Mbona orodha ya matajiri Tanzania, Kenya, Uganda wengi ni Waarabu na Wahindi na si waafrika weusi?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Ukiangia orodha ya watu matajiri Nchini Kenya na Tanzania utakuta Wahindi na Waarabu ndio wanaongoza kwa mali na utajiri

Cheki orodha ya watu matajiri nchini Kenya hapo chini.
1. Vimal Shah: He is the Chairman of Bidco Africa, a leading consumer goods company in Kenya.

2. Narendra Raval: Known as "Guru," he is the Chairman of Devki Group, a conglomerate with interests in steel, cement, and related industries.

3. S. K. Macharia: He is the founder and chairman of Royal Media Services, a prominent media company in Kenya.

4. Uhuru Kenyatta: He served as the President of Kenya from 2013 to 2022. His wealth comes from various business interests, including large land holdings.

5. Naushad Merali: He is a Kenyan businessman and the founder of the Sameer Group, which has interests in various industries, including agriculture and real estate.

Tizama pia list ya matajiri kutoka Tanzania.
1. Mohammed Dewji: Mohammed Dewji, often referred to as "Mo," was one of the wealthiest individuals in Tanzania. He was the former CEO of the MeTL Group, a diversified conglomerate with interests in manufacturing, agriculture, and real estate. Please note that his net worth and status may have changed since my last update.

2. Reginald Mengi (1944-2019): Reginald Mengi was a Tanzanian media mogul and business tycoon. He was the founder of IPP Media Group, one of Tanzania's largest media companies.

3. Said Salim Bakhresa: Said Salim Bakhresa is the founder and chairman of the Bakhresa Group, a prominent Tanzanian conglomerate with interests in industries such as manufacturing, agribusiness, and hospitality.

4. Rostam Aziz: Rostam Aziz is a Tanzanian businessman with investments in various sectors, including telecommunications, manufacturing, and real estate.

5. Ally Awadh: Ally Awadh is a Tanzanian entrepreneur and the founder of Lake Oil Group, a company involved in oil and gas trading.
Na hapo kwenye list ya Tanzania ni kwa bahati mbaya tu Reginald Mengi naye alifariki hivyo orodha kubaki na Wahindi na waarabu watupu.

Uganda nayo list ndio kama ifuatavyo
1. Sudhir Ruparelia: Sudhir Ruparelia is a prominent businessman in Uganda and the founder of the Ruparelia Group, which has interests in real estate, banking, hospitality, and education.

2. Patrick Bitature: Patrick Bitature is a Ugandan entrepreneur with investments in various sectors, including telecommunications, energy, and hospitality.

3. Karim Hirji: Karim Hirji is a Ugandan businessman and the founder of the Karimjee Jivanjee Group, which is involved in textiles and other industries.

4. Mohammed Hamid: Mohammed Hamid is the founder of Aya Group, a company with interests in real estate, construction, and other sectors.

5. Alykhan Kharmali: Alykhan Kharmali is involved in various business ventures in Uganda, including real estate and hospitality.

Ukitizama hizo Top Five yote orodha utaikuta wengi ni Wahindi na Waarabu, na waafrika weusi ni mmoja mmoja.

SWALI: Hivi waafrika weusi wa Kenya, Uganda, Tanzania tunafeli wapi.... Wanakuja waarabu na wahindi wanawekeza kwetu wakishapata pesa za kutosha wananunua uraia hili wasiporwe mali zao. Wazawa kwenye orodha ya Utajiri tumebaki kutoleana macho tukisifia Wahindi na Waarabu kwa kuwekeza kwetu, hawamu inayofuata watakuwa wachina.

Wazungu hawawezi kuwekeza kwa sababu ya hile hali ya kuwatafsiri kama mabeberu au wakoloni, hivyo mara nyingi ulazimika kuoa mke au kupata business partner wa kitanzania hili biashara ziende. Hila hawa Waarabu na Wahindi kwa sababu hawatafsiriwi kama mabeberu na wakoloni wamekuwa wakiteka maeneo, na kuanzisha mambo kadha wa kadha bila vizuizi na wakifanikisha basi wachache kwenye familia inabidi wabadili uraia kuwa watanzania hili mali ziendelee kubaki mikononi mwao, ikumbukwe kwa sheria za Tanzania haziruhusu raia mgeni kumilki ardhi, labda aoe mke wa kitanzania ambaye ndio atatumika kumiliki ardhi au abadilishe uraia, wazungu wamekuwa wakitumia hii ya kuoa, huku waarabu na wahindi wamekuwa wakitumia hii ya mmoja kwenye familia yao kubadili uraia hili kupata kibali cha umiliki wa mali na ardhi.

Wanaijeria kidogo wao ndio wanatamba kwenye ardhi yao, ni ngumu sana kumkuta muarabu au muhindi kwenye list ya matajiri huko Nigeria, South Africa wao wazungu na Wahindi ndio wanakimbiza kwa utajiri huko kwao.

Waafrika mashariki tunafeli wapi mpaka wahindi na waarabu wanatamba kwenye ardhi yetu kwa rasilimali zetu? Nini kifanyike kuweza kuongeza orodha ya matajiri wenye asili ya kitanzania kwenye orodha yetu kama Reginald Mengi?
 
Halafu wote hao, hakuna anayejitapa kwenye social media kwamba pesa anayo.
Sisi weusi ni matajiri wa kujitangaza mitandaoni tu.
Hizo kabila za weupe, wana utamaduni wa kushirikishana kwenye biashara. Biashara alianzisha babu, mjukuu bado ana ziendeleza kwa mafanikio.
kwetu utashirikishwa kwenye biashara baada ya baba/babu kufariki. na kabla ujaijua vizuri biashara na yenyewe inafariki.
 
Alafu kitu kingine, hata kama kwenu zipo utaambiwa katafute za kwako... Kupelekea watu Wengi kwenda kuanza maangaiko upya kujiinua, huku vya nyumbani ulivyokatazwa vikifa...

Ilitakiwa kama Baba ana mashamba makubwa watoto mkasomee kilimo cha biashara.

Kuliko unaambiwa kajitegemee, Mwishowe wote mnajazana Kariakoo
 
Sisi weusi tuna kasumba mboovu, kwanza hatupendani, wabinafsi, mafanikio kidogo mnaanza kuwangiana.

Mzee mwenye mali hasogezi watoto karibu, atakomaa, akili itachoka mwishowe ataishia kufilisika.
Wenzetu biashara za babu mpaka mjukuu inamkuta.
 
Mkoloni aliwaandaa,kumbuka wao walikuwa second class michongo
Mingi walikuwa wanapewa na kuelimishwa

Ova
Kwahiyo mkoloni ndiye aliyewauzia mali za serikali kama viwanda, mashamba Kwa Bei ya kutupwa

Au unamaanisha mkoloni mweusi, watu wenye asili ya Asia walikuja Afrika mashariki na mitaji ya kawaida tu wengine tukawafirisi kwenye azimio la Arusha na wengine Bado wanapambana Kwa biashara za kati.

Ila Hawa wafanyabiashara wakubwa wametajirika kupitia udhaifu wetu na ujinga wa viongozi wetu
 
Mkoloni aliwaandaa,kumbuka wao walikuwa second class michongo
Mingi walikuwa wanapewa na kuelimishwa

Ova
Mzee wa Kino sababu yako ina mashiko ila siikubali 100%. Mwaka 1967 tuliwanyang'anya matajiri hasa wahindi mali zao na kuzitaifisha lakini miaka zaidi ya 50 baadae bado wapo wanaongoza uchumi wetu... miaka ya Sokoine pia watu walifilisiwa lakini hakuna matokeo yoyote yaliyopatikana. Baadae ndo haohao tuliowanyang'anya mali zao tukaanza kuwauzia mali zetu kwa bei ya kutupwa kwa kile kinachoitwa ubinafsishaji. Huwa ninawaambia watu matatizo yetu yameanzia mbali sana tangu enzi za mababu zetu. Jiulize wakati mababu wa kizungu wanaijenga Eiffel Tower pale Paris mwaka 1905, babu zetu walikuwa wanafanya nini? Mzee wa Kino bado tuna shughuli pevu sana kujikomboa. Kuna wapuuzi watasema tatizo ni CCM bila kukumbuka kwamba hata hao wapinzani hawajawahi kuja na suluhisho nini kifanyike zaidi ya kulalamika. Sasa hivi kuna crisis ya dola ila sijasikia mpinzani akitoa suggestion ya kitaalamu zaidi ya kulalamika.
 
Kwahiyo mkoloni ndiye aliyewauzia mali za serikali kama viwanda, mashamba Kwa Bei ya kutupwa

Au unamaanisha mkoloni mweusi, watu wenye asili ya Asia walikuja Afrika mashariki na mitaji ya kawaida tu wengine tukawafirisi kwenye azimio la Arusha na wengine Bado wanapambana Kwa biashara za kati.

Ila Hawa wafanyabiashara wakubwa wametajirika kupitia udhaifu wetu na ujinga wa viongozi wetu
Nakubaliana na wewe ofisaa... Na itikadi zote za sera za Ujamaa bado wanakuja wageni na kutajirikia kwetu, huku wenyeji tukibaki maskini... Sera za Ujamaa ilitakiwa Raia ndio wawe matajiri, maana kila kinachopatikana kilitakiwa kwenda kwa raia. Wageni hawakutakiwa kutusua kwenye sera hizi za ujamaa
 
Mzee wa Kino sababu yako ina mashiko ila siikubali 100%. Mwaka 1967 tuliwanyang'anya matajiri hasa wahindi mali zao na kuzitaifisha lakini miaka zaidi ya 50 baadae bado wapo wanaongoza uchumi wetu... miaka ya Sokoine pia watu walifilisiwa lakini hakuna matokeo yoyote yaliyopatikana. Baadae ndo haohao tuliowanyang'anya mali zao tukaanza kuwauzia mali zetu kwa bei ya kutupwa kwa kile kinachoitwa ubinafsishaji. Huwa ninawaambia watu matatizo yetu yameanzia mbali sana tangu enzi za mababu zetu. Jiulize wakati mababu wa kizungu wanaijenga Eiffel Tower pale Paris mwaka 1905, babu zetu walikuwa wanafanya nini? Mzee wa Kino bado tuna shughuli pevu sana kujikomboa. Kuna wapuuzi watasema tatizo ni CCM bila kukumbuka kwamba hata hao wapinzani hawajawahi kuja na suluhisho nini kifanyike zaidi ya kulalamika. Sasa hivi kuna crisis ya dola ila sijasikia mpinzani akitoa suggestion ya kitaalamu zaidi ya kulalamika.
Walituzidi akili na mipango
Sisi tulijuwa tukiwanyanganya
Tutaweza kuendesha,lakini mwishowe
Ikawa ndivyo sivyo

Ova
 
Kuna wapuuzi watasema tatizo ni CCM bila kukumbuka kwamba hata hao wapinzani hawajawahi kuja na suluhisho nini kifanyike zaidi ya kulalamika.
Sasa mpinzani hawezi kukupa mbinu kwa sababu anajua utatumia hizo mbinu kuendelea kubaki madarakani... Ingekuwa hivyo vyama pinzani vinatoa mbinu za suluhisho kwenye chama cha madaraki, basi vyama vingi vingedumu madarakani toka enzi na enzi.

CCM hata wakipewa suluhisho, hawawezi kutoa credit kwa vyama pinzani. Na vyama pinzani wanaona bora wabaki na suluhisho zao
 
Kwahiyo mkoloni ndiye aliyewauzia mali za serikali kama viwanda, mashamba Kwa Bei ya kutupwa

Au unamaanisha mkoloni mweusi, watu wenye asili ya Asia walikuja Afrika mashariki na mitaji ya kawaida tu wengine tukawafirisi kwenye azimio la Arusha na wengine Bado wanapambana Kwa biashara za kati.

Ila Hawa wafanyabiashara wakubwa wametajirika kupitia udhaifu wetu na ujinga wa viongozi wetu
Sisi tulichelewa kujuwa mambo kadhaa wa kadhaa mkuu
Sisi wenyewe kwa wenyewe tulibaniana vitu vingi kuanzia elimu nk

Ova
 
Back
Top Bottom