Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,513
Habari wakuu,
Niende moja kwa moja kwenye mada yetu isemayo, Dunia inaenda kasi, kulea mtoto wa kiume ni kazi kuliko wa kike.
Hapo zamani kidogo, ilikuwa mzazi kulea mtoto wa kike alikuwa na hofu maana alihofia kuwa angeweza pewa mimba.
Wazazi wote walikuwa wakali kama Simba kwenye malezi ya watoto wao wa kike, vitisho na vipigo vilitumika ili kuwalea.
Malezi hayo yaliambatana na hofu nyingi baina ya wazazi wa jinsia zote yaani wazazi wa kiume na wakike.
Kila mzazi alichukua jukumu la kumlinda Binti yake asijeharibikiwa na kupata ujauzito ukakatiza ndoto za elimu.
Hakika Dunia inaenda kasi maana Sasa imekuwa ni kinyume chake maana kila jicho la mzazi linaangalia mtoto wa kiume.
Mtoto wa kiume saivi amekuwa kama almasi, analindwa zaidi ya almasi halisi.
Akiwa anaenda kucheza mtoto wa kiume anaangaliwa zaidi ya mtoto wa kike, maana anaweza haribiwa.
Hii imetokana na kuwa na vitendo vya ushoga vinavyoendelea Duniani na watoto wa kiume ndio walengwa wakuu.
Wazazi wote wa kiume na kike wana hofu na watoto wao wa kiume zaidi kuharibiwa zaidi watoto wa kike.
Imefika mahali wazazi wamekuwa hawataki watoto wao wa kiume wasome Bweni kwa kukosa Imani.
Wazazi wa pande zote kiume na kike wamewasahau watoto wa kike saivi macho yao yapo kwa wa kiume.
Hofu imetawala kwenye malezi ya watoto wa kiume, wazazi hawana amani tena.
Ndio maana nasema Dunia inaenda kasi, kulea mtoto wa kiume ni kazi kuliko kulea mtoto wa kike..