Hadithi: Kifo cha mwandishi

zittahmore

New Member
Aug 15, 2023
2
1
png_20230807_104111_0000.png
png_20230807_111237_0000.png
png_20230807_104111_0000.png
HADITHI: KIFO CHA MWANDISHI
SEHEMU YA KWANZA
Mtunzi: More
Mawasiliano: 0756320219

Hadi nafika nusu ya safari yangu bado nilikuwa nikijiuliza kama uamuzi wa kuwa na safari hii ulikuwa sahihi. Kila mara nilikuwa nikijaribu kubashiri matokeo ya safari yangu lakini sikuona yaliyo bora mbele yangu.
Ajabu nilikuwa nikitamani kuona mwisho wake.

Safari ya kwenda Jiji jipya ambalo sikuwahi kufika, tena kwenda kwa mtu nisiyemjua mbaya zaidi mwenyeji wangu hakuwa na taarifa ya ujio wangu.

Kuna nyakati tunasikiliza sauti za nafsi zetu, sauti zisizosikika lakini zenye nguvu mno.
Nami nikaisikiliza hiyo sauti.

Nilianza kukumbuka tangu nilipoanza kuisikia sauti hiyo yenye nguvu siku mbili zilizopita, baada ya kuona mwandishi niliyekuwa nikisoma hadithi zake kwa miaka tisa sasa ameacha kuandika chochote kwenye mitandao ya kijamii.

Si kwamba sikuwaza kuwa huenda hakuwa na kifurushi cha intaneti ama hata kupoteza hata kuibiwa simu.
Unaweza kuniona kuwa sikuwa na akili timamu ama nilikuwa nafuatilia sana maisha ya watu na kujipa umuhimu kwayo, siwezi kukuzuia kuwaza hivyo ila huyu bwana alinivuta kwa jumbe zake ambazo wiki tatu mfululizo alikuwa akiziweka kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kisha kupotea ghafla nilihisi palikuwa na jambo.

Nilisahau kujitambulisha , nilipewa majina mawili na wazazi wangu la kwanza ambalo hata kwenye vitambulisho lipo ni Asajile lingine ambalo sijui kwa nini silipendi nikiitwa hapa mtaani ni Kumbuka halafu lile la ukoo ni Mwakitete.

Nadhani majina yangu yameshakuonesha natokea mkoa gani hapa nchini, hujakosea natokea Mbeya ingawa safari yangu imeanzia mkoani Dodoma ambako nafanya kazi ya ualimu.

Utawaza niliomba ruhusa kazini ama nilitoroka kufuata yasiyonihusu , mie siyo mjinga hivyo nimefuata taratibu zote na kupata ruhusa ya kuwa nje ya kituo cha kazi japo silazimishwi kukueleza nilitunga sababu ipi nikaeleweka kwa mkuu wangu wa kazi.

Sijakueleza nilikuwa naelekea wapi, ila jua huyu mwandishi alikuwa akiishi Arusha, nilijuaje hilo siyo swali, huyu bwana mie nilikuwa shabiki ake haswa hivyo nilikuwa namfuatilia haswa na hata sikupata taabu kujua alipokuwa akiishi na nilifika hapo kwake.

Ajabu baada ya kufika kwake ndo kila kitu kikaharibika , huyu bwana hakuwa na uhai , polisi na jirani zake walisema amefariki kizembe, ila mie naona kama hakuuawa basi alijiua.

Chumba kilitoa harufu mbaya, siyo kutoka kwenye mwili usio na uhai wa bwana Brian Mgaya bali kutoka kwenye mfuko ambao bila kuugusa nilijua ulikuwa na mabaki ya vyakula.

Ningeugusaje mfuko ule mbele ya polisi wawili ambao walimtaka kumlamba kofi balozi wa nyumba kumi aliyetaka kusogeza jiko la mkaa lililokuwa karibu kabisa na kitanda.

Sikuamini yule balozi alinyenywea muda ule ndo’ yule yule alikuwa akitukoromea wakati tumemfuata kumuomba awe shahidi wetu wakati tukivunja mlango wa chumba cha mwandishi baada ya kuugonga bila kujibiwa kwa muda mrefu.

Kama siyo mwenye nyumba kumsihi sana yule bwana angeendelea kuangalia mpira banda umiza wakati mie nikijiumiza kwa kumkosa mwandishi niliyemuhusudu sana.

Kuna vitu vinachekesha na muda huo huo vinakarahisha, hivi we ungemfikiriaje huyu jirani aliyejitia alikuwa na ukaribu sana na bwana Mgaya japo hakujua kuwa alikuwa mwandishi, ingawa alinisaidia kufika kwa mwenye nyumba kisha kwa balozi lakini kitendo chake cha kuchukua kontena akidai marehemu hakumrudishia wakati tukiwa kwenye taharuki kiliniacha kinywa wazi.

Polisi walidai marehemu alijisahau kulala na jiko la mkaa linalowaka ndani hivyo kupelekea umauti wake. Akaruhusu taratibu nyingine zifuate huku wakisaidia kuupeleka mwili ule hospitali. Basi hakuna uchunguzi.

Uchunguze nini, hata simu ya marehemu ilishazima na kupasuka kioo, apigiwe nani. Nikatoka kimya kimya nikitafuta sehemu nichakate mawazo yangu.

Nipost kwenye group ama facebook nitangaze kifo chake kabla ya nduguze kujua? Hapana nikaenda Jackies Gaden nikaagiza bia. Ndiyo unashangaa nini.

Niliagiza nikagida kama nusu hivi, kisha nikaanza kuwaza vyema. Kama we unaona nina pepo sijui roho wachafu, sifikirii vyema hadi ninywe pombe shauri yako. Mie niliona nipo sawa ndo maana nikaweza kutegua kitendawili kigumu.

Utaniuliza ama utajiuliza mie jamaa wa Soko Matola , nimepajuaje Jackies Gaden na nimetoka Dodoma na sikuwahi kufika Arusha.

Ngoja nikueleze ninapokuambia nilikuwa nafuatilia kazi zake, maana nilikuwa nafuatilia kila kitu ambacho alikuwa akikiandika. Hata siku akiandika sentensi akaanza na herufi ndogo nilijua alikuwa na sababu.

Niliamini Brian hakuwa mjinga kama wale polisi walivyotaka tuamini, eti Kabonimonoksaidi imemuua.
Wewe ungeamini kweli?

Brian huyu huyu aliyekuwa akiandika ‘tips’ za maisha si alishawahi kututahadharisha juu ya kutokulala na jiko ndani. Kupitia mabandiko yake nikajua ni heri kupikia nje kama huna jiko hasa ukiwa unaishi peke yako maana si rahisi kusahau kuzima jiko hata likiwa la gesi.

Huyu ndiye aliyeshauri sie tunaolala na utajiri wetu wote chumba kimoja tuweke maji kwenye jagi ama ndoo wazi ili wale wanaopuliza sumu sijui dawa ili tusinzie watuibie isifanye kazi.

Bwana Mgaya alikuwa na maarifa mengi sana na alikuwa aki ‘’share” ndo afe kizembe vile? Hapo nikawaza kama ule mlango wake ulifungwa kwa nje ama kwa ndani.

Huenda ni ndani maana funguo ilidondoka wakati tunajaribu kuzungusha kitasa. Hivi sikuwaambia nilipajuaje Jackie’s Gaden, kuna ‘’post” jamaa aliiweka miezi minne iliyopita akiimba Karaoke akawatag hao Jackie’s Gaden.

Nikaona hapo pakuanzia , nikamwita muhudumu aniongezee bia ya nne na nikaagiza chakula.
Unashangaa bia tatu nilizimalizaje. Nilizimwagia tumboni, umeridhika?

Hivi Karaoke ni lini?
Nilimuuliza yule muhudumu, ambaye alihisi pombe zimeanza nielemea. “Unataka kuimba, na hilo sauti kama Mchungaji akikemea mashetani”

“Ndo mlivyofunzwa kuwajibu wateja wenu hivyo, meneja yuko wapi?” Nilijifanya nimechukia. Hata wewe unanishangaa nakasirishwa na vitu vidogo hivyo hata utani siujui.

Nishakwambia mie ni mwalimu ,naijua na kuiishi saikolojia , kwani kupitia sentensi hiyo niliweza kujua ni lini bwana Mgaya alifika pale na zaidi nikajua yule mhudumu alikuwa mpenzi wake rafiki yake Brian.
Waliitana shemeji.

“Mara ya mwisho kuja hapa ilikuwa miezi miwili iliyopita” Aliongea yule muhudumu niliyekuja kumjua alikuwa akiitwa Grace.

“Mie ni shabiki ake sana ila nilipoteza namba yake” Nilijiongelesha nikimwonesha Kwa ishara afungue bia nyingine, wakati huo nilikuwa najikuta natamani kunywa zaidi kila taswira ya mwili wa Brian Mgaya ikinipita akilini.

“Jackie’s walimpost siku ile anaimba wimbo wa Nameless” Grace alinijibu haraka na kuondoka akielekea kumpokea mteja mpya aliyekuwa ameingia.

Licha ya Brian kuwa mwandishi wa mtandaoni kwa muda wa zaidi ya miaka nane ,hata watu wake was karibu hawakuwa wakijua kuwa alikuwa ni mwandishi mzuri na alikuwa na kitabu kimoja sokoni. Kwani hata huyu aliyejiita shemeji yake alikuwa anamfahamu kama mwimbaji wa nyimbo za wasanii na siyo mwandishi.

Saa kumi na moja na nusu jioni ilinikuta nikiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya bei nafuu iliyokuwa karibu na makazi ya Bwana Brian.

Hadi muda huo nilikuwa nimeshawasilina na mpenzi wake Grace ambaye aliniambia angekuja nilipofikia ili tujadiliane namna ya kuifikisha taarifa ya kifo kwa nduguze Brian Mgaya ambaye walikuwa wanatoka kijiji kimoja.

Tuliifikisha taarifa hiyo kistaarabu lakini ilipokelewa kwa namna tulivyoitarajia kwani baada ya muda tulipewa taarifa ya mama yake mzazi kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali kwa kupata shinikizo la damu.
Niliagana na Joseph rafiki wa Brian akimwita ni kaka yake, akidai licha ya kukaa mtaa mmoja iliwachukua hata miezi miwili kuonana.

Nilijua ni mambo ya mjini hayo, ujamaa haukuwa na nafasi kubwa isipokuwa kwenye misiba na kumbi za starehe.

Usingizi uligoma kunichukua licha ya uchovu na ulevi wa kutwa nzima.Ni mara ya kwanza nilikuwa nimemuona Bwana Brian Mgaya mwandishi niliyekuwa namhusudu ile kuuona mwili wake ukiwa hauna uhai ilinifanya nishindwe kupata lepe la usingizi na hata pale nilipoupata niliupata wa mang’amung’amu.

Nikiufikiria ule utanashati kwenye zile picha zake za mtandaoni na ‘usmart’ kwenye maandishi yake uliishia kwenye mwili wake uliokuwa hauna uhai madevu yamejiotea ovyo onyo, nywele zake ndefu zisizochanwa na macho yake yaliyoingia ndani nadhani kwa kukonda na ulevi uliokithiri huku midomo yake ikitamani kuliweka tabasamu wakati anakata roho.

Hakuwa yule Brian ambaye wasichana wengi mtandaoni walikuwa wakimsifia na kutamani kuonana naye , lakini daima alidai asingependa kuonana na wasichana kwa faragha zaidi ya kwenye makutano ya kiuandishi ambayo alipanga kuyaandaa na kuyafanya.

Masikini Brian hakuandaa tamasha zaidi ya hili la kuagwa na kuzikwa kwake ambalo ataandaliwa kijijini kwao na wahudhuriaji wachache kuliko wafuatiliaji wake mitandaoni.

Wazo la kwenda kukichunguza chumba chache lilinijia, ghafla nikakurupuka na kuvaa koti refu na viatu vigumu vya ngozi ambavyo nilipenda kuvivaa siku za ijumaa shuleni nilipowapigisha kwata wanafunzi ambao daima waliinita Mjeshi.

Kimvua kilichokuwa kinanyesha hakikunizuia kupiga hatua kubwa kubwa huku masikio yangu yakijitahidi kudaka kila kilichokuwa tofauti na manyunyu yale.

Mita hamsini kutoka alipokuwa akiishi Bwana Brian nilisikia sauti za nyao za watu wakikimbilia uelekeo niliokuwa nikitokea. Hadi leo hii sijui ulikuwa ni ulevi ama ujinga tu ulinivaa maana sikukimbia wala kujificha licha ya nafasi ya kufanya hivyo ilikuwepo.

Nikaongeza mwendo, nikavaana na kijana mmoja aliyekuwa amebeba kasha kubwa wala haikuhitaji mwanga kujua kuwa ilikuwa ni televisheni.

Kwa kuwa hakutegemea kitendo hicho, likamtoka tusi la nguoni pamoja na lile kasha kuanguka chini. Nami sikumpa pole kwa hilo zaidi akapokea ngumi iliyomfanya akimbilie bisu lake lililokuwa alani na kutaka kulitumia kwani alikuwa amechelewa nilikuwa nimeshamtia ngwala iliyompeleka matopeni wakati huo wale wenzake waliokuwa nyuma yake wakitimua mbiyo.

Alijitahidi kuinuka tena, sijui ili akimbie lakini nikamrudisha tena safari hii nikimkandamiza na buti langu lisilo na huruma mgongoni.

TUKUTANE KESHO
 
View attachment 2718126

Njoo boss
 
HADITHI: KIFO CHA MWANDISHI
SEHEMU YA PILI
Mtunzi: More
Mawasiliano: 0756320219

Safari ya kutoka Dodoma inanifikisha Arusha kwa mwandishi ninayemhusudu lakini simkuti mwandishi huyo Bali mwili wake. Polisi wakituambia kuwa mwandishi huyo alikufa kutokana na , kitendo chake kulala na jiko la mkaa lililokuwa likiwaka.
Sikumwona Brian kama mzembe wa kufa kizembe hivyo. Nikaamua kulivalia njuga suala hilo ambapo baada ya kutoka taarifa ya kifo chake, kwa familia yake nikaamua kwenda kufanya uchunguzi wa chumba chake usiku wa saa saba.
Ajabu nakumbana na jamaa ambao bila kuuliza kuwa walikuwa ni vibaka.
Nikapambana na mmoja wao aliyekuwa amebeba kasha la televisheni.

TUENDELEE....
Yule bwana baada ya kuhisi alikuwa akizidiwa na kipigo nilichokuwa namshushia akalichukua lile kasha na kutimua mbio gizani. Sikuhangaika nikaokota simu yangu iliyokuwa imeangukia topeni wakati wa pambano lisilo rasmi.Nikaiwasha kujua kama ilikuwa imepata tatizo , kama nilivyohisi yule bwege aliikanyaga kabla ya kukimbia na kuipasua kioo chake.
Ule mwanga wa simu uliakisiwa na kitu kidogo cha chuma kilichokuwa pale chini.
Baada ya kukiokota na kufuta tope nikagundua kuwa ilikuwa ni "flash" , nikaitia mfukoni na kuondoka eneo lile haraka ili nisiyekutwa na vibaka ama sungusungu ugenini katika usiku ule mkubwa.
Kichwa changu kilitawaliwa na mambo mengi ,nikijishangaa namna nilivyopambana na kibaka yule aliyekuwa akinuka bange na pombe kali.
Kifo cha Brian kilikuwa kimenifanya nijione mtu mwingine.
Nikawasha Kompyuta mpakato ambayo niliibeba kwa lengo la kusomea hadithi kwani sikuwa napenda sana kusoma hadithi kwenye simu.Nikaipachika ile "flash" kwa lengo la kujua ukubwa wake huku nikiipangia matumizi kutokana na ukubwa wake nitakao ukuta.
Haikuwa na jina, ukubwa wake ulikuwa terabaiti moja.
"Ngoja niifomati, hii nitaweka muvi na documentari za kutosha" nikajiambia huku nikitabasamu.
Badala ya 'right click' nipate opsheni za kuifomati nikajikuta nimeifungua ila flashi. Nikakutana na mafolda mengi yakiwa yamejipanga lililonivutia zaidi liliandikwa HADITHI. Nikalifungua na kukuta kuna mafolda mengine manne RIWAYA, SIMULIZI, HADITHI FUPI na MASHAIRI.
Nikafungua folda la kwanza ajabu nikakutana na riwaya ya MWEHU, ni hadithi ya bwana Brian Mgaya, ya pili ya tatu na ya nne vivyo hivyo zilikuwa ni za kwake.
Kwa pupa nikafungua mafolda mengine Nako nikakutana na kazi za Brian. Nikahis wale mabwana watakuwa wametoka kumwibia marehemu.
Wazo la kuifomati likatoka nikajikuta nikiikagua ile flash nikajikuta natuama kwenye folda moja lililokuwa ndani ya folda lililokuwa limeandikwa KIFO CHA MWANDISHI.
Nikalifungua na kukutana na faili la PDF na kuanza kulisoma.

"Kifo ni kama kisogo, tupo nacho ila hatukioni"

Ilianza kama simulizi nzuri ya Huba , lakini mwishowe ikaja kuwa hadithi mbaya ya visasi na mateso yasiyomithilika.
Ndiyo ile simulizi tamu ambayo niitumai ingekuja kuwa na mwisho mwema , ule wa kufa na kuzikana.Simulizi kati yangu mie na Sarah Binti Tarimo mrembo ambaye alikuja kuwa nguzo ya maisha yangu kabla haijatolewa na kunifanya nikose pa kuegemea.
Nakuchanganya msomaji wangu , enhhe?
Tulia basi nikusimulie hadithi tamu ambayo ilipelekea kifo cha mwandishi wenu.

Nilionana naye miaka kadhaa iliyopita, siku ile nilikuja jijini Arusha nikiwa miongoni mwa waandishi chipukizi waliokuwa wameingia kumi bora ya waandishi wa hadithi fupi kwa vyuo vya Afrika Mashariki.Hakuwa miongoni mwa washiriki wala wageni waliohudhuria hafla hiyo ambayo licha ya hadithi yangu kuwa katika kumi bora haikufanikiwa kuingia kwenye nafasi tano za juu, ambako waandishi wake walipata zawadi ya fedha, vyeti na hadithi zao kuandika kwenye jarida la lugha la jumuhia ya Afrika mashariki.
Hadithi yangu ya NIMPE NINI MAMANGU ilishika nafasi ya kumi ambapo niliambulia kupongezwa na kushikana mikono na wageni waliohudhuria halfa hiyo kwenye ukumbi wa AICC.
Siku ya pili baada ya hafla hiyo nikaamua kulizunguka Jiji la Arusha nikifanya utafiti wa kijiografia na kiutamaduni kwa ajiri ya hadithi yangu niliyokuwa nikiiandika wakati huo, nikiwa nimetumia mandhari ya Arusha.
Nikiwa kwenye mizunguko hiyo nikajikuta nimefika stendi ndogo ambapo zogo flani lilinifanya nisogee karibu kushangaa kilichokuwa kinatokea.
Ilikuwa ni nje ya duka dogo la vipodozi ambapo dada mmoja alikuwa akijaribu kujieleza mbele ya wanaume wanne ambao walikuwa wakizoza.
Kumbe mmoja wa wale mabwana alikuwa akirejesha mafuta ambayo alidai muda wake wa matumizi ulikuwa umepita huku yule dada akieleza kuwa mafuta yale hayakununuliwa pale dukani akionesha mafuta mengine yaliyokuwa kwenye bachi Moja na aliyekuwa ameyauza.
Dada alijieleza Hadi chozi likimtoka.
Nikatoa pesa kwenye simu na kumwambia yule dada kuwa nimetoa pesa.
Hakunisikiliza huku akiendelea kupambana na wale mabwana ambao wakati huo walikuwa wakimtishia kumripoti kwenye mamlaka inayohusika na udhibiti wa vipodozi.
" Dada nihudumie uendelee na zogo lako" Nikaendelea kuvurugura mjadala wao ambao ulizidi kuvuta watu.
" Kaka kuwa mstaarabu basi, si umeniona na wateja?" Aliongea kiukali akiangakia simu ndogo iliyokuwa kwenye droo.
" Dada tupe arobaini na tano yetu ama tukiripoti" Aliongea mmoja wa wale mabwana kibabe baada ya kuona yule dada anataka kunihudumia.
" Kumbe arobaini na tano tu, ndo wanapiga kelele hivyo, wape halafu inayobaki nipe " nikaongea kwa sauti.
"Dogo hayakuhusu" Alitaka kuchimba mkwara mmoja wao akinigeukia lakini nikaona mwenzake akimshtua.
"Mpenzi chukua hayo mafuta tutajipaka wenyewe" Niliongea kwa kujiamini yule dada akanitumbulia macho huku akipokea yale mafuta kwani yule bwana alitaka kuondoka nayo.
Nikapokea chenchi yangu na kuondoka eneo lile nisitake kujua nini kiliendelea.

Itaendelea....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom