Nyumba ile kiboko, niliambulia maji tu kwa siku 2 nilizokaa pale

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,805
12,669
Habari ya usiku wazee.

Nikiwa bado sijalala, nikawa napitia picha za zamani google photo ndipo nikakutana na picha nilizopiga Dodoma nikiwa na rafiki yangu KDG nikakumbuka huu mkasa mfupi.. nimeona nishare hapa.

Ilikuwa mwaka 2018 mwezi wa 10 kuna shida ilinipata kwenye masomo yangu, ilibidi niende Wizarani kuitatua na nilikuwa tayari nishapewa connection.. basi nikiwa nawaza mimi Dom ni mgeni na sijawahi kufika kwa kipindi hiko mara nikapata wazo nimcheki mwanangu KDG ili awe mwenyeji wangu na anisaidie kunipeleka na kunitafutia gesti ya bei nafuu. Huyu KDG nilijuana nae chuo ila yeye akaacha akaenda zake Dom na tuliishi poa kabisa tukiwa na wana wengine. Sasa ilikua hivi.

Mimi:eek: Niaje mwanangu KDG

KDG: Fresh mwanangu za siku nyingi mkuu?

Mimi: Bomba mwana, hivi kaka bado upo Dom au umesharudi DSM?

KDG: Aah nipo Dom kaka, huku ndo nimefika shangazi na Mjomba hawataki niondoke.

Mimi: Sio mbaya mkuu muhimu mishe ziwe zinaenda.

KDG: Kabisa kaka, lete habari

Mimi: Mkuu sasa nina kimeo(nikamsimulia) nimeambiwa nije hapo wizarani makao makuu halafu ukicheki Dom mimi mgeni, sasa naomba nikifika uwe mwenyeji wangu unitafutie gesti ya bei chee na naomba uniescoti mkuu.

KDG: Aah hilo limeisha kaka, kwani unakuja lini bro?

Mimi: Kesho mkuu maana ishu ya haraka..

KDG: Basi poa, sema nini ngoja niongee na Shangazi hapa kama vipi uje ulale tu hapa usiingie kosti mwanangu.

Baada ya dakika kadhaa akanipigia.

KDG: Kaka shangazi kasema fresh so kesho wewe njoo brother.

Mimi:Dah asante kaka umenipunguzia gharama hapo nakushukuru sana..

Tukaagana pale. Kesho yake mapema tu nikawa nipo zangu Ubungo nikapanda Bus la Happy Nation lilitoka saa 2 asubuhi bahati mbaya ile basi ilikuwa na mwendo wa kobe nikajikuta nimefika Dom saa 12 jioni. Kwa bahati mwenyeji wangu nilimkuta pale 88 akinisubiri akanipokea kwa bashasha tukaenda kwao kule Area D mtaa siukumbuki.

Ukweli kwao kwa mazingira ya haraka wanaonekana wanaishi maisha ya standard nyumba nzuri(kwa maisha ya mtaani tunasema wanajiweza) basi nikakaribishwa ndani pale nikatambulishwa then nikapelekwa chumbani. Sasa bwana kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana maana jana yake nilikuwa nimetoka Songea hadi DSM kisha nikaunganisha hadi Dom nikajikuta nkmepitiwa na usingizi nikaja kushtuka saa 5 usiku. Jamaa sikumuona nikaenda zangu toilet (choo kilikuwa ndani ya chumba) nikarudi kulala nikaja kuamka saa 12 asubuhi.

Nikamkuta jamaa kalala pembeni yangu, nikamuamsha tukasalimiana nikamwambia tujiandae twende akasema ule muda ulikuwa mapema sana tuvute hadi saa 2 anywe chai kisha twende! Narudi tena Anywe chai kisha twende(sikuwa nimetilia maanani kauli yake). Basi bwana saa 2 baada ya kujiandaa inaelekea saa 3 nikamsikia wanamuita akaenda Zikapita kama dk 20 akarudi.. akaniambia haya twende mwanangu(sikuhoji vipi mbona chai hatunywi, tukaamua kusepa).

Tumefika wizara tukatumia masaa 5 lakini tukaambiwa turudi kesho yake..basi bwana tumefika town saa 9 alasiri hapo njaa inauma balaa maana tangu nilivyokula jana yake saa 6 mchana pale Moro sikua nimekula chochote hadi time hiyo. Nikamwambia jamaa tuingie mgahawani basi tukaingia akaagiza nami nikaagiza nakumbuka nililipa bill sh 7000 kwa wote wawili baada ya kula tukazurura kidogo kisha tukarudi kwao

Basi tulivyofika kwao saa 1 usiku nikawakuta shangazi na mjomba wake wanaangalia TV, tukasalimia then nikaingia room nimekaa kitandani usingizi ukanichukua. Saa 4 usiku jamaa akaniamsha

KDG: Oya kaka njaa haikuumi?

Mimi: Sio sana kaka, vipi wewe ushakula?

KDG: Aah mimi sijisikii njaa, ila kama wewe njaa inauma toka hapo nje ya geti kuna mgahawa kanunue msosi unaanzia buku tu.

Mimi:(nikiwa nimestaajabu) aah sawa bro hakuna neno...

Hapo sasa nikaanza kujiuliza maswali mmh hii nyumba wanaishije.. basi nikaenda nikapiga msosi wa buku. Nikiwa nataka kulipa yule sista akasema aah wewe si rafiki wa KDG usilipe bwna ila mimi nikakataa nikalipa nikasepa(yule muhudumu alikua sista wa KDG na ule mgahawa ni wa shangazi yao).

Nikarudi ndani nikalala saa 6 usiku nikashtuka namkuta mwana anakula wali, maharage na nyama na ndizi mbivu..kwa aibu akajichekesha pale aah nilikuwa sina njaa sista kaniletea msosi nikamjibu asijali, mimi nikaingia toi kisha nikarudi kulala.

Kesho yake mapema kama kawaida nikamshtua akaniambia anasubiri chai na ulipofika huo muda akaitwa peke yake akanywa tukasepa.. nimefika kule nikafanikisha jambo langu tukarudi saa 8 mchana mimi nikanyoosha chumbani jamaa akaishia sebuleni, akaja chumbani baada ya saa 1 tukacheza gemu kwenye PC hadi saa 2 usiku nikaenda kuoga nilivyorudi jamaa simuoni baada ya nusu saa akarudi akaniambia niende nikale kwenye ule mgahawa ..aisee nikaona hapa noma nikaenda kula pale yule sista akaniambia vile vile nisilipe ila nikagoma nikalipa kisha nikarudi nikalala, Saa 7 usiku nashtuka namkuta mwana anakunywa juice.

Ikabidi nimwambie kaka mimi naona alfajiri nisepe maana nishafanikisha ishu yangu, nikafatilie michongo mingine, jamaa huku akiwa hajiamini akaniambia aah usiondoke bwana mbona mapema basi nikamsihi nikamuelekeza na nikaomba aniagie kwa ndugu zake.. basi asubuhi mapema nikadandia boda hadi ofisi za Kimbinyiko nikapanda Bus safari ya Songea ikaanza(siku hiyo feo zilikua zimejaa hivyo nikata niende hadi Makambako kisha pale ningesubiri za dar).

Wakati nipo njiani jamaa aliniplease sana nimsamehe yaliyotokea hakuyatarajia..nikamwambia asiwaze.

Ukweli mpaka leo bado sina majibu ile nyumba wanaishi vipi ikiwa mgeni walienuruhusu wao nimekaa siku 2 nimeambulia maji ya kunywa tu na ukifika muda wa msosi anaitwa jamaa pekee. Na baada ya hapo mawasiliano yalipungua sana na mwana maana alikuwa akijishtukia hadi yakafa kabisa.

NB: KDG ni kifupi cha jina lake la utani.
 
Dah mkuu nakubali..nilikua nasikia tu KDG akienda akirudi mdomo umenona ndo kmeisha hiyo,yaani ningekua sina kitu mfukoni ningeumbuka.
Sio kila anaejiweza ana roho nzuri wengine hadi maji wananyima wanasema ni maji ya familia tu wananunua supermarket wewe mgeni ukitaka maji kachote bombani unywe hutaki kufa na kiu haiwahusu, sio kila anaejiweza ana roho nzuri wengine ni roho mbaya tu zimewajaa

Wewe unasema chakula tu Mimi nilishawahi nyimwa maji naambiwa ni maji ya familia nikanywe maji bombani sio maji ya Ndani kwao
 
Back
Top Bottom