Ushawahi kupoteza kitu cha muhimu wakati ulipokuwa unakihitaji sana?

Lastmost

JF-Expert Member
Jan 30, 2022
521
516
Salaam wakuu,

Je, ulishawahi kupoteza kitu cha muhimu sana wakati ulipokuwa unakihitaji sana?

Mimi ilinitokea 2013, nilisafiri kwa mara ya kwanza kwenda Mwanza, nilikuwa na mwenyeji wangu aliyekuwa ananisubiria, yeye alikuwa eneo linaloitwa Magu.

Tuliwasiliana hadi nafika nyegezi, huku nikiwa na mizigo mingi ya jamaa.

Tulipofika nyegezi nikamtaarifu kuwa niko Nyegezi, akaniambia nenda hadi nata, hapo Kuna mtu atanipeleka Magu. Hivyo nikishuka Nata nimtaarifu ili amshtue jamaa.

Basi baada ya kuongea naye nikairudisha simu kwenye kibegi (kumbe simu sikuiweka bana, nahisi ilidondoka chini bila Mimi kujua).

Basi kufika Nata nikaitafuta simu, ollllaaa, haipo.

Hapo akili ikakaa sawa, sina namba ya mwenyeji kichwani,na anayenifata stand simjui, Giza lishaingiaaa, Mwanza Mimi ni mgeni, hela ya guest mawazo, daaaa!

Nikasogea pembeni na mizigo yangu, nikamwomba jamaa mmoja simu nipige, nikampa hela ya vocha, akanipa simu, ikabidi nipige simu kwa dada mmoja aliyekuwa Dar ambaye ni rafiki na yule mwenyeji wangu, yeye amwambie kuwa nimefika ila sina simu.

Ilichukua muda hadi Mambo yakae sawa, nikamshukuru Mungu kuwa nilikuwa na hiyo namba ya huyo dada.

Aiseeee! Jitahidi uwe na namba hata tatu za watu kichwani ili ikitokea dharura update msaada.

Kazi iendeleee
 
Back
Top Bottom