Mgoshi Chamviga salama lakini?
Nadhani unajaribu kuupotosha ukweli kwa maslahi ya wazi kabisa yaliyowazi ya chama chako cha ccm.
Niliwahi kushiriki katika jukwaa la Dini siku nyongi sana na nilipoona kuwa badala ya kufundishana na kuelimishana badala yake jukwaa la dini lilikuwa ni uwanja wa kukashifu dini za wengine nikaacha kulitembelea zaidi ya miaka minne sasa.
Kwahiyo hoja yako kwamba niliushambulia ukatoliki ni hoja dhaifu sana kwakuwa ile thread ya wanafunzi wasabato waliofukuzwa Teku nililazimika kuichangia baada ya kuona watu wamepoteza focus ya mjadala badala ya kujadili hoja ya wanafunzi kufukuzwa Chuo wao wakaamua kuushambulia usabato. Nakwakuwa halimuwa jukwaa la dini nisingeweza kukaa kimya nikiona dini yangu inapotoshwa na kudhalilishwa bila sababu ya msingi. Hatahivyo katika comments zangu hakuna mahali niliushambulia ukatoliki au dhehebu jingine lolote.
Na pia nikufahamishe kuwa mijadala ya kidini na hasa inapohusisha ukristo na uislamu hata Mara moja hutaniona nikishiriki kudebate,sana sana nakuwa msomaji. Kwahiyo basi Nina uhakika kuwa sijawahi kuushambulia Uislamu katika hoja yoyote, si katika jukwaa la siasa ama la dini. Nakupa challenge
CHAMVIGA ulithibitishie hili jukwaa kwamba nimekuwa nauchukia uislamu na kuushambulia. PIA ninakupa changamoto ulipneshe hili jukwaa ni wapi niliushambulia ukatoliki. Failure to do so nitakuona mtu wa hovyo sana na sitakutilia maanani kabisa katika mijadala ya hapa JF. Na kama utashindwa kuthibitisha hayo Mashambulizi kwakuwa naamini umeandika tu kwa bahati mbaya lakini intentionally ili kujenga hoja yako ya uongo, basi kwa uungwana kabisa uniombe radhi yaishe na tusonge mbele na hoja Nyengine za msingi.