Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere halmashauri ya mji wa Bunda jifunze kutoka kwa mtendaji wa mtaa wa Nyerere anavyozingatia utawala bora

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
200
433
Ni ushauri tu kwa ndugu yetu Ndugu Hamis Nyamsenda,Mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere ulio katika halmashauri ya mji wa Bunda.Binafsi andiko hili halina maana kwamba tunakuchukia bali tumeamua kufanya haya ili ubadilike na kuwa kiongozi bora.

Binafsi umekuwa ukiitisha mikutano ya hadhara ambapo umekuwa hutaki kukosolewa na wananchi ambao ndio wapiga kura wako.Mara nyingi wanaoonyesha kupingana na mawazo Yako mkutanoni umekuwa ukiwatishia kuwapeleka polisi kwa kigezo cha kwamba wanakuvurugia mkutano!Kumbuka enzi za zidumu fikra za mwenyekiti ziliishia kipindi cha Nyerere!Wapiga kura wana haki kikatiba kukupongeza unapofanya mazuri na pia kukukosoa unapokosea!Kwako anayekukosoa ni adui,ila anayekupongeza kinafiki kwako ni rafiki.Hapa unafeli.

Pili hudumia wananchi bila kubagua itikadi zao,mfano kwa sasa Kuna watu wanafika ofisini kuhudumiwa unapoona ni wapinzani wako ndani ya chama katika kupitishwa kwenye kura za maoni kwa ajili ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unawasumbua sana. Hii siyo fair!Pia wanavyama vyenye mlengo tofauti na wako pia unawanyanyasa sana ndugu yetu.Badilika!

Tatu kuhusu suala la kumgongea mwananchi muhuri kwenye nyaraka zake halihitaji malipo! Ikitokea akakupa chochote basi shukuru ila siyo kwamba atangulize chochote ndipo agongewe muhuri.Hapa nafikiri umenielewa!

Nne nakukumbusha ulipita kipindi cha Marehemu John Pombe Magufuli,sasa hivi ni kipindi cha Dr.Samia Hassan ambapo mshindi wa uchaguzi ujao itabidi ajipambanue kutokana na namna anavyotatua na kupambana na kero za wananchi.Hili unalijua?

Hitimisho:
Unamuona Mtendaji wa mtaa wa Nyerere anavyokubalika kwa wananchi bila kujali itikadi zao?Ni dada mdogo sana kiumri tu ila anazingatia misingi ya utawala Bora!Hata leo akipandishwa ngazi za kiutawala hakuna atakayeguna isipokuwa ni kupewa pongezi tu.Hebu jaribu basi kuwa unamshirikisha hasa kwa mambo yanayohitaji tafsiri za kikatiba katika kuyatekeleza badala ya kuwa unatumia utashi binafsi.
Pia itisha kikao cha usuluhishi na wananchi(reconciliation)ambapo ruhusu mawazo huru,kaa na wale unaohisi ni wapingaji wako kisiasa ambao ni wengi kuliko wanaokukubali.If you can't beat them join them!

Ni hayo tu ndugu badilika Wanaccm tunahitaji ushindi wa kishindo!


Pichani ni mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere Hamis Nyamsenda.
 

Attachments

  • FB_IMG_1709578719859.jpg
    FB_IMG_1709578719859.jpg
    56.1 KB · Views: 1
Mwenyekiti wa mtaa tu unamfungulia Uzi jf, DC si utahama nchi,!!!


Huyo chair mvizie kichochoroni umkate makofi.
 
Back
Top Bottom