USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Moronight walker

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
3,105
4,635
Habari wana JF.

Kuna Ndoa imevunjika hapa ndoa ya miaka 15.

Mke alizaa kabla ya ndoa, sasa mama huyu alimficha mtoto,

Huyu mtoto alikuwa anaishi na Baba yake.

Mume alijua kwa mawasiliano ya simu Mama alipokuwa anaongea na mwanae.

Na mtoto ana umri wa miaka 20.

Mume wa ndoa kazaa naye watoto 4.

Dawati la suluhisho walijaribu kuweka sawa ili wasiachane ila ilishindika. Hata wachungaji walishauri kuwa asamehe tuu kwani hata mtoto kashakuwa mkubwa hakuna shida yoyote lkn ndo hivyo ndoa imevunjwa jana na mahakama.

Huyu mama alizaa kipindi ana umri wa miaka 21.

Sasa wanajamii hivi vitu vinatokana na nini mpk mmoja anaamua kuficha mtoto?

NI NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUJUA HATA KWA MUME KAMA ALIFICHA KUWA ALIKUWA ANAMTOTO.
 
Hapo Mume amewaza kama amefichwa suala la Mtoto kwa miaka yote hiyo, na kulikuwa na mawasiliano ya siri Baina ya Mkewe, Baba Mtoto pamoja Mtoto mwenyewe, basi kuna uwezekano mkubwa kuna vingine vingi vya siri vilikuwa vinaendelea baina ya Mkewe na huyo Baba wa Mtoto.. Na hapo ndipo panampa ugumu kusamehe..
 
Ndani ya hizi ndoa wengi tunaowaita mashemeji mara nyingi huwa ni watoto wa wake zetu.

Unakuta katoto unatambulishwa kama mdogo wa mwisho au mtoto wa dada/kaka kumbe ni mtoto wa mkeo.

Ni nadra kwa wanaume kuficha watoto waliopatikana kabla ya mahusiano ila wanawake mara nyingi wanahusisha kuwa na mtoto kabla na kushuka kwao kwa thamani kupelekea kuficha watoto wao wa kabla ya ndoa/mahusiano.
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Okay.....
Ingekua wewe ndio mwanaume unafikiri ungefanyaje?

Huku kwetu tunamuita huyo ni mwanamke mpumbavu, na amevunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
Hapo chanzo ni uongo, na maumivu ni jinsi alivyo fichwa kwa miaka mingi namnahiyo.

Na hapo mwanaume bilashaka amejenga tayari chuki hadi kwa familia ya mwanamke ilio tunza uongo ule kwa uaminifu kabisa.
 
Nahisi tatizo sio kuzaa kabla bali ni kuficha kuwepo na uzao wa kabla.

Msingi wa ndoa ni kuaminiana, sasa ikiwa wamekaa miaka 15 kukiwa na siri kubwa hivyo unahisi kuna mangapi kafichwa na kubwa zaidi kwanini mwanamke afiche ikiwa ni mtoto wa kabla ya mahusiano yao.
 
Lazima kuwe na sababu ya yeye kutokusema,

Kuna Mama alipokonywa mtoto na Mwanaume aliyezaa nae, mtoto alikua ana miezi 11, yule Mama alihangaika kuanzia Ustawi wa jamii hadi Mahakamani, kote aligonga mwamba basi akamuachia Mungu na kurudi kwao (Mikoa ilikua tofauti) baada ya miaka kupita, akaja akapata Mwanaume akamuoa hakumwambia kuhusu tukio lile yeye anasema alijaribu kulisahau hakuona sababu ya kulizungumzia tena, Mtoto alikuja kumtafuta Mama yake ameshakua mtu mzima na wajukuu akamletea, Mume ndio kujua hilo sakata lakini hakureact tofauti zaidi ya furaha familia imeungana tena.
 
Ok
 
Hata huyo ni walewale wa kuficha.
Mwani mtoto alifariki si alikuwa hai.
Hata huyo naye alifichwa tuu.
 
Okay.....
Ingekua wewe ndio mwanaume unafikiri ungefanyaje?
Huku kwetu tunamuita huyo ni mwanamke mpumbavu, na amevunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
Hapo chanzo ni uongo, na maumivu ni jinsi alivyo fichwa kwa miaka mingi namnahiyo.
Na hapo mwanaume bilashaka amejenga tayari chuki hadi kwa familia ya mwanamke ilio tunza uongo ule kwa uaminifu kabisa.
Ningemsikiliza sababu yake lazima iwe na mashiko na kuendelea na Maisha, nisingeivunja ndoa
 
Back
Top Bottom