Usimwamini mwanamke kwa 100% hata siku moja

Usimwamini mwanamke kwa 100% hata siku moja

USIMWAMINI MWANAMKE HATA SIKU MOJA!

TRUE STORY

Nilikutana na Sharifa mwaka 2015 akiwa anafanya kazi mgahawani maeneo ya posta ya zamani. Nilipomuona tu siku ya kwanza nikampenda. Baada ya siku 3 za kwenda kula pale tukazoeana nikamuomba namba akanipa tukaanza mawasiliano ya mara kwa mara. Baada ya mwezi tukaanza mahusiano. Mapenzi yalikuwa motomoto, karibu kutwa zima tunachati. Muda wote ambao haudumii wateja na mimi nikiwa free tunachati tu, mpaka wenzake wakawa wanamshangaa wanamwambia huyo aliyempata safari hii kanasa pabaya (Nikienda pale kazini kwake kuna rafiki yake alikuwa ananipa udaku).

Nikamuuliza ilikuwaje akawa singo, akasema AMEACHANA NA JAMAA YAKE SIKU SI NYINGI KABLA HAJAKUTANA NA MIMI. Penzi lilikolea hakuna mfano, baada ya miezi miwili tu alikuwa muda wote yupo kichwani mwangu (naamini hata yeye kwake ilikuwa hivo kwa sababu nisipomtafuta masaa mawili mfululizo ni kesi). Nakumbuka kuna siku sijui kulitokea nini sikumtafuta toka asubuhi mpaka jioni, nikampigia saa 3 usiku video call, hicho kilio alicholia ni kama amefiwa.

Toka siku hiyo nikaahidi haitatokea tena kutomtafuta kutwa nzima. (Kumbuka yeye hawezi kunitafuta kwa sababu hajui niko kwenye mazingira gani, nina mke na mtoto). NILIPOMUULIZA ANAKAA WAPI AKASEMA ANAKAA KWA DADA YAKE TEMEKE. Kwamba huyo ni dada yake wa pili kuzaliwa ndani mwao (KUMBE NI MPANGAJI MWENZIE). Wa kwanza yupo kijijini, wa pili ndio huyo anaekaa kwake, wa tatu anakaa Mbagala, wa nne kaka yake anakaa Mbezi na wa tano ni yeye (wa mwisho).

Mapenzi yakapamba moto, kukutana ni jumamosi au jumapili, au wiki zingine jumamosi na jumapili. Tukikutana tunashinda ndani (lodge) mpaka usiku ndio anaondoka kwenda kwao na mimi naenda kwangu. Kwa miaka miwili mfululizo nadhani hatujawahi kuruka jumamosi hata moja bila kukutana. Sijawahi kutaka kufika anakokaa kwa sababu niliona ni mapema kuanza kutaka kwenda kwa dadake, na kuna namna ni kama alikuwa anapotezea nikiuliza habari za anakokaa na mimi nikawa sitilii maanani sana Kwenda kwao.

Lakini kidogo kidogo akawa ananipa maelezo ambayo naweza kufika mpaka mtaani anakokaa. Ila hakuwahi kunikaribisha huko kwao. Tulipendana mnooo, kwa siku alikuwa ananitumia picha hata kumi akiwa kwenye mazingira tofauti. Nikiuliza yuko wapi anafanya nini muda huo jibu lake inakuja picha (selfie). Halafu tunaendelea kuchati. Siku za kukutana mara nyingi yeye ndio alikuwa anakuja maeneo ya Sinza ndio tunakutania huko, ikafika kipindi nikawa naenda maeneo ya Temeke tunaingia gesti za huko, sio mbali sana na anakokaa. Ratiba ikawa inabadilika badilika.

Pamoja na kukutania lodge za maeneo ya kwao, hakuwahi kunikaribisha nikapajue kwao. Ila alinionyesha kwa mbali sana mnara wa simu (vodacom) akasema anakaa karibu kabisa na huo mnara, akanitajia na rangi ya nyumba wanayokaa.

Picha lilikuja kuanza mwaka 2017. Nilipata safari ya kuzunguka mikoa mitano ya Tanzania bara nikaamua kusafiri nae tukale Maisha. Hizo zilikuwa wiki 3 za furaha kubwa kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu, siji kuzisahau.

Baada ya kurudi safari haikupita wiki mbili akaniambia ni mjamzito. Nikafurahi sana, kwa sababu nilikuwa natamani siku zote anizalie mtoto na kama sio kipingamizi cha ndoa nadhani ningemuoa haraka sana tulivokutana. Tatizo nilikuwa na mke tayari. Kuna siku nilienda kufanya mishe Mbagala na yeye asubuhi alikuwa ameniambia anaumwa (mimba ilikuwa inamsumbua sana ile), basi nikaamua kwenda pale bila kumwambia.

Nikafika mpaka pale bila yeye kunielekeza, nilipofika koridoni nikamkuta jirani yao akanionyesha chumba chao nikaingia. Akashangaa sana kwa sababu hakujua kuwa naenda pale, lakini akanipokea vizuri tu tukapiga stori tukatoka wote tukaenda duka la madawa tukanunua dawa akarudi kwao mi nikarudi zangu ofisini.

Sasa humo alimonikaribisha aliniambia ndio sebuleni kwa dada ake, chumba cha pili ndio cha kulala. Ila yeye analala sebuleni (kulikuwa na kila kitu mpaka kitanda). KUMBE NI CHUMBA CHAKE alichopangishiwa na yule jamaa aliyeniambia waliachana (MPAKA WAKATI HUO WALIKUWA BADO WAKO PAMOJA na sikuwahi kushtuka kuwa yuko na mtu na jamaa hajawahi kushtuka kuwa anaibiwa). Jamaa nae alikuwa na mke wake hivo anakujaga mara moja moja sana. Akija anapiga zake bao chap anarudi kwake, halafu haonekani tena mpaka baada ya mwezi au miwili (alikuwa dereva wa magari ya safari ndefu).

Kilichofanya nisishtuke kabisa kuwa tuko wawili ni kwamba jamaa yake hanaga mawasiliano ya simu ya mara kwa mara. Nadhani akimhitaji alikuwa anaenda tu geto alikompangishia bila kupiga simu wala kutuma meseji. Na akienda hakagui simu hata mara moja kwa sababu angekuwa anakagua angeshajua kitambo kuwa demu wake yuko na mimi. Demu hajawahi kufuta meseji yangu hata moja toka tulipokutana. Na picha zote alizonitumia wasap hajawahi kufuta kwenye simu yake hata moja hata zangu nilizomtumia mimi.

Na kumbukumbu ya simu nilizompigia hajawahi kufuta hata moja. Kitu kingine, nikiwa nae lodge simu yake inakaa hapo mezani muda wote haigusi hata mara moja, na ikipigwa au ikiingia meseji na mimi niko karibu nayo, ataniuliza mimi ni nani anapiga au nani katuma meseji. Yani alikuwa demu ambaye hana mambo mengi kabisa, nilimpenda mnooo na alijenga mazingira ya mimi kumuamini asilimia 100 (sipendi kabisa madem ambaye ukiwa naye muda wote yuko na simu mkononi, huyu alikuwa wa kwanza kukutana nae wa aina ya pekee). Kama mara mbili imewahi kupigwa simu tukiwa pamoja, aliempigia akamfokea sana, halafu yeye hakujibu. Nilipokuwa namuuliza huyo nani akawa anasema ni yule jamaa waliyeachana siku hizi anamsumbua sana anataka warudiane, na yeye hataki kwa sababu ameshakuwa na mimi. (KUMBUKA MPAKA HAPO WALIKUWA HAWAJAACHANA ila mimi nilikuja kujua baadae sana walipochana kweli baada ya demu kujifungua na mimi kumuhamisha demu kutoka pale (”KWA DADA YAKE”) nikamleta maeneo ya jirani na ninakokaa ili iwe rahisi kuwaona na mtoto kila siku).

Kuna wakati akaniambia dadake amesafiri kaenda nyumbani Iringa. Basi siku moja asubuhi tu kabla hajaamka nikaenda pale (Kazi alikuwa ashasimama kwa ajili ya ujauzito). Toka siku hiyo tukaacha kwenda lodge, mambo yote tunamalizia hapo (KUMBUKA KAPANGISHIWA NA MWANAUME ila mimi najua ni kwa dada yake). Nikawa naenda mara kwa mara naingiaga tu kama kwangu.

Aliyejifanya dada ake ananipokea fresh nashinda hapo. Wanapika misosi tunakula kila nikienda. Tunakaa chumbani tukitosheka tunakaa koridoni tukichoka tunakaa nje, yani nikawa huru mno. ILA KUNA MACHO WAPANGAJI WENZIE WALIKUWA WANANIANGALIA KAMA YA KUNIAMBIA KITU mi sina hili wala lile, nimezama kwenye penzi zito. Kabla ya hapo nilikuwa nishaanza hata kuchangia kodi, kwamba mle sebleni anamolala kodi nalipa mimi, nikamwambia amwambie kabisa dadake. Na alikuwa na mtoto yuko darasa la sita huko kijijini kwao (kwa bibi yake huyo mwanamke wangu) nikawa nasaidia kumhudumia.

Picha likaendelea. Siku moja akaniambia anaumwa, mimi mapema tu nikatokea pale. Nikaingia chumbani nikavua zangu shati nikabaki na singlet, akaniandalia chai nikanywa baadae tukatoka tukakaa koridoni, nikamwambia sikai sana ntaondoka muda si mrefu.

Tukiwa hapo koridoni akaingia jamaa, alipofika karibu na chumba cha demu (WAKATI HUO MI NAJUA NI SEBLENI KWA DADAKE) akanisalimia mimi HALAFU BILA KUPIGA HODI WALA NINI akaingia humo chumbani. Demu akasimama akamfuata huko ndani, nikasikia jamaa anaunguruma kama analalamika kitu kama dakika moja nzima, ila maneno nilikuwa siyasikii. Halfu demu akatoka akamuacha jamaa huko ndani. Akaniuliza kama anisindikize au vipi kwa sababu nilikuwa nimemwambia naondoka sasa hivi.

Kwa namna yule jamaa alivoingia nikawa na maswali mengi kichwani nikawa nimeghairi kuondoka ili jamaa aondoke nimuulize demu yule ni nani. Kwa hiyo nikamjibu kuwa nimeghairi kuondoka ntaondoka jioni (Hiyo ilikuwa saa 5 hivi asubuhi). Kwa unyonge akarudi kule ndani, nikasikia jamaa sasa linatukana matusi, kuwa halipendi ujinga na u.s.e.n.g.e u.s.e.n.g.e, na maneno mengine makali makali. Mengine nikawa sisikii mengine nasikia, kama dakika 2 hivi. Halafu jamaa likatoka likabamiza mlango kwa nguvu huku linaondoka linamwambia demu aache upumbavu wake kabisa. Hilooooooo likapotea zake……

ITAENDELEA KESHO***
Wewe na huyo jamaa mlikuwa na laana za wake zenu ndiyo maana Sharifa alikuwa anawachezea
 
Wabandueni vizuri ili Waridhike na wasiwe na Tamaa ( Hamu) ya Kubanduliwa nasi sawa?

