Mwambie Kijana Wako asichanganye Gender Equality (usawa wa kijinsia) kwenye Gender Roles (majukumu ya kijinsia) Katika Utamaduni Usioendana

Sweya Makungu

JF-Expert Member
Jun 11, 2023
479
556
Mwambie Kijana Wako Asichanganye Gender Equality (Usawa wa kijinsia) Kwenye Gender Roles (majukumu ya kijinsia) ktk Utamaduni Usioendana..
💫💫💫💫💫
© Mwl. Makungu Ms.
0743781910

Wakumbushe vijana wako kuwa definition ya neno "gender" imebeba neno "social and cultural" likiwa na maana ya "mambo ya kijamii na kiutamaduni/kimila". Kwahiyo wasichanganye tamaduni za uzungu kwny mazingira ya kiafrika kwa mwamvuli wa gender equality. Tamaduni za duniani hazifanani.

The term gender refers to the cultural and social constructed characteristics attributed to men and women on the basis of perceived biological differences.

Mkumbushe binti yako ya kuwa ktk biblia kulikuwa na Wanawake wengi manabii lkn hapakuwahi kuwa na mwanamke kuhani (kiongozi wa dini anayeendesha ibada). Kwahiyo wajifunze kutofautisha kati ya nabii na kuhani.

Usiache kumwambia kuwa mtume Paulo ameandika "siruhusu mwanamke kuwa kiongozi wala kuhutubu mbele ya kanisa, na awapo kanisani akae kwa utulivu".

Lkn mwambie ya kuwa mimi mwandishi sina tatizo lolote na wanawake wachungaji na ninamtia moyo aendelee na huduma kwa kuwa biblia imeandika "lolote mtakalolifungua duniani kwajili ya utukufu wa Mungu na mbinguni litafunguliwa". Mstari huo nadhani unamaliza ubishi juu ya uhalali wa wanawake kuwa wachungaji Ikiwa mmekubaliana kulifungulia Jambo hilo.

Swali langu mm ni moja tu kwa viongozi wa dini, Ikiwa Biblia imetupa kibali na ruhusa ya kufungulia mambo duniani kwajili ya utukufu wa Mungu, "kwanini tunafungulia baadhi ya mambo na tunayaacha yale makubwa yanayolitesa kanisa? Kiasi kwamba tunasababisha mpk ongezeko la single mothers duniani???

Mkumbushe binti na kijana wako waisome vizuri ile mistari ktk biblia inayosema " kichwa cha kila mwanamume ni kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume. Haimpasi mwanaume kufunikwa kichwa kwa sbb yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanaume. Maana mwanaume hakutoka ktk mwanamke. bali mwanamke ktk mwanaume. Wala mwanaume hakuumbwa kwaajili ya mwanamke, bali mwanamke kwaajili ya mwanaume. kwahiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwaajili ya malaika. Walakini si mwanamke pasipo mwanaume, wala mwanaume pasipo mwanamke. Maana kama mwanamke alitoka ktk mwanaume, vile vile mwanaume naye huzaliwa na mwanamke, na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu". (1 wakorintho 11:3> ).

Mkumbushe kijana wako wa kiume kuwa biblia imesisitiza " kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe".

Kwahiyo kijana wako akitaka ndoa yake iwe na amani azingatie matumizi ya akili.

Umkumbushe binti yako agizo lisemalo " enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe," . Usisahau kumwambia kijana wako agizo la " enyi waume, wapendeni wake zenu, kama kristo naye alivyolipenda kanisa. Maana ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe".

Tatizo la siku hizi maagizo haya yamegeuzwa, wanawake wamejipa jukumu la kupenda na wamejisahaulisha jukumu la kutii. Na wanaume wamelipuuza jukumu la kupenda na wamejibebesha jukumu la kutii wake zao. Ndiyo maana ndoa nyingi za sasa zimepigwa pigo zito.

Unaweza kukubaliana na maelekezo ya mke wako kwa kutumia akili, lkn hulazimiki kutii.

Wakumbushe kuwa, tunayo majukumu yetu yanayotofautishwa na uanaume wetu na uanamke wetu. Naona vijana wengi wa vyuoni hawaelewi vizuri juu ya hii mada inaitwa "gender". Wanachanganywa sana na hizi gender equality, gender roles na sex roles.

Gender equality ni usawa kwny fursa kwa mwanaume na mwanamke bila kujali jinsia.

Gender roles ni majukumu ya kijamii ya mwanaume na mwanamke kwa kuzingatia jinsia.

Sex roles ni majukumu ya kiume na ya kike yanayofanywa na viungo vya uzazi kwa kuzingatia maumbile ya kila jinsia.

Na gender yenyewe imebeba neno social and cultural.

Kwahiyo mwambie kijana wako na binti yako asichanganye gender Equality kwny gender roles ktk utamaduni usiohusika. Ataanzisha mgogoro wa ndoa yake mwenyewe.

Mkumbushe tu kwamba, ni kweli kuna tabia nyingine ni kasumba tu (stereotype) kuwa kuna majukumu ya kiume na ya kike ndiyo maana kuna vijana wanawapikia na kuwafulia wake zao. Lkn usisahau kumwambia, pamoja na hayo , hata kijana akimfanyia mke wake majukumu ya kike kiasi gani, hawezi kufanya hivyo mbele ya wakwe zake na wala hawezi kukuta msibani wanapika wanaume. Kwahiyo suala la utamaduni/mila linabaki palepale.

Usichanganye gender equality kwny gender roles ktk utamaduni usioendana.

Mkumbushe kijana wako wa kiume na binti yako ya kuwa, mwanamke anaweza kuwa nguzo na msaada mkubwa wa kiuchumi ktk familia na akabaki kumuheshimu mumewe kama kichwa na kiongozi wa familia. Kuwa na uchumi wa kuendesha familia inamfanya mwanamke kuwa mke mwema (soma mithali 31:10-31) lkn siyo kichwa cha familia. Na mwanaume kuwa kichwa cha familia haimfanyi mwanaume kuwa provider wa kila kitu kinachohusu uchumi kwny familia.. Andiko hilo juu linathibitisha.

Mwambie binti yako ya kuwa, tunayo fursa sawa lkn hatuna majukumu sawa. Mkumbushe kuwa japo siku hizi kuna single mothers na single fathers wengi, haimaanishi single mother anaweza kuwa baba au single father anaweza kuwa mama. Haikuwa mpango wa Mungu mwanaume au mwanamke aishi peke yake. Hiyo ni mipango tu ya wanadamu na shetani ktk kuivuruga dunia na mfumo wa Mungu.

Binti yako akiwa mgumu kuelewa maana, umfafanulie kuwa, tuna fursa sawa za ajira jeshini lkn hatuna majukumu sawa kwenye uwanja wa vita.

Tuna fursa sawa kwny ajira za polisi lkn hatuna majukumu sawa kwny kumkagua mtuhumiwa.

Tuna fursa sawa kwny ajira za ualimu lkn hatuna majukumu sawa kwny ulezi wa wanafunzi.

Tuna fursa sawa kwny uongozi ktk nyanja zote lkn ni nadra sana au huwezi kukuta kabisa mwenyekiti na makamu wake au Rais na makamu wake wote ni wanawake. Labda ktk vyama vya wanawake tu.

Siyo jambo geni kukuta mkutano wa wanawake umeandaliwa na wanaume. Lkn inafikirisha kukuta mkutano wa wanaume umeandaliwa na wanawake.

Tunazo fursa sawa za ufundi makanika lkn injini haishushwi na mwanamke.

Tunazo fursa sawa za kushiriki ktk mambo ya kijamii lkn kaburi halichimbwi na mwanamke.

Tunazo fursa sawa za malezi ya watoto lkn baraka za mwisho za kurithisha/kukabidhi ukoo kwa watoto hazitolewi na mwanamke wala hazitolewi kwa mtoto wa kike (soma biblia yako vizuri).

Waambie vijana wako kuwa , mbinguni hakuna usawa. Mbinguni kuna haki. Kwahiyo wasichanganye gender equality kwny gender roles ktk utamaduni usioendana, wataharibu ndoa zao na jamii. Mambo ya wazungu wawaachie wazungu. Wajivunie kuwa Waafrika ..

Makungu Ms.
0743781910
JN 19 sept 2023
 
Tatizo ni malezi ya vijana wa kiume, hawa wanaoshinda insta, wakikata mauno,akitendwa kidogo, anajiua,
Tatizo la tamaduni za ki Afrika, kuna watu wanaamin kuwa kuna kazi haziwezi kufsnywa na mtoto wa kike,huu ndio upuuzi, taasisi niliyofsnya kazi miaka ya 80,ya wazungu, kulikuwa na mafundi wanawake,madriver wanawake, Wanajeshi wa vyeo vya juu(sio wa bongo wa kupewa),
Niliwahi kukutana na binti mdogo, ni muhandisi wa umeme, anafanya kazi ya kufunga madishi(microwave antena) kwenye minara ya, simu, mtoto wa kike, anapanda mnara wa mita 100,anaendesha cruza kilometa 400 kila siku.
 
Umemuelewa mwamba lakini?
 
Mwambie Kijana Wako Asichanganye Gender Equality (Usawa wa kijinsia) Kwenye Gender Roles (majukumu ya kijinsia) ktk Utamaduni Usioendana..

Mwl. Makungu Ms.

Back
Top Bottom