirate of Dubai, na United Arabu Emirates),

anayetoa nguvu ya kisheria, hatajwi kwa jina wala kwa nyadhifa yake, au cheo chake, au uhusiano wake na serikali hizo mbili na nguvu alizozonazo kisheria, kumpatia mpokeaji. ( kwa tafsili nyepesi, hakuna mtoaji wa nguvu ya kisheria kwa upande wa serikali zote mbili tajwa katika power of attorney hizo.

ila, takwa la pili kwa maana ya mpokeaji anatajwa, kwa maana ya H.E. Ahmed Mahboob Musabih, ambaye ni Chief Executive Officer of the Ports, Customs and Free Zone Corporation ( being referred to as agent).

2. what does it mean? ina maana gani kisheria
jibu ni jepesi, hakuna ridhaa (consent ) ya serikali ya Emirate of Dubai, au United Arab Emirates, iliyoridhia kusainiwa mkataba huo.

itaendelea, ........................................................................................................................kesho sababu tata ya ya pili;


 
tatizo vijana wengi wa siku hizi ni wavivu wa kufanya tafiti, wanasubiri wanasiasa majukwaani wawatafunie kile wanachotaka kupewa, document ya kuuza bandari ya Tanganyika inayotembea mitandaoni ina page 36 tu, utakuta mtu hajasoma anasubiri kusimuliwa, eti hawajauza, au wameuza.

okay kasome tafsiri ya sale, buyer, and saler kweny cap. 214 ya sheria zetu, na disposition ya cap. 113 ya sheria zetu, na kisha zisome kwa pamoja na international document in relation na hizo documents , kisha njoo uniulize kama hatujauzwa au bado.

pili, sifanyi siasa naongea kuhusu rasilimali ya Tanganyika iliyouzwa, tuna watoto, wajukuu, na vitukuu vimezaliwa na havijazaliwa bado, vinasubiri kurithi rasilimali hizo tunazotapanya kwa manufaa ya wachache. ni wajibu wangu na wako kuzilinda kwa wivu, mkubwa
 
tatizo vijana wengi wa siku hizi ni wavivu wa kufanya tafiti, wanasubiri wanasiasa majukwaani wawatafunie kile wanachotaka kupewa, document ya kuuza bandari ya Tanganyika inayotembea mitandaoni ina page 36 tu, utakuta mtu hajasoma anasubiri kusimuliwa, eti hawajauza, au wameuza.

okay kasome tafsiri ya sale, buyer, and saler kweny cap. 214 ya sheria zetu, na disposition ya cap. 113 ya sheria zetu, na kisha zisome kwa pamoja na international document in relation na hizo documents , kisha njoo uniulize kama hatujauzwa au bado.

pili, sifanyi siasa naongea kuhusu rasilimali ya Tanganyika iliyouzwa, tuna watoto, wajukuu, na vitukuu vimezaliwa na havijazaliwa bado, vinasubiri kurithi rasilimali hizo tunazotapanya kwa manufaa ya wachache. ni wajibu wangu na wako kuzilinda kwa wivu, mkubwa
Kwa nn watetezi wakuu wa hili swala upande wa bunge ni wale wabunge vilaza(zero brain) (zero upstairs)?
 
We nae ni mpotoshaji tu, kichwa cha habari tu kina utata, ni uuzwaji au ukodishwaji??? Mda wote tumuogope Mungu jmn
 
Back
Top Bottom