Ataka kumuua mtoto baada ya kujifungua ili kunusuru Ndoa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Msichana mwenye umri wa miaka 19 alietambulika kwa jina la Rehema Erick Mkazi wa Mtapenda Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi ameingia matatani kwa kujaribu kumuua mtoto wake kwa kumtupa chooni baada ya kujifungua ili kulinda ndoa yake isivunjike.

20240120_190634.jpg


---
Msichana mwenye umri wa miaka 19 alietambulika kwa jina la Rehema Erick Mkazi wa Mtapenda Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi ameingia matatani kwa kujaribu kumuua mtoto wake kwa kumtupa chooni baada ya kujifungua ili kulinda ndoa yake isivunjike.

Akizungumzia tukio hilo mama wa binti huyo Winfrida Amosi amesema alipigiwa simu na mume wa binti yake kuwa mwanae anaumwa tumbo hivyo wameenda hospitali ya wilaya kwaajili ya matibabu pasipo kujua kuwa aliolewa akiwa na mimba ya mwanaume mwingine akiwa huko ndipo alipatwa na uchungu kisha kwenda chooni kujifungua na kufanya ukatili huo.

Ester Julius ni shuhuda wa kwanza katika tukio hilo amesema alikua akifanya usafi ndipo aliona damu chooni baadae akaona mtoto ambae alikua amefichwa nyuma ya sinki la kunawia nakutoa taarifa kwa wahudumu wa afya katika hospitali hiyo.

Kaimu Mganga Mkuu Hospital ya Wilaya Nsimbo Grory Sollo amesema mtoto huyo anaendelea na matibabu kutokana na majeraha aliopata ikiwa ni pamoja na kuvunjika miguu huku Afisa Ustawi Halmashauri ya Nsimbo Theresia Mwendapole akidai ni tukio la kwanza kutokea ndani ya mwaka huu.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph ameagiza kukamatwa kwa binti huyo kutokana na kufanya jaribio la kutaka kuua.

Source: NIPASHE
 
Huyu itakua hakupata uchungu wa kujifungua Wala maumivu yoyote wakati wa kujifungua, yawezekana alijifungua Kwa starehe kama vile anakata gogo, ndo maana alimtupa mtoto vinginevyo achunguzwe akili uskute dishi limeyumba
 
Back
Top Bottom