Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Hayo mabilioni anapewa na nani, mbona mnaleta stori za vilabuni jamani. Kama ushahidi upo basi uleteni humu. Hivi ndio viwanda vya uongo.

Bahati mbaya anayehoji haya siyo mhusika. Kimsingi Zitto hana tofauti na magamba wenzako wanaotafuna fedha za umma kwa njia ya kificho.
 
Zitto anaungwa mkono na chadema pamoja na Lema kukataa posho. tatizo ni pale Zitto anapokataa posho kinafiki. Hivi inawezekanaje Zitto akatae posho ya sh 80 elfu, huku anafanya matanuzi makubwa ya kifisadi? Zitto hana biashara nyingine zaidi ya ubunge lakini cha ajabu ana ukwasi wa kutisha. Anatakiwa kuchunguzwa.

Zitto mtu wa ajabu... amekataa posho za elfu 80 za wazi, halafu anapokea mabilioni ya kifisadi kificho tena ya hovyo yenye lengo la kuiangamiza chama ambacho watanzania maskini wamekiamini.
Mungi usilete porojo hapa, weka ushahidi wa UKWASI wa ZITTO. alisha-declare mali zake kwenye tume ya maadili. zitto ahongeki kirahisi kama Godbless J Lema aliyehongwa milioni 30 akaachia ubunge mwaka 2005.
 
Last edited by a moderator:
huyu lema ameota pembe na kujawa na kiburi maana kama si hivyo angesikiliza tulichomwambia.

Lema amekuwa mtu wa ajabu kiasi hiki?lema anasahau kuwa zitto hakuanza kupinga posho leo ,lema anashindwa kujua kuwa zitto amzuii kuchukua posho ndio maana yeye amekuwa akichukua zitto achukui na hakuwa kuja kumsema humu.

Hii leo lema amepata kiburi cha kuja kupinga wenzie tena kwenye mitandao wakati kashindwa kujenga hoja kwenye vikao.

Huyu lema anatakiwa kukemewa kuacha kutumia mitandao vibaya wakati kuna vikao.

Katika hili ndio ntajua busara za mbowe na dr slaa.
Lema ana vuruga chama kwa haya na mitafaruku anailazimisha sasa ni wa kuangalia.

ulipoanza jana kupinga nilijua ni kwa kuwa hujaelewa hoja lakini nimegundua hutaki makusudi kuelewa...
 
Mungi usilete porojo hapa, weka ushahidi wa UKWASI wa ZITTO. alisha-declare mali zake kwenye tume ya maadili. zitto ahongeki kirahisi kama Godbless J Lema aliyehongwa milioni 30 akaachia ubunge mwaka 2005.

kijana wewe ni ccm imekuwaje macho yamekutoka kiasi hiki kumtetea mtu wa chadema..je unajua zitto aliwahi kuhojiwa na JF.. rudi tena hapo kwenye thread lema amesema amzungumzia Zitto na posho na hii itakuwa kabla ya saa nane..
 
Last edited by a moderator:
Mungi usilete porojo hapa, weka ushahidi wa UKWASI wa ZITTO. alisha-declare mali zake kwenye tume ya maadili. zitto ahongeki kirahisi kama Godbless J Lema aliyehongwa milioni 30 akaachia ubunge mwaka 2005.

hahahaaaaa.... eti ccm wanataka ushahidi tena kwa uchungu mkubwa hivi????!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mh Lema naona Ameamua kuweka wazi!! Maana bila chama kuchukua hatua, tutakua tunatwanga maji kwenye kinu!!
Mtu anayefadhiwa na kina Zoka, kweli atakuwa na mustakabali mzuri na chama??? Uponyaji wa kansa ni kuondoa kiungo, vinginevyo utapoteza mwili woote(kufa)
 
Mungi,
Naamini ukombozi wa inchi hii utaanzia arusha kwa kuwa kule siasa sio biashara ila kuwatumikia wananchi ndio nia ya dhati kwa viongozi wa kisiasa. Naamini hilo.

Haya ya Zitto na ufisadi naamini mna ushahidi mzito usiotia shaka maana hii thread inaweza angusha chama.

Laptop ya Mwigamba ina nondo eeeh
 
katika hili lema amekuwa mjinga sana.

Hapana, nadhan kumbukumbu za Mh. zitakuwa na kutu kidogo, na tunaomtakia
mema tuna wajibu wa kumkumbusha kwa kadri ya uwezo wetu

1. Ilani ya CDM (2010-2015) katika suala la posho za vikao iko wazi kabisa. Msimamo ni kuzifuta kabisa, na si kwa wabunge pekee, bali kwenye mfumo mzima wa Utumishi wa UMMA.

Hoja kwamba CDM haiongozi Serikali hivyo kushindwa kuzifuta haina
mashiko, kwan wabunge wake walipaswa walau kuzikataa ili kuonyesha mfano
(kama afanyavyo Zitto)

2. Sheria ya Utawala wa Bunge ya Mwaka 2008 haiitambui posho hii (Sitting
Allowance). Kifungu cha 19 kinazitambua posho za kujikimu, usafiri na wasaidizi.

Lakini kifungu hiki cha 19 ndio kinatoa mwanya kwa Rais kutoa posho zingine kwa wabunge kwa namna anavyoona inafaa, na ndipo tunapopata hii
"Sitting Allowance"

Kimsingi posho hii ya vikao inatolewa kwa kudra za Mh. Rais ambaye pia ni M/Kiti wa CCM, anayetekeleza sera za CCM (kulipana posho za vikao). Sasa kwa mbunge wa Upinzani kumshawishi Rais awaongezee posho hii ni kwenda kinyume na Sera za CDM, ilani ya CDM na Misingi ya CDM ambayo tuliamini ninyi mtaisimamia
 
wewe ni gamba, ajabu ni kwamba umeumia kuliko hata wanachadema kulikoni?

haya ni mawazo ya Lema, siyo tamko la chama. Lema angemtaja mtu moja kwa moja naamini kurugenzi ingekuja kusawazisha.

Kwani katika majibu ya Lema hapo juu hajamtaja Zitto?
 
Lema wewe ni mjinga tena sana na kamwe. Zitto haja kulazimisha usichukue posho, kumpinga mtu kisa hachukui posho ni chuki binafsi.

Wewe ni nani kukaa na kuanza kusema wabunge wenzio kwenye mitandao?

Godbless J Lema wewe ni wa kupuuzwa umepitiliza sasa, umeshindwa kujenga hoja kwenye vikao una kuja kuchafua wenzio kwenye mitandao.

Dr slaa, mbowe, na wana chadema mkae mkijua huyu Lema ndio anachimba kaburi la CHADEMA.

Lema wewe ni mjinga sana.
Kwakweli nitashangaa huyu mtu kuachwa hivi hivi bila kushikishwa adabu huu ni ujinga kabisa.

Wewe Lema naona ndio umetumwa kuanzisha vurugu na huna busara kabisa huu ni ujinga.

Wanachadema lazima tuungane kupinga huu ujinga wa Lema.

Naomba mh Zitto usipoteze muda kujibu huyu mjinga anakiangamiza chama huku anatuhumu wengine.

Kwakweli sitowaelewa CHADEMA wakimuacha Lema aendelee na huu ujinga wa kukivuruga chama.

Watu wanatakiwa kujua Lema ana nia nzuri na kama angekuwa nayo asingefanya haya.

Lema unajaribu kutuonesha kuwa uko parfect kumbe ni mjinga na huna tofauti namwigamba. Kweli nimeamini aliyesema ufungwe speed governor.

Lema acha kuact kama mtoto, huu umaarufu wako umeupatia kwetu sisi unaotuona wajinga na hutaki kutusikiliza.

Huu ujinga kabisa.

NI LAZIMA LEMA AFUNDISHWE ADABU NA AACHE KULETA MITAFARUKU KWENYE CHAMA NA NINA TEGEMEA TAMKO KUANZIA KESHO KUTOKA KWA VIONGOZI WAKUU WA CHAMA.

mkuu kila action ina reaction zake,siyo zitto ,lema,mbowe,slaa watairudisha nyuma chadema
 
Last edited by a moderator:
Mungi,
Naamini ukombozi wa inchi hii utaanzia arusha kwa kuwa kule siasa sio biashara ila kuwatumikia wananchi ndio nia ya dhati kwa viongozi wa kisiasa. Naamini hilo.

Haya ya Zitto na ufisadi naamini mna ushahidi mzito usiotia shaka maana hii thread inaweza angusha chama.

Laptop ya Mwigamba ina nondo eeeh

Mkuu kuna ushahidi usio na chembe ya doa. Wacha tujitibu magonjwa sugu wenyewe kabla hatujaanza kuwatibu wengine.
hili gonjwa la usaliti na unafiki wacha tulifanyie kazi kwa njia hii. chama kimeulea ugonjwa muda sana
 
Tunajua lema ana backup ya slaa kumchafua zitto. We dr heshma yako itashuka sana jama ukiendlea kufuata ushauri wa huyo mwehu lema.
Zitto ana backup kubwa chamani,mfukuzeni muone mbna mnalialia tu pemben kama watoto? Chama tumekjenga kwa shda hiki.
 
Mh Lema naona Ameamua
kuweka wazi!! Maana bila chama kuchukua hatua, tutakua tunatwanga maji
kwenye kinu!!
Mtu anayefadhiwa na kina Zoka, kweli atakuwa na mustakabali mzuri na
chama??? Uponyaji wa kansa ni kuondoa kiungo, vinginevyo utapoteza mwili
woote(kufa)

Wakati mwingine inategemea na kiungo unachotaka kukiondoa, kwan viungo vingine ndio sehemu ya maisha yenyewe.

Kukiondoa kunaweza harakisha kifo chako, kuliko kama ungebaki nacho.

Uchaguzi unapokaribia wenzenu wanafikiria namna ya kuungana na maadui zao na kumaliza tofauti zao ninyi mnafikiria kutengana!
 
Kwani katika majibu ya Lema hapo juu hajamtaja Zitto?

hiyo ni kwenye thread atakayoirusha leo inayohusu posho, hapo ndipo tutakapoujua msimamo wa Lema kwenye posho
 
Wakati mwingine inategemea na kiungo unachotaka kukiondoa, kwan viungo vingine ndio sehemu ya maisha yenyewe.

Kukiondoa kunaweza harakisha kifo chako, kuliko kama ungebaki nacho.

Uchaguzi unapokaribia wenzenu wanafikiria namna ya kuungana na maadui zao na kumaliza tofauti zao ninyi mnafikiria kutengana!

Kansa ya usaliti hata kama ikiwa kwenye koo bora ikatwe
 
We all knows that ZZK is betrayal and hypocrate but i dont think this a good way of judging/ criticise him.
 
Tunajua lema ana backup ya slaa kumchafua zitto. We dr heshma yako itashuka sana jama ukiendlea kufuata ushauri wa huyo mwehu lema.
Zitto ana backup kubwa chamani,mfukuzeni muone mbna mnalialia tu pemben kama watoto? Chama tumekjenga kwa shda hiki.

Ulijuaje kuwa msaliti na mnafiki anayetajwa ni Zitto?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom