Mkurugenzi TRC: Tutaruhusu Wawekezaji binafsi kwenye Mradi wa SGR kuingiza Vichwa cya Treni na mabehewa yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Md.png
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa Serikali itanatarajia kuweka milango wazi kwa wawekezaji binafsi kuwekeza kwenye mradi wa reli ya kisasa (SGR) kwa kuingiza vichwa vya treini na mabehewa yao.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, leo Machi 25, 2024 kuhusu utendaji wa Shirika ndani ya miaka mitatu Rais Samia Suluhu Hassan tokea alipoingia madarakani, amesema kuwa tayari jitihada kufungua milango kwa sekta binafsi zipo kwenye hatua nzuri.



Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu TRC

Esther Zelamula, Mwakilishi wa Wahariri
Amesema kuwa tayari Bunge limepitisha Sheria ambayo itaenda kuweka milango wazi kwa sekta binafsi kuwekeza kwenye mradi wa SGR, ambapo amebainisha wazi kuwa Sheria hiyo tayari imesainiwa na Rais Samia.

Ameongeza kuwa katika mchakato wa kuruhusu uwekezaji binafsi tayari Serikali pia ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha kanuni na taratibu nyingine ambazo zitakuwa zikiratibu suala hilo.

Ambapo amesema kuwa kufikia Mwezi Mei 2024 tayari utaratibu huo unaweza kuwa umekamilika na kuwekwa wazi kwa ajili ya sekta binafsi kuanza kubisha hodi.

"Tunakaribisha sekta binafsi sio tu kuwa na mabehewa kama walivyo wengine tutaruhusu pia kuwa na vichwa vya treini, Mtu anaweza kuwa na mabehewa yake TRC tukazungumza nae namna ya kufanya tukafanya, lakini Mtu anaruhusiwa kuwa na mbehewa yake na kichwa cha treini"amesema Kadogosa

Amesema kuwa utaratibu wa sekta binafsi kuruhusiwa kuweka mabehewa umekuwepo kwenye treini nyingine ambapo amesema wapo wawekezaji ambao walitumia fursa hiyo.


Jamila Mabarouk, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC
Tsh. Trilioni 23.3 zimetumika kwenye ujenzi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema mpaka sasa Serikali imetumia Trilioni 23.3 katika mradi wa treni ya kisasa (SGR), ambapo kati ya hizo Tirioni 10 tayari zimelipwa katika michakato mbalimbali ambayo ni endelevu.

Kutokana na malipo hayo amedai kuwa mpaka sasa Serikali aidaiwi na mkandarasi yoyote kwenye kazi ambazo tayari zimefanyika.

Alipoulizwa swali kuhusu suala la baadhi wafanyakazi kuweka migomo kwa nyakati tofauti amesema "Hivyo ni vitu vya kawaida ambavyo tumekuwa tukikumbana navyo kwenye mradi wetu na kimsimgi tunavimaliza"

Amesema kuwa kuna maeneo ambayo wamekuwa wakipunguza wafanyakazi kutokana na mradi kukamilika kwa asilimia kubwa, ambapo amedai kuwa kuna wakati Mtu anaweza kufukuzwa akaenda asikute pesa zake NSSF, amesema katika mazingira hayo hawawezi kukubali badala yake wanasimamia haki.

"Na sisi kama TRC tunasema huwezi kuwaondoa watu, isipokuwa umewalipa haki yao na ndivyo Sheria zetu za Nchi zinavyosema" amesema Kadogosa.

Ambapo amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kwenye maeneo mbalimbali kulingana hatua zinazoendelea itasaidia kuchochea fursa za kiuchumi kwa watanzania hususani kupitia usafirishaji wa mizigo suala ambalo amesema kuwa wanalitazama kwa jicho la tatu kuingiza mapato zaidi ikilinganishwa na abiria ambao watatumia usafiri huo kama huduma.
 
Back
Top Bottom