johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
makala.jpg

Amos Makalla karibu sana katika mkoa wetu wa Dar es Salaam na ikikupendeza tusaidie pale Magufuli Bus Terminal ujenzi ukamilike kwa eneo la abiria kadhalika sehemu ya kuservice mabasi.

Mengine tutakujulisha ukishafika.

Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu.
 
Mwendazake alimpa ukuu wa Mkoa halafu kamnyanuasa kwa vipi
Mwendazake alitaka Makalla amsulubishe Sugu na chadema yake pale Mbeya, lkn Makalla akacheza fairly.

Mwendazake akafura kama kifutu akamhamishia Makalla mkoani Katavi. Lkn kumbe alikuwa bado anamtafutia visa tu.

Wakati wa zoezi la uuzaji wa vitambulisho vya wamachinga, Amos aliuza vitambulisho 6,000 tu. Maana mkoa wa Katavi wamachinga hawazidi buku 5.

Mwendazake akamtupilia mbali Makalla. Makalla akajaribu kugombea ubunge 2020, kashinda kura za maoni lkn bado mwendazake akalikata jina la Makalla.

Mwendazake hakuwa mtu.
 
Mwendazake alitaka Makalla amsulubishe Sugu na chadema yake pale Mbeya, lkn Makalla akacheza fairly.

Mwendazake akafura kama kifutu akamhamishia Makalla mkoani Katavi. Lkn kumbe alikuwa bado anamtafutia visa tu.

Wakati wa zoezi la uuzaji wa vitambulisho vya wamachinga, Amos aliuza vitambulisho 6,000 tu. Maana mkoa wa Katavi wamachinga hawazidi buku 5.

Mwendazake akamtupilia mbali Makalla. Makalla akajaribu kugombea ubunge, kashinda kura za maoni lkn bado mwendazake akalikata jina la Makalla.

Mwendazake hakuwa mtu.
Ok nilikuwa sijui historia yake.... basi mama kafanya vema sana
 
Mwendazake alimpa ukuu wa Mkoa halafu kamnyanuasa kwa vipi
Kipindi Cha biashara ya Madiwani Mkoa wa Mbeya ni Kati ya Mikoa iliyopitiwa na ununuzi wa Madiwani..

Hivyo wakati wa chaguzi ndogo za Marudio Chadema walishinda kata moja kule Kyela Kati ya kata nyingi zilizofanya Uchaguzi wakati huo.... Mkuu wa Mkoa akiwa Amos Makalla.

Hillo swala Mwendazake lilimkera Sana, ikabidi Amos Makalla amwombe radhi Mwendazake kwa kufanya uzembe na kuruhusu upinzani kushinda...

Mwendazake alihoji kwa nini wapinzani washinde wakati vyombo vyote vya kukwapulia na kufungia wapinzani vipo chini yake?

Kumbuka wakati wa Mwendazake wapinzani walikuwa wanakutwa na makosa ya kujaza fomu, kukosea majina yao, kukosea viapo na mengineyo...hivyo kupelekea wagombea wa Chama tawala kupitia bila kupingwa..

Mwendazake Mungu amsamehe huko aliko, maana sijawahi kuona kiongozi mwenye visasi kama yule jamaa.
 
Back
Top Bottom