Usichanganyikiwe na Dunia, mambo ndivyo yalivyo. Tuna Wanawake Malaika lakini hatuna Malaika wa Kike

Sweya Makungu

JF-Expert Member
Jun 11, 2023
479
556
Usichanganyikiwe na Dunia, Mambo Ndivyo Yalivyo..

Tuna Wanawake Malaika lakini Hatuna Malaika wa Kike..

💫💫💫💫💫
©️ Mwl. Makungu m.s
0743781910

Ndugu yangu unapokuwa katika dunia hii mengine acha tu yakupite au yaende hivyo hivyo Kama unahisi ni mazito kwako. Vinginevyo utajichanganya . Nakusihi usichanganyikiwe.

Duniani;
Tunawaita wanawake malaika (Angel) , lkn tunawaita wanaume majina ya malaika ( Gabriel/ Mikaeli).. Kwahiyo tuna wanawake malaika lkn hatuna malaika wa kike..

Ulishawahi kujiuliza kwanini Kuna suruali za kike lkn hakuna sketi za kiume? Bado hujagundua tu kuwa mwanzilishi alikuwa na matatizo ya kisaikolojia?

We haushangai ! Ukimuita mwanaume malaika (angel) mnaweza msielewane ,lkn ukimuita mwanaume jina la malaika(gabriel/mikaeli) ni baraka kubwa ..

Iko hivi , Wanawake wanatamani kuwa wanaume ( vichwa) na ndiyo maana wengi wanadai dhana ya 50/50 bila kuielewa lkn wanaume halisi hawatamani kuwa wanawake ndiyo maana 50/50 inaapply ktk kila muktadha isipokuwa kwenye ndoa.. Kwenye ndoa huwa Kuna 100/100 , yaani mwanaume atabaki kuwa mwanaume na mwanamke atabaki kuwa mwanamke..

Duniani wote Tunatamani kwenda mbinguni lkn hatupendi kufa . Na wanaopenda kufa kwa makusudi hawaendi mbinguni..

Usichanganyikiwe, Wapiga zumari wa mfalme si sawa na wapiga ramli wa mfalme . Wapiga zumari wa mfalme ni kwaajili ya mfalme lkn wapiga ramli wa mfalme ni kwaajili ya ufalme . Wapiga zumari wanamburudisha,wanamfariji na kumsifia mfalme lkn wapiga ramli wanamtafutia mfalme maono ya utatuzi wa matatizo ya ufalme.. Ndiyo maana nyakati hizo ilikuwa ni heri kwa mfalme kuwa na wapiga ramli wengi kuliko wapiga zumari..

Mtoto wa mpishi hodari asiyejua kupika ana maana kubwa sana kwa mtoto wa mkulima hodari asiyejua kulima kwenye ardhi ya wavuvi hodari..

Kwenye hii dunia , ni rahisi kumkuta mtoto wa kikristo akizungumzia habari za "Mungu anayestahili kusujudiwa" na wakati huo huo akimshangaa mtoto wa dini nyingine ambaye ameanguka kifulifuli kusujudia .. Tunahubiri tusichokitenda na tunatenda tusichokihubiri . Waelezeni watoto ukweli kuwa tafsiri halisi ya kwanza ya kusujudu (kuanguka kifulifuli) ni kitendo cha kupiga magoti na kuinama kugusisha paji la uso kwny ardhi kwaajili ya kumpa Mungu utukufu.. Na kitendo hiki hakijapitwa na wakati maana mpk muda huu ninapoandika andiko hili ,wale wenye uhai wanne na wale wazee 24 wanaokizunguka kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu wanaendelea kusujudia wakisema " wastahili, wastahili wewe Bwana kuabudiwa na kupokea utukufu"..

Binadamu wanaiga mambo vibaya . Kuna wakati Yesu alikuwa akipewa taarifa za wagonjwa haendi anasubiri mpk wanakufa kwanza halafu ndiyo anaenda kuwafufua. Siyo kwamba alikuwa na kiburi bali alikuwa anataka kuonesha uwezo wake..
Na sisi tumemuiga tabia yake . Tunapopewa taarifa za mgonjwa hatuendi wala hatuchangii matibabu tunasubiri mpk akifa ndiyo twende msibani tukaoneshe uwezo wetu wa kuchangia jeneza, vyakula, vinywaji na magari ili msiba uwe wa kifahari..

Usipoielewa hii aya chini Wala hata usichanganyikiwe . Tulia tu mpk nitakapoitolea ufafanuzi kwenye andiko lake.

Iko hivi,
Kuna tofauti kati ya Boss na mtoto wa Boss. Na kuna tofauti kati ya mtoto wa Boss na Boss mtoto . Boss na Boss mtoto wanaweza kuwa na cheo sawa ktk makampuni tofauti . Lkn Boss na mtoto wa Boss hawawezi kuwa na cheo sawa ktk kampuni moja ..

Duniani ,Wapo watu ambao ukiwa kapera huwezi kuwa kiongozi wa dini . Na wapo watu ambao huwezi kuwa kiongozi wa dini mpk uwe kapera . Na dini yao ni moja . Usichanganyikiwe , wote wapo sawa. Maandiko yametoa option. Kwahiyo, ajidhaniaye ya kuwa amesimama aangalie asianguke.

Mwenda juu kipungu hafikii mbinguni.. Kwahiyo ukiwa mtu wa goto, pendelea kugotoa ili usije ukagoteza.. Nawakumbusha kuwa Kuna kamusi ya kiswahili..

Ukijifunza kisa cha mfalme Sauli na nabii Samwel utagundua kuwa ,wanadamu tuna tabia ya kuwakataa hadharani waganga na watu wenye pepo wa utambuzi lakini tunawategemea sirini ..

Tulizoea kuona watu wana kabila na hawaelewi lugha za kabila zao. Lkn siku hizi tuna watu wenye dini na hawaelewi maandiko ya dini zao. Mafundisho yoyote tu yanawachukua .

Ni kawaida duniani kumkuta mtu anaitwa Jesus lkn ni ajabu Sana kumkuta mtu anaitwa Yesu..

Usichanganyikiwe kabisa na mambo ya hii dunia , we tafuta kuujua ukweli na ukiujua uuishi huo ukweli siku zote za kusafiri kwako chini ya jua ....

Mungu awabariki nyote ndugu ktk imani.

Makungu m.s
0743781910
23 March 2023
 
Back
Top Bottom