Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,903
- 945
TRC YAPOKEA VICHWA 3 VYA TRENI YA UMEME SGR KUTOKA KOREA KUSINI
Shirika la Reli Tanzania limepokea vichwa vipya vitatu (3) vya treni za umeme vilivyoundwa na kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya abiria yaliyoundwa na kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) kutoka nchini Korea Kusini.
Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria kwa ajili ya undeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR.
Mpaka sasa Shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne (4) kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) ya nchini Korea Kusini.
Mabehewa matatu (3) yaliyosalia yanatarajiwa kuwasili chini Februari, 2024. Vichwa 13 vilivyobaki vinatarajiwa kuwasili kwa awamu kama ifuatavyo, vichwa sita (6) vitawasili mwezi Machi na vichwa saba (7) vitawasili Aprili, 2024.