Utata wa Mabehewa 'Mapya' ya SGR yaliyowasili ulishamalizwa kitambo na Rais Samia, msiwe na shaka hatujapigwa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,597
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Dunia nzima, issues za Afya, Elimu, Maji, Umeme, Gesi, Usafiri na Usafirishaji ni issues zenye maslahi makubwa sana kwa taifa, hivyo leo tunaendelea na ile issue ya mabehewa yetu yaliyowasili hivi karibuni kama ni mapya au ni used, mitumba, yaliyotumika, yakafanyiwa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi, tukaletewa tukiambiwa ni mapya, brand new kutoka kiwandani, ndio maana yameshushwa na nailoni zake tuya 'b' sisi wenyewe!.

Hii ni story mwendelezo, anzia hapa Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!

Huu utata kuhusu haya mabehewa 'mapya' ya SGR yaliyowasili nchini hivi karibuni kutokea nchini Korea Kusini, yakiwa mapya kwenye manailoni kabisa, huku yakiwa na muundo wa kizamani, hali iliyopelekea watu kujiuliza, je, ni mapya kweli au ni used yaliyofanyiwa ukarabati na kuwekewa nakshi nakshi, kumbe ulishamalizwa kitambo sana na Rais mwenyewe, Mama Samia Suluhu Hassan, hali iliyopelekea sisi baadhi yenu kuhoji kama tumepigwa tena kama kwenye Rada! Hivyo msiwe na wasiwasi wala msiwe na mashaka kabisa, harujapigwa!

Hebu msikilize mwenyewe Rais Mama Samia,

Kama Mhe. Rais, aliisha zungumza haya, kigugumizi cha nini kwa hawa viongozi wetu wengine kuubainisha ukweli huu kama Rais wetu, Mama Samia?.

Kati ya vitu vitakavyomfanya Samia anarikiwe sana na Tanzania ya Samia kupata ustawi, ni kitendo cha huyu Mama kuwa mkweli toka ndani ya nafsi yake!. Ubarikiwe sana Mama Samia, tell the truth, and the truth will set you free!.

Hii maana yake ni mambo mawili;
1. Kuna vichwa na mabehewa mapya ambayo tumeagiza na tunatengezewa, kwa sababu it will take time, tumeagiza pia vichwa na mabehewa used kwa kuanzia ambayo tumenunua. Hivyo vichwa na mabehewa used ni kutoka nchini Ujerumani.

2. Rais amesema mzigo utakao anza kuwasili ni used. Kwa vile haya yaliyowasili kutoka Korea ya Kusini ni mabehewa 'mapya' kutoka kiwandani, na unapoagiza, unaagiza according to specifications zako, hizo box bodies mnazoziona ndiyo specifications zetu tulizoagiza, hivyo haya ni mabehewa mapya kutoka kiwandani, japo muundo wake ni wa kizamani sana.

3. Ina maana zile vichwa viwili na mabehewa 30 used kutoka Eurowagons ya Uturuki, iliyonunua Ujerumani nao utafika.

4. Kama ni kweli haya mabehewa ni mapya, Tanzania inaweza kuingia kwenye Guiness Book of Record kuwa ni nchi ya kwanza Duniani kuundiwa mabehewa kwa muda mfupi ajabu. Hivyo hiki kiwanda cha Korea, sasa ndiyo kiwanda kinachounda mabehewa kwa haraka zaidi kuliko viwanda vyote duniani.

5. Waziri Mkuu. Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa, alipotembelea nchini Korea Kusini kukagua kazi ya uundaji mabehewa yetu 'mapya' toka kampuni ya Sung Shin Rolling Stock Technology Company (SSRST) na hiki ndicho Waziri Mkuu alichokisema


Hii maana yake, mabehewa haya ni mapya kabisa kutoka kiwandani!.

6. Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria ambao ulitegemewa kukamilika ifikapo Novemba 2021. ( mkataba huu ulikuwa ni wa vichwa na mabehewa used!)

7. TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25, 2022 kwa madai kwamba EUROWAGON wamechelewesha kazi na
baada ya kuvunja mkataba huo Februari 25, 2022 na EUROWAGON, TRC wakaingia mkataba mpya na kampuni nyingine kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa na kutia nakshi. Kampuni hizo ni Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany)

8. TRC hawakununua vichwa na mabehewa mapya kwa ajili ya SGR, isipokuwa, EUROWAGON waliopewa zabuni walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 used kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC.

9. TRC ilisitisha mkataba na kuwataarifu kwa barua Februari 25, 2022 na kuendelea na kazi ya kukamilisha ukarabati unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2022,” ambayo ilikamika.

10. Kwa mujibu wa Tanzania Railways Corporation, taarifa waliyoeleza kwa waandishi wa habari June 15, 2022, walisema Mkataba kati yao na EUROWAGON unaipa TRC haki ya kuchukua jukumu la kukamilisha ukarabati iwapo mzabuni atashindwa kuzingatia masharti ya mkataba, hivyo vichwa hivyo 2 na mabehewa 30 used kutoka Ujerumani tayari ni mali ya TRC!.

11. Hivyo kitendo cha kisitisha mkataba mmoja na huku tayari mzigo ni wako, halafu ukaingia mkataba mwingine na mzigo kuwasili nchini ni ndani ya miezi 5 tuu!, this goes without saying, mzigo wa mabehewa uliotua nchini!, ama ni mzigo ule ule wa used za Uerowagons ama kweli haya ni mabehewa mapya kabisa ya dukani, yaliyokuwa yakisubiri mnunuzi, baada ya kununuliwa kiwandani kabisa South Korea's Sung Shin Rolling Stock Technology Company (SSRST) na yametiwa nakshi nakshi na kuletwa nchini!, ama haya ni yale yale mabehewa mitumba ya EUROWAGON, hivyo hoja za jee mabehewa haya ni mapya ama used, bado zinaendelea hadi TRC waseme yalipo mabehewa used ya Ujerumani!

12. Japo ule mkataba wa EUROWAGON uliovunjwa ulikuwa ni vichwa na mabehewa used, by the time mkataba unavunjwa, hao EUROWAGONS waliisha lipwa malipo ya awali na kuvununua hivyo vichwa na mabehewa 30, ambayo tayari ni mali ya TRC, Watanzania tuna haki ya kuelezwa, hivyo vichwa na mabehewa ya EUROWAGONS, vilinunuliwa wapi, viliundwa lini, wapi?, vimetumika wapi na kwa muda gani kabla TRC hatujauziwa?

13. Watanzania tuelezwe ukweli gharama halisi za manunuzi ya hayo mabehewa mtumba ya Euroeagons kule Ujerumani, kuyasafirisha mpaka Korea Kusini, gharama za ukarabati na naksh naksh na gharama za usafirishaji mpaka yamepokelewa nchini, ili tufanyiwe a comparative analysis, kama tungenunua vichwa na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa na mabehewa used ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua hii mitumba used?

14. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila gharama za maintenance ni ndogo, unaweza kununua kitu used kwa bei poa kumbe ni kitu chakavu sana choka mbaya, hivyo gharama ya maintenance ikawa juu kuliko hata ungenunua kipya!.

15. Ukiingia mkataba wa manunuzi, kwa matengenezo, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.

16. Tulivunja mkataba wa Dowans, wanasheria wetu wakatuhakikishia hatutashitakiwa!, tukashitakiwa!, wanasheria wetu wakatuhakikishia tutashinda!, tukashindwa na tukadaiwa tozo ya Dowans, wanasheria wetu wakatuhakikishia hatutalipa na hawatatufanya lolote!, tena kuna wakajiapisha "over my dead body", hatulipi!.
ukweli ni kwa tumelipa every cent kisiri siri bila Watanzania kuelezwa, bila Bunge kujulishwa na kuidhinisha, bila CAG kudhibiti na kukagua!. Kwanini hatuambiwi ukweli?.

17. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe ile mitambo, waheshimiwa Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo chakavu, mitambo mitumba, na kweli kwa wakati huo hatukuwa na sheria ya kununua mitambo chakavu.

18. Tulivunja mkataba ule wa Dowans kwasababu ya gharama kubwa cha capacity charges na umeme wenyewe!, Mitambo ile Dowans ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans!, kwa capacity charge ile ile!, watu wale wale walio ikataa dowams, ndio hao hao danced to the tune na Hilary Clinton kuzindua Simbion!, kwa mkataba ule ule tuliovunja!, kwa gharama zile zile!, na capacity charge ile ile!, na tukawalipa!.

