USIMWAMINI MWANAMKE KWA 100% HATA SIKU MOJA
PART THREE
Ilipoishia
Nikamwambia alinitumia meseji mbili mesenja na zinasema hivi na hivi. Akasema MPENZI WANGU UNANIAMNI? HUYO MTU KAAHIDI ANATAKA KUNIHARIBIA KWAKO, UKIMSIKILIZA UKANIACHA LENGO LAKE LITAKUWA LIMETIMIA. ILA NTATESEKA SANA NA MWANANGU. BASI WE MSIKILIZE TU. Nikamwambia kaaaaaamwe siwezi kumsikiliza jamaa nikamuacha yeye, over.
Tuendelee
Kuingia Facebook jioni tena jamaa kanitumia meseji kuuliza tutaonana lini. Nikamwambia hatutaonana. Yeye kama kuna kitu anamdai demu amdai mwenyewe akitaka niwakutanishe niko tayari. Ila sio yeye kuongea na mimi chochote. Hiyo option akaikataa. Akasema yeye hamdai, ila anajua nimedanganywa sana, anataka kuniambia ukweli ili nikiamua kuendelea na Sharifa niendelee naye nikijua nadili na mtu wa namna gani. Alichomfanyia yeye anaweza kunifanyia mimi. Mi nikaweka msimamo siko tayari kuonana nae. Basi akasema yote aliyotaka kuniambia ataniambia humo humo mesenja kwa sababu sitaki tuonane. Akaanza meseji ya kwanza, Gazeti; ya pili Gazeti, ya tatu gazeti. Nikachoka kusoma nikalala. Halafu wife alishaanza kufuatilia hapo kitandani baada ya kuona niko bize sana Facebook isivyo kawaida. Nilivoamka usiku saa tisa hivi nikamkuta mshikaji ametuma meseji zaidi ya 20, yote magazeti, na bado yuko online. Asubuhi nilivofika ofisini nikawaza yale magazeti kuyasomea kwenye simu macho yatauma. Nikazikopi meseji zote nikapesti kwenye MS Word nikaprint ili nisome. Zilikuwa page 9 za MS Word, font size 11 line spacing 1.15. Jamaa aliandika aisee. Cha msingi alikuwa anajaribu kunithibitishia kuwa yule ni kama mke wake tu, ilibaki hatua moja tu ya Kwenda kwa sheikh. Kila nilichomkuta nacho amenunua akiwa nae na mpaka wiki iliyopita kabla hajahama yeye alikuwa anajua wako pamoja, kumbe demu alikuwa na mipango mingine. Na akaniambia pale demu aliponidanganya ni kwa dada ake ni yeye alimpangishia, na yule sio dada yake ni mpangaji mwenzie. NUSU YA ALIYOYAONGEA YALIKUWA YA KWELI KABISA, ROBO nilihitaji kuunganisha doti kuyathibitisha, na ROBO yalikuwa ya kupika ili nimuache huyo demu. Sababu alikuwa anataja vitu vingine ambavyo nilikuwa na uhakika kuwa havikuwa kweli. Mfano alisema mwaka 2018 mwezi 3 (demu akiwa mjamzito) walienda kijijini kwao na demu kusalimia, ili anihakikishie kuwa mpaka demu akiwa mjamzito walikuwaga wanaendelea na mipango ya ndoa kama kawaida. Na tarehe alizotaja mimi mwenyewe nilikuwa na demu Mbeya, Njombe na Songea. Nilizisoma zile kurasa 9 huku jasho linanitoka. Kitu alichothibitisha tu ni kuwa vyovyote ilivyo YULE MTOTO ALIEZAA SHARIFA SIO WAKE ila yeye aliamua kuishi nae hivo hivo tu kwa sababu anampenda.
Kwa kifupi tu miaka yote mitatu niliyokuwa na demu, na jamaa alikuwemo. Kwa hiyo mimi nilikuwa naiba demu wake.
LAKINI KAMA SHARIFA ALIVOSHAURI NIKAAMUA KUMTOSA MSHIKAJI ILI NIWE NA YEYE. Nikamjibu jamaa Ex kuwa, yoooote aliyoniambia nimemuelewa, ila mimi nimeamua kuwa na Sharifa hivo hivo. Nampokea na mapungufu yake yote, mpaka atakaponiambia kuwa anarudi kwa kwake. Kwa hiyo kama yeye anamtaka Sharifa aangalie jinsi ya kumshawishi arudi kwake, sio kunishawishi mimi nimuache Sharifa kwa sababu ya kunidanganya. Kitu pekee kinachoweza kunifanya nimuache ni kama akisema mtoto LISA ni wake (ambaye yeye alishanithibitishia kwenye meseji za FB sio wake). Jamaa akajua tu stori aliyonipa sijamwamini ndio maana msimamo wangu uko palepale.
Basi akanitakia maisha mema mim na Sharifa (Mama Lisa) akasema ukweli huwa haujifichi. Kuna siku ntathibitisha kuwa yote aliyoniambia ni ya kweli. Mimi na Mama Lisa tukaendelea na maisha. Mpaka hapo nilikuwa sijajua huyo jamaa ndio lile jamaa lilikuja siku ileeeeee kwa sharifa likaingia bila hodi likatukana wakati linaondoka. Na yeye kwenye meseji zake zooote hakugusia hilo, aligusia tu matukio mengine mawili ambayo mimi na yeye tulikutana pale kazini kwa demu lakini tukiwa hatujui wote tuko pale kwa ajili ya demu mmoja. Demu alikuwa ametukalisha maeneo mawili tofauti ya mgahawa, anaenda kule dakika 5 anakuja kwangu dakika 5. Mpaka mi naondoka sikugundua kitu na jamaa hakugundua. Walikuja kumsimulia siku alivorudi pale kumtafuta demu alivomtoroka kule alikokuwa kampangishia Temeke.
Sasa mwaka 2020 nikapata safari ya Dodoma na mtoto akawa amekua. Tukaenda wote na Sharifa tukakaa siku mbili. Siku nyingine nikapata safari ya Mwanza tukaenda wote wakati wa kurudi tukapitia Dodoma tukalala siku moja kesho yake tukaondoka kurudi Dar. Tulivofika Dar baada ya siku kadhaa nikamwambia twende tukamsalimu dada yake, mimi nimemmiss. Tukaenda. Hiyo ilikuwa mara ya pili tunaenda baada ya mimi kumlazimisha lazimisha. Mpaka wakati huo huyo anayesema ni dadake hajawahi kuja makao mapya ya mdogo wake, yaani toka alipohamia 2018 hajawahi kuja. Sasa mimi nilivowatua tu pale Temeke, wife (original) akanipigia simu anataka kwenda maeneo ya huko huko Temeke, nikamwacha Sharifa na Lisa huko Temeke niende nikampeleke wife anakotaka kwenda halafu hawa ntarudi kuwachukua jioni.
Wakati natoka Temeke nianze kumfuata wife home, kuna jamaa jirani (wwa Sharifa) wa nyumba ya pili akaniomba lift, tulikuwa tumeshazoeana kile kipindi nilichokuwa namfuataga Sharifa huko. Njiani akaniuliza tunakujaga kufanya nini huku? Kwanza nikashangaa, lakini nikamjibu kuwa tunakujaga kwa dadake Sharifa kumsalimia. Akauliza dadake yupi? Mbona hana dada maeneo haya? Nikamtajia. Akashtuka kidogo halafu akaniambia wale sio ndugu hata kidogo. Ni wapangaji wenza tuu. Mpaka wakati huo mimi nilikuwa naamini kabisa huyo ni dada wa Sharifa tumbo moja, mpaka namlazimisha kuja kumsalimu. Nikawa nambishia jamaa wale ni ndugu kabisa! Jamaa akanipa na ushahidi mwingine kunithibitishia kuwa wale ni wapangaji wawili tofauti na wamekutania pale pale. Na wote wamemkuta na walihamia kwa nyakati tofauti na wote amewazoea vyumbani mwao anaingia kama kwake. Kwamba pale hakuna chumba na sebule ni vyumba viwili vinavojitegemea. Kwanza hata makabila yao tofauti, huyu anayesemwa ni dada ni wa Kigoma wakati huyu mwingine ni wa Njombe. Moyo ukalia PAAAAAA! Ningeweza hata kuangusha gari.
Jamaa alipofika anakoenda akashuka, bila hata kujua amenivuruga kiasi gani. Hapo ndio nakumbuka maneno ya yule Ex wa Sharifa kuwa aliniambia pale ni yeye alimpangishia. Nikajikaza kiume nikaenda mpaka home nikamchukua wife nikampeleka anakotaka kwenda, uzuri wake ilikuwa ni maeneo ya huko huko Temeke, halafu mimi nikaenda nilikowaacha Lisa na mama yake. Njiani nikapaki gari mahali pazuri pasipo na kelele nikampigia simu yule dada yake wa Mbagala. Hapo sasa picha ishanijia kuwa kweli huyu wa Temeke atakuwa sio ndugu yake Sharifa. Yule wa Mbagala wanafanana. Nikampigia huyo wa Mbagala nikamwomba tu aniambie ukweli kuhusu hivi vitu. Je pale nilipomkuta Sharifa anakaa alikuwa kapanga au anakaa kwa yule aliyesema ni dada yake? Mbili, Je yule wa Temeke ambaye Sharifa aliniaminisha ni ndugu yao, ni ndugu kweli au nayo ni uongo? Akaniambia yule sio ndugu wamekutana nae pale na pale Sharifa alikuwa amepangishiwa na yule Ex. Lakini mdogo wake alishamwambia kuwa yeye ameamua kuachana nae ili awe na mimi ila hajui aniambieje, na yule jamaa kila akipotezewa haelewi wala nini, anakuja tu kwa sababu yeye ndio alimtafutia demu nyumba, na mpaka wakati demu anahama pale mpangaji aliyekuwa anatambulika ni mwanaume. Akasema alishamshauri mdogo wake aniambie ukweli kama nampenda kweli ntaelewa mdogo wake akamwambia haina haja kwa sababu mimi namhamisha pale kwa hiyo hayo yatakuwa yalishapita hayatakuwa na nafasi kwenye mahusiano yetu. KWA KWELI SIKU HIYO MUNGU TU NDIO ANAJUA ILIISHAJE ISHAJE.
Sasa basi jioni ilipofika nikamfuata Sharifa na mtoto kuwarudisha kwao. Sikumuuliza wala nini. Kesho yake asubuhi nikasafiri. Nilipofika Dodoma siku hiyo sikulala. Nikamwambia nimeshathibitisha kuwa mambo mengi aliyoniambia ex wake yalikuwa ya kweli na nimepata uthibitisho kutoka chanzo cha kuaminika kabisa. Akabisha bisha kidogo, nikamkumbusha matukio yote yaliyopita ambayo yanathibitisha kuwa kuna ukweli mkubwa. Ikiwemo yule jamaa alivokuja siku tukakutana pale yeye akiwa mjamzito, safari za dodoma zote tulizoenda hajawahi kuongelea kumtafuta huyo dada yake ambaye alisema yule jamaa ndio mume wake, siku tulizokutana wanaume wawili kazini kwake alivobabaikaga, na mambo mengine. Akawa mnyonge sana. Mwisho wa maongezi akaniambia kama nimeamua kumwacha basi, ila kwa miaka mitano tuliyokuwa pamoja, hajawahi kuwa na mahusiano na huyo jamaa. Ila jamaa alikuwa anaenda pale kwake kutaka wasuluhishe warudi kama zamani na yeye alikuwa anamkatalia, lakini hakuwa na cha kufanya. Akasema yeye toka tulipokutana miaka 5 iliyopita moyoni kwake nilikuwepo mimi tu hayo mengine ilikuwa ni ngumu kutatua kwa sababu za kihistoria. Kwa kifupi alikana kabisa kuwa kwenye mahusiano yoyote na ex wake wala mtu mwingine yeyote. Akasema ndio maana tunachati masaa 24, ananitumia picha masaa 24, video call napiga muda wowote hata saa nane usiku (mfano nikiwa safarini) na hajawahi kuacha kupokea simu yangu wala kujibu meseji yangu hata awe wapi (YOTE HAYA YA KWELI). Kama nilivosema mwanzo kwa miaka yote 7 niliyokuwa nae toka 2015 mpaka leo (BADO TUPO WOTE KAZAA NA MTOTO MWINGINE MWAKA HUU), hajawahi kuchelewa kupokea simu yangu, hata awe anafanya nini, hajawahi kukosa kujibu meseji yangu, hajawahi kufuta meseji yangu wala simu yangu, hajawahi kuacha kunitumia picha nikidai popote alipo, hajawahi kuficha simu yake nikiwepo. Yani nikifika tu kama kuna changamoto ya simu atanipa nishughulikie, kama kuna kitu interesting cha kunionyesha humo kwenye simu yake atanikabidhi simu niendelee kucheki yeye anaenda zake nje kupika. Simu yangu ikizima chaji halafu yeye anapika sina kampani, atanipa simu yake nicheki cheki instagram na FB bila hofu yoyote. YEYE NDIYE MTU AMBAYE NIKIWEKEWA BASTOLA NIKAAMBIWA NIMPIGIE MTU MMOJA TU ASIPOPOKEA WANANIPIGA RISASI, NTAMPIGIA YEYE.
Basi nikaamua kuachana na yaliyopita tusonge mbele. Sikuwahi kuuliza kitu tena kuhusu Ex mpaka mwaka huu 2022.
NAENDELEA KUANDIKA