Raia wa Kenya ni masikini kuliko Watanzania

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
251
638
Watu wasinielewe vibaya, kuna utofauti kati ya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja. Majirani zetu wakenya wametuzidi uchumi wa nchi. Hali ya uchumi katika nchi yao ipo juu kushinda yetu, ndo maana hata pesa yao ina thamani kuliko yetu.

Lakini uchumi wa mtu mmoja mmoja asikudanganye mtu ndugu zetu wana hali mbaya sana. Ukiwa na Millioni 30 ya Tanzania ukaenda Kenya wewe ni tajiri sana.

Kumbuka TZS 30,000,000 kwa ni sawa na Milioni 1 na laki 7 na ushee ya Kenya. Kwa Kenya inaonekana ni pesa ndogo ee? Bro hiyo Millioni 1.7 hukuti Mkenya yuko nayo.

Matajiri wa Kenya wengi viongozi wa serikali. Angalia orodha ya matajiri 10 Africa kama utakuta Mkenya hata mmoja, angalia orodha ya matajiri 100 ukimkuta Mkenya basi lazima ni kiongozi.

Wakenya wengi wanaishi chini ya dolla moja, pesa yao kuipata ni kazi. Mwezi uliopita nilikuwa huko nimejionea kwa macho yangu. Kule maisha ni magumu pamoja na pesa yao kuwa kubwa.

Nawasilisha
 
Ni upuuuzi uliotukuka kujilinganisha n Kenya muda wooooooote.

Kenya wana pesa n mzunguko wao wa pesa ni mkubwa kuliko kwetu. Kenya walishajenga miundombinu n mazingira rafiki kuvutia wawekezaji wa kubwa wa kubwa kutoka pande zote za dunia, sisi ndio kwanzaa tunaanza. Kwa ufupi wa Kenya wapo mbali sana kiuchumi.

Ni aibu kujilinganisha n Kenya ukizingatia wa tanzania tuliiona fly over ya kwanza kwenye ardhi yetu nadhani 2017, mfugale fly over ilhali Kenya iliviona vyote tangu 2008-11. Ndio kwanzaa tumeanza kujenga kibaha highway yetu ilhali Kenya sasa walijenga yao enzi za kibaki.

Kwa ufupi Kenya wapo mbali sana kujilinganisha nao. Ila hili halimaanishi sisi pia tupo nyuma kwenye kila idara. Sifa n moja ya Tanzania ni wananchi wake wenye mioyo ya dhahabu. Wakenya ni makatili sana. Mtu akionekana anaiba kariakoo, 70% ukiskia 'mwizii basi kafa.

Kenya kila mtu ajitegemee. Kuibiwa mchanaaa mbele ya watu ni kawaida. Ukikutana n mtu sehemu yenye kiza Kenya basi ni lazima ujiandae kwa lolote maana watu usiku hawaaminiki.

Pia, pongezi kwa viongozi wetu kwa kutujengea kutujengea infrastructure za kisasa*barabara nadhifu ijapokuwa chache, stendi za mabasi zenye hadhi ya kimataifa kama gerezani, mbezi, mawasiliano nk vitu ambavyo Kenya hawana bus stands, zilizopo kipindi cha masika hazitofautiani na soko la mabibo, matope hatari~ country bus opposite *muthura Market, ile stand yenye iko besides TUK, penye magari za ongata n kite hukuwa.

Classic electric SGR. Tanzania tuna serekali ya kidikteta ambayo inatujali wananchi wake ukilinganisha na wakenya wanaoongozwa na magaidi ambao ukikaa mbele yao, kufa ni pap tu tofauti n sisi serikali yetu inawauwa mahasimu wake kwa ustaarabu kidogo, wachache sana.

Tanzania tuna mapolisi wakarimu, akiuwa wananchi anafungwa, Kenya polisi akinyooshea bunduki lala chini, ukikimbia marehemu. Kenya ugaidi umekithiri, sio kiivyo ila afadhali Tanzania majambazi tu wanajitafutia riziki.

Kwa ufupi Kenya ipo mbali sana kiuchumi. Sisi kimaisha tupo mbaali sana maana ijapokuwa tunapolekeshwa zoblezoble, ina wananchi wake tuna raha n unaishi kwa amani.

So nchi zote zima raha zake na shida zake. Kenya kwa starehe wapo next level, clubs zimejaa kubwa kubwa kama nyumba za wageni zilivyojaa Sinza, hadhi kulingana n mfuko wako. Ni vitu vichache ila ni uhalisia mtupu.
 
Watu wanakujibu bila kuelewa. Unachokisema ni kweli. Nchi yoyote ya kibepari mara nyingi kupata nafasi ya kutoboa ni kazi sana. Utaishia kuwa mfanyakazi wa hao matajiri.

Kenya wana MOPOLISTIC POWER yaani biashara ya wakubwa isiyoruhusu biashara ndogo kushamiri. Kwa muda wote hakuna aliyekuwa anapata kibali cha kuuza maziwa isipokuwa kampuni ya BROOKESIDE.

Kampuni ya Uhuru.
Matokeo yake walikuwa wananunua maziwa ya wakulima kwa bei waliyoitaka wao.

Pamoja na kwamba Kibera ni SLAMS lakini hizo SLAMS zinamilikiwa na kina Odinga. Ukichelewa kulipa kodi unatolewa kama mbwa.

Kupata ardhi ni shida kuliko kitu chochote.

Wakenya wanakula sana ugali. Unga wananunua supermarket. Kwenye mifuko ya kaki. Unga huo unatengenezwa na makampuni makubwa ya matajiri ambao wanasaga na kupeleka supermarkets.

Msagaji mdogo hana nafasi ya kupeleka mifuko yake supermarket. Hawezi kupewa nafasi ya kuweka.

Ndio maana maskini ni maskini kweli. Na tajiri ni matajiri kweli
 
Watu wasinielewe vibaya, kuna utofauti kati ya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja. Majirani zetu wakenya wametuzidi uchumi wa nchi. Hali ya uchumi katika nchi yao ipo juu kushinda yetu, ndo maana hata pesa yao ina thamani kuliko yetu...
Kila nchi Kuna masikini na matajiri
 
Watu wasinielewe vibaya, kuna utofauti kati ya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja. Majirani zetu wakenya wametuzidi uchumi wa nchi. Hali ya uchumi katika nchi yao ipo juu kushinda yetu, ndo maana hata pesa yao ina thamani kuliko yetu...
Kanda ya ziwa mambo Bado sana
 
Watu wasinielewe vibaya, kuna utofauti kati ya uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja. Majirani zetu wakenya wametuzidi uchumi wa nchi. Hali ya uchumi katika nchi yao ipo juu kushinda yetu, ndo maana hata pesa yao ina thamani kuliko yetu...
Subiri wakenya waje wakushambulie
 
Mbaya zaidi ukiwakuta mtandaoni wanavyojitutumua sasa utachoka....ila kwa Africa Tanzania mwananchi wa kawaida ana maisha mazuri kuliko nchi nyingi.
Japo sijafika huko Tanzania yetu watu wamechoka Sana kimaisha unahabari watanzania wengi wanampigia simu mganga mkuu hospital dodoma kutaka kuuza figo habari hii nimepata huko gazeti la mwananchi
 
Back
Top Bottom