19. JPM alipoingia tukavunja tena na mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule alipoitwa huku nyuma, sisi hao hao, sio tuu tumelipa!, bali pia tumeinunua ile mitambo ya Simbion kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni chakavu, mtumba, na serikali yetu hatununui, mitambo chakavu, sasa ndio tumeinunua!, sasa mitambo ile ya Simbion ni mitambo yetu, ni mali yetu! na malipo yote yaliisha fanyika chap chap fasta fasta!, bila bajeti yake kuombwa popote!, bila Bunge letu kuijadili, kuipitisha na kuidhinisha, bila CAG kuidhinisha malipo hayo!, na haya yote yamefanyika bila sisi Watanzania kuambiwa!, kwanini vitu vikubwa kama hivi hatuambiwi?.

20. Kichwa chetu kipya cha ukweli na mabehewa yake ni hiki.
Hyundai-Rotem-800.jpg

Kitawasili kutoka Hyundai mwaka 2024.

Hitimisho
Namalizia kwa msisitizo, hakuna ubaya wowote kununua vifaa used na kutumia vitu used!, tena vingine ni vizuri, imara, bora, na madhubuti kuliko hata vipya!, na Watanzania walio wengi, kutokana na low purchasing power due to umasikini uliotopea, wengi wetu affordability yetu ni mitumba kuanzia magari, nguo hadi mitambo, hivyo tumezoea, tunachohitaji ni kuambiwa ukweli tuu!,
Tunacho demand ni kuelezwa ukweli tuu, tusiletewe mitumba hapa tukaelezwa ni mpya!, tukawa tumenunua mitumba kwa bei ya mpya!.

NB. Makala hizi ni free kutumiwa na gazeti, jarida, mtandao wowote, hazina copyright, ila source na mwandishi

Wasalaam
Paskali
 
Nilimsikia bosi wa TRC Kaduguda kwenye UTV(Upendo TV) akithibitisha kuwa vile vichwa mchongoko alivyovikanusha Profesari navyo vimeagizwa, jambo muhimu hapa ni tujitahidi kula kulingana na urefu wa kamba zetu, angalizo, walafi msitumie kamba za chupi zinazovutika.
 
Huo mkataba uliotolewa mwezi June halafu baada ya miezi sita mabehewa tayari, unatakiwa kuchunguzwa kwa makini sana na wahusika walioingia huo mkataba nao wachunguzwe.

Kwa sababu, kama ni kweli kitu cha kutengenezwa kwa miezi 18 kimetengenezwa kwa miezi sita, basi nalazimika kuamini hayo mabehewa sio mapya, inawezekana kabisa wajanja wametununulia mitumba kwa bei ya mabehewa mapya.
 
Duh... sasa mbona Mr PM yeye alituambia hivyo ndio maalum kwa masafa marefu"trains za Kazi"... akasema hata ulaya hivyo ndivyo hutumika kwa umbali mrefu... Waziri wa sekta husika pia akasisitiza huo ndio mzigo tulio agiza...Leo "Mkuu wa Nchi" kama anavyopenda kumwita Mr PM, ametoa version tofauti na Hawa Senior Cabinet Members wake... binafsi nimechanganyikiwa kwa sababu:

1) Historia ya taarifa muhimu kwa Umma anazotoaga Mr PM punde itokeapo sintofahamu ktk jamii

2) Taarifa ya Waziri mwenye DHAMANA inayothibitisha kwamba kilichokuja ndicho tulichoagiza na delivery iko sawa.

3) Taarifa ya Mkuu wa Nchi yenye details muhimu sana ambazo ndizo zilisababisha minong'ono ktk jamii, inayotuambia huu mzigo wa awali ambao umetangulia kuja ni used na tumeagiza ili tuanze kutumia wakati zile OG tulizoziagiza zikiendelea kutengenezwa,ambazo kwa mujibu wa Mama zinakuja nchini ndani ya miezi 8-10 ijayo.

Swali ni je:

-Hii gharama ya kuagiza hizi used ni kiasi gani?

-Je, pia ilikua ndio makubaliano kwenye mkataba kwamba watatanguliza used wakati tunasubiria mpya.

-Je, hizo used tulizoagiza zitaweza kurudisha gharama tulizotumia kuziagiza ndani ya muda huu mchache wa less than 12months ambao ndio waiting time ya our original order (mpya).

-Kama watanzania tumevumilia kusubiria Cranes za Bwawa la Nyerere kwa utulivu na muda mrefu hivi, kwanini tusingeshauriwa tuvumilie miezi hiyo michache mzigo mpya uingie?!
 
Duh... sasa mbona Mr PM yeye alituambia hivyo ndio maalum kwa masafa marefu"trains za Kazi"... akasema hata ulaya hivyo ndivyo hutumika kwa umbali mrefu....
Jibu rasmi Ni la Rais na aliwahi ongea toka 2021 Ni vile mnakuwaga vichwa maji.

Gharama Ni Kama walivyosema na ziko wazi kabisa.

Swala la kurudisha Pesa halitokaa litokee hiyo reli Ni tembo mweupe na itakuwa sawa tuu na atcl kwa hiyo ichukulieni Kama Huduma zingine sio firm ya kuingiza faida.

Huwezi Jenga reli kusiko na mzigo ukategemea faida, haipo
 
Pia sheria ya manunuzi ya umma inaruhu mambo ya used?
Yaani maswali ni mengi kuliko maelezo... How I wish Wanasiasa wangejikita zaidi kwenye maswala ya kupiga siasa majukwaani na wawe wanasubiri kualikwa kwenye uzinduzi.

Hizi issues ambazo ni technical wangekaa Nazo mbali na wawaachie wataalamu waliobobea watuvushe...ila as per now..hadi wataalamu wameanza kuingiwa uoga na wanafanya Kazi za kitaalamu kisiasa zaidi kuliko kufuata uweledi.Tutafeli sana.
 
Kama Bado jamaa anakombora lingine limebaki arushe tena. Hili Moja tu limeleta taharuki Kila Kona watu wanataka kutoa maelezo na kufanya mambo. Shida wanaenda Kwa pupa sana. Na Alisha sema, no retreat, no surrender, yaani hatengui kauli Wala kuomba radhi.
 
Wanabodi,

Hii ni story mwendelezo, anzia hapa Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!

Huu utata kuhusu haya mabehewa 'mapya' ya SGR yaliyowasili nchini hivi karibuni kutokea nchini Korea Kusini, yakiwa mapya kwenye manailoni kabisa, huku yakiwa na muundo wa kizamani, hali iliyopelekea watu kujiuliza, je, ni mapya kweli au ni used yaliyofanyiwa ukarabati na kuwekewa nakshi nakshi, kumbe ulishamalizwa kitambo sana na Rais mwenyewe, Mama Samia Suluhu Hassan, hali iliyopelekea sisi baadhi yenu kuhoji kama tumepigwa tena kama kwenye Rada! Hivyo msiwe na wasiwasi wala msiwe na mashaka kabisa, harujapigwa!

Hebu msikilize mwenyewe Rais Mama Samia,

Kama Mhe. Rais, aliisha zungumza haya, kigugumizi cha nini kuubainisha ukweli huu?

Hii maana yake ni mambo mawili;
1. Kuna vichwa na mabehewa mapya ambayo tumeagiza na tunatengezewa, kwa sababu it will take time, tumeagiza pia vichwa na mabehewa used kwa kuanzia ambayo tumenunua. Hivyo vichwa na mabehewa used ni kutoka nchini Ujerumani.

2. Rais amesema mzigo utakao anza kuwasili ni used. Kwa vile haya yaliyowasili kutoka Korea ya Kusini ni mabehewa 'mapya' kutoka kiwandani, na unapoagiza, unaagiza according to specifications zako, hizo box bodies mnazoziona ndiyo specifications zetu tulizoagiza, hivyo haya ni mabehewa mapya kutoka kiwandani, japo muundo wake ni wa kizamani sana.

3. Ina maana zile vichwa viwili na mabehewa 30 used kutoka Eurowagons ya Uturuki, iliyonunua Ujerumani nao utafika.

4. Kama ni kweli haya mabehewa ni mapya, Tanzania inaweza kuingia kwenye Guiness Book of Record kuwa ni nchi ya kwanza Duniani kuundiwa mabehewa kwa muda mfupi ajabu. Hivyo hiki kiwanda cha Korea, sasa ndiyo kiwanda kinachounda mabehewa kwa haraka zaidi kuliko viwanda vyote duniani.

Mkataba ulitolewa mwezi June, baada ya miezi 6 tuu mabehewa tayari. Standard time ya kuunda behewa ni miezi 18.

Kichwa chetu kipya cha ukweli na mabehewa yake ni hiki.View attachment 2432020
Kitawasili kutoka Hyundai mwaka 2024.

Itaendelea...

Paskali

Acha tuendelee na mapambio tu!
 

