Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
same to me bro...I go for ZZK mpaka hawa shwaini wasepe. ZZK kapigania mambo mengi yenye mantiki kwa taifa sio hawa kina Lema,ben na mbowe eti wanatambia kulala sero, sasa kulala kwao sero kumesaidia nini ama kuleta nini katika taifa. Pumbaf, GO GO ZZK wenye akili zao tupo nyuma yako braza
Hivi inaingia akilini kwamba kama kuchagua kati ya Zitto na Lema then mtu umchague Lema kweli??? Kwa uanaharakati au kipi hasa??
 
Au Masalia, walifanya kwa akina Mtela Mwampamba na Juliana Shonza , lakini kama unavyojua dhambi ya ubaguzi haikomi kirahisi, basi wakanogewa, sasa wanadanganyana kuwa wanaweza kumfukuza Zitto na SACCOS ikabaki shwari bila kuyumba.

Mkuu hao uliowataja ni waathirika wa huyu Mnafiki au Msaliti tunayemjadili. Huyu huyu Mnafiki na Msaliti alisababisha madiwani wetu wakafukuzwa, akatusababishia gharama zingine za uchaguzi
 
Last edited by a moderator:
Wallahi, sasa Chadema wanakaribia kugawana mbao za jahazi.
Waliambiwa CDM kufika 2015 , chama kitakuwa marehemu.
Ama kweli Wassira ana uchuro!!!
 
Na huu ndio uungwana mkuu wangu, tunaweza kumchukia Zitto kwa tabia zake lakini kamwe si misingi anayoisimamia kwan ndio misingi ile ile ya
kuasisiwa kwa CDM

Kuichukia misingi anayoisimamia yeye ni kuichukia misingi ya CDM. Zitto ni mmoja kati ya wale wachache wanaojitahidi kuiishi misingi ya CDM

Nimeipenda hii! Good observation
 
kijana wewe ni ccm imekuwaje macho yamekutoka kiasi hiki kumtetea mtu wa chadema..je unajua zitto aliwahi kuhojiwa na JF.. rudi tena hapo kwenye thread lema amesema amzungumzia Zitto na posho na hii itakuwa kabla ya saa nane..

Kwahiyo hilo taifa LEMA analolamikia kuwa linaangamia ni la CHADEMA tu? Acha kukurupuka! huyo kanjanja mwambieTunasubiri hizo pumba zake, maana hajawahi kuongea kitu cha maana, LEMA ni muongo, kitu anachosema cha ukweli ni jina lake tu!
 
Zitto ana matatizo yake ambayo pia yanaweza kukigharimu chama asipoyarekebisha, lakini ni ukweli usiopingika kuwa wafuasi na wanachama wengi vijana wa CDM sasa hivi zaidi ya 45% ni matunda ya kazi ya Zitto. Hata hawa wachawi wanaotafuta namna ya kumwengua kwenye chama wanalifahamu hilo. Ndiyo maana siku zote wamekuwa wanalia kuwa Zitto anakihujumu chama lakini wanashindwa kumchukulia hatua.

Mrema amewahi kuwa maarufu sana NCCR kipindi cha nyuma kiasi cha kutishia uhai wa waliomkaribisha kwenye chama. Yuko wapi leo hii? Simtofautishi Mrema wa miaka ile na Lema wa leo. CDM ikishindwa kum-handle Lema inaelekea shimoni. Nafahamu pasipo shaka yoyote kuwa anayofanya Lema sasa hivi yana baraka za Mbowe, they just got to know that Zitto is smart and you don't deploy a hooligan like Lema to deal with such a brilliant young man. Watch out .

lini atajirekebisha na aache kukigawa chama..
 
Chadema wanatakiwa wajadili na kukubaliana maana pana ya "USALITI WA CHAMA" lasivyo wanachama watakua hawana uwezo wa kuhoji baadhi ya mambo na pia ugomvi wa watu binafsi unaweza kuingizwa kwenye hii kadhia ya Usaliti wa Chama
 
Nimefuatilia mjadala sana leo ukizingatia ilikuwa ni Jumamosi kwamba hatukuwa na kazi nyingi sana za Kibunge hasa baada ya kuanzisha mjadala unaosema " Usaliti na Unafiki unavyoliangamiza Taifa " na nimeona mjadala na nimejifunza mambo mengi sana sikumtaja Mtu ila Watu wengi wametaja majina ya Watu , sijui kwanini ? ila naendelea kutafakari , kesho nitaandika kuhusu mada inasema " UNAFIKI WA ZITTO KUHUSU POSHO " na mpaka saa nane mchana nitakuwa nimewasilisha na jambo hili halina mgogoro na kanuni za Chama kwani ni jambo liko wazi kwenye vyombo vya habari .

Asanteni

Haya mkuu tunasubiri kufamu kile unacho kusudia pia hongera kwa kuwa muwazi na nakusema yale uliyo yalenga bila woga wala kuhofia mpasuko ndani ya chama ikiwa ni kwania Njema.
 
Hivi inaingia akilini kwamba kama kuchagua kati ya Zitto na Lema then mtu umchague Lema kweli??? Kwa uanaharakati au kipi hasa??

Kheri ya Lema kuliko zitto sababu ya undumilakuwili,rejea suala la ugaidi juu ya lwekatale alisema nn? zitto hafai kwa usura 2 wake
 
Mkuu hao uliowataja ni waathirika wa huyu Mnafiki au Msaliti tunayemjadili. Huyu huyu Mnafiki na Msaliti alisababisha madiwani wetu wakafukuzwa, akatusababishia gharama zingine za uchaguzi

Kumbukumbu zangu zinaonyesha madiwani walifukuzwa baada ya kukataa kuburuzwa na LEMA kwa hoja zake za kitoto za kumkataa MEYA aliyechaguliwa kihalali. mtu kama ESTOMIH MALLAH aliyewahi kuwa diwani wa Kimandolu, ni mtu mzima msomi, mwanasheria, leo hii uje umwambie awajibike kwa huyu LEMA, nani atakubali?
 
Nartdia tena lema leuel ya john komaa,mulugo na lusinde,vita anayoanzisha sisi tumeshnda tayari! Wamemshndwa babu zake sembuse yeye mhamiaji chamani? Aite ukoo wake wote kina kileo,ben,mungi,yericko a.k.a jb na misukule ya makao makuu! Tutawakimbza!
 
Au Masalia, walifanya kwa akina Mtela Mwampamba na Juliana Shonza , lakini kama unavyojua dhambi ya ubaguzi haikomi kirahisi, basi wakanogewa, sasa wanadanganyana kuwa wanaweza kumfukuza Zitto na SACCOS ikabaki shwari bila kuyumba.
Ni kweli mkuu hii SACOS ya chadema haiwezi kubaki salama endapo watamgusa zito na hakuna mtu wa kumgusa zito ndani ya chadema vinginevyo nguo watazimaliza mikojo kwa kile kitakachowakuta.
 
Viongozi gani wameshambuliana au mkuu na wewe siku hizi umeachana na ujenzi wa hoja kwa facts na kuziamini zaidi hisia katika debate humu?

Mkuu Ben Saanane hivi unaona ni jambo la kiafya kichama kiongozi kama Lema kutoa kauli nzito kama hiyo tena kwenye mtandao. Kama ni hisia basi ameanza Lema na kutuambukiza sisi. Lema yeye ndiye anayehisi kwa sababu ameshindwa kumtaja mtu huku akiishia kusema kuwa waote tunamjua.

Naamini katika facts na vivyo hivyo viongozi wa CHADEMA nao waamini katika fact badala ya kuleta hoja JF. JF si ulingo wa CHADEMA, ulingo wa CHADEMA ni Kamati Kuu na Baraza Kuu. Huko mnaweza kuitana wasaliti na hata kupigana ila si hapa JF.
 
