Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,842
- 3,616
'Ndagu' nyingi zinazotangazwa na FM radios za Mbeya ni za feki. Hao waganga wanatafuta pesa kuwa ule utaratibu wa 'wajinga ndio waliwao'Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.
Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.
Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k
Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.