Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Moronight walker

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
3,105
4,635
Habari wana JF.

Nina ndugu yangu mmoja upande wa mama, yeye KE.

Miaka kama 10 hivi iliyopita alikuwa na mahusiano na Jamaa mmoja hivi, walikaa muda tuu mpaka mahusiano yao yakazaa mtoto. Lakini baada ya kujifungua Jamaa alimkwepa sister.

Si unajua wanaume kwa kukimbia watoto wapo. Jamaa akawa hata huduma hatoi wala nini, ila mtoto anamtaka kumuona, kuna wakati alikuwa anajitokeza hata baada ya 3 month mara 1 tuu kumuona mtoto hatoi chochote. Baadae katokomea kabisa.

Sasa sister angu huyu akakutana na jamaa mwingine kipindi mtoto wake alikuwa na umri wa miaka 3 kwenda minne.

Jamaa hakuwa tayari kuwa nae si unajua single mother wanaume hatupendi sana, ila sister alijaribu kumshawishi mpaka kukubali. Na alimueleza kila kitu kuhusu Baba mtoto.

Jamaa akasema kwa vile Baba mtoto kasepa kapotea basi tutakuwa fresh, ila alitoa sharti hataki kuona Baba mtoto anajitokeza au mama anajipendekeza.

Wakafanikiwa kufunga ndoa.
Na kuchukua mtoto wakawa wanakaa nae dogo alipofikisha miaka 6 akampeleka shule nzuri ya 2 million per year akawa anasoma huko.

Sasa Baba mtoto aliposikia bibie kaolewa si akarudi bwana kuanza kutaka mtoto. Sister akagoma kabisa tena bila kumwambia mume wake. Na alirudi kipindi sister ana watoto wadogo mapacha aliyezaa na mume wake.

Waliangaishana kama mwaka 1 hivi. Sister alikataa kabisa kumpa dogo.

Sasa kipindi mtoto kafikisha miaka 8. Jamaa si akaenda ustawi wa jamii kwa lengo la kuchukua mtoto, sister kweli aliitwa ustawi wa jamaii na alienda tena bila kumwambia mume wake. Yeye alieleza kwao na kwao waligoma na kumwambia asiende. Ila ustawi wa jamii walilazimisha na kumwambia Mtoto ana haki ya kumjua Baba yake halisi. Hio ni haki ya mtoto.

Sasa mume wake baada ya kujua hilo akachachamaa kabisa ukawa ni ugomvi sana kati ya yeye na mke wake.

Mume wake akaamini kuwa Sister alimficha au niseme alimdanganya jamaa kakimbia kumbe laa. Waligombana sana.

Sasa jamaa akafanikiwa mpaka kubadilisha jina mtoto la mwisho maana sister aliandika jina la kwao la mwisho la mtoto.

Jamaa akaweka jina la kwao. Na jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa. Maana sehemu ya Baba ilikuwa empty nafikiri.

Mume wake baada ya kuona hivyo akamwambia kuwa kuhusu kitu chochote cha mtoto wake asimwambie mpk ada. Na mtoto aende kwa Baba yake pale home kwake amtaki tena.

Sister akaona kwa vile anataka kuokoa ndoa yake ampeleke mtoto kwa Baba yake. Sasa ishu kule kwa jamaa , dogo alikuwa anasoma shule ya over 2 million per year. Jamaa wa kawaida tuu.

Kwa kifupi dogo baada ya kwenda kwa Baba mawasiliano yakazidi kupelekea mpk mume wake kuanza kugombana. Sister akasema yule mwenzie anamsumbua sana na anamfanya mtoto kama kung'ang'ania kumuona mama yake, muda wote. So anajikuta muda mwingi anakuwa anawasiliana upande mwingine.

Baada ya kuona drama ni nyingi mume alimtimua sister home kwake. Na walisumbuana kama 2 years kutaka kuachana.

Mume wake ni mtu mwenye wivu. Walitaka kusuluhisha kwa kumuita jamaa yule msumbufu ila jamaa aligoma kuja na wala mume wake alikataa kusikiliza suluhisho. Wiki mbili zilizopita waliachana baada ya purukushani kwa miaka 2.

Alikuwa single mother na kuingia kwenye ndoa na mwishowe karudi tena single mother. Dogo anasoma shule za kawaida tuu hizi japo ni private pia kule kashatoka shule ya bei kubwa.

Hivi ishu kama hii mnaisolve kivipi jamani, IKIJA KWENYE FAMILIA, KARIBUNI.
 
Mara nyingine wanaume wanaokimbia watoto wanarudi kudai watoto kwa Sababu vifuatazo.

1. Huyo mtu kaingia kwenye Ndoa afu kashindwa kupata mtoto.

Sasa akikumbuka ameacha mtoto sehemu flani basi anarudi.

2. Huko kwenye ndoa yake kashidwa kupata mtoto wa kike pale akiona ana watoto wa kiume tupu au ana watoto wa kike tupu afu kaacha mtoto wa kiume sehemu huyo lazima atarudi tu.

3. Kaona Baby mama kaolewa sasa wivu umemkumba anarudi kwa sababu ya wivu tu.

4. Baby mama amefanikiwa na analea mtoto vizuri au kaolewa na mtoto analelewa vizuri na kusoma shule mzuri na kama akionekana anaakili sasa jamaa anaona mtoto anaweza kuwa na future mzuri baadae hicho kinamrudisha.

5. Mtoto kafanana na yeye kabisa kuliko mwanzo.

Huwa wanarudi kwa Sababu.
 
Aaa mimi kuna rafiki yake Dada mmoja alikuwa na jamaa mmoja hivi baadae si akabeba ujauzito jamaa akakimbia.
Alipojifungua akajifungua watoto mapacha 2 tena wakike tupu.

Yule Dada aliangaika nae ustawi wa jamii kudai child support, jamaa alikuwa kaajiriwa Serikalini.
Mwishowe jamaa alihonga maafisa ustawi wa jamii. Na kukana watoto si wake kule kule ustawi wa jamii.

Watu wakamwambia wa ustawi wa jamii kuwa jamaa kahonga pesa hutashida.
Yule dada anaondoka zake. Mama yake alifariki siku nyingi tuu.
Baba yake akamwambia kuwa utakaa hapa hapa home kwa sasa nagalia jinsi ya kuwalea watoto wako.

Yule dada alipata shida mpaka akawa yupo stable kipesa. Kwa sasa watoto wana umri wa miaka 6 anawasomesha shule mzuri tuu ya over 1 miilion per year. Anaishi Kigamboni.

Alimtembelea sister angu siku moja alimpelekea zawadi kibao.

Jamaa nasikia kuna kipindi alikuwa anamtafuta wayamalize, alikuwa anaomba msamaha kwa baby mama. Ila kagoma kabisa na alimblock.

Nafikili jamaa huyu itakuwa ngumu kwenda tena ustawi wa jamii, maana alikana kule kule watoto. Sasa naona itakuwa ngumu kwake.

Nafikiri anaumia sana moyoni jamaa.
 
Habari wana JF.

Nina ndugu yangu mmoja upande wa mama, yeye KE.

Miaka kama 10 hivi iliyopita alikuwa ba mahusiano na Jamaa mmoja hivi, walikaa mda tuu mpaka mahusiano yao yakazaa mtoto. Lkn baada ya kujifungua Jamaa alimkwepa sister...
Akishazalishwa halafu wewe ukaoa,
issue kama ya sister wako haikwepeki.

Kwa wengine hupelekea mauaji kabisa kunusuru ndoa ambayo mtu alishakata tamaa ya kuolewa.
Huyo jamaa msumbufu mwenye mtoto alikutana na single mother mpole na soft,
kwingine angepotezwa kabisa
 
Kiufupi single moms kazi tunayo.......
I’m a single mama…kitu alichokwama mwenzetu ni kuruhusu mawasiliano ya yeye na mzazi mwenzie moja kwa moja.

kuna wakati hata sisi single moms tunazingua big time😌😌.kulingana na huu uzi..single mom ndie aliyeanza kumkaribisha shetani.unatolea wapi ujasiri wa kwenda ustawi wa jamii bila kwenda na mumeo?huo ni upumbavu mzito na hakuna mwanaume yeyote mwenye kupenda Amani ya moyo angevumilia💔💔

Hivi unakuwaje na mume kabisa ambae amekukubali wewe na mtoto wako wote kuwalea halafu eti from nowhere ***** unakuja kuwasiliana na mzazi mwenzio just namna hiyo😳
 
I’m a single mama…kitu alichokwama mwenzetu ni kuruhusu mawasiliano ya yeye na mzazi mwenzie moja kwa moja.

kuna wakati hata sisi single moms tunazingua big time😌😌.kulingana na huu uzi..single mom ndie aliyeanza kumkaribisha shetani.unatolea wapi ujasiri wa kwenda ustawi wa jamii bila kwenda na mumeo?huo ni upumbavu mzito na hakuna mwanaume yeyote mwenye kupenda Amani ya moyo angevumilia💔💔

Hivi unakuwaje na mume kabisa ambae amekukubali wewe na mtoto wako wote kuwalea halafu eti from nowhere ***** unakuja kuwasiliana na mzazi mwenzio just namna hiyo😳
Mi ndiyO Sitaki MazoEa KabIsa
 
Kosa la kwanza alilofanya dada yako ni kutomshirikisha mume wake kuanzia mwanzo Hilo ni kosa kubwa Sana alilofanya angemshirikisha tangu awali jamaa angejua apambane vipi kiume na Kama jamaa yupo vzr kiuchumi angempeleka hata nje ya TZ mtoto akaishi

Anyway pole yake
Hapo sasa kama alikubali kumuoa akabeba na majukumu ya kulea mtoto. Nimfiche kipi. Kwa kweli kabisa,,binafsi ikitokea mwanaume anamkataa mtoto nalea napambana mwenyewe nije nipate mtu wa kunipa heshima na usingle maza wangu. Hakuna cha sheria ya mtoto,,,wala afisa Ustawi atayetoa hukumu kumchukua mtoto mikononi mwangu.

Binafsi kwenye majukumu yangu tunashirikiana na ustawi kwenye majukumu ya watoto kwa mashauri hayo ya malezi wanaume wanapewa ulezi wa watoto ni wanawake wenyewe ndo wanaamua kwa mapenzi yao. Na hata hao huwa wanashauriwa ni mara mia mtoto alelewe na mama kuliko kwenda kwenye mikono ya mama..

Tena kwa mwanaume ambaye alimtelekeza looooh.
 
Back
Top Bottom