Last edited by a moderator:
Mwita maranya with all of my due respect,

Sijawahi hata siku moja kuingia kwenye vita vya maneno na wewe,iwe kwa namna yyte ile,

Sikiliza sasa nikufahamishe,


1.Mimi si MWALIMU KWA TAALUMA,na kamwe katu sitokuja na siwez kuidharau taaluma ya ualimu kwani kupitia taaluma hiyo nilijifunza kuondoa ujinga na kunipa msingi nilionao kwa sasa,


2.Mimi sio mchumia tumbo na kikaragosi kama hawa jamaa zako wanaokesha humu 24/7 kulamba buti za viongoz na kutumikia matumbo yao,hilo likae kichwani mwako na ulitambue,


3.Nina taaluma yangu,ninfanya biashara zangu binafsi naganga nazo njaa,na ninafanya kilimo changu MTWARA,kilimo safi kabisa cha korosho na mazao mengine na ufugaji,situmikii tumbo na wala situmwi na jamaa zenu kwa namna yyte ile,

SUALA LA GESI MTWARA HALIKUWA NI LA KISIASA,NA WATU WA KUSINI HATUJASHINDWA KATIKA KILE AMBACHO TULIKUWA TUNAKIPIGANIA,NA TUNAKIPGANIA KILE KWA MASLAHI YA TAIFA,WEWE KAMA UNADHANI HARAKATI HIZI NI ZA KIKANDA KAMA ZINAVOZUNGUKA AKILIN MWENU BASI YAWAPASA KUWAZA TENA,

KAMA CHAMA HAKIMUHITAJI ZITTO KABWE HAKUNA HAJA YA KUMEZA MEZA MANENO,MFUKEZ SASA RASMI TUJUE MOJA NA TUGANGE YAJAYO,KIPI MNAHOFIA??

Umeandika kwa ufasaha sana Big show.
Hata mimi ninakuheshimu sana kwa mtazamo na mawazo yako kadri ninavyokusoma hapa JF.

Tatizo kubwa na la msingi ninaloliona kwako kadri ninavyokusoma ni kukumbatia udini na kuuhusianisha na kila jambo linalotokea.
Hata unaposema kwamba mtaeneza sumu Kanda ya kusini na Kanda ya Kati ni katika Ku advocate udini kwa vile mmekuwa mkisema kwamba Dini yenu ndiyo inapopulation kubwa katika mikoa hiyo.

Ni Mara nyingi sana ninakusoma ukishabikia utengano wa kidini,nimekusoma sana kwenye makala za Mohamed Said,nimekusoma kwenye ule Uzi wa Yericko Nyerere,mimekusoma katika mijadala ya nani mwenye haki ya kuchinja kitoweo pamoja na mijadala Mingi ya kisiasa ambayo kwa bahati mbaya sana Kuna watu wanasiasa wakiguswa tu hata kama wamefanya makosa makinwa kiasi gani basi mmekuwa mkiwatetea kwasababu ya Dini Yao.

Kila mmoja Ana haki ya kuwa na maoni yake na msimamo wake lakini ni muhimu maoni hayo ama msimamo hip usiwe wa kupandikiza chuki na utengano baina yetu watanzania, aidha wa kidini, wa kikanda ama wa kikabila.
 
Mkuu Ben Saanane hivi unaona ni jambo la kiafya kichama kiongozi kama Lema kutoa kauli nzito kama hiyo tena kwenye mtandao. Kama ni hisia basi ameanza Lema na kutuambukiza sisi. Lema yeye ndiye anayehisi kwa sababu ameshindwa kumtaja mtu huku akiishia kusema kuwa waote tunamjua.

Naamini katika facts na vivyo hivyo viongozi wa CHADEMA nao waamini katika fact badala ya kuleta hoja JF. JF si ulingo wa CHADEMA, ulingo wa CHADEMA ni Kamati Kuu na Baraza Kuu. Huko mnaweza kuitana wasaliti na hata kupigana ila si hapa JF.

