Mimi hapa naingia 2nd year na nilianzia direct ghetto. Fanya yafuatayo:
Tafuta chumba mapema usitafute siku za baada ya usajiri, bora upate hata sasa kuliko kupata chumba kipo mbali baadae. Pata chumba karibu sio uanze kupanda daladala kufika chuo, hizo 300 ni nyingi sana njoo kuna siku utakuwa unaamka na 100 tu. 1st wenzio wanakuja, 2nd na 3rd year wanatafuta kuhamia kutoka hostel ukichelewa ndo unapandishiwa bei, chumba kibaya, kiko mbali.
Uwe na bajeti ya kununua vitu muhimu. Kitanda, godoro na mashuka, feni, pazia, ndoo, kapeti etc. Unaweza nunua vitu used kwa mawakala walio chuoni. Mimi sikununua used kama hela ya kipya sina naacha. Utanunua vitu kulingana na mfuko wako na mahitaji yako.
Pata chumba cha uhakika, chenye hadhi ya kuishi kwani vingine unakuta choo kipo Kivietnam, mwenye nyumba yuko humo, kuna wadangaji. Kwetu sisi tupo wanachuo tu, hakuna taarab, ugomvi wala mtoto kujiliza usiku.
Kuhusu kujitegemea. Nilikuwa na laki kadhaa nikasema ngoja nizoee mazingira nitafanyia kazi, hela zote nikamaliza. Nikaanza issue flani corona ikaingia nikakwama. Sahivi naenda kuanza kitu kingine nikifeli sawa.
Expectations zinakuwa nyingi sana hasa wakikwambia uza hiki na kile unajiona unatoboa as if hela imechuchumaa inasubiri uiokote. Wanaofanya ujasiriamali pekee wanalia, sembuse anayeongeza na kusoma .
Wapo walevi, wahuni, wala bata, wanaokesha church na kila mkesha au mfungo, wanaosoma sana, wapenda mademu, wapenda michezo yeye kila siku ni mazoezi uwanjani, wavuta bangi, wajasiriamali, bila kusahau wanasiasa (wengi wao wababaishaji) hasa UVCCM ambao hujifanya wameyapatia maisha. Kaa upande wako.
Nimejitahidi kufupisha sana hapa. Huwa naandika gazeti