Baada ya basi kupata ajali nikajikuta nimekwama Zimbabwe mwaka 2014

Wamamba

Senior Member
Jan 5, 2024
125
226
Habari zenu wakuu,

Nisiwachoshe, niwape kisa kifupi kilichonitokea 2014 katika mishe zangu za utafutaji.

Nilipanga kwenda nchi fulani kwenye utafutaji na nilikuwa mwenyewe Bahati mbaya njiani tulipata ajali mbaya na alhamdullillah nilisalimika kutoka mzima, wapo waliopoteza uhai na majeruhi wengi, binafs nilipata tu michubuko na maumivu ya kawaida tu nashukuru.

Watu wasio na nia nzuri walivamia gari baada ya kusaidia wakaiba mizigo na simu niliibiwa pia pochi yangu sijui niliipoteza vipi? Ila nashukuru pas ya kusafiria nilibahatika kuikuta mfukoni ikiwa na hari nzuri kabsa.

Dereva na kondacta hatukujua walipopotelea sijui kama walikimbia au walipata matatizo kwa ajali, wana usalama walifika na kuokoa na tuliokuwa wazima wakatushahuri tuamue nini? Cha kufanya, kumbuka sikua na pesa wala simu ya kumpigia yeyote.

Nikaanza safari ya kutafuta kituo cha mabasi kidogo na kwenda kueka kambi hapo bahati nzuri nilifanikiwa kukipata na nikaanza maisha hapo, so sad.

Nilikuwa nimefanikiwa kukutana na majamaa wanauza vitu aina tofauti hapo kituo cha mabasi madogo na kuungana nao katika kuwaelezea kuwa nimepata ajali na sina chochote, walinipa ushahuri nitafute kanisa au msikiti ninaweza kupata msaada ila sikupata mtu wa kuniongoza, nikakomaa nao kama mwezi hivi baada ya kuangaika sana kuuza vitu vyao kwa deiwaka -day work ili nipate chochote cha kujistiri, sehemu ya kulala ilikuwa tunalala hapo hapo stand.

Kimuonekano nilikuwa smart sana coz nilivaa nguo mpya mpya na nilinyoa vizuri tu nafikiri hiyo nayo ilikuwa imenibeba na kulikuwa na kijisehemu cha kufua na kuanika nguo so washikaji ilikuwa wamenipa muongozo kama nahitaji kujifanyia usafi niende na nifanye usafi wa nguo na vitu vingine.

Kuna siku nilikuwa nauza uza bidhaa Kama kawaida ilee kung’ang’ania na kugombea mteja, kwa bahati mbaya kuna jamaa akanipush na kuniangushia vitu kwenye kikapu changu, jamaa akanisaidia kuviokota na mishe zikaendelea.

Yule jamaa aliyenipush kwa bahati mbaya baadae akanitafuta na kutaka kujua kwanini? Nipo palee before sikuwa na ukaribu naye tulikuwa tunaonana tu maana hapo kituoni kuna kambi tofauti za washikaji wauzaji vitu na huwa hawaelewani ni kama vijikundi hivi- so jamaa akanitafuta na kuanza kunihoji.

Nikampa kisa chote tangu natoka nyumbani na mpaka napata ajali na kupoteza vitu vyote mpaka simu na sikubahatika hata kuwa na namba kichwani ya mtu ambaye ataweza kunipa msaada kwa pale nilipo ndipo jamaa akanambia nitakusaidia na kuniuliza kuwa nna pesa ngapi? Mfukoni nilihofia ila kwa kuwa nahitaji msaada nikamwambia pesa ambayo nimesave tangia nianze kupiga dai waka hapo stand.

Jamaa akanambia wewe ni tajiri ambaye unapiga dai wala yaani kwa kumaanisha kuwa nna pesa ya mtaji mara mbili na ninao wapigia kazi kwani naweza kuwa na kikapu changu na kikawa na bidhaa zote na nikapata pesa nyingi kuliko kupiga day waka, sikuwa na cha kusema nikamwacha aamue kwani lengo langu halikuwa kulowea palee ila niliwaza nikiwa na kikapu mwezi tu naweza pata nauli nikaenda ninapotaka kwenda, ambapo ni lengo kuelekea huko na ramani yote nilikuwa nayo.

Kesho yake mapema tuliamkia kwenye soko kununua kapu na kuanza kununua bidhaa ndogo ndogo na kujaza kapu, nilishangaa sana na nikakumbuka ule msemo kuwa mimi ni tajiri ambaye napiga dei waka, na pesa ilibaki na tulirudi stand na kuendelea na kazi baada ya siku mbili walee jamaa waliokuwa wananipa dei waka wakaanza kuchukia na kutaka kujua nani kanishawishi kunipa kikapu cha kufanya kazi kwa ujumla- niligundua kuna watu watataka wakutumie kwa faida zao hata kama upo kwenye shida/matatizo na hawatajali.

Nilimwambia jamaa , jamaa akanambia leo utaama kambi kweli niliona jamaa hawanitakii mema nikaama kambi, Na kimuonekana hiyo kambi/kikundi cha pili ndio kilikuwa Na nguvu na hata maendeleo kuliko kikundi kile cha kwanza, kweli nikaama kambi na nikaanza kupata pesa.

Jamaa akanishahuri nitafute chumba nipange baada ya mwezi, ila nikamwambia kuna sehemu nilikuwa naenda na ni lazima niende jamaa alinielewa, nilikuwa nasave sanaa kuliko matumizi baadae nikamuomba jamaa anisaidie kupata simu ya smart na hakuwa na hiyana nilinunua na kuweka taarifa zangu za email na ku -download app na kuweka account zangu kwenye mitandao ya kijamii na kutafuta jamaa zangu ambao nilikuwa nawafata na maswali mengi kuwa nipo wapi? Nikawaelezea na tukakubaliana natakiwa nianze Safari nikawaambia mwezi ujao nitaanza safar sababu nauli nimeshapata.

Nilimuaga yule jamaa na kumuomba anisaidie kutafuta tkert mda wangu ukifika wa kuondoka.

Kweli baada ya mda jamaa aliulizia bei ya tkert mpaka nilipotakiwa kwenda kuunganisha gari akanipa maelekezo nikapata muongozo.

Nikajinunulia baadhi ya vitu kwa ajili ya safar, pesa nilipata katika biashara ilee ya umachinga hapo kituoni niligundua kuwa wafanya biashara wadogo wadogo sio wa kuwachukulia poa.

Siku ya safari nilimpa bure jamaa kapu na kumwambia kuwa ni mali yake jamaa hakuamini na aliniambia siku yeyote niende palee maana mimi ni ndugu yake kabsa tukuwa na mawasiliano ila kwa sasa nimepoteza, I wish nikutane nae jamaa.

Kweli nilipata gari na kufika salama nilipokuwa naelekea na baada ya kufika nilimjuza jamaa alifurahi sanaa aisee kweli yule ni ndugu yangu.

Watu wema bado wapo banah.

Shukrani kwa mda wako wa kusoma hiki kisa kilichonipa mafunzo mengi katika maisha yangu japo ilikuwa ni kipindi cha mienzi mitatu tu lakini kilinijenga sanaa aisee.

Asalaam
 
Stori nzuri sana, mimi pia nimepanga kutembelea Malawi, Botswana, Zimbabwe, na Zambia December ya mwaka huu.

Kikubwa nikutaka kujifunza maisha yanaendaje huko kwa wenzetu, pia kutalii mazingira utamaduni... kujifunza biashara wanavyo fanya wenzetu.

Yaani ninacho kitafuta hasa ni kupata ujanja wa kibiashara mbinu n.k naamini hii ita nisaidia sana binafsi. Now i'm 27 yrs naamini bado sija chelewa sana.

Pia sija oa bado naamini nikitoka huko nitakua nimeongeza kitu kwenye kichwa changu. Kingine cha mwisho situmii ndege naamini usafiri wa bus utanifaa zaidi, kutalii njiani na kubadilisha ma bus stend kwa stendi
 
Stori nzuri sana, mimi pia nimepanga kutembelea Malawi, Botswana, Zimbabwe, na Zambia December ya mwaka huu.

Kikubwa nikutaka kujifunza maisha yanaendaje huko kwa wenzetu, pia kutalii mazingira utamaduni... kujifunza biashara wanavyo fanya wenzetu.

Yaani ninacho kitafuta hasa ni kupata ujanja wa kibiashara mbinu n.k naamini hii ita nisaidia sana binafsi. Now i'm 27 yrs naamini bado sija chelewa sana.

Pia sija oa bado naamini nikitoka huko nitakua nimeongeza kitu kwenye kichwa changu. Kingine cha mwisho situmii ndege naamini usafiri wa bus utanifaa zaidi, kutalii njiani na kubadilisha ma bus stend kwa stendi

Fanya hivyo Chief na hautajilaumu aisee, maana ni utapata maarifa sana ukiamua kutoka tena ni kwa lengo lako maalum
 
Back
Top Bottom