Mrejesho safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Jifunafu

Senior Member
May 25, 2020
182
603
Wanajanvi Salaam,

Ni matumaini yangu wanajanvi mko wazima na mnaendelea na harakati za upambanaji wa kutafuta mkate wa familia.

Napenda kuleta mlejesho wangu kuhusu safari yangu ya kwenda Mpanda kufanya kilimo Cha mahindi.
Wadau kama mnakumbuka mwaka jana nilileta Uzi hapa uliosema, NAITAJI KWENDA KUFANYA KILIMO MKOA WA KATAVI. Baadhi ya wadau walitoa michango Yao ya kunitia moyo na kunipa usahuri zaidi nmna ya kufanya kilimo uko.

1. SAFARI YA KUTEMBELEA MAONYESHO YA KILIMO YA NANE NANE MWANZA KUPATA MBINU ZA KILIMO.
Ikumbukwe wakati nafikiria kwenda mkoa wa KATAVI nilikuwa nime acha kazi ambayo nilikuwa nikifanya Moja ya 5 stars Hotel uko Zanzbar, mshahara ulikuwa ni mdogo na muajiri anachelewesha kulipa na kazi ni manyanyaso na haina pumziko Wala likizo. Mkataba haieleweki Wala Nini.

Kwakweli nilikuwa nikienda kazini lakini akili yangu inawaza mbali kila uchao. Baada ya kuwa nimeacha kazi nilirudi Nyumbani na ndipo nikaanza kufikiri ni wapi nitaenda kufanya kilimo, ndipo wazo likaniijia nitakwenda mkoa wa KATAVI. Nilileta Uzi hapa jamvini kutaka kujua maoni mbalimbali kutoka Kwa wadau na kujua namna gani ya kuanza kilimo.

Ikumbukwe kilimo sio mara ya kwanza nilikuwa naanza hapana, nyumbani tumekuwa tukilima na pia kabla ya kujiingizia kwenye mambo ya ajira nilikuwa nafanya kilimo na nilianza kuona mafanikio lakini niliacha na kutimkia kwenda kuajiriwa, lakini sikuona faida ya ajira iyo.

Kwaiyo nilikwenda kulima nikiwa naamini nitaweza, maana uzoefu nilikuwa nao.

Niliamua kutembelea maoanyesho ya wakulima NANE NANE, Ili kupata kujua abc kuhusu mbegu na madawa.
Baada ya kujua mengi hapo, ndio safari yangu iliwadia kuelekea mkoa wa KATAVI.

2.SAFARI KUTOKA MWANZA KUELEKEA KATAVI.
Mnamo mwezi wa nane mwaka jana ndipo safari yangu ilianza, nilikata tiketi stand ya nyengezi katika kampuni ya NBS na atimae majira ya alfajiri safari ikaanza.

Kuhusu mwenyeji wa kunipokea kule kulikuwa na jamaa ambae tuliwai kufanya nae kazi uko Zanzbar na kwao ni Mkoa wa KATAVI na yeye pia alikuwa amecha kazi miaka mitatu iliyopita ivyo tulikuwa tuna wasiliana, japo yeye alikuwa mjini na maeneo mengi ya viijiji alikuwa hayajui lakini aliniambia Kuna jamaa anafahamiana nae yupo Kijiji cha MWESE NO4 anafanya kilimo Cha maharage.

Baada ya kuniunganisha na uyo jamaa wa MWESE niliongea nae na akaniambia maeneo aliopo mashamba yanapatika, ukitaka ambalo limefyekwa unakodi Kwa 50000,Hadi 30000. Ni maelewano tu, ukitaka upewe pori ufyeke ulime ni bure lakini kunakuwa na makubaliano baina Yako na mwenye eneo ni misimu mingapi utalima na kumuachia shamba lake.

Mazungumzo na uyo jamaa wa MWESE tuliyafanya kabla sijaondoka Rock City, hivyo alinipa abc kuhusu uko aliko.

3.NIMEFIKA TAYARI MKOA WA KATAVI.
Baada ya kuwa nimewasili salama majira ya Saa kumi na mbili jioni, nilipokelewa na mwenyeji wangu hapo mjini na kuelekea kwake, nilifurai sana kuonana na jamaa yangu ambae tuliachana kwa muda mrefu.

Usiku tulikula na kupiga story za kule zanzbar wakati tukiwa pamoja na na ndipo nilikwenda kupumzika, huku akili yangu ikiwa na shauku ya kuingia pori kuchapa kazi. Ikumbukwe wakati naelekea kule nilikuwa tayari nimebeba baadhi ya vitendea kazi na nguo nzito za bariadi pamoja na sora yangu kwaajili ya Matumizi ya kuchage simu na mwanga pia. Pia nilibeba dagaa wa kutosha mafuta ya kupikia, vitabu vya kusoma wakati nikiwa pori, radio, dawa za aina mbalimbali kumbuka ni shamba lazima uwe na Huduma kama hizo.

4. SAFARI INA ANZA KUTOKA KATAVI MJINI KUELEKEA KIJIJI CHA MWESE NO4.
Baada ya kuamka asubui tulisalimina na mwenyeji wangu na ndipo tukafanya mawasiliano na yule jamaa wa mwese, akanipa ramani ya kufika kule na akasema yeye anapandisha kutoka alipo na nitamkuta stand ya MWESE NO4 ananisubiri, kitendo Cha kuniambia ANAPANDISHA KUTOKA ALIKO. akili yangu nikajua tu kumbe uyu jamaa ayupo kijijini hapo Bali yupo pembezoni, kwakuwa nilikuwa nimeamua kujidunga sindano nilisema moyoni litakalo kuwa na liwe poa tu. Nilichojionea mkoa wa KATAVI wageni ni wengi sana hususani jamii ya kisukuma.

Sitaki kusema uongo, kama Kuna kabila ambalo nalikubali hapa Tanzania ni Wasukuma, ni jamii ambayo haina wivu Wala chuki Kwa mgeni ukifikia katika malango ya msukuma yupo tayari kukusaidia Kwa kile alicho nacho Ili wewe upate. Nitaelezea uko mbele ukalimu wa wa wasukuma.

Kutoka Mpanda mjini hadi MWESE NO4 ni kama masaa manne kufika hapo kijijini, katika hii almashauri ya wilaya ya Tanganyika Ina vijiji vingi ikiwamo center maalufu ya wakulima wa mahindi na ndipo kituo kikubwa Cha wanunuzi wa Mahindi kutoka mikoani na nchi jirani za SADEC.

Kwakweli center hiyo imechangamka sana na harakati ni nyingi. Japo vijiji ni vingi lakini sivijui vingine Kwa majina yake.

Kitu kingine kilicho nishangaza ni namna kulivyo na majina ya vijiji ambavyo vinajulikana Kwa namba, kwaiyo ukisema unaenda MWESE lazima useme unaenda namba ngapi? Kuna NO 10,NO 9 NO 8, NO 7,NO 6,NO 5,NO 4, NO 3,NO 2, na NO 1.

Na iyo namba 4 ndio Kijiji cha mwisho kinaenda kupakana na Wilaya ya uvinza Mkoa wa Kigoma.

5. TAYARI NIMEFIKA KIJIJI CHA MWESE NO4.
Kwakweli ni safari ya masaa kama manne lakini yenye shuluba kali, maana ilikuwa wakati wa kiangazi kwaiyo barabara ni vumbi kweli kweli yani unafika utamaniki kama ni binadamu, kama una roho nyepesi safari Yako inaweza kuishia hapo NO 4.

Lakini siku zote waenga walisema ukitaka Mali utaipata shambani, msemo huu ni kweli na hakika.

Wakati Niko njia nikawasiliana na Jamaa yangu wa MWESE NO4 akaniambia yeye anapandisha kutoka alipo hivyo akanielekeza kwamba nikifika hapo stand nitaulizia kwenye mji wa jamaa flani tumpe jina la Kapumputika haya ni majina ya wabende wa mkoa wa KATAVI. Baada ya kuwa nimefika stand niliuliza kwenye mji huo na ndipo nichukua pikipiki na akafunga mizigo yangu tukaelekea hapo Katika mji huo alipo nielekeze kwamba atanikuta.

Kitu kilicho nivutia katika kijijini hicho ni uwepo wa maziwa mengi, Yani kidumu Cha Lita Tano Bei ni 2000, kwakweli nilishaanga sana, Wenyeji wakasema kijijini hapo wafugaji ni wengi na mifugo Iko maporini huko. Kwakweli maziwa ni mengi sana.

5.SAFARI INAANZA KUTOKA MWESE NO4 KUELEKEA IGONGE KWA JAMAA YANGU, AMBAPO KUNA SHAMBA.
Baada ya kuwa nimefika katika mji huo nilijitambulisha na kusema nimeelekezwa na fulani, tumpe jina la Kasukari.

Nilikaa kama masaa mawili ndipo mwenyeji wangu Kasukari akawa amefika, tukasalimia na kutambulishana maana hatujuwani na hatujawai kuonana na nimemfahamu kupitia jamaa yangu yule tuliekuwa nae Zanzibar.

Kumbe uyu Kasukari nae ni mtu wa kutoka mkoa wangu japo kabila tofauti lakini katika mazungumzo tunaelewana vizuri tu.

Uyu Kasukari na yeye sio mzaliwa wa uko ila alienda tu kusaka furusa na alikuwa amejikita katika kilimo Cha maharage, mahindi na ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Baada ya maongezi mafupi aliniambia sasa tuchukue mizigo tuanze safari, nilimuuliza vipi kama ni mbali tuchukue pikipiki, alisema mwamba!! hapa tukisema tuchukue pikipiki atatupiga bei kubwa na njia ya pikipiki ni mzunguko. Hivyo tupite short cut, lakini akaniambia mwamba!! Maisha ya uko utaweza? nilimuwakikishia Niko imara na ujio wangu sijalazimishwa na mtu, nimekuja mwenyewe kulima.

Kwakweli nilikuwa na mizigo mingi, tuligawana Kila mtu akabeba na safari ikaanza kuelekea IGONGE shambani. Tulipanda milima na kushika mabonde kama vile tuko vitani,mithili ya wanajeshi walio vitani wakiwa na mabegi mazito na siraha migongoni mwao.

Ni mwendo wa lisaa limoja na nusu tukaingia ndani ya IGONGE, uko IGONGE sio kijiji ni mashambani ambako watu wanafanya kilimo lakini makazi Yao ya kudumu Yako MWESE,japo ni kama vile niliona wengi wameshafanya makazi ya kudumu huko.Huduma zote za mahitaji mhimu hadi uende NO4 , ndipo utapata huduma za kifedha na maitaji yote uko, kwaiyo unapoingia kule Make sure umefanya window shopping ya mahitaji yote.

6.MAISHA NDANI YA IGONGE.
Baada ya kuwa tumefika IGONGE Kwa Jamaa yangu Kasukari, ni mtu ambae alikuwa anakaa peke yake maana hakuwa na mke wala mtoto, hivyo maisha yalikuwa ni ya kijeda zaidi ndani geto fulu nyasi juu na miti, wakati godoro likiwa ni la nyasi ndani yake, maisha yakaanza hapo, kweli Kuna wakati nilikuwanawaza mbona nimekuja kuteseka huku? roho nyingine inaniambia nirudi mjini, lakini nikajiambia hivi nitakuwa na akili kweli?. Nimeacha kazi kuja kulima alafu tena nirudi mjini nitafanya nini? ndipo nilisema nitapambana kufa na kupona hadi kieleweke. Yani sikati tamaa hadi mwisho.

Kesho yake asubui kulivo pambazuka sikutaka kupoteza muda nilimwambia Kasukari ni wakati sasa tufanye survey nicheki hayo mashamba Ili nianze kusafishia, ni kweli Jamaa yangu Kasukari alikuwa ni mtu muelewa sana aliniambia Kuna Mzee flani anamashamba makubwa hivyo tungependa kumuona kwake.

Lakini usiku huo niliona kwangu ni mgumu sana maana sikulala Yani panya ilikuwa ni vurugu kama vile ni panya watu, ukizubaa unaliwa kidole, kumbe ni sababu jamaa alikuwa kutunza mahindi umo geto kwaiyo walikuwa wanakimbizana kutafuta chakula maana ilikuwa ni kiangazi hivyo mashambani watu wameshavuna hakuna chakula tena. Ndo maana ilikuwa vurugu.

Mnamo saa tatu asubui safari ya kuelekea kuona shamba lifika na tukaenda Kwa uyo mzee, maana haukuwa mbali sana na Kwa jamaa yangu Kasukari . Baada ya kuwa tumewasili Kwa uyo mzee hatukumkuta, tuliambiwa na mke wake yuko shambani, tulielekea kule shambani na tukamkuta na ndipo jamaa yangu Kasukari alinitambulisha na kumueleza lengo langu la kuitaji SHAMBA, ikumbukwe Mimi sikuwa na fedha za kununua bali nilikuwa naitaji kukodi tu. Hivyo Mzee aliniuliza unataka SHAMBA la kufyeka ulime bure alafu utaniachia au unataka ambalo limeisha fyekwa tayari? ,Kwakuwa lengo halikuwa la kufyeka msitu, nilimwambia naitaji ambalo liko tayari, aliniambia bei ni elfu 70 Kwa heka.

Si unajua tena wakiona watu tumetoka town wanajua tuna ela kumbe njaa Kali.Kwakuwa Jamaa yangu Kasukari alikuwa ameniambia Bei,sikutaka kuwa mzungumzaji, yote nilimuachia Kasukari akasimamia mazungumzo na ndipo Mzee alikubali 50000/Kwa heka Moja. Baada ya kuwa tumezungukia maeneo ya uyo mzee, Kuna eneo nililipenda maana lilikuwa karibu na mto, target yangu ilikuwa ni kuweka bustani ya mboga mboga kwaajiri ya Matumizi yangu ya kambi. Hivyo nilimwambia anikatie sehemu iyo.

Basi Mzee aliniambia utaanzia hapa na kuishi kule akaweka alama, kwakweli ni kama alikadilia tu, maana Mimi niliitaji Eka mbili tu kulingana na bajeti yangu, lakini nilivokuja kupima na Jamaa yangu Kasukari zilikuwa kama ekari 3 na nusu.

Nilimpa laki Moja, hakuna Cha maandikiano mzee, kazi kazi tu.

7.KAZI YA KUSAFISHA SHAMBA INA ANZA RASIMI NDANI YA IGONGE.
Wakuu sikutaka kupoteza muda kabisa Yani ndio ivyo uelewe au usielewe, kwakuwa SHAMBA nililikuwa nimelimwa mahindi na alikuwa amemaliza kuvuna hivyo kulikuwa na vichaka vichaka maana jamii ya pale hawana utamaduni wa kuchapa kazi kwaiyo kilimo Chao ni Cha mazoea, unakuta amelima hapa, ameluka akalima pale, Yani hata kama Kuna kakichacha hana muda wa kufyeka, na kitu kingine hata shamba hawalimi ndio wakapanda, Yani wanafyeka na kuchimba mashimo na kuweka mbegu, lakini mahindi yanavyo Toka asikwambie mtu. Mahindi yanasimama sema hawana utamaduni wa kupanda mbegu Bora na kupuliza madawa ya kuuwa wadudu. Wao wanapanda zile mbegu za kienyeji ndefu lakini mahindi yanatoka tu.

Basi kazi ikaanza ya kusafisha Yani kukata vichaka na kupanua eneo kiaina, maana eneo lilikuwa ni kubwa sema upande wa kuelekea mtoni ilikuwa ni vichaka, kwangu niliona huko ndo Kuna mzigo hvyo sikutaka kuona kichaka , nilisafisha Hadi Mzee akashanga, Kwa vile sikuwa na masihara Yani ndani ya wiki moja SHAMBA likawa jeupe pee, raia wakaanza kushangaa na kuanza kumuuliza Jamaa yangu Kasukari hivi uyo ndugu Yako ni mwanajeshi ? Au labda atakuwa ni mpelelezi? Kwakuwa Mimi nilikuwa nimetumwa na kijiji, hivyo sikutaka kupoteza muda Wala mazoea yaliyopitiliza, maana tayari nilikuwa nimepata story ya jamii tunayoishi nayo,nilikuwa makini sana. Kazi ikaendelea .

8.KUFOKEANA NA MKE WA MZEE MWENYE SHAMBA NILILO KODI.
Wakuu ikumbukwe hapo ninaendelea na kazi ya kusafisha shamba. Naamka alfajiri natokea geto Kwa Kwa jamaa yangu Kasukari naenda shambani, ilikuwa ni mwendo wa nusu saa kutoka Kwa Kasukari kuja shambani.
Siku Moja nikiwa SHAMBA naendelea na harakati za kusafishia ndipo alikuja Bibi mmoja maana nilikuwa si mfahamu na sijawai kumuona, kumbe alikuwa ni mke mkubwa wa yule Mzee niliekodi kwake SHAMBA, lakini walikuwa wamesha achana na Mzee, na Mzee alikuwa ameoa bii mdogo ambae Mimi nilikuwa namfahamu.

Basi Wakuu baada ya kufika nilipo akaniuliza!! We kijana ni nani amekuruhusu usafishe Ili SHAMBA? Hapo anafoka kinoma nikamwambia kabla ya kunifokea tufahamiane we ni nanj ? Ili na Mimi nikupe maelezo. Dahhhh Bibi aelewi, anasema nani amekukodishia na umetoa Bei Gani? Nikaona uyu mama ngoja na Mimi nimkolomeee maana amekuja kigaidi. Basi nikamwambia sikia, kwavile umekuja Kwa shali na wewe ni mzazi wangu nimekupa heshima lakini uelewi nakuomba utoke hapa,mambo yote na majibu atakujibu yule Mzee kule, maana Mzee nae hakuwa mbali sana , hivyo akaondoka kaelekea Kwa Mzee baada ya kuona nimewasha moto.

Kumbe Mzee alikuwa anamuona wakati yuko pale shambani, baada ya kufika kule Kwa Mzee, Mzee nae akawa anamgombeza na uyo Bibi akarudi kwangu na kusema maneno haya.........Wewe kijana unajidai unajua sana tutaona kama utavuna kwenye hili shamba.

Na Mimi nikamjibu tena nitavuna sana zaidi Yako na utashangaa.

Baadae yule Mzee akaja pale shambani na kuniambia kijana usimskilize uyo ni mjinga, akaendelea kusema.. uyo alikuwa ni mke wangu mkubwa na tulisha achana na nilimgawia mashamba yake na mji wake ni ulekule, lakini bado ananifata katika mashamba yangu, Kila nikikodisha SHAMBA anataka nimpe ela. Kijana we chapa kazi Wala asikubabaishe we niangalie Mimi tu..

Itaendelea Nini kilitokea.

Sehemu ya Pili: Mrejesho safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa katavi- Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Sehemu ya Tatu: Mrejesho safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa katavi- Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Sehemu ya Nne: Mrejesho safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa katavi- Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4
 
Wanajanvi Salaam,

Ni matumaini yangu wanajanvi mko wazima na mnaendelea na harakati za upambanaji wa kutafuta mkate wa familia.

Napenda kuleta mlejesho wangu kuhusu safari yangu ya kwenda Mpanda kufanya kilimo Cha mahindi.
Wadau kama mnakumbuka mwaka jana nilileta Uzi hapa uliosema, NAITAJI KWENDA KUFANYA KILIMO MKOA WA KATAVI. Baadhi ya wadau walitoa michango Yao ya kunitia moyo na kunipa usahuri zaidi nmna ya kufanya kilimo uko.

1. SAFARI YA KUTEMBELEA MAONYESHO YA KILIMO YA NANE NANE MWANZA KUPATA MBINU ZA KILIMO.
Ikumbukwe wakati nafikiria kwenda mkoa wa KATAVI nilikuwa nime acha kazi ambayo nilikuwa nikifanya Moja ya 5 stars Hotel uko Zanzbar, mshahara ulikuwa ni mdogo na muajiri anachelewesha kulipa na kazi ni manyanyaso na haina pumziko Wala likizo. Mkataba haieleweki Wala Nini.

Kwakweli nilikuwa nikienda kazini lakini akili yangu inawaza mbali kila uchao. Baada ya kuwa nimeacha kazi nilirudi Nyumbani na ndipo nikaanza kufikiri ni wapi nitaenda kufanya kilimo, ndipo wazo likaniijia nitakwenda mkoa wa KATAVI. Nilileta Uzi hapa jamvini kutaka kujua maoni mbalimbali kutoka Kwa wadau na kujua namna gani ya kuanza kilimo.

Ikumbukwe kilimo sio mara ya kwanza nilikuwa naanza hapana, nyumbani tumekuwa tukilima na pia kabla ya kujiingizia kwenye mambo ya ajira nilikuwa nafanya kilimo na nilianza kuona mafanikio lakini niliacha na kutimkia kwenda kuajiriwa, lakini sikuona faida ya ajira iyo.

Kwaiyo nilikwenda kulima nikiwa naamini nitaweza, maana uzoefu nilikuwa nao.

Niliamua kutembelea maoanyesho ya wakulima NANE NANE, Ili kupata kujua abc kuhusu mbegu na madawa.
Baada ya kujua mengi hapo, ndio safari yangu iliwadia kuelekea mkoa wa KATAVI.

2.SAFARI KUTOKA MWANZA KUELEKEA KATAVI.
Mnamo mwezi wa nane mwaka jana ndipo safari yangu ilianza, nilikata tiketi stand ya nyengezi katika kampuni ya NBS na atimae majira ya alfajiri safari ikaanza.

Kuhusu mwenyeji wa kunipokea kule kulikuwa na jamaa ambae tuliwai kufanya nae kazi uko Zanzbar na kwao ni Mkoa wa KATAVI na yeye pia alikuwa amecha kazi miaka mitatu iliyopita ivyo tulikuwa tuna wasiliana, japo yeye alikuwa mjini na maeneo mengi ya viijiji alikuwa hayajui lakini aliniambia Kuna jamaa anafahamiana nae yupo Kijiji cha MWESE NO4 anafanya kilimo Cha maharage.

Baada ya kuniunganisha na uyo jamaa wa MWESE niliongea nae na akaniambia maeneo aliopo mashamba yanapatika, ukitaka ambalo limefyekwa unakodi Kwa 50000,Hadi 30000. Ni maelewano tu, ukitaka upewe pori ufyeke ulime ni bure lakini kunakuwa na makubaliano baina Yako na mwenye eneo ni misimu mingapi utalima na kumuachia shamba lake.

Mazungumzo na uyo jamaa wa MWESE tuliyafanya kabla sijaondoka Rock City, hivyo alinipa abc kuhusu uko aliko.

3.NIMEFIKA TAYARI MKOA WA KATAVI.
Baada ya kuwa nimewasili salama majira ya Saa kumi na mbili jioni, nilipokelewa na mwenyeji wangu hapo mjini na kuelekea kwake, nilifurai sana kuonana na jamaa yangu ambae tuliachana kwa muda mrefu.

Usiku tulikula na kupiga story za kule zanzbar wakati tukiwa pamoja na na ndipo nilikwenda kupumzika, huku akili yangu ikiwa na shauku ya kuingia pori kuchapa kazi. Ikumbukwe wakati naelekea kule nilikuwa tayari nimebeba baadhi ya vitendea kazi na nguo nzito za bariadi pamoja na sora yangu kwaajili ya Matumizi ya kuchage simu na mwanga pia. Pia nilibeba dagaa wa kutosha mafuta ya kupikia, vitabu vya kusoma wakati nikiwa pori, radio, dawa za aina mbalimbali kumbuka ni shamba lazima uwe na Huduma kama hizo.

4. SAFARI INA ANZA KUTOKA KATAVI MJINI KUELEKEA KIJIJI CHA MWESE NO4.
Baada ya kuamka asubui tulisalimina na mwenyeji wangu na ndipo tukafanya mawasiliano na yule jamaa wa mwese, akanipa ramani ya kufika kule na akasema yeye anapandisha kutoka alipo na nitamkuta stand ya MWESE NO4 ananisubiri, kitendo Cha kuniambia ANAPANDISHA KUTOKA ALIKO. akili yangu nikajua tu kumbe uyu jamaa ayupo kijijini hapo Bali yupo pembezoni, kwakuwa nilikuwa nimeamua kujidunga sindano nilisema moyoni litakalo kuwa na liwe poa tu. Nilichojionea mkoa wa KATAVI wageni ni wengi sana hususani jamii ya kisukuma.

Sitaki kusema uongo, kama Kuna kabila ambalo nalikubali hapa Tanzania ni Wasukuma, ni jamii ambayo haina wivu Wala chuki Kwa mgeni ukifikia katika malango ya msukuma yupo tayari kukusaidia Kwa kile alicho nacho Ili wewe upate. Nitaelezea uko mbele ukalimu wa wa wasukuma.

Kutoka Mpanda mjini hadi MWESE NO4 ni kama masaa manne kufika hapo kijijini, katika hii almashauri ya wilaya ya Tanganyika Ina vijiji vingi ikiwamo center maalufu ya wakulima wa mahindi na ndipo kituo kikubwa Cha wanunuzi wa Mahindi kutoka mikoani na nchi jirani za SADEC.

Kwakweli center hiyo imechangamka sana na harakati ni nyingi. Japo vijiji ni vingi lakini sivijui vingine Kwa majina yake.

Kitu kingine kilicho nishangaza ni namna kulivyo na majina ya vijiji ambavyo vinajulikana Kwa namba, kwaiyo ukisema unaenda MWESE lazima useme unaenda namba ngapi? Kuna NO 10,NO 9 NO 8, NO 7,NO 6,NO 5,NO 4, NO 3,NO 2, na NO 1.

Na iyo namba 4 ndio Kijiji cha mwisho kinaenda kupakana na Wilaya ya uvinza Mkoa wa Kigoma.

5. TAYARI NIMEFIKA KIJIJI CHA MWESE NO4.
Kwakweli ni safari ya masaa kama manne lakini yenye shuluba kali, maana ilikuwa wakati wa kiangazi kwaiyo barabara ni vumbi kweli kweli yani unafika utamaniki kama ni binadamu, kama una roho nyepesi safari Yako inaweza kuishia hapo NO 4.

Lakini siku zote waenga walisema ukitaka Mali utaipata shambani, msemo huu ni kweli na hakika.

Wakati Niko njia nikawasiliana na Jamaa yangu wa MWESE NO4 akaniambia yeye anapandisha kutoka alipo hivyo akanielekeza kwamba nikifika hapo stand nitaulizia kwenye mji wa jamaa flani tumpe jina la Kapumputika haya ni majina ya wabende wa mkoa wa KATAVI. Baada ya kuwa nimefika stand niliuliza kwenye mji huo na ndipo nichukua pikipiki na akafunga mizigo yangu tukaelekea hapo Katika mji huo alipo nielekeze kwamba atanikuta.

Kitu kilicho nivutia katika kijijini hicho ni uwepo wa maziwa mengi, Yani kidumu Cha Lita Tano Bei ni 2000, kwakweli nilishaanga sana, Wenyeji wakasema kijijini hapo wafugaji ni wengi na mifugo Iko maporini huko. Kwakweli maziwa ni mengi sana.

5.SAFARI INAANZA KUTOKA MWESE NO4 KUELEKEA IGONGE KWA JAMAA YANGU, AMBAPO KUNA SHAMBA.
Baada ya kuwa nimefika katika mji huo nilijitambulisha na kusema nimeelekezwa na fulani, tumpe jina la Kasukari.

Nilikaa kama masaa mawili ndipo mwenyeji wangu Kasukari akawa amefika, tukasalimia na kutambulishana maana hatujuwani na hatujawai kuonana na nimemfahamu kupitia jamaa yangu yule tuliekuwa nae Zanzibar.

Kumbe uyu Kasukari nae ni mtu wa kutoka mkoa wangu japo kabila tofauti lakini katika mazungumzo tunaelewana vizuri tu.

Uyu Kasukari na yeye sio mzaliwa wa uko ila alienda tu kusaka furusa na alikuwa amejikita katika kilimo Cha maharage, mahindi na ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Baada ya maongezi mafupi aliniambia sasa tuchukue mizigo tuanze safari, nilimuuliza vipi kama ni mbali tuchukue pikipiki, alisema mwamba!! hapa tukisema tuchukue pikipiki atatupiga bei kubwa na njia ya pikipiki ni mzunguko. Hivyo tupite short cut, lakini akaniambia mwamba!! Maisha ya uko utaweza? nilimuwakikishia Niko imara na ujio wangu sijalazimishwa na mtu, nimekuja mwenyewe kulima.

Kwakweli nilikuwa na mizigo mingi, tuligawana Kila mtu akabeba na safari ikaanza kuelekea IGONGE shambani. Tulipanda milima na kushika mabonde kama vile tuko vitani,mithili ya wanajeshi walio vitani wakiwa na mabegi mazito na siraha migongoni mwao.

Ni mwendo wa lisaa limoja na nusu tukaingia ndani ya IGONGE, uko IGONGE sio kijiji ni mashambani ambako watu wanafanya kilimo lakini makazi Yao ya kudumu Yako MWESE,japo ni kama vile niliona wengi wameshafanya makazi ya kudumu huko.Huduma zote za mahitaji mhimu hadi uende NO4 , ndipo utapata huduma za kifedha na maitaji yote uko, kwaiyo unapoingia kule Make sure umefanya window shopping ya mahitaji yote.

6.MAISHA NDANI YA IGONGE.
Baada ya kuwa tumefika IGONGE Kwa Jamaa yangu Kasukari, ni mtu ambae alikuwa anakaa peke yake maana hakuwa na mke wala mtoto, hivyo maisha yalikuwa ni ya kijeda zaidi ndani geto fulu nyasi juu na miti, wakati godoro likiwa ni la nyasi ndani yake, maisha yakaanza hapo, kweli Kuna wakati nilikuwanawaza mbona nimekuja kuteseka huku? roho nyingine inaniambia nirudi mjini, lakini nikajiambia hivi nitakuwa na akili kweli?. Nimeacha kazi kuja kulima alafu tena nirudi mjini nitafanya nini? ndipo nilisema nitapambana kufa na kupona hadi kieleweke. Yani sikati tamaa hadi mwisho.

Kesho yake asubui kulivo pambazuka sikutaka kupoteza muda nilimwambia Kasukari ni wakati sasa tufanye survey nicheki hayo mashamba Ili nianze kusafishia, ni kweli Jamaa yangu Kasukari alikuwa ni mtu muelewa sana aliniambia Kuna Mzee flani anamashamba makubwa hivyo tungependa kumuona kwake.

Lakini usiku huo niliona kwangu ni mgumu sana maana sikulala Yani panya ilikuwa ni vurugu kama vile ni panya watu, ukizubaa unaliwa kidole, kumbe ni sababu jamaa alikuwa kutunza mahindi umo geto kwaiyo walikuwa wanakimbizana kutafuta chakula maana ilikuwa ni kiangazi hivyo mashambani watu wameshavuna hakuna chakula tena. Ndo maana ilikuwa vurugu.

Mnamo saa tatu asubui safari ya kuelekea kuona shamba lifika na tukaenda Kwa uyo mzee, maana haukuwa mbali sana na Kwa jamaa yangu Kasukari . Baada ya kuwa tumewasili Kwa uyo mzee hatukumkuta, tuliambiwa na mke wake yuko shambani, tulielekea kule shambani na tukamkuta na ndipo jamaa yangu Kasukari alinitambulisha na kumueleza lengo langu la kuitaji SHAMBA, ikumbukwe Mimi sikuwa na fedha za kununua bali nilikuwa naitaji kukodi tu. Hivyo Mzee aliniuliza unataka SHAMBA la kufyeka ulime bure alafu utaniachia au unataka ambalo limeisha fyekwa tayari? ,Kwakuwa lengo halikuwa la kufyeka msitu, nilimwambia naitaji ambalo liko tayari, aliniambia bei ni elfu 70 Kwa heka.

Si unajua tena wakiona watu tumetoka town wanajua tuna ela kumbe njaa Kali.Kwakuwa Jamaa yangu Kasukari alikuwa ameniambia Bei,sikutaka kuwa mzungumzaji, yote nilimuachia Kasukari akasimamia mazungumzo na ndipo Mzee alikubali 50000/Kwa heka Moja. Baada ya kuwa tumezungukia maeneo ya uyo mzee, Kuna eneo nililipenda maana lilikuwa karibu na mto, target yangu ilikuwa ni kuweka bustani ya mboga mboga kwaajiri ya Matumizi yangu ya kambi. Hivyo nilimwambia anikatie sehemu iyo.

Basi Mzee aliniambia utaanzia hapa na kuishi kule akaweka alama, kwakweli ni kama alikadilia tu, maana Mimi niliitaji Eka mbili tu kulingana na bajeti yangu, lakini nilivokuja kupima na Jamaa yangu Kasukari zilikuwa kama ekari 3 na nusu.

Nilimpa laki Moja, hakuna Cha maandikiano mzee, kazi kazi tu.

7.KAZI YA KUSAFISHA SHAMBA INA ANZA RASIMI NDANI YA IGONGE.
Wakuu sikutaka kupoteza muda kabisa Yani ndio ivyo uelewe au usielewe, kwakuwa SHAMBA nililikuwa nimelimwa mahindi na alikuwa amemaliza kuvuna hivyo kulikuwa na vichaka vichaka maana jamii ya pale hawana utamaduni wa kuchapa kazi kwaiyo kilimo Chao ni Cha mazoea, unakuta amelima hapa, ameluka akalima pale, Yani hata kama Kuna kakichacha hana muda wa kufyeka, na kitu kingine hata shamba hawalimi ndio wakapanda, Yani wanafyeka na kuchimba mashimo na kuweka mbegu, lakini mahindi yanavyo Toka asikwambie mtu. Mahindi yanasimama sema hawana utamaduni wa kupanda mbegu Bora na kupuliza madawa ya kuuwa wadudu. Wao wanapanda zile mbegu za kienyeji ndefu lakini mahindi yanatoka tu.

Basi kazi ikaanza ya kusafisha Yani kukata vichaka na kupanua eneo kiaina, maana eneo lilikuwa ni kubwa sema upande wa kuelekea mtoni ilikuwa ni vichaka, kwangu niliona huko ndo Kuna mzigo hvyo sikutaka kuona kichaka , nilisafisha Hadi Mzee akashanga, Kwa vile sikuwa na masihara Yani ndani ya wiki moja SHAMBA likawa jeupe pee, raia wakaanza kushangaa na kuanza kumuuliza Jamaa yangu Kasukari hivi uyo ndugu Yako ni mwanajeshi ? Au labda atakuwa ni mpelelezi? Kwakuwa Mimi nilikuwa nimetumwa na kijiji, hivyo sikutaka kupoteza muda Wala mazoea yaliyopitiliza, maana tayari nilikuwa nimepata story ya jamii tunayoishi nayo,nilikuwa makini sana. Kazi ikaendelea .

8.KUFOKEANA NA MKE WA MZEE MWENYE SHAMBA NILILO KODI.
Wakuu ikumbukwe hapo ninaendelea na kazi ya kusafisha shamba. Naamka alfajiri natokea geto Kwa Kwa jamaa yangu Kasukari naenda shambani, ilikuwa ni mwendo wa nusu saa kutoka Kwa Kasukari kuja shambani.
Siku Moja nikiwa SHAMBA naendelea na harakati za kusafishia ndipo alikuja Bibi mmoja maana nilikuwa si mfahamu na sijawai kumuona, kumbe alikuwa ni mke mkubwa wa yule Mzee niliekodi kwake SHAMBA, lakini walikuwa wamesha achana na Mzee, na Mzee alikuwa ameoa bii mdogo ambae Mimi nilikuwa namfahamu.

Basi Wakuu baada ya kufika nilipo akaniuliza!! We kijana ni nani amekuruhusu usafishe Ili SHAMBA? Hapo anafoka kinoma nikamwambia kabla ya kunifokea tufahamiane we ni nanj ? Ili na Mimi nikupe maelezo. Dahhhh Bibi aelewi, anasema nani amekukodishia na umetoa Bei Gani? Nikaona uyu mama ngoja na Mimi nimkolomeee maana amekuja kigaidi. Basi nikamwambia sikia, kwavile umekuja Kwa shali na wewe ni mzazi wangu nimekupa heshima lakini uelewi nakutomba utoke hapa shambani hapa, mambo yote na majibu atakujibu yule Mzee kule, maana Mzee nae hakuwa mbali sana , hivyo akaondoka kaelekea Kwa Mzee baada ya kuona nimewasha moto.

Kumbe Mzee alikuwa anamuona wakati yuko pale shambani, baada ya kufika kule Kwa Mzee, Mzee nae akawa anamgombeza na uyo Bibi akarudi kwangu na kusema maneno haya.........Wewe kijana unajidai unajua sana tutaona kama utavuna kwenye hili shamba.

Na Mimi nikamjibu tena nitavuna sana zaidi Yako na utashangaa.

Baadae yule Mzee akaja pale shambani na kuniambia kijana usimskilize uyo ni mjinga, akaendelea kusema.. uyo alikuwa ni mke wangu mkubwa na tulishaa achana na nilimgawia mashamba yake na mji wake ni ulekule, lakini Kila Bado ananifata katika mashamba yangu, Kila nikikodisha SHAMBA anataka nimpe ela. Kijana we chapa kazi Wala asikubabaishe we niangalie Mimi tu..

Itaendelea Nini kilitokea.
Surviver
 
Back
Top Bottom