Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Mkuu Voice of Reason, vionjo vya mapenz ni hisia za penzi.. Onyesha kweli umefika kwa mwenzio! Mapenzi yapesa huua hizi hisia!
Duh ni vigumu kukataa....

lakini umeshaongea na mtu anayependa kwa kuvutiwa na pesa akasema hana hizo hisia za penzi na kuonyesha kweli amefika kwa mwenzake na je furaha zao zikipimwa huyo mpenda pesa enjoyment yake ni ndogo kuliko huyu mwingine?
 
Duh ni vigumu kukataa.... lakini umeshaongea na mtu anayependa kwa kuvutiwa na pesa akasema hana hizo hisia za penzi na kuonyesha kweli amefika kwa mwenzake na je furaha zao zikipimwa huyo mpenda pesa enjoyment yake ni ndogo kuliko huyu mwingine?
Wapenda pesa hawana hisia za mapenzi, hufanya nyeti zao km mtaji!
 
Dah! Hili liuseful thread limenipita.
Mapenzi ya pesa huwa si mapenzi ya dhati kwa sababu unapenda alichonacho na sio yeye kama yeye ila hii isiwafanye wenye pesa wahisi hawapendwi..
 
Hii thread nzuri sana,

pesa siyo kila kitu,
ila kwa maisha ya sasa/kipindi hiki/karne hii, pesa hurahisisha kila kitu,
japo haiwezeshi kila kitu/jambo.

Kivitendi kwa maisha ya sasa ni vigumu sana upendo, mapenzi na pesa kuvitenganisha.

Kwa hiyo basi anayependa pesa kwanza asilaumiwe bali aelimishwe.

Aelimishwe nini?
mimi naona kupenda mtu kwa pesa zake ni poa sana,
lakini wanaosema kuwa ati akipata mwenye peza zaidi atakukimbia si kweli hasa.
Pesa ni kweli sabuni ya roho,
ni kweli pia chakula kitamu ni ufunguo wa moyo wa mwanaume,
pia ni kweli urembo wa msichana ni pambo na liwazo kwa wanaume

kwa wenye kujua commitment, hivo vigezo japo vikiondoka, vinaleta utata na majaribu kwenye mahusiano, wajanja tayari wameshakuwa creative na kujenga uhusiano, kwa pupitia personalities zao. hivyo mahusiano hayaharibiki.

ila kwa wale walioishia kupensa ile pesa, chakula, sura badala ya kujifunza kumpenda mtu, lazima watakimbia.

JAMANI PESA SABUNI YA ROHO,

kuna lecturer wangu siwezi kumsahau aliwahi kuwaambia wavulana waliokuwa wanalalamika eti washichana tunapenda wavulana wenye pesa
quote '........usikubali mwanamke akudharau, ili uhakikishe unaheshimika nyumbani kwako, usimtegemee, hakikisha una pesa nyingi, fanya kazi usiku na mchana, ili mradi umzidi kipato......' unquote.
Sio habari nzuri sana kwa wanaume, hasa wale wanaotafuta wasichana wenye kazi zao, lakini ni ukweli kuwa pesa inaleta heshima. hasa kwa wanaume
jamani fanyeni kazi, mpate pesa
 
Dah! Hili liuseful thread limenipita. Mapenzi ya pesa huwa si mapenzi ya dhati kwa sababu unapenda alichonacho na sio yeye kama yeye ila hii isiwafanye wenye pesa wahisi hawapendwi..
Leo ndio natoa mchango ktk hii thread kwa mara ya mwisho! MAPENZI YA PESA SIO MAPENZI!
 
Kama watu wanapenda sababu ya Uzuri wa mtu, au Personality ya mtu, Kwanini mwingine asipende sababu ya pesa za mtu

Utasikia watu wanasema "thats not true love anampendea pesa zake".., au "Siku hizi hakuna mapenzi ni pesa tu"...., yeah, kama anampendea pesa zake whats wrong with that, je kuna utofauti wa wewe unayempendea sura yake...?

My Take on This ni kwamba kila mtu anazo priority zake na kama wapo wanaopenda zaidi pesa its okay na community isiwaangalie kama "Gold Diggers" kama wanampa mtu mwenye pesa furaha.., I think its a fair trade....

Money, Looks, Personality, Ucheshi, Powerfullness, they are all features and if they attract someone who are we to say that is true love or not....?

Mapenzi yana cost sana more than hizo hela wanazozisema, bila hela mapenzi hamna....angalia nchi masikini hazina upendo maana cash ina maana, watu hawaendi shule maana hamna hela, mahitaji hamna maana hamna hela...kujirusha hamna cuz no hela..Huwezi mfurahisha mwenzio kama huna hela wala huwezi kuwa mwenye furaha.....acha watu wapendwe kwa ajili ya pesa zake, hata mwenye hela anahitaji kupendwa vile vile.....
 
lakini wanaume kuweni wakweli, mkiwa na pesa mnapendeza, mnakuwa na authority, mna decisions, mnajiamini, mnaweza cope namazingira ya ushindani. Sasa kwanini msivutie mkiwa nazo?
Mwanaume asiye na hela hajiamini, anajishukushuku, anatafuta visingizio, anahasira, hana mipango ya maendeleo, anaogopa kufanya maamuzi nk.
JAmani pesa ni muhimu...
Ndio sababu mko sensitive sana mwanamke anapokuwa na pesa zaidi.

Pesa senyewe sio lazima ziwe kama za Chenge, kila mazingira na kiwango chale cha pesa,
mfano kwangu mie mwanaume bila ya kuwa na ...... bado bado kabisa. Na kila msichana ana kiwango chake cha chini.
 
Pesa senyewe sio lazima ziwe kama za Chenge, kila mazingira na kiwango chale cha pesa,
mfano kwangu mie mwanaume bila ya kuwa na ...... bado bado kabisa. Na kila msichana ana kiwango chake cha chini.
Lakini pesa tamu ni zile ambazo tunazitafuta wote.., au unasemaje..??, kwahiyo mi naona itakuwa bora kupata mtu hardworking ambae mnaweza kutafuta nae pesa au unasemaje; sababu unaweza ukapata mtu akakusaidia kuongeza pesa ambazo unazo wewe
 
  • Thanks
Reactions: LD
Ili mwanamke awe na furaha na amani katika mapenzi aliyo nayo kwa huyo mpenzi, kuna kitu kinaitwa "security".
Hii ni pamoja na kumuondolea mashaka na wasiwasi alionao juu ya maisha yake kiuchumi. Aweze kupata kile anacho hitaji, asiwe na mashaka kuhusu kesho yake, awe anajua kabisa tatizo fulani hili mpenzi wangu huyu anao uwezo wa kunisaidia, nikishindwa mimi.

Hapo haah hata huko Kibo atafika, lakini ukikuta mwanaume mwenyewe hajui hata kesho yake, hakuna amani hapo bana.
Tuwage wa kweli tu, hizi habari za kujikaza kisabuni hatuwezi sasa hivi, waliyaweza mama na bibi zetu.

Mwanaume hujiamini zaidi pale anapokuwa na uwezo wa kumsaidia mke/mpenzi wake kwa jinsi yoyote ile.
 
Lakini pesa tamu ni zile ambazo tunazitafuta wote.., au unasemaje..??, kwahiyo mi naona itakuwa bora kupata mtu hardworking ambae mnaweza kutafuta nae pesa au unasemaje; sababu unaweza ukapata mtu akakusaidia kuongeza pesa ambazo unazo wewe
Mie naona swala hapa ni furaha ya kila mtu inatokana na nini haswa, kama ni pesa, ok, mie mwenzenu ni kuwa mume wa ukweli, ninayemtegemea kwa mambo makubwa na madogo, mie anitegemee ka upande mwiningine, sasa tukitafuta pesa wote, mambo mengine ya kifamilia atafanya au kusimamia nani?
familia ina nyanja nyingi
mojawapo ni la kiuchumi,
ila pia tusisahau maadili, emotions, habits, vitu ambavyo havipimiki wala ujenzi wake hauna muda wala vipimo maalum, inataka commitment, na muda mrefu kuvijenga. Sie wanawake wa sasa tumejiunga na waume zetu katika serious busines ya kutafuta hela, tumesahau, hatupendi majukumu yetu ndio unaona matokeo yake, dunia inavyokwenda
 
Utatu huu kwanini unakuwaga na utata? Haijalishi kabila, taifa wala rangi.

Inakuwaje watu wanapopenda na ikatokea hivi vitu vitatu vipo basi maneno hayaishi?

Someni hii habari hapo chini mtaona nina maana gani. Kwani mara ngapi tumeona, kusikia au kusoma watu kama hawa wenye umr mkubwa kuoana lakini maadam hakuna hivyo vigezo vitatu kwa pamoja basi maneno hata kama yapo ni ya kichinichini zaidi.

Ukiwa na mali/pesa utaandamwa wee! Je watu wajifukarishe ndipo waaminike kuwa wanapendana kweli?

Maria del Rosario Cayetana Alfonsa Victoria Eugenia Francisca Fitz-James Stuart y de Silva (yes, that's one name) is one of the wealthiest women in all of Spain. She is worth somewhere between $850 million and $5 billion--but not for long. The Duchess of Alba, 85, is giving it all away so she can marry the man she loves. This sounds like a plot to the latest Nicholas Sparks novel, but we assure you, this is nonfiction to the core. So, why is she giving her vast fortune away? The duchess's six children were dubious about their mother's plans to marry Alfonso Diez, a civil servant who is 24 years younger.

To help assuage their fears that the love may not be genuine, the duchess is going to give her fortune to her children. According to an article from the BBC, the duchess's six children had been against the wedding. Earlier this year, the duchess remarked, "Alfonso doesn't want anything. All he wants is me."

Not surprisingly, news of the impending wedding sparked a flurry of web searches. Online lookups for "duchess marries" and "spain duchess fortune" were both incredibly popular, as computer users have sought the scoop on the unlikely love story.

The duchess's children were all from her first marriage to Pedro Luis Martinez de Irujo y Artazcoz, son of the Duke of Sotomayor. He died in 1972. The duchess remarried in 1978 to a onetime Jesuit priest named Jesus Aguirre y Ortiz de Zarate. He passed away in 2001. The duchess has been friends with Diez for several years. In fact, there were rumors of a wedding in 2008, but nothing occurred after the children "vetoed" the idea of marriage.

No word on whether the duchess's children and grandchildren intend to be on hand for the ceremony. She likes to point out that each of her kids is divorced, even though she has never split up with any of her husbands. According to the UK Guardian, the duchess has given her children and eight grandchildren "a palace each." That ought to keep them quiet.
 
ha haaaa hii ni very interesting niliiona kwenye tv but sikuifuatilia.......

mimi huwa nashangaaa kitu kimoja kuhusu binadamu

mfano we ni mwanaume ukiwa na mwanamke watasema ni pesa ndio kafuata
but watu hao hao wataawambia dada zao waolewe na watu wenye pesa hivi
wasiolewe na malofa.....its funny
 
Waoooooo..

Well,
Anacho kila akitakacho (mali, fedha, familia)
Sasa amezeeka hizo fedha na mali hazina
Msaada sana kwake..

Anataka upendo na mtu wa kuwa naye
Karibu ..... maana anauwezo wa kununua
Upendo... lakini ameona pesa hazi nunui
Kila kitu......
 
ha haaaa hii ni very interesting niliiona kwenye tv but sikuifuatilia.......

mimi huwa nashangaaa kitu kimoja kuhusu binadamu

mfano we ni mwanaume ukiwa na mwanamke watasema ni pesa ndio kafuata
but watu hao hao wataawambia dada zao waolewe na watu wenye pesa hivi
wasiolewe na malofa.
....its funny


Hapo sasa. Kuna pesa na pesa Boss. Pesa ndefu inaendana na umri mrefu alo! Pesa ndogo nayo hivyo hivyo umri mdogo.
Utata upo hapo kwenye urefu wa pesa na udogo wa umri!

Waoooooo..

Well,
Anacho kila akitakacho (mali, fedha, familia)
Sasa amezeeka hizo fedha na mali hazina
Msaada sana kwake..

Anataka upendo na mtu wa kuwa naye
Karibu ..... maana anauwezo wa kununua
Upendo... lakini ameona pesa hazi nunui
Kila kitu......

Hapo sasa!! Ukiwa nazo unaonekana hupendwi wewe bali pesa yako.Kwanini lakini?
 
mimi nafikiri its natural kwa binaadamu ku prefer a more comfortable life
given a choice.....

but ni adhabu mno kufunga ndoa na mtu humpendi kisa ni pesa....
ni taabu hasa....its a punishment....kwa kweli..

sasa hali ikitokea kama hivyo bora kuwa na balanced view....sio kukimbilia kuhukumu...
 
Back
Top Bottom