Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,832
Oxfam imesema matajiri wanne nchini Kenya, utajiri wao unazidi karibu nusu ya wakenya wote(40%) wakichanganywa kwa pamoja. Matajiri hao wana utajiri unaofikia Ksh. bilioni 333( Tsh. trilioni 6.26).
Utafiti unaonesha ukuaji wa tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho ambapo wakenya 130 matajiri zaidi wanamiliki mali sawa na 70% bajeti ya Kenya kwa mwaka. Matajiri watano zaidi nchini Kenya ni Merali, Shah, Bedi, Kenyatta na Mahendra wakiwa na utajiri wa jumla ya dola za kimarekani 3.2.
Duniani, watu walijizalishia mifukoni $ trilioni 42 miaka miwili iliyopita, asilimia moja ya watu duniani wamechukua 2/3 ya utajiri huo huku 99% ya watu wakigombania 1/3 iliyobaki. Kwa mara ya kwanza katika miaka 25 utajiri wa kutisha na umasikini wa kutisha vimeongezeka kwa pamoja.
Hali ya watanzania ikoje kwenye dunia hii ya kibepari!
Pia, jisomee HAPA