Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,131
- 35,167
Kituko kikubwa cha karne kuhusu hesabu leo kimeonekana huko Kenya baada ya makamishina wanne wa tume ya uchaguzi waliotangaza kujitoa kwenye mchakato wa kutangaza matokeo ya urais kuja na hoja finyu za ukilaza wa mahesabu.
Mbali na sababu zingine walizozitoa, kubwa lilikuwa ni wao kujenga hoja kwenye mahesabu ya matokeo kwenye mambo mawili.
-Wao kushangaa hesabu ya jumla ya kura zilizovutwa (round off) kuwa 100.01% (Kitu ambacho kimahesabu kiko sahihi)
-Kudai kuwa hiyo 0.01% iliyozidi wao wanaitafsiri katika kura zote (milioni 14) ni sawa na kura 140,000. (Kitu ambacho sio sahihi, usahihi ni kura 1400)
Ajabu ni kuwa, wahusika waliojenga hoja hizo walijitamba kuwa wao ni wasomi na karibu kila mtu kwa Kenya ni msomi wa kuweza kuchambua hayo mahesabu. Na mwisho hoja zao zikachukuliwa na kupigiwa debe na mamilioni ya wakenya wanaomuunga mkono upande wa Raila Odinga.
Hizo hesabu za desimali na makadirio huwa zinazofundishwa watoto wa darasa la nne hapa Tanzania na nyingine kurejewa kwa kina kidato cha kwanza.
Ni aibu kubwa kwa taifa la Kenya, ukilaza unaposhabikiwa na kuungwa mkono.
Poleni Wakenya kwa hii aibu.