Utajiri wa masharti ni mateso

Utajiri wa masharti ni mateso

Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.

Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.

Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k

Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.
Kwa masharti hayo tuu, kama kwel unakua pesa mbona mepes, jmn umaskini ni mbaya askwambie MTU,..
Yani unafata mashart bila ht kuagizwa na mgang, mfn hull nyama, huvai vizur ,hulali pazur nk
 
Mambo mengine bhana... ila nimecheka vitu viwili humu, kwanza ni "usinye choo cha nyumbani" na pili ni comment namba 35 na 38
 
Ngalikihinja,
Usipoishi propprtional na hela zako, hasa kama una hela halafu unaishi kama huna hela, lazima uonekane mchawi....

Hii kauli umeiweka too general unless if your target audience is Africa, kama umefika nchini Marekani kuna mji unaitwa Silicon Valley unapatikana kusini mwa eneo la San Francisco ktk jimbo la California. Huku ndiko kiini cha ugunduzi na teknolojia, ni kawaida kabisa kukutana na mtu mwenye ukwasi wenye thamani zaidi ya trilioni 10 za ki-Tanzania na anatembea kavaa flip flops, kaptura na plain t-shirt kwenda ofisini kwake kwa mfano kuna watu wanaitwa Jack Dorsey na mwenzie Biz Stone ukikutana nao mtaani utadhani wahuni wa mtaani kumbe ndo wagunduzi na watendaji wakuu wa mtandao wa Twitter . Pia kuna mtu anaitwa Gabe Newell huyu naye ni mtu mzito sana ni mwanzilishi wa kampuni ya Valve inayotengeneza video games ukikutana nae utadhani ni maskini yeye anaishi mji wa Bellevue, jiji la Waashington.

Hoja yangu hapa ni kwamba watu wenye ukwasi mkubwa wengi wao hawanaga flashy lifestyle unless labda wawe new money yaani umeupata ukwasi huna kipindi kirefu au wewe ni mtu wa sanaa au kipaji kama mpira au mwanasiasa mwizi mwizi ndo utaishi Maisha ya mbwembwe to maintain your status and fame. Matajiri walio wengi wanaishi Maisha ya kawaida as long as unapata mahitaji ya msingi huna haja ya kujionyesha kama shughuli zako hazikuhitaji kujionyesha nunua gari ambalo ni practical kukutoa mahala A kwenda mahala B labda kama wewe ni mtu unayependa magari same applies to house sio lazima uwe na lijumba kubwa kisa una pesa hata kama hulihitaji.

Tafuta kitabu kinaitwa The millionaire Next Door kimeandikwa na Thomas J. Stanley na mwenzake William D. Danko. Utashangazwa sana na watu wanavyoweza kutengeneza ukwasi mkubwa kwa ku-avoid the high life na kuwa more practical Zaidi ili kukwepa expenses zisizo za lazima ambazo zitakufanya uwe ktk endless consumption treadmill.
Kaka naomba kitabu mkuu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Masharti ya;
Kulala chini freshi... ni mazoezi
Kula chukuchuku poa... ni nzuri kiafya
Kula michemsho tu shega... ni balanced diet
Kuvaa na kujiweka simple gudi tu... ni kubana matumizi
Kufanya lolote barida tu... ilimradi halihatarishi uhai wangu na wanaonizunguka

Lakini masharti ya;
Kuua wenzako bila sababu big NO... nitakosa furaha daima
Kufuga vitu vya ajabu ajabu mfano majoka laa... nitauwawa nayo bure
Kutoa makafara hapana... siku nitatolewa mimi
Kuvaa hirizi sikubali... ni uchizi wa walio wazima
Kuvunja amri za kijamii mfano kumzini mzazi hapana... bora nife kapuku
 
Maneno mengi mliyo yaandika humu, ni ya kufikirika na pia yamekaa kimapokeo zaidi.

Ila ukweli ni kwamba, siri kuu ya utajiri ni nidhamu ya fedha na kujituma, na pia mikopo ya benki kwa wafanyabiashara.

Mfano huyo Makambako nasikia anakopesheka benk mpaka kiasi cha bilions pesa za Kitanzania! Atashindwa kweli kupiga hatua!! Na tayari biashara ameshakuwa nazo kitambo!!

Ukiamini katika uchawi, kamwe huji kuendelea! Uchawi ni imani tu. Binafsi siamini hata kama una exist!! Ingawa natokea Tanga kunani (kwenye vifuu vinavyo ongea eti!!! Uongo huu!!!)
Mkuu endelea kuamini hivyo hivyo ila kuna mambo ukija kukutana nayo utabadili mawazo. Usiyoyafahamu ni mengi kuliko unayoyajua.
 
Waganga ni watu wajanja sana. Kwa masharti hayo umakuwa unabana matumizi ya fedha uliyonayo na itabaki kwenye mzunguko wa biashara tu. Utakosaje kuwa na pesa nyingi wakati unazalisha sana unakula kidogo. Tufunguke akili
Kuna mwanamke mmoja alikua anagombana na mume wake kila siku. Mwanamke akaenda kwa mganga na mganga akagundua kuwa Yule mwanamke anaongeaga sana na ndio chimbuko la ugomvi. Mganga akampa vimawe 2 akamwambia mumeo akiingia tu viweke hivi vimawe mdomoni halafu weka maji mengi mdomoni. Hayo maji usiyateme Wala usiyameze ukiwa mbele ya mumeo. Logic ya mganga Ni kwamba kwasababu Yule mama atakua na maji mdomoni inamaana hawezi kuongea na kumkorofisha mumewe. Kweli kila mume akiwapo karibu na mkewe, mama Ni bubu. Ugomvi wa Mara kwa Mara uliisha, jamaa kazidisha mapenzi kwa mkewe ambae kawa Kama bubu na mganga alifaidi pesa za bure na mengine ziwezi kuyasema hapa maana mume anaweza kusoma hii posti
 
Itoshe tu kusema kaka mganga alitunukiwa kibox manyoya.
 
Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.

Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.

Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k

Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.
Majungu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Attachments

  • IMG-20210201-WA0002.jpg
    IMG-20210201-WA0002.jpg
    37.4 KB · Views: 22
Nilishamtukana mlinzi mmoja wa Hotel nzuri sana pale Makambako baada ya kuchelea kufunguan gate ...Mlinzi hakujibu kitu akawa mnyenyekevu tukaingiza gari ....

Wakati wa dinner akaja Manager kuuliza if we're ok!! tukasema tupo sawa ila position ya Mlinzi waiangalie maana yupo slow saana...

Manager akaonyesha sura ya mshangao kidogo kisha akatabasamu akaondoka..

Akaja Mhudumu tukamuuza kuhusu mlinzi aktuambia ndiye owner wa Hotel na ndiyo anapenda kazi hiyo...hataki kuajiri mtu anafanya yeye

Loooh; tukabaki midomo wazi
Hapo ulijiona fala kumtukana tajiri
 
Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.

Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.

Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k

Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.
Mbona masharti hayo Ni mazuri
Usitembee na mchepuko ...hii inakulinda wewe dhidi ya magonjwa.
Uvae open shoes. Hii inashauriwa hata na daktari...
Usinye choo Cha chumbani... Hii Ni kuepuka kumuudhi wife akiwa ametulia ndani....
Mwanga Lutila ongea jingine.
 
Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.

Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.

Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k

Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.
Hizi huwa ni imani za wasio na kitu,mafukara,waliopigika na maisha,watu wanachapa kazi,Kuna jamaa wanamkwanja mrefu Songwe,nikiwa hapo,nikasikia huyu anatembea na mama yake mzazi,Yule katoa kafara ndugu yake,kuchunguza,ahaa wapi,jamaa Wana mashamba makubwa ya kahawa,wame hustle muda mrefu sana,sasa hv wanamiriki mahotel,mwingine ana maduka ya nguo,na flem kibao za kukodisha,wengine walikuwa watumishi wa benk,wakaacha kazi wakafungua hotel maarufu sana Songwe,sasa hv Wana nyumba kadhaa za kulala wageni.hakuna uchawi,tafuta chapaa,
Mi hapo nje nimepaki V8 new model,hakuna uchawi ni kazi tu.
 
Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.

Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.

Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k

Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.
Kama wewe ni mtu timamu na unawaza hivo nakupa pole sana umechelewa.still unawaza ndagu
 
Hakuna uchawi hapo bali wana masharti ya kubana matumizi tu.
Ukishabana matumizi unakuwa na akiba kubwa kwa hiyo utakuza mtaji katika biashara husika au kuwekeza zaidi.
Acha michepuko
Acha matumizi ya anasa
Acha pombe
Kwa nini usipate muda wa kutosha kusimamia biashara na fedha za kuweka akiba na kuwekeza.
 
Siyo kwa chuki...naishi Uchagani, vichaa ni wengi Sana tena wale anaoishi majumbani (anayeifhamu vizuri tarafa ya Mkuu-Rombo) naweza kumtajia familia hadi familia, sijui kisa au chanzo ni nini....Mungu tusaidie
 
Back
Top Bottom