Ametoa mawazo yake JF.Umekereka na nini mkuu?Mbona Mwenyekiti na katibu mkuu kwa nyakati tofauti wameonya juu ya usaliti na kunukuliwa na media

Aliyesema kuna kirusi ndani ya CHADEMA mbona hukukemea na kukereka kihivi mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Machozi na damu za mayatima na wajane waliopoteza waoendwa wao kwenye harakati hizi za ukombozo daima zitamlilia mshirikina ZITTO ZUBERI KABWE na wasaliti wengine ndani ya CDM
 
Kilewo eti naye anasema anakuja kutoa siri za zitto jins alvyofanyiwa gerezani sijui alikua wapi au alikua anasubir adandie kwa lema.
Lazima ukanda na uchaga ukomeshwe chadema.

Ni kweli Lazima watanzania tusimame tuseme basi kwa haya wanayofanyiwa ndugu zetu huko CHADEMA.
 
lini atajirekebisha na aache kukigawa chama..

Kuwa na mawazo tofauti katika uongozi sio kugawa chama, inaitwa independent thinking.

Kusema kiongozi fulani hafai kwa sababu kadha wa kadha sio kugawa chama inaitwa freedom of expression.

Kusema nafikiria kugombea uraisi kwa tiketi ya chama changu sio kugawa chama, inaitwa expression of interest.

Kutekeleza sera za chama kwa vitendo wakati wanachama wengine hawajapata courage ya kutekeleza sio kugawa chama, inaitwa leading by example

Kufanya harakati ndani ya chama kupromote new ideas and new way of thinking sio kugawa chama, inaitwa influencing for change

Hivi vyote kwa pamoja na vingine vingi, vina constitute kinachoitwa democracy ambao ndio msingi mkuu wa CDM.

Kukigawa chama ni kwenda tofauti kabisa na misingi mikuu ya uwanzishwaji wa chama. Huwezi kusema mtu anaye promote misingi yote ambayo chama kimejegwa juu yake, anakigawa chama!
 
Mkuu ukimsoma vizuri kamanda Lema utamuelewa,

Anatoa onyo kwa huyo mnafiki msaliti a.k.a Mzee wa Tunguli, kaaga Kigoma
Anatoa elimu kwa vijana tusiwe wasaliti... katoa na mifano ya vijana waliokatishwa ndoto zao za kisiasa...
Anatutia moyo ni mtu moja tu anaetuvuruga ni mnafiki hata wanaomtumia wanamuona mnafiki.

vile vile anatoa hamasa kwa vijana
Kumbuka tu CHADEMA ilikuwepo, lakini tangu hao unao waita wasaliti washikem hatamu chamani ndipo chama kikaonekana thabiti nakuenea kwa kasi ya ajabu, walipoona sasa wamesimama kwa miguu miwili wakaanza kuota pembe za kibaguzi (wa aina yeyote ile), ile dhana ya kuwa chama cha demokrasia ikapotea, ikawa waliokalia madaraka ndio hao hao yaani hastahili au hakuna mtu anayeweza kukalia nafasi hizo.
Baada ya kuona watu hawakatishwi tamaa na wanaendelea kukitumikia chama sasa kile kikundi kilicho hodhi madaraka kinatumia wtu wachache wenye mtazamo sawa na wao kuwaita watu fulani eti ni wasaliti..
Swali, je kuhoji jambo linalo husu mwenendo wa chama ama matendo ya viongozi waliopo madarakani ni usaliti? je kuwa huru kutoa maoni ama dukuduku lako ni usaliti? je kutokukubaliana na ama kutofautiana mitazamo ni usaliti?
Ikiwa mnafikiri kuwa sasa mmesimama Imara kwa miguu yenu wenyewe mmekosea, Na ole wenu mfanye hilo mnalofikiria kulifanya sasa..hapo ndipo ile nguvu iliyotumika kuwafikisha hapo mlipo itakapo warudisha mlipo toka na kujigundua kwamba si lolote wala chochote kwa watanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom