Utajiri wa masharti ni mateso

Utajiri wa masharti ni mateso

Kuna kijana mmoja Dsm amekosa amani na furaha moyoni ingawa ana hela ya kufa mtu.

Utajiri wake aliupata kwa mganga
Alipokwenda kuomba dawa aliambiwa atoe kafara mojawapo kati ya mama yake au kizazi chake. Akaamua kutoa kizazi chake(kwamba hataweza kumpatia mimba mwanamke yeyote maishani)

Ni kweli akawa tajiri mkubwa tu, akaoa na maisha yakawa safi kwa kitambo kidogo.

Lakini miaka kadhaa ikapita bila mkewe kupata mimba (hata kupata miscarriage tu)

Ndugu wa kijana wakaanza kumsimanga mkewe na kumtaka jamaa aoe mke mwingine(ingawa ni mkristo)

Mambo yalipomzidia yule kijana ikambidi amwambie mkewe A to Z sababu ya wao kutopata mtoto. Wakakubaliana kuwa mdogo wa mume awasaidie kupata mtoto ili kuilinda ndoa yao. (Ndugu wengine hawakujuzwa jambo hili)

Mdogo mtu akakubali, mke akapata mtoto.

Mtoto wa kwanza alipokuwa, mdogo mtu akapiga game tena. Wakapata mtoto wa pili.

Hapo shida ndipo ilipoanza. Mke akaanza kumpenda zaidi mdogo mtu.
Mdogo mtu naye akaanza kiburi na jeuri kwa kaka yake. Akaanza kudai watoto wake na kutaka jambo hili liwe wazi kwa kila ndugu.

Sijui walimalizana vipi lkn jamaa mali anazo ila hana amani moyoni.
 
Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.

Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.

Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k

Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.

Maadamu unasaidia kukuza mapato ya nchi kupitia kodi na kutoa ajira si tatizo
 
Nimeishi huko miaka 15 ninefanya kazi halmashauri za mbozi,Makete,Njombe,songea na mbeya jiji
Ni kweli mtupu vitajiri uchwara vya huko vinalala nje,vinashindia andaz vimepaukaaa
Utajiri wa huko ni wa kudonoa kwa mwandulami ,mwakipande hovyo kbs
Kweli umeishi huku Mzee hao wazee tuna waeshim mwishoo
 
Dogo usibishebishe vitu usivyovijua. Nenda Makambako mtafute tajiri mmoja anaitwa Mchape utaelewa mtoa mada anachomaanisha.
Hahaha aise huyu sifazake zimeanza Ku tambulika
 
Leo ndio naamini kuna tofauti kati ya Tajiri na Masikini KIMTAZAMO,KIFIKRA NA KIMAONI
 
Ila mbona pale mlowo kuna kijana nae wanasema ana pesa yake niya hivyo lakini hayupo kwenye masharti ya hivyo

Ukimtazama anapiga pamba safi gari safi and coster za kumwaga mbeya tunduma

Labda hizi mambo zipo za aina tofauti sana
Uyu itakuwa alipata utajiri wa kuku Kula mahindi sasa kuku zilidonoa mahindi 50. Utajiri wake wa miaka hamsini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana yule dogo siyo ndagu namfahamu sana ameishi maishs magumu sana alipata mtaji baada ya kupiga udalali wa nyumba alipata around 20 mil ndo kachomoka.Kwa huko songwe king kong wa haya mandagu ni dingi mmoja wa vwawa mkinga anaitw chau.....nini sijui??
Wakinga wanapenda ndagu .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miiko mingine bhana eti usitembee na mtu tofauti na mkeo , je siku amekunyima wengine punje za mahindi 6 zikidonelewa n'a kuku unaishi miaka 6 tu , bora niwe maskini huru kuliko majipu ya matako yasyopona et tajiri , uboyaa
 
Waganga ni watu wajanja sana. Kwa masharti hayo umakuwa unabana matumizi ya fedha uliyonayo na itabaki kwenye mzunguko wa biashara tu. Utakosaje kuwa na pesa nyingi wakati unazalisha sana unakula kidogo. Tufunguke akili
Mpaka kulala kwenye cement kavu Tena uchi ni kubana matumizi. Na nguo uvae wiki nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka makonda awatukane kule Machame naona mmekaa kikao Cha kuchafua makabila Mengine, Maana toka hiyo siku nyuzi za aina hii zimekuwa nyingi Sana, kwenye majukwaa mbalimbali.
Hizo ndagu Kama zinasaidia tafuta nawewe uwe tajiri.
Utajiri kusini, unapatikana shambani, na Msituni.
Sasa hiyo suti unataka avae saa ngapi Mkuu.
Huko hakuna wachuuzi, Kuna wakulima, na Hawa ndio wenye pesa.
Nao Hawa wa Moshi ni wachawi sana eti. Ila Hawa nao kwani wana ela za aina gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio uongo mkuu,ni kweli,Njombe,Iringa na Mbeya zinaongoza kwa tabia hizo ovu.Mauaji ya watoto Njombe ambayo yaliitikisa nchi miezi michache tu iliyopita yalisababishwa na tamaa za utajiri wa kishetani.
Lakini huwezi msikia Mnyaki, safwa ambaye mchawi. Ila wakumbozi ,wakumakete, wanapenda utajiri wa ndagu ni kweli eti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom