Nilimaliza siku nne bila kula chochote, Nilikuwa naona kifo hiki hapa

Jun 17, 2023
93
220
Baada tu ya kumaliza Elimu nikawa nimefanyiwa kajisherehe flani pale home wakanipa na zawadi kati ya zawadi hizo kulikuwa na pesa.

Nikaona hapa hapa nianze mchakato wa kuhama home. Maana niliona home ni kama wameanza kunizoea sasa. Kuna vi ishu vidogo dogo wananiambia nami niwe nafanya wakati madogo wapo. Nikaona tu hapa mzee anaanza kujenga mazoea nami.

Nikawaza nikaona huko mbeleni wataniambia niwe namsaidia dada kuosha vyombo. Maana mzee alishaanza kusema niwe nikiamka asubuhi kama siku hiyo sitoki nihakikishe uwanja upo safi, niwe naosha gari pia. Niwe nawaandalia dogs msosi.

Nikaona mazoea yameanza. Halafu kale kadada ka kazi nikaanza kugundua kumbe ni kazuri bwana. Sikuwa tu nakaangalia kwa utulivu siku za nyuma. Nikaona kananawiri na kuanza kujengeka.

Nikaona haka naweza kukala kuliko kusubiria nipate pesa then ndo nionane na Fatou maana Fatou ilikuwa mpaka guest house. Mbayo angalau standard tsh 15,000 hamjala na kunywa soda. So angalau 40 kwa siku na usafiri. Kuipata hiyo ni baada ya kujichanga mwezi au zaidi. So nikawa nawaza naanzaje maana sina uzoefu.

Mazeri naye akawa anani check sana.akiona nipo kimya sana room anakuja kugonga ananipa kazi...nikawa nasema sijui anahisi najichukulia sheria mkononi?au nacheck porno?

Wakati huo huo ananicheck namwangalia vipi dada mwanaisha toka Tanga.ndo alikuwa dada yetu wa kazi.basi nikawa sina raha home.

Nilipopata zile zawadi na pesa nikaona nitafute ghetto.maana nlikuwa nawaonea wivu sana wenzangu waliokuwa wanaishi ghetto.nikaona hapo niongee na jamaa yangu ambaye naye alikuwa na mawazo kama yangu.

Tukaamua kuzichanga.tukaenda tafuta room ubungo riverside.tukanunua godoro jiko,masufuria,ndoo na vyombo kadhaa vya kuanzia TV na subwoofer yangu nilinunua nikiwa chuo.maisha yakaanza.

Home niliwaaga kuwa nimepata kakibarua sehemu sasa inabid niwe karibu na ofisi coz pia nitakuwa nasafiri safiri au narudi late hours so ili kuepusha usumbufu ni bora nikae karibu.hawakupinga.mi nlishachoka kaa home aiseee....home kuna chosha sana.

Basi huo mpaka kitaa ghetto na mshkaji.asubuhi na bahasha Zetu za khaki town. Ulikuwa mwendo wa pass ndefu goal.mkikomunika asubuhi mpaka jioni tena mnakula mnalala.

Tukagundua mihogo ndo inakaa sana tumboni so ikawa ni mapande ya mihogo asubuhi.mpaka jioni tena.kisha kesho.tumesambaza sana bahasha miaka yetu.mpaka siku jamaa yangu anasema kuna kazi ya marketing and selling sehemu flani kesho tuulambe twende.

Twende tumevaa Kikristo.yaani tai na shati kuchomekea....daaah nami pigo hizo si zangu kabisa.nikaazima kwa Medi. Nikagonga vitu na viatu very smart.hao mguu kwa mguu mpaka mitaa flani Kurasini huko. Tulikaa sana kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 jamaa ndo wanakuja kutuita tupo wengi kinyama.

Wakaanza kutupa darasa kwanza....kazi ya marketing na sales ikoje mpaka saa 11:30 wakasema tuje kesho na picha tatu,barua serikali za mitaa,kitambulisho cha kura na barua ya udhamini. Na tuwe very smart.

Wale mabwege kesho yake tumeenda wanatukabidhi mabeseni,vacuum flask,na mazaga zaga mengi tubebelee kutembeza kitaa. Daaah....nikaona haya mambo ya kiwaki sana.nikaondoka na vile vitu tukaachana na jamaa yangu kuwa kila mtu aendelee hadi kesho. Nikapita pita mitaa nikauza beseni 2 nikapanda gari.huyoooo ubungo home.nikatua mzigo nikazima simu.

Jamaa kuja niamsha saa 3 hoi.ananiuliza vipi.nikamwambia ule mzigo ndo umefika home.siwezi ile kazi.naye akaniambia ametembea kitaa kaenda gonga nyumba flani kumbe anaishi demu mmoja alimfukuzia kipindi tunapiga kitabu.akajisikia fedheha sana.so hivyo vitu ndo vimefika hapo ghetto.

Yale maisha yalikuwa magumu kuna siku 4 nilikuwa sijatia msosi njaa inauma mpaka nakaribia kufa nikawa nakula nyanya na vitunguu ambavyo vilikuwa pale home.na maji ya ku download. Siwezi sahau.kumbe vitunguu ni vitamu tu wala havina shida.ingawa nliharisha sana mwanzoni.

Baadaye tukawa tunanunua unga tunachemsha uji tunaweka na mafuta ya kupikia.tunakunywa. ugali na kachumbari tumegonga sana. Yale maisha hata demu humtamani kabisa.mpaka tulipokuja kukaa sawa akili ilitengamaa ilikaa kwenye mstari vizuri.leo mwana akiniambia ana njaa namwelewa sana. Zile siku zingeongezeka nadhani ningekufa.maana nliishiwa nguvu hata kutema mate nlikuwa siwezi.yanaangukia kifuani.

Maana unatoa kohozi lina acid kali unawaza umeze au uteme.ukisema uteme huwezi tema kwa nguvu maana umechoka. Hapo jamaa yangu alikuwa karudisha mpira kwa kipa kwa siku hizo chache....nikawaza kuna siku watanikuta nime danja mle ndani kwa njaa. Mi nlikuwa mbishi kinoma kurudi home.nligoma kabisa.

Jamaa kanikumbusha kuwa hata mkojo ukiwa na njaa hiyo ukikojoa hauruki. Ni kweli unachuruzika tu. Maana hata nguvu ya kuupush unakosa.

NITAENDELEA.......
 
Msoto na maisha ya geto noma sana hasa michongo ikiyumba, kuna kipindi flani huko nyuma hali ilikuwa mbaya sana kila siku nafunga bila thawabu,

ilibidi kujilipua kwa bidada mmoja hivi muuza misosi ili tu ni-survive, hakuwa mzuri kimuonekano ila sa ningefanyeje,

Ila nashukuru hapo ndipo nilipojifunza kusimamia kucha kisawasawa na kunyoosha goti mpaka lukwiri, maana nilihofia show ikiwa mbovu msaada unaweza kukata nikarudi kusota na nenge
 
Baada tu ya kumaliza Elimu nikawa nimefanyiwa kajisherehe flani pale home wakanipa na zawadi kati ya zawadi hizo kul

uwa siwezi.yanaangukia kifuani.maana unatoa kohozi lina acid kali unawaza umeze au uteme.ukisema uteme huwezi tema kwa nguvu maana umechoka. Hapo jamaa yangu alikuwa karudisha mpira kwa kipa kwa siku hizo chache....nikawaza kuna siku watanikuta nime danja mle ndani kwa njaa. Mi nlikuwa mbishi kinoma kurudi home.nligoma kabisa.
Hahaha..
Dogo, ila una kipaji, unaweza kuwa comedian mzuri😁.
Halafu ikawaje, ulitoboa?!
 
Njaa mbaya sana aisee, ni kweli kbsa mate hayatemeki, imenikuta hyo juzi tu hapo. Na sauti lazima ipotee
Koo linakauka.... Sauti inagoma kutoka. Mate unayapata kwa mbali halafu machungu kinoma. Unakuwa dhaifu hata mashine haisimami hamu inakata... Ikisimama unasikia maumivu tu na kero maana ukipata na ukipiga demu unatoa upepo tu... Kama tairi lililotobolewa.
 
Back
Top Bottom