Sasa kama Mke wa Mtu ukiwa Unambandua anakupa kabisa Madhaifu ya Mumewe kuna Kosa?

Mfano kuna Mke wa Mwanajeshi mmoja ( tena wa Cheo cha Major ) pale Makongo Jeshini huyu kila nikimkwepa na kumwambia Mimi na Yeye iwe basi anasema hawezi na hataki kwani Mumewe japo ana Hela na Maendeleo kibao ila hajui Kumkojolesha kama akiwa nami sasa hapa Mimi Kosa langu ni nini au lipi Mkuu?

Na nitawabandulieni kweli kweli Wake zenu hadi mjifunze Kuwabandua vyema hasa hasa kwa Kuwakojolesha sana sawa?

Hamna Akili.
Kama yule wa Futui

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Wakati mwingine umbali au ubize huchangia kuchelewa kugundua kuwa mnachanganywa, enzi hizo ilinichukua karibu mwaka kugundua tupo zaidi ya wawili tunashea mbunye, mbususu
 
Kosa la mke wako Ni nini ..je siku ukijua anamegwa ? Cha mtu huliwa na mtu
Kumegwa kwangu sio ishu. Kwani kuna uhakika gani kuwa hamegwi? Amegwe sana, ila huduma nyumbani ziwepo na asirudi baada ya muda niliompangia na pia asimegewe humo kwangu. Mimi namega na huduma zote ziko palepale, isipokuwa moja tu ya kumega!
 
Halafu wote mna wake zenu mnampapasa kisha kila mtu anaenda kwa mkewe, alikuwa mjasilia pesa
 
ungekuwa unatuelezeaga kipindi cha maraha muda huu uzi ungekuwa mfupi tu, ungekuwa ni kuhusu kisa halisi pekee.
 
Story km hii hii kuna binti aliwai kutuzungulusha na jamaa mmoja mimba hiyo mpk anazaa ina watu wawili.
Nikamuacha kumuachia jamaa mimba yake alivyodai na mahari alishatoa.
Wakaendelea huko baada ya kusameheana.
Mungu si Yakobo baada ya miaka miwili yule jamaa tukakutana tena kikazi ofisi moja,kitengo kimoja.
Sijui ikawaje yule mtu baadae akawa anamtuma yule mkewe x wangu hapo wanalea mtoto wangu aje pale ofisini kufata mahitaji akiwa hayupo.
X anakuja na mtoto wangu nawapa mizigo yao wanaondoka.
Hapo mi na x hatuna stori kabsaa.
Baada ya muda bana yule jamaa ikabidi siku awashirikishe staff wenzetu pale kazini kuhusu mtoto.
Akawasimulia kisa chote huko nyuma na hapo tulipofikia.
Akamleta yule binti na mtoto.
yule binti akiwa pale reception wale Staff wakawa wanaenda kusalimia na kuthaminisha mtoto ni wa nani.
Aisee mpk mwisho kura ikaangukia kwangu.
Kwamba jamaa analea mtoto si wake.
Yule jamaa akabwaga manyanga kwa hasira na kweli yule mwanamke alipiga magoti akanigeukia kukiri kweli mtoto sio wa jamaa.
Namimi ujana ule nikamtosa,akaondoka analia huku akiapa mtoto ni wangu.
Basi kiukweli tuliparaganyika ila kijana tumeonana baada ya miaka 22.
 
Sijui na mimi nisimulie!?
 
USIMWAMINI MWANAMKE KWA 100% HATA SIKU MOJA

PART FOUR

Ilipoishia

Kama nilivosema mwanzo, kwa miaka yote 7 niliyokuwa Sharifa toka 2015 mpaka leo (BADO TUPO WOTE KAZAA NA MTOTO MWINGINE MWAKA HUU), hajawahi kuchelewa kupokea simu yangu, hata awe anafanya nini, hajawahi kukosa kujibu meseji yangu, hajawahi kufuta meseji yangu wala simu yangu, hajawahi kuacha kunitumia picha nikidai popote alipo, hajawahi kuficha simu yake nikiwepo. Yani nikifika tu kama kuna changamoto ya simu atanipa nishughulike nayo, kama kuna kitu interesting cha kunionyesha humo kwenye simu atanikabidhi simu yake niendelee kucheki yeye anaenda zake nje kupika. Simu yangu ikizima chaji halafu yeye anapika sina kampani, atanipa simu yake nicheki cheki instagram na FB bila hofu yoyote. YEYE NDIYE MTU AMBAYE NIKIWEKEWA BASTOLA KICHWANI NIKAAMBIWA NIMPIGIE MTU MMOJA TU ASIPOPOKEA WANANIPIGA RISASI, NTAMPIGIA YEYE. Basi nikaamua kuachana na yaliyopita tusonge mbele. Sikuwahi kuuliza kitu tena kuhusu jamaa Ex husband mpaka mwaka huu 2022.

Tuendelee

Siku moja, mwezi sikumbuki lakini mwanzoni mwa mwaka huu (Sharifa akiwa tayari amejifungua mtoto wa pili - tumwite Venance) nilimpigia simu kumpa hai na watoto. Akaniambia Ex msumbufu kampigia simu kwa namba tofauti alivopokea akaanza kumwongelesha vitu havieleweki yeye akamkatia simu. Alivokata simu jamaa akarekodi audio kama 4 akamtumia na meseji nyingi (Hawezi kupiga kwa namba yake kwa sababu alishamblock). Akanitumia audio clip 2 mimi nikazisikiliza. Muda huo huo nikaenda. Nilivofika tu akanipa simu yake nisome mwenyewe na nisikilize clip zote. Kwa kifupi jamaa anamuambia amemmisi sana ila hana la kufanya, anaomba tu kama kuna kitu alimlisha arudi kwa mganga akakitoe kwa sababu anapata mateso makubwa. Atakuja kupata ajali. Muda wote akiwa anaendesha gari anamuwaza yeye, amejaribu kujifariji na wanawake wengine kadhaa ili amsahau Sharifa ameshindwa. Kwenye moja ya hizo clip jamaa akaweka mtego, akamkumbusha tu kuwa mimi ni mkristo kwa hiyo siji kumuoa kamwe, huu ni mwaka wa 7 mbona sijamuoa bado?. Nadhani ndio maana Sharifa alinipa nisikilize.

Zile clip alizonitumia Sharifa (Mama Lisa na Venance) nikaziforward kwa jamaa Ex ajue kuwa meseji zake natumiwaga. Huko nyuma amewahi kutuma zingine kama mara 2 hivi, hazikuwa na uzito kama hizi. Nikamwambia ujumbe wake nimeupata. Na yeye akaniambia anajua nampotezea tu muda mwanamke wa watu baada ya kumpora yeye, sina mpango wa kumuoa, anaamini kwamba nishaujua ukweli kuwa Sharifa alinichezea akili miaka mitatu, naye ye alivomkataa kabisa mtoto ndio mwanamke akaamua kuja kwangu mazima. Ila angekubali mtoto, asingefuatilia vile vyeti wangekuwa pamoja mpaka leo na yeye bado anampenda sana sana. Daaa! Tukarudi kule kuleeeeeeeeeeee!

Nikataka kuthibitisha zaidi kama kweli mtoto wangu alishakuwa amepewa yeye, kwamba angekubali tu, sasa hivi mtoto asingekuwa wangu!!! Ninavokapenda kabinti kangu hivi jamaniii! Nikasema sasa naingia kwenye misheni ya kujua ukweli mwenyewe hata kama yamepita. Ila moyoni kwangu nikajiahidi chochote nitakachogundua simuachi Sharifa (Mama Lisa na Venance) kamwe wala simwambii. Mtu pekee anayeweza kunithibitishia kuwa waliendelea na mahusiano mpaka Sharifa alivohama kule Temeke na kama kuna uwezekano mtoto Lisa akawa sio wangu ni wa yule jamaa, ni mtu mmoja tu. Aliyejifanya dada yake kumbe mpangaji mwenzie. Na namna ya kupata hiyo Habari kutoka kwa yule ni kumsogeza karibu na kumpa mpa vihela hapa na pale halafu siku moja nimuite sehemu nimuahidi kitu kikubwa halafu nimdodose kama kweli toka 2015 mpaka 2018 yule Ex wa Sharifa alikuwa anakuja pale na je yule tuliyekutana pale siku ileee akagombagomba alikuwa nani. Si ni shoga yake, atakuwa alimsimulia.

Basi nikaanza misheni impossible mnamo mwezi wa 4 hivi. Nikampigia simu siku moja huyo shoga wa Sharifa (dada feki) kumsalimia, yeye akawa yuko poa ila mtoto wake anaumwa. Nikauliza kama kampeleka hospitali akasema hana hela. Mpesa chap bila kuchelewa nikamrushia elfu 20. Akaenda hospitali akanitumia kile kicheti wamemuandikia dawa za elfu 40. Nikajiongeza, kumwona daktari buku 5 nauli buku 5 atakuwa kabaki na buku 10. Chapa nikamrushia elsu 30. Alishukuru sana sana sana. Sasa ikawa mara moja moja tu namtumia buku 10 namwambia awanunulie watoto wake chips. Anafurahi balaa. Ikafika wakati akawa yeye ndio anaomba na wala hamwambii shoga yake chochote kuhusu tunavowasiliana. Mwanzo alikuwa anamwambia kila tukiongea, na Sharifa hana shida sisi kuwasiliana kwa sababu mara nyingi tu shoga yake akipiga simu wapeane udaku, yeye mwenye huwa ananipa simu nimsalimu. Sasa juzi kati nikasema ameshakuwa karibu sasa nimwite nimuulize zile maishu. Nikampigia simu tuonane akauliza wapi nikamtajia maeneo, akasema poa. Siku hiyo hakuja, akatoa sababu. Tukapanga siku nyingine hakuja. Nikajua misheni imefeli. Nikasema nijaribu mara ya mwisho. Nilivompigia akasema naonaje tukionana keshokutwa yake, kwa sababu siku hiyo hayuko vizuri, yuko kwenye siku zake ndio anamalizia! KHAAAAAAAAA! Nikawazaaaaaa yamekuwa hayooooooo!!!!! Nikashangaa sana kwa sababu wazo hilo mimi halikuwepo kichwani. Japo limewahi kunijia wakati ananipiga chenga kuonana, niliwaza labda anajua nataka mapenzi. Anyway, shetani ana nguvu sana, nikaamua kutembea nae kwenye reli yake hiyo hiyo. Keshokutwa yake tukakutana, itoshe tu kusema shetani alinishinda nguvu, tukajikuta tu tuko lodge. Kilichojiri mungu anisamehe.

Sasa siku hiyo hata sikumuuliza chochote ili asijeshtuka akajidharau kuwa mimi lengo la kukutana lilikuwa lingine, humo kwenye lodge kajichomeka mwenyewe. Tukaachana kwa minajiri ya kukutana siku nyingine. Tukakutana tena mara ya pili, sikuongea chochote. Mara ya 3 ndio nikamuuliza. YEYE NDIO AKATHIBITISHA KUWA NI KWELI TOKA 2015 MPAKA 2018 JAMAA ALIKUWEPO KWENYE PICHA JAPO RAFIKI YAKE ALIKUWA HAMTAKI LAKINI ALIKUA HANA JINSI KWA SABABU ALIKUWA ANAKAA MWENYE NYUMBA AMBAYO JAMAA NDIO KAMPANGISHIA. Na akasisitiza kuwa wakati Sharifa anapata hiyo mimba jamaa alikuwa hajawahi kuonekana pale miezi mitatu, jamaa mwenyewe alimlalamikia sana yeye kuwa rafiki yake kamsaliti mpaka kashika mimba. Na jamaa alimwambia kuwa mimba haitambui ila bado anamtambua Sharifa kama mke wake. Mpaka mtoto LISA anazaliwa jamaa aliendelea kumsisitizia kuwa mtoto hamtambui ila Sharifa hamuachi. Mpaka Sharifa alivohama pale jamaa akamkosa yeye ndio alikuwa jamaa anamdai maelezo kama vile yeye ndio kamtorosha. Kwa hiyo akaniambia ukweli wote, kwa sababu yeye ndio anaujua vizuri na wameishi vyumba jirani kwa muda mrefu wakisaidiana kwenye kila kitu. Walikuwa wanapika pamoja kama familia moja. Kila kitu walikuwa wanashirikiana.

Kwa kifupi stori ndio iko hivo. Na sasa hivi nafsi yangu imetulia baada ya kuujua ukweli wote. Kumbuka kwenye majadiliano yote, Sharifa au mama Lisa au mama Venance hajawahi kukiri popote kuwa na mahusiano yoyote na mtu yoyote kwa kipindi chote cha miaka 7 tuliyokuwa pamoja. Hata siku rafiki yake aliponiambia ukweli wote niliongea nae kuwa ukweli wote nimeshaujua lakini sina mpango wowote wa kumuacha. Nikamuuliza kwanini alitaka kumpa yule jamaa mtoto wangu?? Akasema hajawahi kufanya hiyo kitu. BADO ALIENDELEA KUKATAA KUWA HAJAWAHI KUNISALITI. Swali lake kubwa hizo taarifa natafuta za nini? Ni sijiulizi wanaoniambia wanataka nini? Sioni kuwa Ex wake anawatumia wanaonimbia ili tuachane?? Ukiachilia mbali kuwa ana watoto wangu wawili, yeye mwenyewe nampenda sana sana sana (Inawezekana nimelishwa alicholishwa Ex).

SASA NILICHOTAKA KUSEMA NI KWAMBAAAAA, USIMUAMNI MTU KWA ASILIMIA 100. Maisha tuliyoishi na Sharifa 2015-2018 nilikuwa namwamini kupita maelezo. Ningeweza kufanya chochote kwa ajili yake. Alitengeneza mazingira ambayo ilikuwa lazima nimuamini asilimia zote. Yani na mawasiliano yote, na ukaribu wote, na kukutana kote, bado aliweza kunificha kitu kikubwa hivo, na jamaa yake aliendelea kuja pale kwake na yeye aliendelea kukutana na mimi kwenye lodge akihofia tutakutana wanaume wawili. Nilikuwa nikitaka tukosane siku hiyo nimuulize tu kuhusu huyo jamaa, nikisisitiza kuongelea mpaka analia machozi. Utasikia ”Alichonifanyia yule mtu, sitaki kabisa kumsikia kwenye maisha yangu, bora nife kuliko kurudi kwake. Ukiniacha wewe bora nirudi kijijini kwanza nikajipange kuliko kurudi kwake”

MWISHO
Mhh fikirishi kwa watuwazima Ila hongera kunamengi katika to ya mistari kuweza kujifunza,vipi watoto umeshawatambulisha kwa shangazi zao,maana nadhani nawe ni miongoni mwawale sheria za dini zinawabana 2,Ila hongera tena,umeenjoy furaha ya kimapenzi na mtu umpendae nae akakupenda.amekufanya Moyo ukatulia haswa maana amekuwa zaidi ya mchepuko
 
USIMWAMINI MWANAMKE HATA SIKU MOJA!

TRUE STORY

Nilikutana na Sharifa mwaka 2015 akiwa anafanya kazi mgahawani maeneo ya posta ya zamani. Nilipomuona tu siku ya kwanza nikampenda. Baada ya siku 3 za kwenda kula pale tukazoeana nikamuomba namba akanipa tukaanza mawasiliano ya mara kwa mara. Baada ya mwezi tukaanza mahusiano. Mapenzi yalikuwa motomoto, karibu kutwa zima tunachati. Muda wote ambao haudumii wateja na mimi nikiwa free tunachati tu, mpaka wenzake wakawa wanamshangaa wanamwambia huyo aliyempata safari hii kanasa pabaya (Nikienda pale kazini kwake kuna rafiki yake alikuwa ananipa udaku).

Nikamuuliza ilikuwaje akawa singo, akasema AMEACHANA NA JAMAA YAKE SIKU SI NYINGI KABLA HAJAKUTANA NA MIMI. Penzi lilikolea hakuna mfano, baada ya miezi miwili tu alikuwa muda wote yupo kichwani mwangu (naamini hata yeye kwake ilikuwa hivo kwa sababu nisipomtafuta masaa mawili mfululizo ni kesi). Nakumbuka kuna siku sijui kulitokea nini sikumtafuta toka asubuhi mpaka jioni, nikampigia saa 3 usiku video call, hicho kilio alicholia ni kama amefiwa.

Toka siku hiyo nikaahidi haitatokea tena kutomtafuta kutwa nzima. (Kumbuka yeye hawezi kunitafuta kwa sababu hajui niko kwenye mazingira gani, nina mke na mtoto). NILIPOMUULIZA ANAKAA WAPI AKASEMA ANAKAA KWA DADA YAKE TEMEKE. Kwamba huyo ni dada yake wa pili kuzaliwa ndani mwao (KUMBE NI MPANGAJI MWENZIE). Wa kwanza yupo kijijini, wa pili ndio huyo anaekaa kwake, wa tatu anakaa Mbagala, wa nne kaka yake anakaa Mbezi na wa tano ni yeye (wa mwisho).

Mapenzi yakapamba moto, kukutana ni jumamosi au jumapili, au wiki zingine jumamosi na jumapili. Tukikutana tunashinda ndani (lodge) mpaka usiku ndio anaondoka kwenda kwao na mimi naenda kwangu. Kwa miaka miwili mfululizo nadhani hatujawahi kuruka jumamosi hata moja bila kukutana. Sijawahi kutaka kufika anakokaa kwa sababu niliona ni mapema kuanza kutaka kwenda kwa dadake, na kuna namna ni kama alikuwa anapotezea nikiuliza habari za anakokaa na mimi nikawa sitilii maanani sana Kwenda kwao.

Lakini kidogo kidogo akawa ananipa maelezo ambayo naweza kufika mpaka mtaani anakokaa. Ila hakuwahi kunikaribisha huko kwao. Tulipendana mnooo, kwa siku alikuwa ananitumia picha hata kumi akiwa kwenye mazingira tofauti. Nikiuliza yuko wapi anafanya nini muda huo jibu lake inakuja picha (selfie). Halafu tunaendelea kuchati. Siku za kukutana mara nyingi yeye ndio alikuwa anakuja maeneo ya Sinza ndio tunakutania huko, ikafika kipindi nikawa naenda maeneo ya Temeke tunaingia gesti za huko, sio mbali sana na anakokaa. Ratiba ikawa inabadilika badilika.

Pamoja na kukutania lodge za maeneo ya kwao, hakuwahi kunikaribisha nikapajue kwao. Ila alinionyesha kwa mbali sana mnara wa simu (vodacom) akasema anakaa karibu kabisa na huo mnara, akanitajia na rangi ya nyumba wanayokaa.

Picha lilikuja kuanza mwaka 2017. Nilipata safari ya kuzunguka mikoa mitano ya Tanzania bara nikaamua kusafiri nae tukale Maisha. Hizo zilikuwa wiki 3 za furaha kubwa kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu, siji kuzisahau.

Baada ya kurudi safari haikupita wiki mbili akaniambia ni mjamzito. Nikafurahi sana, kwa sababu nilikuwa natamani siku zote anizalie mtoto na kama sio kipingamizi cha ndoa nadhani ningemuoa haraka sana tulivokutana. Tatizo nilikuwa na mke tayari. Kuna siku nilienda kufanya mishe Mbagala na yeye asubuhi alikuwa ameniambia anaumwa (mimba ilikuwa inamsumbua sana ile), basi nikaamua kwenda pale bila kumwambia.

Nikafika mpaka pale bila yeye kunielekeza, nilipofika koridoni nikamkuta jirani yao akanionyesha chumba chao nikaingia. Akashangaa sana kwa sababu hakujua kuwa naenda pale, lakini akanipokea vizuri tu tukapiga stori tukatoka wote tukaenda duka la madawa tukanunua dawa akarudi kwao mi nikarudi zangu ofisini.

Sasa humo alimonikaribisha aliniambia ndio sebuleni kwa dada ake, chumba cha pili ndio cha kulala. Ila yeye analala sebuleni (kulikuwa na kila kitu mpaka kitanda). KUMBE NI CHUMBA CHAKE alichopangishiwa na yule jamaa aliyeniambia waliachana (MPAKA WAKATI HUO WALIKUWA BADO WAKO PAMOJA na sikuwahi kushtuka kuwa yuko na mtu na jamaa hajawahi kushtuka kuwa anaibiwa). Jamaa nae alikuwa na mke wake hivo anakujaga mara moja moja sana. Akija anapiga zake bao chap anarudi kwake, halafu haonekani tena mpaka baada ya mwezi au miwili (alikuwa dereva wa magari ya safari ndefu).

Kilichofanya nisishtuke kabisa kuwa tuko wawili ni kwamba jamaa yake hanaga mawasiliano ya simu ya mara kwa mara. Nadhani akimhitaji alikuwa anaenda tu geto alikompangishia bila kupiga simu wala kutuma meseji. Na akienda hakagui simu hata mara moja kwa sababu angekuwa anakagua angeshajua kitambo kuwa demu wake yuko na mimi. Demu hajawahi kufuta meseji yangu hata moja toka tulipokutana. Na picha zote alizonitumia wasap hajawahi kufuta kwenye simu yake hata moja hata zangu nilizomtumia mimi.

Na kumbukumbu ya simu nilizompigia hajawahi kufuta hata moja. Kitu kingine, nikiwa nae lodge simu yake inakaa hapo mezani muda wote haigusi hata mara moja, na ikipigwa au ikiingia meseji na mimi niko karibu nayo, ataniuliza mimi ni nani anapiga au nani katuma meseji. Yani alikuwa demu ambaye hana mambo mengi kabisa, nilimpenda mnooo na alijenga mazingira ya mimi kumuamini asilimia 100 (sipendi kabisa madem ambaye ukiwa naye muda wote yuko na simu mkononi, huyu alikuwa wa kwanza kukutana nae wa aina ya pekee). Kama mara mbili imewahi kupigwa simu tukiwa pamoja, aliempigia akamfokea sana, halafu yeye hakujibu. Nilipokuwa namuuliza huyo nani akawa anasema ni yule jamaa waliyeachana siku hizi anamsumbua sana anataka warudiane, na yeye hataki kwa sababu ameshakuwa na mimi. (KUMBUKA MPAKA HAPO WALIKUWA HAWAJAACHANA ila mimi nilikuja kujua baadae sana walipochana kweli baada ya demu kujifungua na mimi kumuhamisha demu kutoka pale (”KWA DADA YAKE”) nikamleta maeneo ya jirani na ninakokaa ili iwe rahisi kuwaona na mtoto kila siku).

Kuna wakati akaniambia dadake amesafiri kaenda nyumbani Iringa. Basi siku moja asubuhi tu kabla hajaamka nikaenda pale (Kazi alikuwa ashasimama kwa ajili ya ujauzito). Toka siku hiyo tukaacha kwenda lodge, mambo yote tunamalizia hapo (KUMBUKA KAPANGISHIWA NA MWANAUME ila mimi najua ni kwa dada yake). Nikawa naenda mara kwa mara naingiaga tu kama kwangu.

Aliyejifanya dada ake ananipokea fresh nashinda hapo. Wanapika misosi tunakula kila nikienda. Tunakaa chumbani tukitosheka tunakaa koridoni tukichoka tunakaa nje, yani nikawa huru mno. ILA KUNA MACHO WAPANGAJI WENZIE WALIKUWA WANANIANGALIA KAMA YA KUNIAMBIA KITU mi sina hili wala lile, nimezama kwenye penzi zito. Kabla ya hapo nilikuwa nishaanza hata kuchangia kodi, kwamba mle sebleni anamolala kodi nalipa mimi, nikamwambia amwambie kabisa dadake. Na alikuwa na mtoto yuko darasa la sita huko kijijini kwao (kwa bibi yake huyo mwanamke wangu) nikawa nasaidia kumhudumia.

Picha likaendelea. Siku moja akaniambia anaumwa, mimi mapema tu nikatokea pale. Nikaingia chumbani nikavua zangu shati nikabaki na singlet, akaniandalia chai nikanywa baadae tukatoka tukakaa koridoni, nikamwambia sikai sana ntaondoka muda si mrefu.

Tukiwa hapo koridoni akaingia jamaa, alipofika karibu na chumba cha demu (WAKATI HUO MI NAJUA NI SEBLENI KWA DADAKE) akanisalimia mimi HALAFU BILA KUPIGA HODI WALA NINI akaingia humo chumbani. Demu akasimama akamfuata huko ndani, nikasikia jamaa anaunguruma kama analalamika kitu kama dakika moja nzima, ila maneno nilikuwa siyasikii. Halfu demu akatoka akamuacha jamaa huko ndani. Akaniuliza kama anisindikize au vipi kwa sababu nilikuwa nimemwambia naondoka sasa hivi.

Kwa namna yule jamaa alivoingia nikawa na maswali mengi kichwani nikawa nimeghairi kuondoka ili jamaa aondoke nimuulize demu yule ni nani. Kwa hiyo nikamjibu kuwa nimeghairi kuondoka ntaondoka jioni (Hiyo ilikuwa saa 5 hivi asubuhi). Kwa unyonge akarudi kule ndani, nikasikia jamaa sasa linatukana matusi, kuwa halipendi ujinga na u.s.e.n.g.e u.s.e.n.g.e, na maneno mengine makali makali. Mengine nikawa sisikii mengine nasikia, kama dakika 2 hivi. Halafu jamaa likatoka likabamiza mlango kwa nguvu huku linaondoka linamwambia demu aache upumbavu wake kabisa. Hilooooooo likapotea zake……

ITAENDELEA KESHO***
...FUPISHA. USIRUDIE RUDIE. TUMEISHAELEWA! SASA UNATAKA TUKUSAIDIEJE ???
 
Ni huzuni kusema, na samahani kama nakukwaza mkuu, lakini umepata unachostahili.

Kumbuka unatakiwa utambue kwamba mwanamke wa nje ni mtu wa aina gani mapema, unatakiwa uzuie kuweka makazi ya kudumu kwa mchepuko, na vilevile si vema kuzaa watoto nje kwa sababu watakaoteseka ni watoto kwa kukosa mapenzi ya wazazi wote wawili (Baba na Mama). Sikatai unaweza kuwa unapata muda wa kuwaona hata kila siku lakini wakikua watakuwa na maswali mengi kwa nini hukuwepo muda wote.
Na kama anawapenda kwanini asiwepo muda wote,hakuna kosa kuzaa,kutowapenda ndiohuwa kosa,kama uliwazaa kwa kuelewa nadhani ni jukumu lako kuwawekea wigo kuonyeshakweli unawapenda hata kwa do 5,unazozipata.
 
majina ya Sharifa nahisi yana tatizo. kuna Sharifa zaidi ya wanne nnao wafahamu kama mambo yao yanafanana hivi.
naomba nizungumzie mmoja wao japo natoka nje ya Story naomba nivumiliwe niwape kisanga kilichomkuta mdogo wangu kabisa.

Huyu bwana nae alikuwa na mahusiano na moja kati ya hawa kina sharifa, kipindi hivyo ndio tunaanza maisha tulikuwa tukiishi chumba kimoja mimi na huyu ndugu yangu. wakati huo sisi wote ni madereva wa masafa marefu, sasa ndugu yangu na sharifa wake walikuwa wananikera kitu kimoja, simu za usiku. ndugu yangu anaongea na simu, unalala unastuka saa tisa ile ng'ombe unaikuta bado inaongea na simu na miguu imeweka ukutani maongezi ya kipuuzi puuzi tu, yaan mda mwingine anakesha kabisa, kuna wakati unakuta safari hakuna hali ngumu tumeyumba labda tuna buku nne tunagawana mbilimbili tuishi usiku yule jamaa buku mbili anatia vocha analala njaa ili tu aongee na Sharifa.

Sasa kuna siku mimi sina kitu alafu mwanangu( mdogo wangu tunaishi kishkaji zaidi ) ametoka safaro yuko njema nikamwambia oya babu niungie mwanangu kabla Sharifa ajakukamua ndwange maana najua wewe ni pimbi kwa manzi ako utaenda kutoa ndwange zote huko, kumbe kweli asee Sharifa ashasoma ramani anataka akampukutishe mzigo wote, jamaa akaniambia hapa sina Cash twende TipTop mimi naenda kuonana na Sharifa alafu umuone shemeji yako kisha nitoa ndwange kwa wakala nakupa pesa unayotaka unajikataa mimi naenda kulala Lodge leo na Shemeji yako nataka kuudestroy ule mk**** ah mm nikaona poa shida yangu pesa hayo mambo mengine atajua mwenyewe.

Sasa tumefika Tipi ya Top pale kwenye nakutana na shemeji yangu Pisi imesimamia kucha, nikamsalimia ikabidi nimuache mwamba ajimwambafy sasa mimi nimebaki kwa nyuma nawafuata polepole ukumbuke hapo yule mbuzi ( mdogo wangu hajatoa ndwange bado kwenye simu) na ndio kilichokuwa kinanisubirisha nikawa mpole, wao mnele mm nyuma naangalia mkia wa shemeji na jinsi nnavyomjua dogo mipango aliyokuwa nayo kuhusu ule mkia mm nkakausha.

sasa tumefika apo alikosema anaenda kufanya uzinzi akaniambia Man kaa hapa na shemeji yako agizen msosi mm naenda kufanya muamala pale, nje ya hiyo bar na Lodge ni hapo hapo. mm nikaagiza, shemeji akaagiza mwamba akaenda kutoa mzigo haikupita mda akawa amewasili. akaongea kitu na mwanamke wake akaniita pembeni akanitoa la 20. mm nikamwambia Man nikimaliza kula mm nasepa we si haurudi akasema yap. sasa namaliza pale, mwamba akauliza vip mwanangu hustui japo mbili za kukuboost mpaka home? home kipindi hicho Mabibo. nikaona yap hii fresh, nikasafiri mara mbili fasta fasta. huku shemeji Sharifa yeye akijipigilia savanna taratiibu. sasa cjui ibilisi gani akatokea pale, shemeji akadai jamaa alipie chumba anataka akajisaidie room na sio public toi, mwamba fasta akajitosa mapokezi akafanya yake. akarudi na funguo akampatia.

Sharifa alikuja na kipoch hiki cha kwapani sasa alipoondoka akawa amekiacha juu ya meza, alipotokomea tu, mdogo wangu akachukua ile pochi akafungua zipu akatumbukiza mkono ndani, vikatoka vimlio flan hivi, mwamba akatoa macho, nikamuuliza vipi bab? akajibu k******mae, akautoa mkono chap! akasema mwanangu huyu dem, kabla hajamalizia akaingiza tena mkono ulipotoka akawa ametoka na condom kama tisa hv ziko moja moja, akaziweka mezani, akazama tena akatoka na zingine za kutosha, dah mimi nilicheka sanakwa sababu ni tukio ambalo lilikuwa linafurahisha mno ukizingatia mimi nilishamchanaga dogo yule demu anaonekana dhahir shahiri ni chura., sasa wakati anaendelea kuingiza mikono mle ndani akaibuka na Uume bandia mkubwa tu wa zambarau yaani kipisi tu cha kutosha, hapo nilicheka mpaka beer nikamwaga. nikainuka zangu, jamaa akakibidua kilebki mkoba akaanza kukikunguta, kufungua zip ya pembeni akakutana na ki uume kingine hichi kidogo kidogo cha rangi ya maziwa. Akaniambia X leo naua. nikamwambia man mm ngoja niende zangu home. msubiri dem wako akakubandue sijui mkabanduane, nikaondoka nacheka, dogo nikamuacha kapanic sana. kutoka tu pale mimi nikazima simu..asubui nikaenda kumuwekea dhamana dogo pale Urafiki police.
🤣🤣🤣mkuu hii story ilitakiwa iwe na uzi wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom