Ushauri kuhusu uchaguzi wa godoro bora

Bro,kama unataka Godoro zuri kabisa chukua Tanfoam Arusha,wasiliana nao wakupe namba za wakala wao katika mkoa husika ili upate Original. Option inayofuata ambayo najua ni nzuri ni QFL godoro Dodoma. Tanfoam ni mazuri sana na bei yake imechangamka sana. Vita supreme sifahamu kabisa lipoje. Lakini nikupe personal experience,mimi nilienda kununua godoro nikiwa sina elimu ya magodoro,option yangu ilikua QFL la Dodoma,yule muuzaji hakuwa nalo hilo kwahiyo akaanza kunishawishi nichukue ARUSHA DELUXE. Hii heka heka unaniona nayo leo natafuta godoro la Tanfoam ni sababu ya makosa niliyofanya kipindi hiko,miaka mitatu nyuma kununua godoro la hovyo.
Ahsante kwa huu uzoefu wako
 
Nimenunua Tanfoam PREMIUM MATTRESS,watu wa Tanfoam wenyewe wamenishauri nichukue hili,wanasema hata hotels kubwa nyingi ndio chaguo lao.Actually ndio nimepanda kitandani kulilalia kwa mara ya kwanza. Karibu
FINE ME TANFOAM IS MY FAVOURITE
 
Kuna godoro ni gumu utasema kitandani umepanga tofali ni kampuni gani hile
Miaka ya nyuma nililinunua la Super Banco baada ya kushsuriwa na fundi, tena nililifuata mwenyewe kiwandani! Mbona nilikoma😀

Mwanzoni lilikuwa gumu, ukililalia utafikiri umelala juu ya "sakafu", na baada ya muda likawa linabonyea lakini "halinesi"

Lilikuwa godoro la "hovyo" kuwahi kulimiliki.
 
Waafrika iwanafikiria kulala tu, badala ya kupeana deal za pesa wao wanapeana deal za kupiga usingizi
Wakati wa kazi iwe kazi kweli kweli, na wakati.wa kulala, ulale usingizi bora

Usingizi bora ni muhimu kwa afya ya akili na mwili.

Afya bora huchangia ufanisi mzuri kwenye kazi.

Na ili update usingizi bora, unahitaji kitanda kizuri. Na godoro zuri ni sehemu ya kitanda kizuri.

Godoro la Tanfoam ndilo godoro bora linalotengenezwa Tanzania.
 
Nimenunua Tanfoam PREMIUM MATTRESS,watu wa Tanfoam wenyewe wamenishauri nichukue hili,wanasema hata hotels kubwa nyingi ndio chaguo lao.Actually ndio nimepanda kitandani kulilalia kwa mara ya kwanza. Karibu
Umelionaje?
 
Wakuu,

Anayeweza nisaidia kupata godoro la TanFoam (Orthopaedic) la spring 5 x 6 au kuniconnect na muuzaji.

Mahali : Nzega - Tabora.

Nicheck WhatsApp : 0612332310.

Sababu ya kuja hapa : nimetafuta bila mafanikio Nzega na maduka ya karibu Tabora. Pia nimevutiwa na discussion ya huu uzi, nategemea kupata msaada
 
Sidhan kama usiku mmoja ni experience ya kutosha kutoa mrejesho lakini Godoro halipo kama nilivyofikiria. Nilivyoambiwa ni luxurious na linatumika kwenye hotels kubwa nikapata picha ya mneso fulani wa kipekee sana. Lakini halipo hivyo,lina ugumu wa kutosha kiasi kwamba sihisi mneso wowote. Mgongo wangu bado unauma sababu ya heka heka za kubonyea kwa godoro la awali lakini hili linakunyoosha vizuri mwili wako. Nina miaka mingi sana sijapaga usingizi wa moja kwa moja kama leo,kwa mara ya kwanza nimeamka saa mbili asubuhi. Hivi ndio nachemsha maji ya moto niende kazini, nimechelewa.
Habari ya siku mkuu, ukirejea utakumbuka ulisema usiku mmoja hautoshi kutoa mrejesho. Nadhani sasa una confidence kidogo ya kutoa mresho. Tunaomba ili na sisi tufanye maamuzi sahihi
 
Back
Top Bottom