Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
Hello habari za asubuhi!

Hii story nimewahi kuwasimulia wachache sana.

Ni rahisi kumtia moyo mtu kuwa magumu yatapita, Mungu atakusaidia kipindi uko vizuri na umeshiba. Ila ukipitia kipindi kigumu hata ushauri na courage utasikia kama kelele tu unapigiwa.

Nilihitilafiana na wazazi pamoja na ukoo nzima 2009 kwasababu ya kuingia katika Imani tofauti.
Kwakweli yule baba yangu ana roho mbaya sana, hata sasa hajawahi kunitafuta. Nami natamani kwenda kumsalimia na kumpa msaada lakini msimamo wake ni kwamba niende kwake nikairudie dini yangu ya zamani kitu ambacho Mimi sikiafiki, sitakiafiki na hakitatokea hata kwa kuchinjwa.

Sasa katika maisha ya kuhangahikia ugali pasi na sapoti ya mtu (mzazi, mlezi, ndugu n.k) nikajiendea mgodini. Nikaenda kupiga kibarua kwa siku elfu 7, nilienda Mgodini November , December mgodini pakawa na mapumziko ya sikukuu hivyo watu wote tulipaswa kuondoka mgodini mpaka January.

Nikiwa na pesa kidogo sijui nifanye nini au niende wapi nikaamua niende Mkoa wa Ruvuma Tunduru.
Safari ya kwenda Tunduru nikitokea Nachingwea (Lindi) ikaanza. Kwakuwa nilitumia Lori Tunduru tulifika siku ya pili . Nimefika Tunduru mchongo niliouendea ukagoma hivyo nikaunga mpaka Songea. Nafika Tunduru mfukoni nina pesa ndogo sana hata elfu 2 haifiki. Safari ikaendelea barabara chafu maana ni masika. Njaa inauma Lori likisimama naangalia huku na kule kama kuna mwembe nikaangalie maembe.

Njaa ikaongezeka Songea tulifika kwa kuchelewa, Lori lilibeba nazi hivyo sometimes nilipata nazi zilizovunjika zenyewe na kuanza kula. Tumefika Songea usiku wa saa 4, sina ndugu, Sina hata mia na ni mgeni huko
Am back. Basi ile sijui niende wapi, nikaanza kuelekea mahali kwenye kelele nikafika stand kuu sasa pale nina njaa plus usingizi. Nikajichanganya kwa machokoraa wa stand, Mungu awainue huko waliko, wakanipa andazi moja na chai kikombe kimoja. Niliwashuru sana, pale stand hapakuwa na lounge ya abiria kipindi hicho. Sijui sasa kukoje. Nikapita mitaani kuzurura kutafuta mahali nilale nikapata mahali pembezoni mwa mji nikalala kwenye shamba la mahindi. Asubuhi nikashikwa na polisi nikiwa stand na kupewa kesi ya uzururaji, jumla ya watuhumiwa tulikuwa kama 15-20.

Tukiwa korokoroni gari ya super Feo iliyokuwa ikitoka Songea kwenda Dar es salaam ikapata ajali. Sasa mkuu wa kituo akaamuru tubebwe tupelekwe Central halafu wale maaskari wakaatend ajali. Ile tunapandishwa kwenye gari tukitokea ndani kituoni kuingia kwenye karandinga mmoja mmoja Mimi nikafichwa na wingu la Mungu hawakuniona wakawasha gari wakaondoka . Polisi si chini ya watano wote hawakuniona ilhali nilisimama mbele yao na wengine niliwagusa.

Next day tena nikarudi stand, nikachujua nguo zangu nzuri nikaziweka mkononi na kujigeuza mmachinga. Nilizunguka manispaa yote, Aisee katika kipindi kigumu kila solution hugeuka kuwa ngumu. Nguo nilianza kutangaza nauza kwa elfu 5 , nikashushe bei ikawa elfu 3 na mwishowe nikawa nauza buku buku lakini hata moja sijaiuza.

Siku ikaisha njaa Kali, nikalala nje. Kila nikijaribu kuomba kazi yoyote hata kulima au kulishia ng'ombe nilikosa. Watu wanasema hawanijui hivyo hawawezi kuniamini. Hapo nilikuwa nimeibiwa vitu muhimu ikiwemo daftari la namba za simu, I'd ya kupigia kura na I'd ya skuli maana nilikuwa ndo nimetoka kumaliza form four.

Siku moja nikiwa taabani fundi viatu akanisaidia 500 ila suala la kunisaidia makazi ya kulala hakuweza sijui kwanini . Nikifurahi sana nikaanza kuzungukia migahawa nikaupata mmoja nikapewa ubwabwa wa 500 mwingi sana nikala huku nahemea maana nilikuwa nikikuta chocote kitu barabarani changu iwe muhindi, karanga au hata dagaa namla.

Kwa ufupi sasa niko Da es salaam, nimeajiriwa na Kaisari, nina familia yenye furaha na amani, niko kwenye uchumi wa kati.










Am happy.
YESU ni BWANA
 
Hello habari za asubuhi!
Hii story nimewahi kuwasimulia wachache sana.
chafu maana ni masika. Njaa inauma Lori likisomama naangalia huku na kule kama kuna mwembe nikaangalie maembe.
Njaa ikaongezeka Songea tulifika kwa kuchelewa, Lori lilibeba nazi hivyo sometimes nilipata nazi zilizovunjika zenyewe na kuanza kula.
Tumefika Songea usiku wa saa 4, sina ndugu, Sina hata mia na ni mgeni huko
Am back
Ulikuwa hujaiona misikiti, au huzijuwi nyumba za Waislam?

Hakuna msikiti au Muislam atakunyima kula, siku nyingine ukisikia njaa, jitose msikitini tu uwaambie Waislam shida yako, utakula mpaka ukitazame macho chakula.

Hivi unaishi Tanzania au wapi?
 
Ulikuwa hujaiona misikiti, au huzijuwi nyumba za Waislam?

Hakuna msikiti au Muislam atakunyima kula, siku nyingine ukisikia njaa, jitose msikitini tu uwaambie Waislam shida yako, utakula mpaka ukitazame macho chakula.

Hivi unaishi Tanzania au wapi?
Watanzania wengi tabia zao za ukarimu, uungwana na kusaidiana huwa zinafanana. Hivyo hii hoja yako ya kuhusu misikiti, sijui waislam na bla bla nyingine! kwa mtazamo wangu naona ni hoja ya kidwanzi..
 
Ulikuwa hujaiona misikiti, au huzijuwi nyumba za Waislam?

Hakuna msikiti au Muislam atakunyima kula, siku nyingine ukisikia njaa, jitose msikitini tu uwaambie Waislam shida yako, utakula mpaka ukitazame macho chakula.

Hivi unaishi Tanzania au wapi?
Huyu inaonekana alikua ameshakua Murtard adhabu yao ni kifo, naona mateso yali muanza mapema tu kwa hicho kitendo......baba mzazi alikua sahihi kama kweli ulikua Murtadi na mimi siwezi kukutafuta tena.
 
Ulikuwa hujaiona misikiti, au huzijuwi nyumba za Waislam?

Hakuna msikiti au Muislam atakunyima kula, siku nyingine ukisikia njaa, jitose msikitini tu uwaambie Waislam shida yako, utakula mpaka ukitazame macho chakula.

Hivi unaishi Tanzania au wapi?
Mshukuru mungu Kama hujawahi kutana na nyakati za dhiki, na omba mungu usishuhudie kizazi chako kikikumbana na nyakati za dhiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom