Ushuhuda: Mungu amekuwa Mwema kwangu

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,414
Habari za Jioni ndugu zangu, Amani ya Bwana iwe nanyi ,

Nisipoteze muda niseme hakika Mungu amenitendea Wema na muujiza katika maisha yangu ,sio kwamba Ni mwema au nini naweza kusema katika waovu ,wenye dhambi wa kutupwa nami Ni mmoja wapo ,ila huyu Mungu usipomuelewa utajihisi amekukataa kumbe sivyo, ukiuelewa upendo wa AGAPE utajua Nini naongea.

Mimi Ni muadventista Msabato , sio wa kuzaliwa. (Nitakuja kueleza siku Moja nilivyotoka katika Uislamu na kuingia katika Ukristo).

Mara kadhaa nilihangaika kupata ajira ,nilijiunga na Ajira portal na kweli niliitwa interview nyingi lakini zilikuwa zinaangukia Jumamos ambayo Ni siku yangu ya ibada ,Hali hii ilinipa tabu Sana , kusema kweli awali nilienda kufanya zile interview Hadi jumamos , sikufanikiwa japo nilikuwa naingia Hadi Oral interview, siku Moja nilihisi hatia baada yakuwa nasikiliza mahubiri na kusoma Maandiko,na historia nikiona mashujaa wa imani walivyojitoa kuacha ya dunia na kumtetea Mungu, niliazimia sitafanya Tena Interview jumamos kipindi hicho Sina ajira ,Nina mke na ana mimba , kula yangu ya tabu Sana, nilimwambia Mungu naomba Hadi mwezi ujao nipate ajira , Mwanamke wangu nyumbani alikuwa akinisimanga ,akininyanyapaa ,yote Ni sababu Sina ajira Sina kipato Kodi ya nyumba Sina na sijui nalipa Nini , niliendelea kushikilia msimamo sitafanya Tena Interview jumamos na rasmi naitelekeza akaunt ya ajira portal .

Kwakweli sijui hata nilikuwa nakulaje ,naishije ,maana sikuwahi kulala njaa ,hata mwenye nyumba Kodi yake ilipofika hakuwahi kuja kunidai had nikasahau nadaiwa Bei gan maana nilikuwa nimelimbikiza nahisi hata miezi 6-8, Siku Moja mwenye nyumba alikuja akasema hanidai Kodi Bali Kuna miezi Kama miwili mbele yeye ndiye namdai ,nilishangaa Sana , kipindi hicho nilikuwa napata interview makapuni mengi tu lakini tulikuwa tunashindwa kwenye Swala la IBADA , .Kuna wakati nilikuta kwenye Emali yangu meseji kutoka bodi yangu ya uhandisi ,nitume detail zangu na namba ya benki, kwakweli nilifanya vile , haikupita wiki nikawekewa laki 9 ,bila kufanya kazi yoyote ,na ndio Kipind ambacho ile miezi miwili ya Kodi niliyoambiwa inaishia ( japo binafsi kwakumbukumbu zangu nilikuwa nadaiwa miezi 6-8),ile laki 9 ilinisaidia Sana kipindi hicho.Nyingine nilianzisha biashara ya matunda lakini haikufanikiwa (ukisikia mtu anakwambia jiajiri wewe msikilize tu)

Lakini bado swala la ajira lililuwa gumu Sana hasa upande wa IBADA ,Kuhusu interview huwa naiitwa kila wiki hata Mara 2 ,Awali nikiwa nimehitimu nilitafuta ajira nikapata katika kampuni ya Uzalishaji mikaa ya briquette huko kusini, nilikutana na meneja mtata Sana, hofu yake kubwa ilikuwa nimekuja kuchukua cheo chake ,alihangaika kwa waganga kunifanyia figisu lakini alishindwa kabisa ,mwisho niliamua kuacha kazi, sio sababu yake ila sikupenda mazingira ,binafsi nakanuni Moja katika maisha , huwa simkimbii mchawi popote pale iwe kwenye kazi au nyumba ,maana kumkimbia mchawi Ni Kumdhalilisha Mungu ambaye tunajinasibu ana nguvu kuliko upande wao .,

Baada ya kurudi nyumbani ,nilisemwa na majirani na jamaa wanaonizunguka maana wanaona unaamka asubuhi had Jioni unarandaranda tu ,nikamwambia Mungu nataka mwezi fulani usipite nipate hata ajira kwanza iniweke sawa , Nilikuwa na rafiki yangu tumehitimu wote chuo darasa Moja , alikuwa hamuamini Sana Mungu, nayeye alihangaika Sana kuhusu maisha na Ajira , kipindi nipo kusini nilimtumia tangazo la ajira kampuni Moja kubwa hapa TZ ya Gesi , aliomba ,niliporudi Dar , tukawa wote majobless , lakini nilikuwa nae karibu kuhusu Mungu anavyofanya kazi, tukisoma Sana Maandiko, (huyu ana stori ndefu jinsi Mungu alivyomtendea,) ,alikata Sana tamaa alifikia hatua hata ya kujiua ,siku Moja akiwa amejiandaa amepaki mizigo yake na vyeti akijiandaa kurudi kwao Kaskazini mwa TZ , asubuhi anapigiwa simu kutoka ile kampuni ya Gesi aende kwa interview , alijiandaa tukiwa wote ,tuliomba , nami nilimwombea nilimwambia Mungu naomba apate hii kazi ili UTUKUFU WAKO UDHIHIRIKE

Kwakweli alifanya interview 3 na zote alitoboa na kupata kazi katika hiyo kampuni ya Gesi, Imani yake kwa Mungu iliongezeka Sana, hirizi na mafuta ya manabii ,maji yote nilikuta amezichoma .

Kwangu hali haikuwa nzuri niliendelea kuwa Jobless ,maisha ya kuungaunga ,biashara ya matunda ilikwama kabisa , .Nikamwambia Mungu Sasa nahitaji kazi ,maana maadui zangu wananisema vibaya na kusema ona anamtegemea Mungu mbona hamsaidii Sasa, binafsi najua hatua zote hizi za maisha Ni shule ,Maana hata Waisrael walikaa jangwani miaka 40 ili kufundishwa .

Siku moja nikaitwa interview katika kampuni Moja ya Tajiri mkubwa hapa TZ , nikafanya interview nikapita ,kosa nililofanya nilisahau kuweka masharti ya ibada wakati nasaini mkataba , Nilipoanza kazi nikawa nasumbuliwa Sana nije jumamos , Bosi akaniita nikamwambia siwezi kuja Jumamosi hata kazi nipo tayari kuacha , Bosi akachukua peni akapiga hesabu pesa ambayo nitakatwa kwa mwaka mzima kwasababu ya kutokwenda jumamos tu, akanikazia macho akasema upo tayari kupoteza kiasi hichi Cha Pesa kisa kusali tu? Je ukienda kanisani unapata Nini ? Mwisho akasema fine sikufukuzi kaz maana umeshasaini mkataba ila Tutakukata pesa .

Kuanzia hapo Bosi akaanza figisu, Pesa za bonus, hanipi anazuia, pesa za communication, n.k zote anazuia ,wenzangu wanapewa Mimi natengwa, mshahara ukija nimekatwa pakubwa Sana , .Wafanyakazi wenzangu na watu wakaribu wakasema fanya uje kazini jumamos tu utakatwa pesa na mshahara unabaki kidogo .,hata mke wangu pia akasema Nenda kazini Jumamosi.

Nikawaambia Sitaenda , Hali ikawa mbaya Sana, Bosi akazidi kunikazia kamba , Nikamuuliza Mungu Nimekutetea kwa watu na wewe nijibu Sasa, Nahitaji unijibu, Nikaweka ratiba nikawa nasoma Sana Zaburi ya 40 .,na maombi na kufunga , Haikupita muda nikapokea simu kutoka mgodi mmoja hapa Tanzania, nikaandaliwa interview online ,nikafanya ,nikaulizwa hapo unalipwa Bei gani nikajibu , lakini nikasema ngoja nimuulize Mungu je amenijibu yeye ,nikasema Kama wataniruhusu ibada jumamos Basi hiyo kazi imetoka kwa Mungu, kweli wakasema Hilo halina shida , nikatumiwa nauli na hela ya kula , nikafika nikagharamiwa accommodation ya Hali ya juu.

Nikaambiwa unataka tukulipe Bei gani nikataja mshahara mzuri tu nikaambiwa tunakuongeza zaidi, nikaambiwa tunataka uwe meneja hapa na tutakupa nyumba kubwa hapa.

Nikasema hakika Mungu umenijibu

NB: MIMI NI MDHAMBI SANA, ILA MUNGU AMEKUWA MWEMA KWANGU , NINAPOMKOSEA NATUBU KWA KUTAJA DHAMBI JINA LAKE BILA KUPEPESA MACHO ILI ANIREHEMU

Nimejifunza hii kutoka kwa Daudi ,nilijiuliza kwanini MUNGU alimpenda Sana Daudi kuliko sauli ?

Ukisoma Maandiko utagundua Kati ya Sauli na Daudi, Daudi ndiye kavurunda Sana , ameua ,amezini, amenyang'anya wake za watu, lakini alikuwa mtu wa toba ya kweli ,imefikia hatua Daudi ana mji /mtaa mbinguni

Unaitwa MJI WA SAYUNI
 
Ni suala la mda tuu, utakuja kuona kumbe ilikuwa ni jambo la kawaida
 
Usifanye dhambi au upuuzi Kama kufanya Ngono au kufanya uzinzi na hujaoa au kuolewa ukasema utatubu huu ni uhasi Mbele za Mungu na shetani ndo Binadamu Mwenyewe


Nimekuwa hapa madhabauni najionea uchafu wa walokole kuzini huku lawama wakimpa shetani this is not good


Swala la usafi wa Mwili
Roho na Matendo lipo ndani ya huwezo wa mwanadamu na sio SHETANI Wala Mungu Cha kuomba ni kuomba hekima ya Mungu iyawatale maisha yako.
 
ni neema tu ya Mungu, ila unachosali Mungu hata hakitambui. unasali siku ya jumamosi, wasabato mnahitaji kufunguka akili mjue hatuokolewi kwa sheria tena ni kwa neema, mmemkataa Yesu bila ninyi wenyewe kujijua kwasababu mnaamini kwa uwezo wenu mnaweza kutimiza sheria wakati kwa njia ya sheria hakuna aliyewahi kumpendeza Mungu.

Elen white aliwapoteza sana, yule nabii mke, hua namfananisha na Yezebel aliyekuja kupotosha kundi kubwa sana la watu wanaoishi kimwili na kumwabudu MUngu kimwili badala ya kuenenda kwa Roho. hii ndio maana hamtakuja kumwona Mungu.

Hata akionekana kwako ni neema yake tu anakuvuta pengine utafunguka na kufuata njia sahihi ila haimaanishi unaabudi kiusahihi. Mungu hapatikani mwilini, anapatikana Rohoni kwasababu yeye mwenyewe ni Roho.
 
ni neema tu ya Mungu, ila unachosali Mungu hata hakitambui. unasali siku ya jumamosi, wasabato mnahitaji kufunguka akili mjue hatuokolewi kwa sheria tena ni kwa neema...
Umeandika vitu vingi usivyovijua ,na inaonesha una chuki kubwa imekujaa juu ya wasabato ,pole Sana

Unaomba nivutwe nije kwenye haya makanisa yenu mnayouziwa maji ,mafuta, na keki?pole Sana ,nilishapita huko nilipofika ndio penyewe ,unataka niende wapi Tena ?kwa mwamposa nikajimalize au wapi nitajie

Kuhusu kuokolewa kwa Neema sio Njia ya kuvunja amri za Mungu ,someni Biblia vizuri

Kama unapanga kuwa mtakatifu lazima uwe mtu wa aina gani???

Kama unapanga kuwa mtakatifu, ama wewe u jamii ya watakatifu, Lazima uwe miongini mwa wale ambao inasemwa kwao kwamba wanazishika Amri za Mungu na Imani ya Yesu. (Ufu14:12)

Ni amri zipi hizo?

Ni amri kumi, kwani Amri kumi ni kanuni za Upendo. Amri ya kwanza hadi ya nne inatutaka kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa roho yote,nguvu zote na akili zote. Amri ya tano hadi ya kumi inatutaka kuwapenda wanadamu wenzetu kama nafsi zetu wenyewe.(Luka10:27,Math22:36-40,Waru13:9-10)

Je! Waweza kuwa na upendo bila kuzishika Amri kumi??

Wapo wanaodhani kuwa wanaweza kuwa na upendo bila kuzishika amri moja moja kama zilivyotajwa ktk Amri kumi. Huo ni udanganyifu. Haiwezekani kuwa na upendo na huku unavunja Amri hata moja ktk Amri kumi.(1Yoh5:2,Yao2:8-11)

Je tu tunaagizwa kuzishika amri kumi ili tuokolewe???

Mwenye dhambi haagizwi na maandiko kuzishika amri kumi ili aokolewe au kuhesabiwa haki. Bali ili mwenye dhambi apate kuyajua mapenzi ya Mungu anapaswa kuzisoma amri za Mungu, na kufahamu matakwa yake yote, na kutafakari hali yake ya kiroho, na kupima maisha yake na kanuni zake. Ikiwa ataonekana kupunguka hata Nukta Moja, basi atambue ya kwamba Yeye ni mwenye dhambi na kwamba ana dhambi za kuziungama na kuzitubu mbele za Yesu. Na hiyo ndiyo kazi ya sheria. (Gal2:16,War3:19-20, War7:7-9)

Kazi ya sheria ni nini?

Sheria daima ni kiongozi wa mdhambi, akimwonyesha mdhambi kosa lake na kumwelekeza kwa Kristo. Mwenye dhambi akimwendea Kristo kwa imani na kutubu na kuziungama dhambi zake, anasamehewa na kuokolewa. Yesu ndiye anayeokoa na sii sheria. Sheria haina uwezo wowote wa kuokoa ama kusamehe dhambi.(Gal3:23-24)

Uongozi wa sheria unakoma lini?

Uongozi wa sheria unakoma pale sheria inapompeleka mdhambi kwa Yesu na mdhambi kumpata Yesu. Sheria humwonyesha mdhambi kosa lake, lakini haina uwezo wa kuiondoa, na hivyo humwongoza mdhambi kwa Yesu. Mdhambi akiisha kuja kwa Yesu anasamehewa na kuhesabiwa haki na kuokolewa. Kristo anakaa ndani yake na kuwa kiongozi mpya. Uongozi wa sheria unakoma kwani unakuwa umetimiza lengo lake. Ndo maana Biblia inasema kwamba Kristo ni Mwisho wa sheria ili kila aaminiye ahesabiwe haki, kwa maana kwamba Sheria ikiisha mwongoza mdhambi kwa Yesu, basi Uongozi wa sheria unakoma, na Uongozi wa Kristo unaanza. (Gal3:25, War10:4)

Kristo kama kiongozi mpya anafanya nini???

Kristo akianza kama kiongozi mpya, anaziandika zile amri kumi ktk nia za watakatifu na mioyo ya watakatifu. Amri za Mungu zinakaa ndani ya watakatifu sii kama kiongozi tena bali kama tabia. Na amri kumi zikiwa tabia ndani yetu, Utii hudhihirishwa kwa nje kama tunda la Uongozi wa Yesu kwa njia ya Roho wake. Mtu huyu sheria zilizoandikwa ktk mawe haziwezi mhukumu, maana nakala yake ipo moyoni, na ni sehemu ya tabia yake.(Ebr10:16-17,Gal5:6,War8;4)
 
ni neema tu ya Mungu, ila unachosali Mungu hata hakitambui. unasali siku ya jumamosi, wasabato mnahitaji kufunguka akili mjue hatuokolewi kwa sheria tena ni kwa neema...
Nakushangaa unavyosema Ninachosali Mungu hakitambui ,kisa umejaa chuki dhidi ya SDA , pole Sana ,Mungu atakusaidia atakutoa huko

Chuki yote Ni sababu ya Amri ya 4 inayosema IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE , Wala sio kingine

Unasema nije huko ,Ni wapi ? Kwenye haya madhehebu yenu yaliyojaa utapeli , haya mnayouziana maji , mafuta, udongo, keki ,na Upagani mwingine

Wakristo kwa mujibu wako unawaona Ni wale wanaobadili Amri za Mungu ,kuabudu na kuchonga masanamu, kula kenge,nguruwe, mende ,kuuza Mafuta, udongo,keki,leso kwa mgongo vina upako ,ibada za kipagani ,x mass paganism,Easter paganism,Dominica paganism, n.k

Watu Kama nyie mlikuwepo hata enzi za Yesu ,

Mathayo 7:7

6Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa,

Watu hawa huniheshimu kwa midomo

Ila mioyo yao iko mbali nami;

7Nao waniabudu bure,

Wakifundisha mafundisho

Yaliyo maagizo ya wanadamu,

8Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. 9Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. 10

ILA YESU MUANZILISHI WA UKRISTO ANASEMA

“Msidhani [wengi mno leo mnadhani] ya kuwa nalikuja kuitangua torati [Sheria] au manabii;” akasema, “sikuja kutangua [kuifutilia mbali], bali kutimiliza [kuitekeleza]. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka [bado zipo], yodi moja [,] wala nukta moja [.] HAITAONDOKA hata yote yatimie [yaani, mpaka hapo mbingu na nchi zitakapoondoka].

Basi [kwa hiyo] mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo [Yak.2:10-12], na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa [mnyonge hataingia – Ufu.21:27] katika ufalme wa mbinguni; bali mtu ATAKAYEZITENDA [Amri Kumi] NA KUZIFUNDISHA, huyo ataitwa mkubwa [mtawala/mfalme – Ufu.20:4; Dan. 7:27] katika ufalme wa mbinguni.” Mathayo 5:17-19.
 
ni neema tu ya Mungu, ila unachosali Mungu hata hakitambui. unasali siku ya jumamosi, wasabato mnahitaji kufunguka akili mjue hatuokolewi kwa sheria tena ni kwa neema, mmemkataa Yesu bila ninyi wenyewe kujijua kwasababu mnaamini kwa uwezo wenu mnaweza kutimiza sheria wakati kwa njia ya sheria hakuna aliyewahi kumpendeza Mungu. Elen white aliwapoteza sana, yule nabii mke, hua namfananisha na Yezebel aliyekuja kupotosha kundi kubwa sana la watu wanaoishi kimwili na kumwabudu MUngu kimwili badala ya kuenenda kwa Roho. hii ndio maana hamtakuja kumwona Mungu. hata akionekana kwako ni neema yake tu anakuvuta pengine utafunguka na kufuata njia sahihi ila haimaanishi unaabudi kiusahihi. Mungu hapatikani mwilini, anapatikana Rohoni kwasababu yeye mwenyewe ni Roho.
Mtume paulo anaandika hivi: "maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; [War5:13].

Andiko hili limechanganya sana wanaojiita wakristo wengi kudhani kuwa uwepo wa dhambi hauhitaji sheria na kwamba hata sasa sheria haihitajiki kufafanua dhambi ni nini? lakini hili ni kweli?

Ni kweli kwamba Mungu kama mtawala wa dunia yote hana sheria za kuongoza utawala wake???

Paulo anaposema kwamba kabla ya Sheria dhambi ilikuwepo ulimwenguni, hapa alikuwa akimaanisja kuwa kabla Sheria za Mungu kuandikwa katika vibao vya mawe na katika magombo ya Musa pale mlimani sinai, dhambi ilikuwepo.

Kwa wanadamu sheria huanza kutambulika na kuwa na mamlaka baada ya kuandikwa. Na hili ni kweli. dhambi ilikuwepo hata kabla ya tukio la mlima sinai la Mungu kuandika Amri zake katika mbao mbili za Mawe.

Lakini paulo yupo wazi kuwa dhambi haiwezi kuhesabiwa pasipo sheria. Maana yake ni kwamba kila penye dhambi, maana yake kuna sheria fulani ya Mungu imevunjwa. Haiwezekani dhambi kuwepo bila sheria kuvunjwa. Kwa hiyo ni wazi kwamba Sheria za Mungu zilikuwepo hata kabla ya tukio la Mlima sinai. Paulo anaposema kuwa dhambi ilikuwepo kabla ya sheria, hana maana kuwa dhambi inaweza kuwepo bila sheria, ila anamaanisha kwamba dhambi ilikuwepo kabla ya Mungu kuziandika rasmi amri zake katika mbao za mawe pale mlimani sinai.

Hivyo ni dhahiri kuwa Amri za Mungu zilikuwepo hata kabla ya tukio la Mlima sinai.

Hapo Mwanzo Mungu alipomuumba Mwanadamu aliiandika sheria yake katika dhamiri zao na mioyo yao[War2:15]. Hata baada ya Uasi, Sheria za Mungu zilibakia ktk Mioyo ya wanadamu. Hata wanadamu waasi wanajua kabisa kanuni za haki na kanuni ziziso za haki. Haihitaji kufundishwa na mtu kuwa ukichukua mke wa mwenzako, ama ukimwibia mwenzako, ama ukimtukana mwenzako ni jambo baya. Sheria ya Mungu ya Upendo imo mioyoni mwa wanadamu wote.

Ni hali ya uasi ambayo Mwanadamu amerithi baada ya uasi ndo inamsukuma mwanadamu kuichukia sheria ya Mungu na kuivunja. Lakini Katika moyo wa kila Mmoja Mungu amejiachia ushuhuda wa sheria zake.

Amri ya Sabato ilianzishwa na Mungu Mwenyewe tangu Uumbaji, na hivyo kuwa Amri iliyozeeka na ya zamani sana kama Umri wa dunia. Sabato iliwekwa na Mungu kuwakumbushia wanadamu kuwa waliumbwa na Mungu na hivyo wanawajibika kwake katika kumwabudu na kumtii. Msingi wa Ibada uliwekwa mapema sana pale Mungu alipoianzisha sabato. Taz Mwa2:1-3.

Amri zote Kumi, ambazo ni mafafanuzi ya Sheria ya Mungu ya Upendo zilikuwepo tangu Uumbaji. Baadhi ya wakristo wanawaza kwamba kwa sababu Amri kumi ziliandikwa katika Mbao mbili za Mawe pale mlimani sinai, basi Amri hizo ni torati ambayo haiwahusu wakristo kabisa. wanawaza na kufikiri kuwa kwa sababu Agano la kale liliundwa kwa misingi ya utii wa Amri kumi, pamoja na Sheria zile zingine na maagizo yake na hukumu zake, basi kuondolewa kwa agano la kale kunafagilia mbali Amri kumi na Sabato. Huu ni udanganyifu Mkuu.

Na udanganyifu huu kwa sababu unalenga sabato tu, unakuja udanganyifu mwingine kuwa injili imezitaja sheria zingine zote tisa katika zile kumi kasoro sabato tu,na hivyo tuna uhalali wa kuzishika sheria zingine zote tisa kasoro sabato!!! Huu ni udanganyifu wa makusudi unaolenga chuki dhidi ya amri moja tu ya Mungu katika zile kumi.

Bwana wetu Yesu Kristo akiongelea juu ya Umilele wa Amri za Mungu, na kuwaonya watu dhidi ya kuzitangua, aliweka bayana hivi: "Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati. [Luka16:16].

Kama vile mbinguna nchi vitakavyoendelea kudumu, daima vitaendelea kushuhudia kuwa Sheria za Mungu ni za Milele. Amri za Mungu ambazo zilikuwepo kabla ya Agano la kale la mlima sinai; husimama kwa zenyewe hata bila Agano la kale.

Agano jipya halikuondoa Amri za Mungu bali linazirudisha Amri za Mungu katika sehemu yake ya hawali yaani mioyoni mwa wanadamu, na kuwawezesha wanadamu kuzitii Amri zake.
 
Back
Top Bottom