Vichwa 3 na mabehewa 27 yaingia nchini; kuanza kufanyiwa majaribio hivi karibuni

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,123
Serikali imeingiza nchini Mabehewa 27 na vichwa vitatu vya treni kwa ajili ya kuanza majaribio ya SGR.

Ni yapi maoni yako kuhusu kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na JPM? Je, waliolalamika kuwa mabehewa ya awali siyo ya SGR wanakauli gani leo? Hongera Mhe. SSH kwa hatua hii yautekelezaji wa miradi ya kimkakati.
---
Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo December 30,2023 limepokea vichwa vipya vitatu vya treni za umeme vilivyoundwa na kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya abiria yaliyoundwa na kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) kutoka nchini Korea Kusini.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano- TRC, Jamila Mbarouk amesema “Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR, mpaka sasa Shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) ya chini
Korea Kusini”

“Mabehewa matatu yaliyosalia yanatarajiwa kuwasili nchini Februari, 2024 na vichwa 13 vilivyobaki vinatarajiwa kuwasili kwa awamu ambapo vichwa sita vitawasili mwezi Machi na vichwa saba vitawasili April 2024”

“TRC itaanza kupokea seti ya kwanza kati ya seti 10 za treni za Kisasa (EMU) mwezi Machi 2024 Mei seti 2, Juni seti 2, Julai seti 2, Septemba seti 2 na seti ya mwisho mwezi Oktoba 2024”

“Vichwa vilivyopokelewa, kiutendaji vina mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa, mabehewa 27 katika madaraja ya uchumi na biashara, daraja la biashara (Business class) ni mabehewa 13, kila behewa lina wezo wa kubeba abria 45 na mabehewa ya daraja la uchumi ni 14, kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 78 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kumuwezesha abiria kusafiri kwa amani na salama”
 
Serikali imeingiza nchini Mabehewa 27 na vichwa vitatu vya treni kwa ajili ya kuanza majaribio ya SGR.

Ni yapi maoni yako kuhusu kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na JPM? Je, waliolalamika kuwa mabehewa ya awali siyo ya SGR wanakauli gani leo? Hongera Mhe. SSH kwa hatua hii yautekelezaji wa miradi ya kimkakati
Picha ziko wapi sasa
 
Serikali imeingiza nchini Mabehewa 27 na vichwa vitatu vya treni kwa ajili ya kuanza majaribio ya SGR.

Ni yapi maoni yako kuhusu kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na JPM? Je, waliolalamika kuwa mabehewa ya awali siyo ya SGR wanakauli gani leo? Hongera Mhe. SSH kwa hatua hii yautekelezaji wa miradi ya kimkakati
Panapostahili pongezi ni wajibu tupongeze 🙏🙏
Hongera Mhe Rais SSH na kazi iendelee 👍🙏🙏🙏
 
Haya kwa wale mnaotaka picha.

red-wagon-train-free-vector.jpg
 
Mabehewa na vichwa vyote hivyo sahizi vya nini wakati reli yenyewe ni kakipande tu?

Reli hii kukamilika, si chini ya miaka 8 ijayo. Inaonekana vichwa na mabehewa vinaletwa ili vipate kutu.

Kama ni kati ya Dar na Dodoma tu, robo ya vichwa na mabehewa, vingetosha. Miaka 8 ijayo, hayo mabehewa na vichwa vyake, vitakuwa nje ya modern technology.
 
Na hakuna aliyechukuliwa hatua baada ya akina msukuma kujiliza bungeni kama vile kuna kitakalifanyika. Hapo kuna upiganu wa almost bilion 500.
Haki watu wanakula mema ya nchi
Wapambe wanatuambia humu

Kazi iendelee...Mama yuko kazini.

Huko kazini kila siku mama yao anaingizwa mkenge na majizi anaishia tu kusema stupid na hili nalo mkalitizame.
 
Back
Top Bottom