Attachments

  • twitter_20221028_162308.mp4
    478.7 KB
Pia sheria ya manunuzi ya umma inaruhusu mambo ya used?
Yes, wakati wa Richmond na Dowans, sheria ilikuwa hairuhusu, hapa kati tulikuja kubadili sheria yetu ya manunuzi ya umma, sasa tunaweza kununua mitambo chakavu.
Ndio maana tumeinunua mitambo ya Simbion, sasa ni mali yetu. Haya mabehewa ni mabehewa chakavu, ila tumeambiwa ni mapya, kazi ya a proper IJ, italimaliza hili jambo!.
P
 
Yes, wakati wa Richmond na Dowans, sheria ilikuwa hairuhusu, hapa kati tulikuja kubadili sheria yetu ya manunuzi ya umma, sasa tunaweza kununua mitambo chakavu.
Ndio maana tumeinunua mitambo ya Simbion, sasa ni mali yetu. Haya mabehewa ni mabehewa chakavu, ila tumeambiwa ni mapya, kazi ya a proper IJ, italimaliza hili jambo!.
P
Yaani Serikali ningewapongeza sana kama wangekusanya Technicians wenye uzoefu mtaani na wale wakali kutoka vyuo vya ufundi hapa nchini VETA, wakawanunulia materials kama rangi za magari zenye standard ya juu, compressors ,nyaya na accessories zake kwa ajili ya kufanya wiring, gadgets za WiFi, welding machines na nyenzo nyingine muhimu za ufundi. Wakawafungulia karakana hapo Dar au Mwanza wakawapatia Yale mabehewa ya TRC na karatasi za nylon kwa ajili ya kuyajaradia baada ya renovations...Vijana wangefanya Equally, na zaidi Kazi nzuri na mpunga wetu mwingi ungebaki hapa na tungeokoa pesa nyingi za kigeni na hiyo tofauti ingekomaza uchumi wetu kwa kiasi japo kidogo, au wachumi wetu wanaamini kukuza uchumi wa nchi ni kuuza kahawa na korosho tuu Ng'ambo!? Binafsi ninaamini matumizi Bora ya resources kidogo uliyonayo pia inaweza kuleta chachu na innovative desires katika kukuza uchumi...sasa tumeagiza chuma chakavu nyingine na wakati tunayo nyingine inaozea kwenye makarakana ya shirika la reli Tanzania...Are we really THINKING DEEP or WE ARE SINKING DEEP!?
 
Wanabodi,

Huu utata kuhusu haya mabehewa 'mapya' ya SGR yaliyowasili nchini hivi karibuni kutokea nchini Korea Kusini, yakiwa mapya kwenye manailoni kabisa, huku yakiwa na muundo wa kizamani,

Wasalaam
Paskali
Mkuu Paskali, umeeleza kwa kirefu sana, na tumekuelewa, ila sasa unajichanganya mwenyewe na unafananua tatizo ambalo silo linalolalamikiwa.

Kitu kinacholalamikiwa na watu sio kwamba wameona mabehewa used ambayo wanadhani yamenunuliwa kwa bei ya mabehewa mapya, bali wameona mabehewa mapya ambayo yana muonekano wa mabehewa used au design ya mwaka 47.

Na inawezekana tatizo ni design ya upakaji rangi tu. TRC wamekosea sana hizo rangi, ziko dull mno! Walipaswa kufanya consultation juu ya rangi sio Bodi ya TRC kuamua.

Kumbuka kwamba mabehewa used hayatakuja kutoka Korea, bali Ujerumani au Uturuki - na sijui kama huo mpango wa mabehewa used bado upo. (by the way, sio policy ya serikali kutonunua vitu used? Tulibadilisha?)

Sasa TRC na viongozi wanajichanganya kwa sababu wanaona sura ya mabehewa mapya kutoka Korea hairidhishi ukichukulia kwamba design na sura za mabehewa kwa karne hii ni tofauti sana na haya tunayopokea toka Korea. Nakiri kwamba kwa ndani yana mwonekano mzuri sana, lakini kwa nje ni design ya kizamani sana. Ni sawa na kutengeneza bodi mpya ya Landrover Station Wagon 109 leo 2022, lakini ndani uiwekee injini na viti vya Land Rover Defender ya 2022 halafu ukamuuzie mtu. Watu watamwambia umepigwa!

Nadhani umeelewa tatizo liko wapi

Watu walitarajia mabehewa kama ngoma hii hapa chini. Unaingia kwenye treni unasema Dreamliner za Magufuli kitu gani bwana!

1669893484734.png
 
Back
Top Bottom