WANAUME WENZANGU: Umewahi kufanya jambo ukaja kujuta baadae kama mimi ninavyojuta mpaka sasa?

mr Dude

Member
Jun 14, 2023
43
116
Habari wana Jf nipo na ID nyingine niliifungua karibu siku 26 zilizopita. Twende kwenye mada.

Mimi nina umri wa miaka 35 kwa sasa nina watoto 3. Nimeoa na nina mke nimezaanae watoto 2. Mtoto wangu wa kwanza nilizaa na dada mmoja chuoni. Mama yake sikumuoa nilioa mwanamke mwingine ila mtoto ninaishi nae mimi. Kitu hiki ndo kinanifanya kuwa na majuto kitendo nilichomfanyia mama yake. Daa kinaniumiza sana sometime nawaza bora ningemuoa mama yake.

Kipindi nipo chuo mwaka wa 3 naingia. Mwaka wa kwanza ndo walikuwa wanafika chuoni. Sasa si unajua mambo ya chuo mabinti wapya kutoka form 6 ndo wanakuja. Vijana mambo ya chuo naamini mnaelewa. Sasa nikamuona binti mmoja, nikaanza kumvizia sana, nakumbuka kipindi kile na rafiki zangu tulikuwa tunagawana mabinti, mimi huyu wewe yule.

Nilizoeana nae na kuanza kumfuata ili kuanzisha mahusiano nae. Nilijitahidi kuvizia na kupeana mbinu wa friends. Wenzangu walifanikiwa baadhi hadi kuwa nao first year. Ila mimi bado ananiangaisha.

Yeye alisema issue ya mahusiano hapana labda kuwa friends kawaida tuu. Mimi nikaona poa ila bado namvizia yule dada. Japo alikuwa mgumu sana.

Siku moja chuoni night watu walikuwa wanafanya discussion. Sasa nilikuwa na yule binti night siku ile tulipiga story kadhaa. Nilipanga kusex nae anytime nitakapo pata chance.

Siku ile nilipanga leo ni leo nitafanikiwa. Nakumbuka niseme kwa kifupi tuu nilimlaghai sana kwa kumshika shika akawa anasema tuu acha. Baadae akatoka akaamua kuondoka kurudi hostel, mimi nilikuwa sikai mbali na chuoni ghetto langu ni maeneo hayo ya chuoni tuu.

Nilimshikashika mpk akasema usinishawishi kuzini mimi siitaji.

Niliendelea tu.

MWISHOWE alilainika na akajikuta anakubali , nilienda nae ghetto tukasex na alilala mpk morning.

Asubui anashituka daa nikamkuta analia sana na kunilaumu, aliondoka na kwenda hostel .

Hatukuwa karibu kama 2 weeks hivi. Baada ya wiki 3 na siku kadhaa akaniambia siku zake haziona. Mimi eeeeeee. Nilishituka sana. Kumbe siku ile alikuwa siku zake za hatari . Nikili tuu nilitake risk sikutumia condom.

Niliisi kama kuchanganyikiwa hivi nikaona au ananimbambikizia nini. Niliwaeleza wadau wakasema Katoe , mimi daaa kitu hicho sijawahi hata kufanya , nikimuangalia binti yeye namuona she is not okay muda wote mpk wenzie wanamuliza shida nini.

Nikaa kimya tuu siku zinaenda naona tumbo hilo. Baada ya miezi kama 3 hivi ujauzito ukaanza kumsumbua sana. Mpk akaanza kunilaumu mimi. Akalazimika kwenda kwao. Kwao walimzingua sana tena sana.

Alikuwa ananipigia simu huku akinilaumu kwa siku ile.

Akalazimika kusitisha chuo. Baada ya kujifungua mimi nilikuwa nishamaliza chuo.
Mbaya zaidi akajifungua kwa operation mda wa kukaa home ndo ukazidi.

Akarudi chuo wenzie wako mwaka wa 3 yeye anaendelea na semester ya 2 mwaka wa kwanza. Mshono wa operation ulimsumbu sana.

Mimi nilisena tuu home wakanitupia maneno sana kwani wazazi wangu ni watu wa dini sana. Tukio lile lilinifanya niache kuzini kabisa.

Ila baadae nilikutana na binti mwingine. Na kumuoa .
Japo mama alinisisitiza sana muoe mama mtoto wako. Kwa sababu pale umemuaribu mtoto wa watu. Mimi wala sikujali.

Ila mzazi mwezangu yule. Tangu kamaliza chuo akipata mwanaume, akijua anamtoto jamaa anamuacha. Kila anayepata anamuacha. Baadae nikaona ngoja nimchukue mtoto nikae nae. Ili na yeye apate mtu amuoe . Ila wapi.

Mwaka juzi alipata mmoja alikubali ila alivyokuja kugundua alijifungua kwa operation akamuacha. Mara nyingine anakuwa ananilalamikia sana nimemualibia system mzima ya life yake.

Kwa sasa anaumri wa miaka 32. Rafiki zake wote tayari wameolewa ila yeye bado , mara nyingi anakuwa ni mtu wa huzuni sana , she is not happy always.

Hiki kitu mara nyingi kinaniumiza sana , maana naona kama nimemuaribia maisha binti wa watu.

Na mimi hapa home nina mtoto wa kike nafikilia na yeye akikutwa na tukio kama lile itakuwaje huwa nafikilia sana na kumuangali binti yangu huyu hapa home.

Daaa we acha .

KAMA NIMEKOSEMA UANDISHI NAOMBA RADHI.🤲🙏🙏🙏
 
Mimi nimechoma zaidi ya milion 300 kwa muda wa miaka 15,Mzee alikua kila siku ananiambia achana na biashara achana na maproject hayo ni rahisi kwa makaratasi na Sio hali halisi.

We Jenga apartment za kupangisha zitakusaidia mbeleni kipindi Hicho pesa zinatiririka tu,basi naelewa ni dream ya kufanya makubwa anzisha project hii nachezea za uso hasara hii mwanzo vizur mwisho hasara.

Ni Bora uchome pesa kwenye starehe utoumia kuliko kwenye project then ikazama utaumia maisha yako yote kila ukipigika unazikumbuka pesa zako.
Kwa starehe hata ukipigika utajipooza na kujifariji "enzi zangu bwana" hii in relief pain ya kupoteza pesa kwa project utaishia kuwa na experience tu,itakusaidia kwa second chance ya kupata Kama ikitokea.
 
Kipimo ulichompimia mwenzeko ndo hicho hicho utakachopimiwa.
Wazazi wako walikua sahihi kabisa kukwambia umuoe ona Sasa umemuaribia bint wa watu life kwa Dunia ya Leo Miaka 32 nani amuoe.

Ushauri wangu kwako kama upo vizuri Muombe msamaha then Muombe Mungu wako msamaha ufunge kabisa hizo Roho za malipiz kwa wanao wasije fanywa kama wewe ulivyo fanya, na jinsi unavyo fikiria ndugu ndo hivyo hivyo mambo hutokea wakati mwingine sis Binadamu huwa tunawaza mambo yatakayo tokea mbelen na tunajua Alfu tunapuuzia, so nakushauri Mawazo unayo yawaza usiyapuuzie Muombe sana Mungu wako akusamehe hiyo dhambi na isiipate familia yako pia huyo Binti Muombe msamaha,

Kingine mshauri awe mkweli,, mm nafikiri kumficha mtoto siyo chanzo Cha kupta Mme wa Kumuoa yeye apambane akipata mwanaume asimdanganye Kuwa Hana mtot Bali amwambie ukweli maisha mengine yaendelee

Kila la kher
 
Aisee! Umeandika kwa hisia Sana.

GUILTY CONSCIOUSNESS inasumbua sana pole mkuu, Pole pia kwa mwenzako maana wote mnateseka

Kwenye maisha huwaga tuna mess up sana Lkn Kuna Mambo mengine Very delicate kidogo tu unakuta umeharibu pakubwa (Mapenzi, Familia na Ajira ) Ni ya kuzingatia mno.

Vijana wadogo mlioko humu mjifunze kutokana kisa hiki Of course Vipo vingi. Kila Mara mnapotaka kufanya maamuzi concerning this issue (take this as ur reference ) itakusaidia

Sijui alikua na kitu gan ukaona hafai kua mke ? Ukaenda kumuoa mwengine. Kama vipi muoe na huyo mhifadhi Binti wa watu 32yrs 🤦

Na Kama haiwezekani make it more worse mpe MIMBA NYINGINE. Huyo ni wako, Mpe maisha cause ana low chance ya kupata ndoa angalau wewe ndie wa kumponya jeraha.

Huko kwingine ataishia tu kuombwa "utelezi" of which inavyoonekan hakupaswa pitia hay maisha(umempitisha)

Kama ingekua Ni mimi basi afadhali hio ndoa yang ilege lege
 
Back
Top Bottom