Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
mkuu kila action ina reaction zake,siyo zitto ,lema,mbowe,slaa watairudisha nyuma chadema

ni afadhali turudi nyuma kwa muda lakini tuje kuwa imara milele.!
Hata siku moja mtu aliyetimamika kiakili na busara hawezi ku muacha nyoka aishi ndani ya nyumba yake.!
 
Mnyonge mnyongeni ilabhaki yake mpeni.

Maelezo ya Lema juu ya CHADEMA kuwafukuza wanafiki kwa kufanya maamuzi magumu ni ya kutafuta kuungwa mkono na wanachama wa
CHADEMA, sioni ubaya kabisa kwa kusema ndani kuna wanafiki. Wale
wanaosema angeongelea kwenye vikao nadhani ameonyesha kutekeleza ilo
kwa kusema chama kifanye maamuzi
magumu hata kama 2015 hawatashika dola lakini watakuwa wamebadilisha
watu fikra.

Maelezo yake hayatofautiani na Zitto
aliposema Kuna mbunge wa upinzani anadai kuwekewa kauzibe kwenye posho. Na hii mngesema basi Zitto angeitolea kwenye vikao vya chama na si kwenye
majukwaa ya kijamii. Zitto aliitoa ili apate huruma ya jamii kwasababu inagusa jamii.

Lema hapa ni kwa wanaCHADEMA suala la wanafiki litakapofika kwenye chama.

Niseme tu kwamba namuhusudu Zitto kwa ujasiri wake wa kupambana lakini
anashindwa kuelewa lengo la yeye kuwa
mpinzani ni nini na kwanini yuko CHADEMA.

Ninachokiona kwa watu hawa wawili hasa upande wa Zitto ni kuwinda pointi
za kisiasa zaidi kuliko kupeperusha itikadi ya chama. Itikadi ina umuhimu kwenye chama kwani ndo inatoa
mwelekeo na inaunganisha wanachama.
Hivyo lazima itikadi itetewe, ifagiliwe na
itafutiwe pointi za kisiasa ili kuvuta watu zaidi kwenye chama na hii ndo lengo la
Lema. Zitto anaenda kinyume ni yeye tu yani anamwangalia Zitto atoke vipi.

Kwa mambo yanayogusa maslahi ya
umma ni vizuri kuwa na msimamo wa ki-chama. Ukianzia suala la posho, kukaguliwa na CAG ni wazi Zitto mbali ya kuwa naibu katibu hakuwahi kuuliza chama chake msimamo juu ya posho
na kama kimekamilisha hesabu kwa mujibu wa taratibu kabla ya kulifikisha
mbele ya kamati za bunge.

NI KWANINI ALILIPELEKA SUALA LA HESABU KAMATI YA BUNGE?

Anajua kabisa kwamba maono ya wengi ni kwamba CHADEMA ni cha wenyewe, yeye anatengwa kitu ambacho si kweli, alijua kabisa watu watasema jamaa wa
Kanda ya kaskazini hawajakamilisha hesabu na kuna kitu hapo. Lengo lake lilifanikiwa.

Utategemea Naibu katibu mkuu ahakikishe Chama chake kinakamilisha
hesabu ili kisimwaribie uhadilifu wake mbele ya wanakamati, hiyo miaka yote alisema hawawakilishi hesabu alikuwa haudhulii vikao na kuuliza kama
walishawakilish a kwa Msajili? Ni kucheza na fikra za watu "chama cha
kikanda, chama cha wenyewe". Na anaelewa kabisa mwisho wake
ungekuwa hivyo.

Mahojiano na clouds fm alisema ikifika zamu ya CHADEMA yeye hatakuwa
mwenyekiti wa kikao cha kamati kuondoa mgongano wa kimaslahi. Hii inaonyesha anajua yeye ni CHADEMA,
kwanini hakuwapelekesha wahasibu wa chama na viongozi wenzake kulinda
heshima ya chama ambacho ye ni kiongozi.

Tukirudi kwenye suala la posho hivi hawakuitana wabunge wa CHADEMA kabla ya kikao cha bunge na kuwa na uhamuzi wa pamoja?. Lakini akasimama mwenyewe na kusema hataki posho. Ikalazimu Chama kutoa taarifa badae kumuunga mkono juu ya posho.

NANI AMESIKIA WABUNGE CCM NA
WINGI WAO WANAKATAA POSHO HATA MABILIONEA KAMA MO DEWJI? Hakuna. Wali-caucus na kuja na uamuzi wa pamoja kwa manufaa ya chama wa
kuunga mkono posho.

Kama ingewazamisha ni wote si mmoja mmoja.

Hii ndo ilikuwa hoja ya Lema kwa kila nafasi mtu aliyonayo awe mbunge, mwanachama au kiongozi ni kukipigania chama, kukipa pointi za kisiasa, kujua lengo ni chama kuchukua dola, kuvutia
wanachama.

Inawezekana lugha ya Lema haikustahili lakini ujumbe wake ni kwa watu kujitambua kwanini ni wapinzani na kwanini wako chama fulani.

Natambua Zitto analitumikia taifa kama mbunge lakini haiondoi wajibu wa kukikuza chama kwa hoja za pamoja. Hatutaki kumpa mtu urais alafu aanze kutafuta pointi za kisiasa za jumuiya ya
Afrika Mashariki.
 
tatizo watanzania ni wavivu wa kufanya research!
Wengi hawamjui zitto ni mtu wa namna gani! Huyu jamaa ni hatari sana kwa survival ya chama cha kizalendo kama chdm..
Zitto ni kibaraka mkubwa, and he has been for a long time!

kwanini hachukuliwi hatua bwana! Anafugwa kwanini? Mmesubiri uchanguzi umekaribia ndio mnataka kuanza fukuzafukuza! Au wote mmehongwa na ccm ili mvuruge chama!
 
Siasa za haki au majitaka??

Iweje kutumia nguvu nyingi sana kumchafua zitto hali ya kuwa ni kiongoz mkuu ndan ya chama na msitumie vikao kama hizo hoja ziko sahihi??

Na kila anaoeonekana kuisema chadema na kupingana nayo lazima aonekane ni msalit au ana mapenz na CCM,,huo ni ujinga wa hali ya juu sana,

Nawaambien,zitto hawez kutoka ndan ya chama hiki,nyinyi nyote mmekuta na hakuna mlilolifanya la maana la kuja kujifananisha na zitto na mnalitambua hilo,mnataka kuleta ukanda na ubaguz,,

Kama kweli mnaweza mfukuzen zitto ndan ya chama hiki,kisha mtaona picha litavyokuwa

Hatuwezi kumuacha mtu aendelee na usaliti wake kisa yeye ni wa zamani kwenye chama. Aliondoka Katibu mkuu Dr. Kabouru itakuwa huyu? Imani ya CHADEMA imo mioyoni mwa waTz maneno yenu hayana nafasi ever
 
tatizo watanzania ni wavivu wa kufanya research!
Wengi hawamjui zitto ni mtu wa namna gani! Huyu jamaa ni hatari sana kwa survival ya chama cha kizalendo kama chdm..
Zitto ni kibaraka mkubwa, and he has been for a long time!

Basket of lazzy bones!!!!!

Watanzania gani unawazungumzia hapa!!!????Tuna akili na uzalendo kuliko wewe mara 1,000,000 ila tunaangalia kwa nje bila ya attachments!!!! Unajua kwa nini siasa hazina permanent enemy wala friend!!!!!

Unaongelea research,umefanya lini wapi methodlogy,sample,analysis,findings,conclusion na reccomendation ziko wapi!!!!! Ume present wapi???!!! Dissemination!!!!!!Kama haya umeyafanya na umekalia hii wewe mchawi wa mchana kweupe!!!!!

Unaweza kusema umefanya research wewe na kutuita uje ufanye presentation!!!?????

Acheni kubwabwaja na kuafuta umaarufu huku mkilaumu watanzania kuwa wavivu sababu mmepata nafasi ya kufuta ujinga!!!!!

I dare you
 
Napenda nimwombe Zitto asijibu mapigo acha tu hawa watu waendelee kuongea sana na kuzidi kujianika ni aina gani watu walioko ndani ya Chadema,Naamini Zitto ana busara nzuri sana,Elimu ya kweli na upeo mpana wa kuchambua mambo kiasi cha kutambua kuwa akijibu mapigo hatawakomesha maadui zake tu bali anaweza kukizamisha Chama mazima pia.Ninaamini hii ndio sifa kuu ambayo Zitto anayo ambayo wengi wenu mnaokesha humu JF kumshambulia Zitto hamna.Najua siku Zitto akisema enough is enough....Akaanza kuanika mambo mazito yanayotendeka nyuma ya pazia na baadhi ya Viongozi wetu wa Chama nadhani hakutatosha humu.
 
Mh. Zito ni naibu katibu mkuu na ni kiongozi wa kanda ya magharibi, na ndiyo tegemeo letu wana magharibi. Kumwita msaliti maana yake ni kwamba kanda yote ya magharibi ni wasaliti sasa sisi tunasema, Chadema tutaiua kwani ni rahisi sana. Tunawaomba viongozi wakuu wakiokoe chama na hasa Dr. Slaa kama kweli anataka kuwa rais wa Tanzania. Dr. Hataweza kuwa rais ikiwa maneno haya yataendelea kujadiliwa na kukifanya chama kugawanyika. Angalizo: hakuna mtu wa kanda ya ziwa, magharibi, nyanda za juu kusini wala kanda ya kati atakayewaunga mkono KASKAZINI kama mtaendelea kuleta za kuleta!!! Acheni ujinga na fanyeni kujenga chama kila mtu alipo na kwa nafasi yake.

Cheap politics .CHADEMA ni taasisi.Kujadili kanda na watu ni ujinga
 
Naona Lema amekuja kusaidia kamati ya majungu mitandaoni dhidi ya Zitto.

Zitto msaliti kama W Kaburu lakini akae akijua hatofanikiwa kamwe kuisambaratisha CHADEMA, nani asojua jinsi anaandaliwa na magamba kugombea uraisi na kampeni meneja wake atakuwa Mr dhaifu.
 
Kweli CCM kiboko na
inastahili kuheshimiwa. Msaliti ama wasaliti wamepandikizwa ndani ya
Chadema na kushika nafasi nyeti sana hivyo wanaijua Chadema nje ndani
kitu ambacho inawapa urahisi kuiua Chadema. R.I.P Chadema.

naomba nikusahihishe!
Zitto hakupandikizwa, Zitto alinunuliwa!
 
Hatuwezi kumuacha mtu aendelee na usaliti wake kisa yeye ni wa zamani kwenye chama. Aliondoka Katibu mkuu Dr. Kabouru itakuwa huyu? Imani ya CHADEMA imo mioyoni mwa waTz maneno yenu hayana nafasi ever

Acheni kupumbaza wananchi na kuwajaza jazba wafuasi wakati kumtimua haizidi masaa 24 fanyeni hivyo ili amani ya wafuasi ipatikane na chama kianze ajenda mpya!!!!!!

Maneno yenu ndio hayana nafasi tena sababu sasa mnatakiwa mfanye vitendo maneno mnayarudia tu kwa tone na tune tofauti!!!!!
 
Ndivyo mnavyotiana ujinga? utakesha sana hapa jamvini ikulu mtaiskia kwenye vyombo vya habari na magazeti tu.
Mchukueni msaliti wenu zitto mgombea wenu uraisi lakini CHADEMA huwezi kuihujumu kamwe iwe mchana usiku.Mlifanikiwa kwa CUF TLP NA NCCR MAGEUZI, kwa CHADEMA hamtofanikiwa kamwe.
 
Hii ni kampeni nzito ya kumuondoa Zitto kabwe Chadema, inaonekana kuwa imeratibiwa na kikundi cha watu ndani ya chadema. Nafumba macho na kukiona kikundi hicho kikijipongeza na kusema ''safari hii lazima ang'oke''. Baraka na nguvu hiyo imetoka wapi? What is the Motive?? Hii inakuja kuwa game kali zaidi ndani ya chadema na siasa za Tanzania ya ''Who is smarter?''. I declare my Interest, am Team Zitto!
same to me bro...I go for ZZK mpaka hawa shwaini wasepe. ZZK kapigania mambo mengi yenye mantiki kwa taifa sio hawa kina Lema,ben na mbowe eti wanatambia kulala sero, sasa kulala kwao sero kumesaidia nini ama kuleta nini katika taifa. Pumbaf, GO GO ZZK wenye akili zao tupo nyuma yako braza
 
kwa huu mwenendo wa
majungu ya chadema kuchukua dola ni ndoto! Huu upuuzi wa kurumbana bila
sababu ya msingi hauwezi kuitoa ccm madarakani.ninachokiona mbinu ya
ccm kushinda kwa kushindo ipo mlango na mkakati umekamika!

nimeshasema hapo awali, na nitasema tenatna tena! Ni heri chadema kisichukue dola lakini kikawa ni chama imara chenye wazalendo wanaofanya kazi kama team, kuliko kuchukua dola huku mkiwa 'handcaped' kwa kujaza wasaliti na wanafiki.! Hatutaweza kuongoza nchi na itakuwa dissappointment kubwa zaidi!
 
Zitto ndugu yangu usijitokeze kujibu upuuzi wa hawa jamaa sana sana utajishusha tu-a stupid person will always try to drag you down to his level of argument and beat you with experience,That's what they trying to do right now.When they want to drag you down to their level,Drag them up to your level!!!!




Hawa jamaa akili zao kama za vilabuni,

Umemuona huyo mjela mjela KILEO nae kaja na shutuma zake za mambo ambayo alikuwa anafanyiwa na zitto enz hizo yuko selo??

Hebu sasa aulizwe kipindi chote alikaa kimya huku akichelea kitu gani kusema??kwanin hakupeleka tuhuma kwenye chama??

ANASEMA ANATAKA KUZIANIKA HAPA JF KWA FAIDA YA NANI?NA ILI IWEJE??

UNAJUA HAYA MAMBO MENGINE WALA HAYAHITAJI SHULE ILI KUWEZA KUJUA UJINGA NA UTAAHIRA ULIOPO,

THATS WHY WATU WENYE AKILI ZAO TIMAMU KAMA LISU,MNYIKA HATA MBOWE MWNYEWE HUWEZ KUWASKIA WANATOKEA HAPA HADHARANI KUONGEA UJINGA UJINGA KAMA HUU,

NI HAWA HAWA MAPIMBI WASIO NA UPEO NDIO TUNAWAONA SIKU ZOTE WANAONGEA PUMBA NA KUJIDHALILISHA,

WANAPIGANA VITA KALI NA MTU MMOJA AMBAE HATA HUKO NDAN YA CHAMA KUMKABILI WANASHINDWA,WANAWEZAJE KUSHIKA DOLA NA KUKABILI CHANGAMOTO ZA UTAWALA ZA NDAN NA NJE YA NCHI??

FAILURES HAWA,WATU KAMA LEMA HATA HII NAFAS YA UBUNGE INAONESHA NI KAMA NGEKEWA NA HAKUWAHI HATA KUIWAZA MAISHAN MWAKE NDIO KWA MAANA UNAONA WAZ WAZ UPEO WAKE ULIVO FINYU HATA KATIKA KUJENGA HOJA NA KUISIMAMIA,

AMEONA ASHATOLEWA MAANA KWA UROHO WAKE WA KUDAI POSHO SASA ANATAFUTA SYMPATHY KWA KUTAKA KUONESHA MAPUNGUFU YA MWENZAKE ILI KUIFISHA HOJA ILE,YEYE NI MNAFIKI SIO TUH KWA CHADEMA,LEMA NI MNAFIKI KWA TAIFA ZIMA.,ANAEJIVISHA NGOZI YA UANAHARAKATI HUKU AKIPIGANIA MASLAHI YA TUMBO LAKE,

ATAFUTE MISUKULE WA KUMPA BACK UP KAMA YULE NJAA KALI SAA NANE NA YERICKO,ATAFUTE WATU HOPLESS NA WALIOJIKATIA TAMAA ZA MAISHA KAMA HAO MAY BE WANAWEZA KULAMBA BUTI ZAKE,

KWA WENGINE WOTE WENYE AKILI ZAO TIMAMU WANAPUUZA UTOTO KAMA HUU NA SIASA ZA KIJINGA KAMA HIZI,

2015 HII HAPA KWENYE KONA BADALA KUJIKITA KATIKA KUJENGA CHAMA NA HAYO MAMBO YA MIGOGORO WAKAYASOLVE NDAN YA CHAMA WAO WANAKUJA HADHARANI KUONESHA MPASUKO NA UDHAIFU THEN WANASEMA WANA NIA YA KUIANGUSHA CCM MADARAKANI,HILO LINAWEZEKANA VIPI??

AKILI ZA KITOTO HIZO,,,JF INAWAONGOPEA SANA HAWA,WAJE HUKU MTAANI WAONE UHALISIA WA CHAMA,NA WASIENDE TUH MOSHI NA ARUSHA,WAMULIKE KWA NGAZ YA TAIFA ZIMA WAONE UPEPO UKOJE
UNAJ
N
 
Sasa kumekucha, ile minong'ono ya chini chini sasa inapanda juu na kupaza sauti, si siri tena ni dhahiri sasa CHADEMA kutofautiana ambako kumepelekea kutoamianiana.

Mkuu lema, wewe unachokifanya hapa ni tofauti na alicho kifanya Mwigamba? je kwa nini chama chenu kisiwe ndicho kinachotoa shutuma ama tuhuma hizi adharani?

Pia huoni kwamba hao unao waita ama mnaowaita wasaliti watapata pakushikilia ikiwa mtaendeleza mwenendo huu huu wa kutumia majukwaa haya kuwasilisha hisia zenu?
 
nimeshasema hapo awali, na nitasema tenatna tena! Ni heri chadema kisichukue dola lakini kikawa ni chama imara chenye wazalendo wanaofanya kazi kama team, kuliko kuchukua dola huku mkiwa 'handcaped' kwa kujaza wasaliti na wanafiki.! Hatutaweza kuongoza nchi na itakuwa dissappointment kubwa zaidi!

Clean the house guys if you mean buziness!!!!!!
Too much of hearsays!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom